Thursday, 9 August 2018

SEMINA SEHEMU YA 11(ZINAA)

🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
   By Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp  0755444078)
......................................
_Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu_
     *SEHEMU YA 11*
*Tambua Nguvu Kuu 3 Zinazo Pambana na Huduma yako*
..........
..........
..........
_Yesu Kristo Bwana wetu apewe sifa tangu sasa na milele Amina,nikukaribishe mtumishi wa Kristo katika sehemu yetu ya 11,na katika kuitazama Silaha ya 3 iliyo hatari sana kuliko zote inayosukumwa kwenye huduma ikiwa ni ya mwisho ili kusambaratisha huduma kabisa na kukuacha ukiwa Mkame Jangwani. Lakini kwakuwa Bwana ametufunulia siri hizi hatuta sambaratishwa bali tutamsambaratisha adui mwenyewe na silaha zake_  KARIBU.
💣3⃣ *Silaha ya 3 ni Zinaa(Uzinzi na Uasherati)*⚰⚰
👉 Miongoni mwa Silaha inayotesa Huduma nyingi,( *Madhabahu nyingi*) ni Zinaa. Zinaa imekuwa biashara ya shetani makanisani, siyo waumini,siyo waimbaji,wainjilisti,wachungaji mitume na manabii Zinaa inawaka moto katika nyakati hizi.
👉Huduma nyingi zimefutika,zimepoteza mwelekeo,kibali na uwepo wa Kimungu mara baada ya mbeba huduma *Kunaswa na Zinaa* kila jambo linaanza kuporomoka kwenye huduma (maombi yanazima,kusoma neno kuna zima,maisha ya utakatifu yanazima)na hayo ndiyo malengo makuu ya Ibirisi.
👉Silaha hii ya zinaa *Inatumiwa sana na shetani* kama silaha ya mwisho endapo Mtumishi wa Mungu ameshinda silaha mbili za mwanzo( *Kiburi na tamaa ya mali na pesa*) au amenaswa katika hizo silaha za mwanzo basi zinaa inaletwa kama Kifuniko cha Kukamilisha usajili na Umiliki halali wa ufalme wa kuzimu. ( _Zinaa inakuwa chapa maalumu ya utambulisho wa kumilikiwa na ufalme wa kuzimu,ukitaka kujua  Zinaa kwenye huduma ni Muhuri wa kuhamisha umiliki wa Kimungu kwako na kumilikiwa na kuzimu, kawaulize Watumishi wote Fake( *Fake pastors,fake Prophets,fake Apostles, fake Singers etc*) wanaoenda kuzimu kutafuta Upako,mvuto,utajiri miongoni mwa masharti yao ya kuimalisha Upako wao Sharti wafanye ZINAA SANA aidha na waumini wao,waumini wenzao, ndugu zao,watoto wao na viumbe vya ajabu kuzimu(majini maalumu) nk_ ) hii ni Silaha iliyo na Muhuri wa Moto wa Madhabahu ya shetani,ni nguvu ya YEZEBELI mama wa Makahaba.
👉Kwa nini silaha hii ni hatari kuliko zote na huwa inajaribiwa ikiwa ya mwisho aidha umeshinda au umeshindwa na silaha 2 za mwanzo? Ni kwa sababu silaha hii inapotumwa kwa mtumishi yeyote katika huduma inakuja ikiwa na Nguvu na Kazi kuu 3.
💪 *_1.Kuondoa ujasiri na Nguvu ya Kukemea dhambi katika maisha yako yote ya utumishi_* Fatilia kwa makini huduma nyingi hautakuja kusikia Madhabau siyo leo au kesho ikiikemea dhambi wala kusimamia misingi ya Utakatifu kwa watu(mafundisho ya Utakatifu). Kwa nini? Zinaa ikiingia katika Nafsi ya mtu, *Inazalisha Hatia katika Nafsi,na kuondoa ujasiri wa Kweli* nguvu ya kuusemea utakatifu ipasavyo inapotea,kukemea dhambi na hasa ya zinaa inapotea ndipo mtu ujielekeza katika jumbe nyepesi za mlengo mmoja wa kuwafurahisha watu tu.
👉Ikumbukwe Injili ya Yesu Kristo mwanzo wake inaanza na *Tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia* yaani ile Kiki,starter tu ya Yesu inaanza na Toba(ndo kusudi kubwa la Injili ya Yesu) MATHAYO 4:17,yaani Injili ya Yesu Kristo ukiondoa Toba haibaki kuwa Injili tena inabaki kuwa Taarifa zifurahishazo(kama uponyaji,miujiza nk) siyo lengo kuu la Injili japo ni sehemu ya Injili.
💪 *_2.Kazi ya 2 ni Kuondoa Hali ya Kujiamini Mbele za Mungu_* Ujasiri mbele za Mungu katika huduma ndo upelekea huduma yoyote kutimiza kusudi la Mungu. Lakini dhambi ya zinaa ikiingia kwenye huduma ya mtu,tayari anapoteza hali ya kujiamini,anakuwa mtu wa mashaka,anafanya mambo kwa kujikakamua ila siyo kwa mwongozo na nguvu ya Roho mtakatifu.
👉Na huduma nyingi za watu *_Hazina mafuta ya Roho mtakatifu,ni Kavu_* wengi wao ukiwafatilia wameisha mezwa na nguvu ya zinaa, *Hata ujikaze Vipi Mambo hayaendi* ndo maana utaona kama ni waimbaji _Wamejikita kutunga nyimbo nyepesi sanaaa zenye mlengo wa kufurahisha watu,wanasikiliza watu wanapenda nini sasa ndo wanaimba, siyo Roho wa Bwana anapenda nini sasa kuwahudumia watu wake, mpaka imefikia wengi wao kubadiri tu maneno ya mziki wa msanii wa bongo fleva na kuweka tumaneno twa Yesu, anaweza, nakupenda ila biti, maadhi yote ni wimbo wa msanii flani_) *Utapataje mafunuo ya wimbo wa kuimba verses,wakati umetoka Kuzini na Producer wako,umetoka kutoa mimba,utaingiake kwenye maombi wakati mwalimu wako wa kwaya ni kama mme wako,au mke wako, kwaya zimekuwa shida humo humo wanakulana,pigana mimba,utukufu wa Mungu utatoka wapi? Inabidi mjikite kwenye kutafuta step za sarakasi watu wacheke na kufurahi ila hakuna ujumbe wowote* mara chache sasa wagonjwa kupona na mapepo kuondoka kipindi wanaimba waimbaji kwaya au PRAISE TEAM( Praise team hivi madhabahu mbona imeguzwa Guest house yenu) mpaka sasa uwepo wa Mungu kwenye ibada ni adimu kuupata zinaa imekuwa zinaa na nado nakuja kushika Mic na kutupigia vyombo tumwabudu Mungu(OMG) mbona hii ni aibu? Uanona watu hawazami unalalamika,kwani unataka tuzame na wewe kwenye zinaa,wewe umejazwa na roho ya zinaa sisi tumejazwa na Roho Mtakatifu wapi na wapi utatuzamishaje?(MUOKOKE UPYA)
👉Ndo maana nyakati hizi tunaabudu na mapepo mwanzo mwisho January to December mpaka *Aje mgeni kufaya semina au mkutano ndo mapepo yanalipuka mpaka kwa Wana kwaya,wana Praise team pepo zinawaangusha*) hii ni hatari, na mapepo yakiripuka makanisani watu wote wanayakimbia anabaki pastor tu wengine wanajifanya wako busy na mambo mengine au wanawahi nyumbani kumbe *wanajijua njia zao ni fake wanaweza kuumbuliwa na mapepo* Ewe Muhudumu wa Madhabahu Tubu na Umrudie Bwana atakusamehe na uanze upya.
👉Ndugu zangu Mitume na Manabii huduma yenu ni nzuri sana na watu wengii wanaitamani na kuikimbilia ila *_Huduma Nyingi zimejaa Tope la Zinaa_* kila anaye kuja kufanyiwa Deliverance hatoki ofisini bila kuvuliwa nguo 👙👙wake za watu hawaponi, *Mafuta ya Upako siku hizi yanapakwa sehemu za Siri*❗❗⁉🤔🤔Mnatupeleka wapi,tunafungua watu kwa *Romance* ma waumini mpo mmekaa mnashangilia Haujui madhabahu yako ulipo ipo chini ya uongozi wa YEZEBELI( *Zinaa*)⁉ Na kwakuwa watu wamewaamini,wanashida lolote unalomwambia anakubali Maskini ya Mungu. Wachache wenye ufahamu ndo Utimua mbio na kuwagomea kufanya Ngono ila wengi wao mmewaharibu,wengine wadada bado mabikira,na kuzimu wamewaagiza mlale na mabikira mnaharibu watu wa Mungu.( *Hamtasalimika, Jehanamu inawangoja*) Uzuri si kwamba hamfahamu mnalofanya mnajua kabisa, Polee ni kwa Waumini wenu wanaoona mnafanya maajabu na miujiza wanashangilia na kuwaita BABA na kuwa pigia magoti,kuwasujudia kama Mungu kumbe mashetani waharibifu walovaa ngozi ya malaka. Ikumbe tiyari mmewaunganisha kwenye madhabahu ya kuzimu ni ole kwao maana hamuwapeleki popote wanaishia motoni.
👉Wewe mwanini hushtuki,unahisi Kuzini na Nabii au mtume au mchungani inakufanya kuondolewa dhambi nakuwa Special? Huyo hana mbingu ya kukupeleka adhabu yako iko pale pale. *Dada,mama kijana baba KIMBIA TOKA KWENYE KANISA HILO* Upo kuzimu kwenye madhabahu ya shetani na muda wowote waweza tolewa kafara.
💪 *_3.Kazi ya 3 ya Zinaa ni Kuharibu maono yako yote yaliyo mbele yako_* kuna watu wengi wakianza huduma wanakuwa na maono makubwa Mungu anawasemesha na anatia ndani yao ya kuelekea sehemu flani,ila Waki naswa na Zinaa kila kitu kinapanguliwa wanabaki kwenda wakiwa Vipofu. *Zinaa ina futa Maono yako huwezi kuyatimiza* labda ufanye njia mbadala ya kujiungaisha na kuzimu utumikie upande wa pili wa shilingi(ufalme wa shetani)Kwa kulijua hilo ndo maana Biblia ikasema IKIMBIE ZINAA(1WAKORINTHO 6:18-19)
👉Mbeba maono mmoja anaitwa YUSUFU(Mwanzo 39:6-12,21-23) anaonyesha msimamo wa kuukataa ubaya(zinaa)ili alinde maono yake.
👉Wewe unayeingia kwenye Huduma hakikisha unaipinga zinaa kwa nguvu zote ili ubaki katika maono yako sahii ya Kimungu.
👉Nilitoa angalizo mapema watu wengine wanadanganyika kwa kuona mtumishi yule mbona ana upako kama atakuwa ni fake? Upo upako wa kishetani na upako wa Kimungu( Biblia imetuambia  Tutawatambua kwa matunda yao)watajitahidi kuigiza mambo yoote ya Mungu lakini sharti wachepuke watimize Matakwa ya Ufalme wa kuzimu. Lazima tutaona tu mambo yanayo pingana na Neno la Mungu ndo hayo wanayafaya kwenye huduma zao mara moja moja au muda wote.
👉 *_Mimi leo niishie hapa niseme neno moja,Anashambulia kwa Awamu na kwa Plan,lengo kuu Usitimize Ndoto zako na malengo ya Kuujenga Ufalme wa Mungu,kwa namna yoyote atatumia silaha zote aidha akufute katika Tasnia ya hutumishi uitwe mpagani,au Utumike chini ya Madhabahu ya shetani na uovu uikose mbingu na utumike kuwapoteza wengi.Hii ni hatari ombi langu kwako ni kwamba jipange kumshinda shetani na silaha zake zote kwakuwa Aliyeko ndani yetu na tunaye mtumikia ni mkuu ana nguvu kuliko huyo anaye tuwinda. ZABURI 147:5_* USIKOSE SEHEMU YA 12 YA NAMNA YA KULINDA HUDUMA YAKO IKAE NA KIBALI MBELE ZA MUNGU NA MBELE ZA WANADAMU.
_Ulikuwa nami katika uchambuzi wa somo hili la Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu Ev Elisha Kazimoto( *Mjumbe Mkali Mithali 17:11*)_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
Call 0657557570
_Kwa ushauri na maombezi_
@Pia google andika MATERIAL ADIMU utapata masomo mengi ya kukusaidia,tafuta somo la IPO GHARAMA YA KULIPA BAADA YA DHAMBI YA ZINAA. Utaichukia na kuikimbia.
      *Mungu akubariki*

No comments:

Post a Comment