💢💢 *CHAGUO LA KWANZA NI LA WENYE SIFA ZOTE,CHAGUO LA PILI NI KWA BAADHI YA VIGEZO - USICHEZEE UJANA*💢💢
_By Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto_
WhatsApp 0755444078
Call 0657557570
Facebook Elisha Kazimoto
.........................................
*_Shalom karibu katika Meza ya Uchambuzi wa Kisaikolojia katika Mahusiano na Ndoa, na mchambuzi Ev Elisha Kazimoto_* Ambapo leo naangazia Changamoto ya Kisaikolojia inayo sumbua mahusiano na ndoa baadhi za watu zimeyumba. Ili kuwasaidia vijana wa aina mbili wajipange vizuri Kisaikolojia......
1⃣Kwa vijana wote ambao bado wao ni vijana haswa kwa maana ya kwamba hawajakutana na changamoto ya *_Kuzaa mtoto/watoto kabla ya ndoa_* bado ni vijana na bado ni Bikira hao ndio nawaita *Chaguo la Kwanza*(First Selection/First Priority ) Naomba ufuatane nami hatua kwa hatua waweza ukapata *Ukakasi wa kunielewa mwanzoni* kwakuwa wewe ni Muhanga wa Daraja hili(Haumo) hapa nazungumzia mambo ya Kisaikolojia na Kanuni za Kisaikolojia ili kukusaidia wewe uliyemo kwenye Daraja hili au ambaye Haumo kwenye Daraja hili, *_Ili ujue namna ya kuendesha maisha yako usije jipa stress na baadaye ukafanya maamuzi mabaya ya kukugharimu_* Lakini usije ishi maisha flani kama mwenye sifa zote kumbe hauna,au ukaishi maisha kama asiye na sifa zote kumbe unazo, hapa mimi nakupa Experiences za Kisaikolojia.
2⃣Vijana ambao kwa *Bahati mbaya* wao wamejikuta wanaishi maisha ya Uzazi lakini bado ni vijana kwa maana kwamba *Hawako kwenye ndoa* wanahitaji bado kupata wenzi wao,ila changamoto ni *_Kwanza anamtoto/watoto amezaa kabla kuoa au kuolewa_* amepoteza ubikira wa kike au wa kiume katika maisha ya *Duniani* kabla ya kuokoka, na wengine ndani ya wokovu lakini *_Amemrudia Mungu na anampenda Mungu kweli_* lakini anakutana na changamoto kubwa za kupata mtu anaye mpenda jinsi alivyo baada ya kupoteza sifa kadhaa( _Nitegee sikio, siyo muda wa kujilaumu,Inuka uwe hodari na moyo wa ushujaa Bado liko Tumaini kwa Bwana_) Imarisha Saikolojia yako umgojee Mungu mme wako/mmke wako yupo.
*_Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto_* naendelea kukufunulia siri za kisaikolojia namna uwezavyo kuishi na ukafanikiwa kupata mwenza wako.
🌡Kwanza kijana inabidi ujue kuwa kila mtu( mwanadamu) *_Anapenda Upekee na Usiri(Uniqueness & Privacy ) hiyo ni kanuni ya kisaikolojia na mara nyingi hata asiye na sifa hizo mbili upekee na usiri utafuta watu wenye sifa ya upekee na usiri. kuamua kuzipotezea sifa hizo siyo Nia ya moyo Ni Mazingira yamelazimisha_* ila nafsi yake ilitaka sifa hizo.
🌡Kwa maana hiyo kijana jua *Chaguo la kwanza* la kijana au binti moyoni mwake ni _Apate Kijana au Binti aliyejitunza, ambaye niyeye kama yeye hana majukumu nyuma yake ya kiuzazi,au anauzoefu wa miili ya watu tofauti tofauti_ *Swali ni kwa nini wana taka hao na wana sita kwa waliopoteza sifa hiyo ya usiri na upekee?* Ni kwasababu ya hofu yakuweza Kumiliki mahusiano ya Ndoa kwa mtu ambaye ameisha tangulia mbele yake(kimajukumu na kisaikolojia), uwezo wa kukidhi mahitaji ya kihisia kama au zaidi ya walio mtangulia mbele yake (kuujua na kuutumia mwili wako)kama atakuwa chini ya viwango je itakuwaje, au akiwa juu ya viwango itakuwaje, Hofu ya Kulinganishwa(Worry of Comparison)kati yake na alopita, Uwezo wa kudhibiti mawasiliano,mahusiano kati ya mwenza wake na Mzazi mwenza wa mwenzake( Ex-B/G) wa mwenza wake aliyefanikiwa kuujua mwili si mara moja wala mara mbili wa mwenza wake, haya ni maswali ya Kisaikolojia,wewe unaweza usiyawaze sasa kwakuwa bado hujaingia katika Ligi la Utafutaji au Utafutwaji na kuona milango inagoma kufunguka,ila *_Nakushauri kama mwanasaikolojia, Kijana kama bado Huja Zaa/Kuwa na mahusiano ya Kimapenzi_* usijaribu kabisa Linda sifa zako za chaguo la kwanza( *_Utakuwa na Nafasi na Uwanja mpana wa Kuchagua au Kuchaguliwa_*)
👉Unapaswa kujua jambo la msingi katika Saikolojia za watu wanatofautiana mtu na mtu,Unavyo tazama sivyo mwingine anavyotazama, _Ukidhani unavyoona ndivyo wote wanaona waweza walaumu watu wengi kumbe ni mtazamo wako tu_ ila unapaswa kujua kuna *Variation of Perceptions* Kuna vijana ambao kwenye maisha wako Tayari wakae hata miaka 45 bila kuoa ila *Asioe mtu Mwenye Mtoto Nje* hivyo hivyo na wadada kuna ambao walishajiapiza *Heri achelewe kuolewa au asiolewe kuliko kulea mtoto wa mwanamke mwenzake* hawa wote ni vijana wenye haki zao za kisaikolojia kuwaza hivyo na kusimamia maamuzi yao ( *Hapa Tunaondoa mambo ya Mapenzi ya Mungu*) Saikolojia ni Saikolojia na Mapenzi ya Mungu ni ya Mungu lakini ni muhimu kujua kuwa Kuvuruga Kanuni moja wapo ya Kisaikolojia inaweza kuvuruga pia Mapenzi ya Mungu(Kwa sababu Saikolojia haipingani na Mapenzi ya Mungu)
👉Kwa maana hiyo Kuna namna ya Kuishi Kisaikolojia kama *Huja Poteza Sifa zako za Kimwili,kiujana na Kuna namna ya Kuishi kama Umepoteza sifa moja wapo ya Ujana* Huu ni ushauri wa Kisaikolojia utakusaidia.
👉Ukiwa mwenye sifa zote za ujana jua *Upo kwenye Mioyo ya Watu wote wenye Listi ya Chaguo la kwanza la watu wanao pendwa kama chaguo la kwanza hivyo punguza Stress za nimechelewa,na ondoa Nyodo za Chambua chambua sana Be Smart and Focused* ila kama umepoteza sifa moja wapo utakuwa kwenye Listi ya Chaguo la Pili la *Kama nikikosa wooote,na nisione njia basi Hata wa sifa hii naweza mchukua* Vijana kuwa Makini, mengine si Mapepo,wala Roho za Kukataliwa ila Sifa(Qualifications)zimepungua ndo zinaongeza changamoto ya kukataliwa
🌡 *Kwako kijana ambaye ni Kijana ila ni Mzazi au umepoteza Heshima ya mwili wako* Kwanza jikubali,usijione asiye faa ili ujenge Ujasiri wa Kisaikolojia ila ukweli unabaki palepale kuwa Sifa moja,mbili au tatu Umepoteza ila haujapoteza Maisha umepoteza nafasi ya Kwanza ila bado ipo ya pili,( *_Tafuta somo langu la Uzaliwa wa kwanza kwenye Google, by Ev Elisha Kazimoto_*) na bado Unauwezo wa Kufanya vizuri sana katika nafasi ya pili ukawashangaza watu hata wa nafasi ya kwanza.
👉Pili hakikisha Unampenda Mungu sana, sana yaani miongoni mwa watu wanao upendeza moyo wa Mungu nawe uwe miongoni mwao kwa kujiachilia kwa Bwana ili *_Akuvike Vazi la Heshima_* katika nafasi yako hiyo ya Pili uonekane *Unafaa* hapa ndo watu wanapoteza mwelekeo, *_Sifa za Kimwili Hana na Sifa za Kiroho hana_* unategemea muujiza gani? Muujiza ni wewe kuvaa sifa za Kiroho ili pamoja na mapungufu yako uonekane bado wee ni dhahabu yaani watu waone kwa sifa zako *_Pamoja na kuwa upo changuo la pili ila unafaa kuliko walio daraja la chaguo la kwanza_* sasa hapo unahitaji kufanya kazi ya ziada na inawezekana kwa kanuni za Kimungu tu,siyo kusoma sana,kumiliki pesa na vitu ndo utamshawishi mtu wa kuwa nawe kama mke au mme, No, kama siyo sifa za Kimwili basi sifa za kiroho.
🔭 *Vitu vinavyo tizamwa kwa Darubini*🔭
♦Nidhamu ya mahusiano kati yako na watu wa jinsia nyingine. _Kuwa makini unavyo husiana na watu wengine,kuwa na nidhamu,adabu na heshima_ na hasa ukiwa na watu wa upande wa pili wa jinsia yako kuwa makini sana, usije ukajirahisisha ukaruhusu kuchezewa mwili wako kwa namna yoyote kwa sex,au sexual plays( *Wakati unakovu la sifa*) eti kwa kisa una mlinda asije akakuacha hapo ndo utakuwa unazidi kupunguza CV yako na kuonyesha makosa yako ya Awali hayakuwa ya bahati mbaya ilikuwa ni Tabia yako.
♦ *Kauli zako* Hapa ni seme na vijana wa kike,kuwa makini na kauli zako unapo kuwa unatafutwa kuingizwa kwenye safari ya mahusiano, kauli za Dharau,Kibabe, kuchagua sana zinaweza kukugharimu pale *_Aidha umri ukianza kupanda sana,au umeisha poteza sifa moja wapo,umeingia daraja la pili_* utakuta umejizalishia jaribu la kusubiri sana watu ambao wengi wanataarifa Hasi juu yako.( *_Uwe Daraja la Kwanza,au la Pili Chunga Kauli zako kwa jinsia nyingine isiyo yako_*)waweza poteza nafasi mara 2.
♦ *Tabia yako* Tabia ni matendo yako ya kila siku,huwa yana nguvu ya kushawishi watu kukubalika au kutokubalika(Personality yako). _Hapa kuna tabia za Kiroho na za Kimwili_ wapo wanaopendelea tabisa za kiroho kuliko za kimwili na wengine za kimwili kuliko za kiroho sasa mjanja wa Kisakkolijoa *_Anajitahidi Kumiliki zote za Kiroho na za Kimwili_* asionekane ana pwaya eneo.
♦ *Namna ya Kuwasilisha Maisha yako ya Nyuma* hapa kuna changamoto kubwa, Nimekwambia kila anaye kuja kwako awe ni kijana wa kike au wa kiume, Kisaikolojia hataki kusikia Historia yenye Hitirafu, anataka asikie ulivyo pambana na kushinda, sasa kama ulishindwa unafanyaje?
👉Wapo ambao ufanya kosa la kuficha hali halisi ya maisha yao ya nyuma,wakiogopa kukataliwa, *_Ndugu wee unatengeneza bomu moja hatari kwa ndoa yako_* lisilo poa wala pozwa na mtu yeyote pale ukweli utakapo julikana wa uhalisia wa maisha yako na tayari safari imeisha enda mbali katika mahusiano au mmeishaoana.
👉Saikolojia ya mwanadamu inahitaji ijijenge katika kweli kama kuna mapungufu iji *Adjust* (ijisogeze)mpaka ikubaliane na matokeo hapo amani inakuwepo,ila ikiaminishwa kisicho unazalisha *Intra conflict and enter conflict*(Vita,ugomvi wa ndani kwa ndani Nafsini Mgogoro wa mtu na mtu)usio isha hapo No Adjustments.
👉Na kuna ambao Uwa wawazi sana bila kupima Mazingira nao ujikuta wanabeba sifa mbaya kila mtu anawaona hawafai. ( *Ndo maana nikasema namna ya kuwasilisha Maisha yako ya awali kwa mwenza wako ndo changamoto*) unahitaji kutumia saikolojia kubwa kujua saikolojia ya mwenzako ndo ujue namna ya kuwasilisha maisha yako ya nyuma.
1⃣Hakikisha Haujidharau kama asiye faa baada ya kupoteza sifa,onyesha uwezo wako wa upya wako wa sasa na uwezo wako kwa mwenzako na unavyo chukia kosa la awali.
2⃣Usipende kuongelea ma ex, ex zako sana na huyo mtu anayeanza kuonyesha kama anakuhitaji hata kama walikujeruhi sana au walikupa raha sana. Ongelea sana maisha ya wapendanao sasa(upendo wenu) na namna ya ku care,ku love na kulinda mwenzako ulo mpata.
3⃣Usipende kujieleza in and out kabla ya kujua mtazamo wa mtu huyo juu ya *watu wenye sifa kama zako* anawachukuliaje...Unaweza jikuta unapoteza muda naye kumbe hana mpango na watu kama wewe tumia mifano aidha ya kutunga ukiwazungumzia watu wenye sifa kama zako walivyopata shida kwenye mahusiano, na wewe onyesha kama vile watu hao unawakubari nusu na nusu huwa kubari na muulize angekuwa yeye,au yeye watu wa aina hiyo anawachukuliaje?, zoezi hilo liwe endelevu kabla ya kutoa siri ya Asili yako.
4⃣Jiridhishe kama ni miongoni mwa watu wanaofaa kuwa nao,anasifa ulizokuwa unatamani.
5⃣Mwonyeshe wasiwasi wa kumkubalia,lakini kuwa Caring person kwake,chunguza kama amezamilia kukupenda kwa ndoa au kwa sex.
6⃣Muulize kama anauwezo wa kulea mtoto asiye wake kama wake,wakati baba au mama yake yupo, na Kwa nini amlee au asimlee. Zoezi hilo liwe miongoni mwa maswali yakujirudia rudia si kila siku ila baada ya muda flani.
7⃣Utakaye jiridhisha amekupenda pia,mwambie Mistake yako ya kimaisha uloifanya lakini unaichukia isimtokee mtu yeyote wa karibu nawe,lakini onyesha jinsi ilivyo kuchonga na kukufundisha na kukupa kuwa bora zaidi ya awali.
*_Ukianza mahusiano onyesha uwezo wako wa kupenda na kupendwa na kujali sana,mahusino yanahitaji Akili kubwa sana kuliko Nguvu_* haya yote ni mambo ya kisaikolojia usipo kuwa nayo makini waweza subiri sana bila majibu.Lakini kuna wengine wanadharau na kuchezea maisha ya ujana sana kwa mlo mmoja( *Tafuta kwenye google somo langu ka Usichee Mwili wako Tena by Ev Elisha Kazimoto*)utaona mambo niloweka bayana.
_Niishie hapo ulikuwa nami mchambuzi wa Masuaka ya Mahusiano na Ndoa, Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
Wednesday, 22 August 2018
CHAGUO LA KWANZA NA CHAGUO LA PILI KATIKA KUOA NA KUOLEWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment