💈💈 *Swali nirefu ila Mahudhui yake ni: Kijana ni mtumishi wa Mungu,alianzisha mahusiano ya urafiki na binti kanisa anako sali(tumika),baadaye yakavunjika bila (bila kufikia uchumba na kuoana),akachumbia binti kanisa lingine,akafunga na ndoa...Shida ni Watu wanamlaumu kwa kumuacha yule wa kwanza na kuoa mwingine*💈💈
..........
..........
_Anajibu Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na ndoa Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
.........................................
*KATIKA MADA HII NI AINISHE VITU AMBAVYO WAHANGA, NA WASOMAJI TUVIFAHAMU* Ntachambua kimoja kimoja.
1⃣Kulingana na maelezo ya sms hii.....( *Hawa watu kijana na dada wa kwanza walikuwa Marafiki,urafiki uliolenga kuelekea uchumba*)
2⃣Mahusiano ya urafiki yalikuwa makubwa kiasi cha kuwashawishi watu kujua hawa watu watakuja kuoana(makosa pande 2, wahusika na kanisa)
3⃣Hawa watu wakavunja mahusiano ya Urafiki( *Siyo uchumba wala ndoa*) Tafsiri potofu ya hisia.....
4⃣Kijana akapata msichana mwingine,kanisa lingine wakawa wachumba mpaka kufunga ndoa( *Dhambi iko wapi kwa kijana,kanisa,au binti wa zamani*)ntachambua
5⃣Kuna lugha ya kijana amewachezea wengi wadada( *Chumbia chumbia.....Tutatafuta Kosa na tatizo*)
6⃣Kijana amepewa sifa ya kuwa alikuwa anatumika(mtumishi wa Mungu) *Je,mtumishi ndo hana hisia? Akubali udhaifu kisa ni mtumishi, asimame vipi kulinda nafasi yake* ntachambua.
7⃣Tunamsaidiaje maneno yaliyozagaa ya kulaumiwa?( *Swali la msingi, break up zote alizopitia alizihitimishaje*) ntachambua
1⃣ Hapa niweke mambo kama mawili sawa,utofauti wake,usahihi wake na ubaya wake.......
_Mtoa mada anasema kijana alikuwa *Rafiki na binti* urafiki unaoelekea *Uchumba*_
👉Usahihi wake, kijana yuko sahihi katika hatua za kuelekea ndoa kuna aina 2 za kutumia, moja Ni kuanzisha URAFIKI na msichana ambao lengo kubwa ni kumdadisi,kumsoma mtu kujua kama anafaa *Kupewa Tamko,Nia ya Kuanza safari ya uchumba* (Njia ya Pili ni Kuchumbia moja kwa moja bila kupitia urafiki)
Urafiki una level, kuna urafiki wa kawaida wa mbali ambapo mna mahusiano ya kimajukumu.... Kama ni kwenye kwaya,praise,idara ya vijana,wanachuo mnasoma wote nk, kuna urafiki wa Kuzoeana na Kushirikishana na kusaidiana mambo kadha wa kadha, hapa pamoja mnaweza kuwa mnaunganishwa na majukumu au mazingira lakini huyo rafiki anakuwa mshauri mkuu na mtu wa kutafuta msaada kwake akiwa wa kwanza,na aina nyingine ni Urafiki wa uliokolea wa kutafuta Kujua uwezo wa mtu kuthamini maisha yako kama akitokea anakuwa ndiye mchumba au mme au mke. Hapa mawasiliano,kujaliana,kusaidiana kwa mzigo mkubwa kupo hapa....Lakini katika level hizi zote, kila mmoja anakuwa Anamshtuka mwenzake, *Anataka nini,anaweza akanitamkia kunichumbia?anaweza kukubali ombi langu?* hapa hakuna anaye jua maana Hawajatamkiana,ila kuna SENTENSI ZA KUTEGANA zinazo ashiria NIA YA MTU ya ndani juu ya urafiki wenu.
NB: *_Kwenye urafiki hakuna Agano,hakuna kisingizio cha huyu wangu, hatumilikigi Rafiki,Hatuna wivu kwa Rafiki, Hatuna masharti kwa Rafiki, Hatuna Idadi ya Rafiki,hata kama urafiki wenu ni mkuuubwa, Usijipe Asilimia 9⃣5⃣za kuchumbiwa na huyo. UNAWEZA KUWA RAFIKI ANAYE FAA KWAKE ILA HUWEZI,HUNA VIGEZO VYA KUWA MME AU MKE WAKE. Ndo maana wengi wamejikuta wanashangaa, yaani katika urafiki uliokolea sana Akiingiza Wazo la Kumchumbia Anakataliwa au Urafiki unakufa,au Anasubiria aambiwe Nakupenda uwe mke wangu mtarajiwa,anashangaa Anapewa kadi ya Harusi 🙄🙄🙄🙄anajiuliza urafiki ule amechumbia mwingine ameniacha mimi‼Ndiyo amekuacha, unafaa kuwa Rafiki ila siyo kuwa mme au mke.(Mambo ya Kisaikolojia hayo,usipo jua utawalaumu sana wakaka,au wadada.... Usijichumbie kabla Hujachumbiwa_* Tafuta google/Facebook Somo langu la *Saikolojia ya Wavulana katika Mahusiano*( _By Ev Elisha Kazimoto_) utapata majibu zaidi.
👉Kutokuwa sahii ni pale ambapo kijana amemtamkia binti kutaka uchumba,binti akakubali,na wakawashirikisha baadhi ya watu,halafu kijana akavunja uchumba kinyemela kwa kumpata mtu mwingine bila Kufikia maridhiano na wa kwanza kuachana kwa Amani.( Tunapaswa kujua Urafiki, Uchumba si Ndoa Muda wowote Unaweza kuvunja ila ufuate taratibu za Amani siyo za kihuni katika kuvunja.)
2⃣Mahusiano yao ya urafiki inaonekana yalikuwa ya ukaribu wa daraja la 3 nililosemea la ndani,kiasi cha watu kuhisi uwenda wanachumbiana.
👉Kosa la kiufundi la kijana na binti ni kutoweka mipaka ya kirafiki wakati wanajua hawaja kubaliana kuwa wachumba,katika ukaribu wao wangeonyesha bado wao ni marafiki siyo wachumba hata kwa wadadisi wangejua kuwa hawa urafiki umezidi ila siyo wachumba.(japo ni vigumu ku Control urafiki wa daraja la 3)
👉Kosa la jamii au kanisa ni Kuwachumbisha watu wakati hakuna ambaye ameisha letewa Taarifa Rasmi kuwa Nataka kumchumbia au namchumbia huyu dada,au kaka flani ananichumbia.(shida ni kutokuwa na ufahamu wa Saikolojia ya Mahusiano)kila wakiona watu wanaelewana sana basi NIWACHUMBA hayo ndo yametapakaa makanisani, *_Kujadiri ukaribu wa vijana na kuwachumbishana au kuwazinishana bila ya watu walio na Hekima kuwaita pembeni aidha mmoja au wote na kutaka kujua Ukaribu wao unamaanisha nini_* ili kuponya mioyo ya watu wawaonao, kuponya wokovu wao walio marafiki, kulinda ushuhuda wa kanisa. *Huu ndo udhaifu wa makanisa yetu ya sasa* tofauti na tuliko toka miaka ya 1995 kurudi nyuma.(pale wamama,wazee wa kanisa,mama mchungaji,kiongozi wa vijana wameisha kufikia na kukwambia kwa upendo ndugu VIPI hatuelewi,tuweke wazi tusiingie kwenye dhambi ya uzushi,uongo na makwazo,ndo unatiririka...Basi wanakushauri,punguza ukaribu,au Toa msimamo mjulikane Rasmi su Jitahidi kulinda Ushuhuda kuweni na mipaka na kiasi.
👉(Labda niwape siri ya Saikolojia ya Mahusiano ya Kirafiki au Uchumba, *_Wale wanaohusiana(Marafiki/Wachumba) Hawaonagi Ukaribu wao kama ni Mkubwa,uwa wanaona bado wako mbali wanapambana sana kuwa karibu,ila mnao tazama mnashika vichwa kuwa wamezidi_* ndo maana ukiwambia mpo karibu sana wanakushangaa na wanaweza kukatalia kuwa sisi tuko mbali mpaka Washirikiane kimwili ndo uona na kujua kuwa ukaribu wao ni mkubwa.Sasa hawa wanahitaji kusaidiwa kwa upendo si kuwalaumu na kuwanungunikia pembeni.
👉Kwa hiyo hapo Wanao mlalamikia Kijana,baada ya kuoa mwingine ukiwauliza nani aliongea naye wakati anamahusiano na binti wa kwanza kujua ni wachumba au rafiki tu,hayupo,au alipo chumbia mwingine walio mfuata kumuuliza vipi yule wa kwanza utakuta hayupo.
*_Tuache Kuhisi na kuzungumzia Hisia huo ni Umbea wa Kiroho_* Tafuta kweli na Usaidie kama huwezi mwambie anayeweza afanye kazi hiyo badala yako.Huo ndo Wokovu.
3⃣Nisahii kabisa *Kuvunja Mahusiano* yoyote yawe ya Urafiki au Uchumba pale unapo hisi kuna shida ambayo haibadiriki,au haitaruhusu mfike kwenye ndoa na muishi kwa amani, ni vema kuvunja kabla hamjaingia hatua muhimu na za ndani kama kulipa Mahari na kusambaza kadi...Lakini siyo urafiki kuvunjwa hata Uchumba Unavunjwa hata *Siku hiyo hiyo ya Harusi kabla ya kuweka Pete ya Agano* Ndo maana huwa wanaulizwa _Kuna neno lolote la kukufanya USIFUNGE NDOA na huyu kijana au binti?_ kila mtu anaulizwa mmevaa shera na suti, ukisema NDIYO kwisha biashara mpaka sababu hiyo itatuliwe au ndo uchumba umeishia hapo na hapo HAKUMA DHAMBI YOYOTE, watu ndo mtalia,mtalaani,mtatukana ila ni heri kuvunja urafiki,uchumba Kuliko kuvunja Ndoa( unajikaza ile ya watu watanielewaje unahisi kwenye ndoa ni Soka ⚽ linalo chezwa vipindi viwili tofauti, 45 halafu Half time dk 15 halafu 45 za mwisho🤸♀🤸♀🤸♀🤸♀ ukishaingia umeingia ukiingia kwa bahati mbaya nenda kazibe bati hizo mbaya ziache kuvuja,au vumilia kuvuja mpaka kaburini.
👉Wanao sema au mlaumu kijana walimuuliza kujua kwa nini amevunja urafiki? halafu sasa ni Urafiki si uchumba 😏😏? Je walimsikia binti analalamika, na kama analalamika amesema makosa yake katika mahusiano yaliyopelekea kijana avunje mahusiano? Je,walitaka kijana aoe mtu ambaye amegundua hawataishi kwenye ndoa kwa amani,ajikaze amuoe kwakuwa watu wengi wanajua ni marafiki wataoana? Kwani anawaolea watu au anaoa mke wake? Kwani kwenye ndoa watu watakuwepo *_Watakapo kuwa wanalala mzungu wanne_* wacha mtu afanye maamuzi atakayo jilaumu mwenyewe si kuwalaumu ninyi mlio *Mshinikiza kuingia kwenye ndoa na huyo mtu* hii tabia imeua ndoa nyingi za vijana wa kiroho makanisani
4⃣Kijana kupata mchumba mwingine siyo dhambi, isitoshe mpaka anachumbia,mpaka anafunga ndoa binti muhusika alikuwepo,hajalalamika, *_Kisheria uwa kuna siku 21 za kutangaza uchumba na tarehe ya ndoa,huo muda ndo una ruhusiwa kupeleka kipingamizi kwa msajili wa ndoa atakaye fungisha,hata siku ya harusi ukiweka pingamizi lenye mashiko,kati ya mmoja wapo alikupotezea muda akakuaminisha kukuoa na una vielelezo,ndoa aifungwi mpaka usuluhishi ufanyike uridhie_* Je binti alifanya lolote? Kama hakuna maanake BINTI ALIBARIKI NDOA YA EX WAKE.
5⃣Lugha hii ya chumbia chumbia, ina tafsiri 2, moja kijana anamatatizo ya kupanga mabinti foleni yaani anawatu zaidi ya mmoja wote amewaahidi kuwaoa *Hilo ni kosa kubwa katika mahusiano na kiroho* (Tafuta google au Facebook somo langu la *_Athari za kuwa na mahusiano ya uchumba zaidi ya mtu mmoja, By Ev Elisha Kazimoto_* Lakini kama kijana anachumbia wanafika mahala hawaelewani,wanaamua kuvunja anachumbia mwingine, shida ikowapi? Walitaka waoane watu wasiopatana? Lakini kuchumbia hata watu 100 siyo shida,shida unapoenda kuchumbia mtu mwingine *_Wakwanza mmeachanaje?_* kwa makubaliano au kihuni umedanganya ukampotezea? Na je ulikuwa ni uchumba au urafiki? Uchumba ni kitu kingine Rasmi,kwa kanisa,rasmi kwa familia zenu nk.
6⃣Kijana analaumiwa sana kwakuwa ni Mtumishi *Swali la msingi, Mtumishi anaishi mbinguni au duniani?* na yeye ni binadamu ila Neema aliyo nayo ndo inamtofautisha na wengine.Lakini Tunategemea mtu mwenye Viwango vya kiutumishi Afanye mambo ya Maana, ya staha maana anauwezo flani mkubwa wa Kimungu kuliko wengine,na anaonekana sana kuliko wengine kwakuwa yuko mbele anatazamwa na watu wote. *_Ila sifa hizo hazimfanyi kutokutana na changamoto_* kwa hiyo asilaumiwe kama Malaika aishiye mbinguni bado anamwili ila tumsaidie alinde Heshima ya Nafasi yake ya utumishi. Lakini pia anaweza kuwa vizuri eneo hili, eneo lingine likawa linanampa Changamoto ndo maana *Tunakamilishana kama viungo katika mwili wa Kristo* Ukimtazama mtumishi kama Alfa na Omega,akija kukoseshwa akakosea ndo mwisho wa wokovu wako. _Still is a humani being he can meet a challenge like other humani being_ Ila Neema yake ni tofauti na yako,usiige utapotea hutoonekana. (Jifunze kwa Miriam na Haruni *Hesabu 12*)Dhambi moja vichapo tofauti.
7⃣Namna ya kumsaidia kijana, *_Atulie na mke wake ameishaoa hatachumbia tena,ampende mke wake kwa bidii, amridhishe mkewe na Mungu aachane na kusikiliza watu huku ameisha oa,sasa atamwacha mkewe aoe yule wa kwanza waridhike? Ajue Huwezi wapendeza,kuwaridhisha watu wote,kila mtu ana mtazamo wake kwa kila tendo na tukio na mawazo,asiishi kwa kelele za watu aishi kwa mapenzi ya Mungu_* kama alimjeruhi ex wake kinyume na taratibu amwombe msamaha ambariki maisha yaende halafu aimarishe mahusiano yake na Mungu.
_Binadamu wote mara nyingi wanapenda ufuate wanacho kiamini wao, siyo unachojiamini vyovyote vile ufuate sasa kumbuka katika kundi la watu 50 kila watu 10 wana mawazo tofauti na kundi lingine,utafuata yupi.... Katika mskunfi 5 kila kundi linataka uamini na ufuate wanachokiamini? Hapo ndo tunashauri Sikiliza nafsi yako ina kupa Kuona nini na Mungu wako anasemaje, Achana na lugha za sauti ya wengi sauti ya Mungu...(Eliya na manabii wa Baali 450 Mungu alijibu yupi? Jua jambo moja huto waridhisha watu mpaka unaingia kaburini_
*_Ulikuwa nami mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
Saturday, 25 August 2018
KUCHUMBIA NA KUACHA KOSA LI WAPI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment