🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
By Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)
......................................
*_Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu_*
*SEHEMU YA 8*
_Sifa 7 za Mtumishi wa Kweli wa Yesu Kristo_
.....
.....
.....
_Haleluya mtumishi wa Mungu utumikaye na unayejiandaa kutumika madhabahuni pa Bwana nikukaribishe tena katika sehemu ya 8,kipengele cha 5.Karibu tujifunze_
5⃣ *Ni Mwenye Kutii na kuongozwa na Roho Mtakatifu* Maisha ya Ukristo halisi(usio fake) ni ule ambao Roho mtakatifu ni kengele,( *Alarm*) ya mwamini katika maisha yake. Na huduma yoyote ikiwa chini ya uongozi wa Roho mtakatifu kuna vitu vya kipekee vinatokea,kibali,wepesi,utukufu na Neema ya pekee katika huduma hiyo inaonekana na muhudumu na wahudumiwa. Ni muhinu kujua Mtekelezaji mkuu wa majukumu yote ya Kiroho(Vipawa,karama na huduma mbalimbali)ni Roho Mtakatifu ( *Huwa napenda kumuita Katibu Mkuu wa ofisi zote za kiroho kihuduma*) (WARUMI 8:14,16)..... 14( _wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu_) kwa lugha nyingine kama uta feli kumsikiliza na kutembea na Roho wa Mungu katika utumishi wewe utakuwa hujakidhi vigezo vya kiutumishi,wote wanao tumika kwa Bwana lazima kwanza wawe wana wa Mungu ndo waongozwe na Roho wake katika kutekeleza majukumu yote ya Kiroho.
♦Huduma yoyote isiyo chini ya Maongozi ya Roho mtakatifu uishia kuwa na vituko na uchafu,fatilia kwa makini nyuma ya mtumishi huyo kuna maroho machafu yanamwendesha katika huduma ila yanajivika sura ya Roho wa Bwana(kama Biblia isemavyo shetani ujigeuza kuwa malaika wa nuru).
♦Roho mtakatifu ndo mgawaji wa karama na vipawa( *1Wakorintho 12:1,3,11*) na ndiye anaye toa Mafunuo yote yasiyo na Maswali wala uchafu wala aibu wowote katika kutekeleza kazi ya Mungu.( *_Mfano ukiona mtumishi anamfungua mtu wa Romance(denda) kunyonya mate ya mmama,mdada_ hayo ni mafunuo ya Kipepo naya Aibu* Roho wa Bwana mafunuo yake ni Universal Standard and Ethical.
♦Lakini Roho mtakatifu ndiye nguvu ya utayari na ujasiri wa kutumika madhabahuni pa Bwana,kama hakuna Nguvu ya Roho mtakatifu utakuwa mvivu sana na mwoga katika kutekeleza majukumu ya kiroho. ( *Matendo ya Mitume 1:8*)
♦Wewe unaye tamani kumtumikia Mungu,mtake sana Roho Mtakatifu maishani mwako na ujazwe Roho mtakatifu uwanja wa huduma yako hautakuwa mgumu maana Roho Mtakatifu ni Mafuta( Lubricant oil)katika huduma.
6⃣ *Awe Amebatizwa ubatizo wa Kweli wa Yesu Kristo* Kuna mambo mengine ya Kiroho siyo ya kuyadharau nakuyaona ni mambo ya nyongeza tu,yape uzito sawa kwakuwa yana nguvu katika utumishi. Yesu Kristo hakuanza kazi mpaka alipo batizwa ndipo alipandishwa na Roho wa Bwana nyikani kufunga na kuomba kwaajili ya kazi kubwa ilokuwa mbele yake.
♦Kuna changamoto ya tafsiri za ubatizo karibu 5 mpaka 7,mimi huko siendi namwangalia Mwasisi wa maisha ya Kiroho na utumishi wote Yesu Kristo alibatizwa ubatizo upi na kwa umri gani na kwa neno lake ameagiza watu gani wabatizwe ndiye kioo chetu mengine ni mavumbuzi na hekima za kibinadamu zisizo na nguvu kiroho. ( *Mathayo 3:13-17*) Angalia Roho wa Bwana alishuka kwa Yesu baada ya Kubatizwa wakati anatoka Majini( *Mto Yorodani*)mbingu zikafunguka na Maelekezo yakaanza palepale. Maisha mapya yanazaliwa baada ya ubatizo wa Kweli wa Yesu Kristo( *Matendo ya Mitume 2:38-39*) Ishara na miujiza zinaambatana na watu waliokubali kutimiza Haki yote ya Mungu(Ubatizo)mbali na hapo utakuwa na mapungufu mengi katika huduma yako hata kama utatumika kuna raha utazikosa katika huduma yako. ( *Yohana 3:1-6*)
7⃣ *Ni mtu anayewaza Zaidi juu ya Wengine kuliko Yeye mwenyewe* Sifa hii ni kubwa na muhimu katika utumishi,na yeyote anayeingia katika Tasnia ya Utumishi Lazima moyo wake ujazwe na sifa hii.
♦Angalia tafsiri ya mistari hii uone jinsi ambavyo mtumishi yeyote wa Mungu lazima awe mtu anayetanguliza wengine kwanza kabla yake,ndo sifa ya Bwana wetu Yesu Kristo. ( *Kuacha Enzi na Heshima yote mbinguni kuja duniani atukomboe ni sifa ya Kujali na kuwatanguliza wengine kwanza*) waulize watumishi wa Mungu wote wanaotumika chini ya Mkono wa Mungu watakwambia kuna Haki zao nyingi uzipoteza kwanza kwaajili ya watu wengine baadaye ndo Mungu uwarejeshea mara dufu. ( *Yohana 10:10,Luka 4:16-19*) tuna watumishi wengi wahuni sana wanajitanguliza wao kwanza,wanatazama kufanikiwa wao,heshima kwanza wao mengine baadaye hawa ni mbwa mwitu.Wararuaji wa kundi siyo walinda kundi na walisha kundi.
♦Lakini siri ya kuinuliwa zaidi katika huduma,kuwa mtu wa kuwatanguliza wengine kwanza kwa faida ya ufalme wa Bwana,mtangulize Mungu kwanza. Shida kubwa na matokeo ya huduma zilizo poa sana,au zakawaida sana ni matokeo ya watu kujitanguliza wao kabla ya Bwana na watu wake.( *Wafilipi 2:8-11*)
♦ Swali la msingi kwako katika kipengele hiki cha mwisho, *_Kwa nini unatamani Mungu aonekane kwa viwango vikubwa sana katika huduma yako(kupitia wewe) ni ili iweje?_* Usikilize moyo wako unacho taka ndicho kinasababisha huduma yako iwe na nguvu au yakawaida sana. ( *1Wafalme 3:5-13*) anza kumwambia Bwana nipe neema ya kuwatazama na kuwawaza wengine wainuliwe kupitia mimi hata kabla yangu kuinuliwa,tamani kuwasaidia wengine wafanikiwe hata kama wewe hujafanikiwa,tamani heshima na utukufu apewe Bwana wewe ubaki kuwa mtumwa tu.
*_Mungu akubariki sana katika sehemu hii ya sifa za mtumishi wa kweli wa Yesu Kristo,endelea kufatilia sehemu zinazokuja zilizo nzuri sana za kukufanya utumike kwa viwango vya Kiroho_*
Ulikuwa nami *Ev Elisha Kazimoto*
Facebook Elisha Kazimoto
Whatsapp 0755444078.
Thursday, 2 August 2018
SEHEMU YA NENO SEHEMU YA 8
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment