🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
_By Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)_
......................................
*_Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu_*
*SEHEMU YA 7*
*Sifa 7 za Mtumishi wa Kweli wa Yesu Kristo*
.....
.....
.....
_Shalom mwana wa Mungu na mtumishi wa Mungu unaye hudumu na unaye jiandaa kuhudumu Madhabahuni pa Bwana,nikukaribishe sasa katika sehemu ya 7 ya Sifa unazo takiwa kuwa nazo kama mtumishi wa Mungu unaye taka kumtumikia Mungu aliye hai_.
🎤Jambo la msingi katika utumishi ni kujua kuwa mahala popote iwe ni ofisini,serikalini na maeneo mengi wanahitaji watu wenye sifa husika sawa sawa na matakwa ya eneo hilo na hata katika Madhabahu ya Bwana wanahitajika watu wenye sifa maalumu.
🎤 Sasa kama wanadamu wanahitaji sifa flani ndo wamwajili mtu Je,Mungu si zaidi? Hapo jua Mungu ni zaidi,ndo maana Bwana akanifunulia hizi sifa za mtumishi wa Kweli,wale feki wanapishana na sifa hizo.( je,Mungu si zaidi)?
*_"Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?"_*
(Mathayo 7: 11)
🎤Kwanini kutaka watu wenye sifa maalumu, *_ni ili kulinda heshima na sifa ya ofisi,lakini kutimiza lengo lililo kusudiwa,lakini kuepusha hasara katika ofisi_* kwa sababu hiyo tuangalie sifa hizo:
🎤 1⃣ *Ni mtoaji* Sifa ya kwanza na muhimu kwa mtumishi wa Kristo ni mwenye tabia ya Kimungu ambayo ni *Utoaji*. Utoaji ni sifa ya Mungu iliyo kuu,na wote wanaoingia katika utumishi lazima kwanza waipokee sifa hiyo.
🎤Kwakadri ya unavyo toa ndivyo unavyopokea. Ukiwa mbahili katika mambo ya Mungu ndivyo unavyokosa kupokea vitu muhimu vya Kimungu katika huduma yako.
*_"Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu."_*
(2 Wakorintho 9:6 )
🎤Chochote unacho kitoa kwenye maisha yako kwaajili ya Bwana ndivyo unavyopokea mambo ya Kimungu,na ukipanda ubahili utavuna ubahili katika huduma yako.
(Wagalatia 6 )
------------
7Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
8Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
9Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.(Mathayo 25:24,Luka 6:38,Methali 11:24,19:17)
🎤 2⃣ *Ni mwenye kujizuia na Kunena*, hapa naomba uwe makini mtumishi wa Mungu,hii ni *_Sifa ya kulinda upako/uwepo wa Mungu juu yako_* hapa ni kiwango cha kupokea siri za Kimungu na kuzihifadhi kwaajili ya kazi uliyopewa.
*_"Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu."_*
(Yakobo 3:2 )
🎤Jifunze kwa manabii katika enzi za agano la kale,ni watu waliojitenga na watu ili kuruhu utulivu na mazingira ya Mungu kusema nao na kusikia sauti yake.
*_"Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku, Umenihakikisha usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,"_*
(Zaburi 17:3 )
🎤👆Unahitaji kutembea na Mumgu linda kinywa chako kisikose.
🎤Kuongea ongea ovyo,kunakufanya kupoteza mazingira ya umakini wako katika huduma,kunaleta kuzoeleka,kudharauliwa yale unenayo na kujaza makosa mengi katika huduma yako yatakayo kupunguzia nguvu ya kutumika.
*_"Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili."_*
(Methali 10:19 )
🎤3⃣ *Mwenye Imani Thabiti*, Imani ni sifa ya mtumiahi wa Kweli wa Yesu Kristo. Kazi ya madhabahuni inahitaji kumwamini Mungu nje ya unachokiona. Ukitaka kutembea kwenye huduma kwa kutegemea unachokiona huwezi enda mbali.
*_"(Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)"_*
(2 Wakorintho 5:7)
🎤Watumishi waliotumiwa na Mungu kwa viwango vikubwa ni wale waliokuwa na imani ya kumsikiliza Mungu na kumwamini kwa kile alichosema,bila kuona kile wanachobiwa kitatokea.
(Waebrania 11 )
------------
8Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.
9Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
10Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.
🎤Kwa imani utafanya mambo makubwa katika huduma yako,na itakua kwa viwango vimubwa,nje ya imani huduma yako itakuwa ya kawaida mno na dhaifu.
🎤4⃣ *Mwenye Ushirika (Umoja)katika mwili wa Kristo*, Kuma tatizo kubwa sana kwa utumishi wa sasa ambapo *$kila mtumishi anahitaji apambane yeye kama yeye,ajulikane yeye, ainuliwe yeye,afaidike yeye* ndiyo maana utakuta kila mmoja amejifungia kwenye kakanisa kake hana ushirika na wengine watiane moyo katika kazi hii ya Mungu, badala yake shetani amewageuzia kibao *_Amewafanya watumishi kupigana wao kwa wao,kudharauliana,kugombana na kuchafuana_* kusudi la kuwaua na kuua huduma za kiroho.
🎤Yesu akiagiza umoja,umahitaji kukua kiroho kihuduma *shikamana na watu wengine* wenye wito mmoja na wako, *penda challenge kutoka kwao,jifunze kutoka kwao* huduma yako itakuwa na kuwa na nguvu sana.
(Yohane 17 )
------------
9Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;
10na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.
11Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
🎤Yaani *Laiti watumishi walioko madhabahuni tayari na wale mlio na shahuku ya kuingia madhabahuni wangegundua kauli ya Yesu hii basi huduma zingekuwa kubwa na kuleta mapinduzi makubwa kwenye ufalme wa giza* kauli ya Yesu ni tuwe wamoja.
*_"Mimi na Baba tu umoja."_*
(Yohane 10: 30)
🎤Kosa la kiufundi la kihuduma wanalofanya watumishi ni kujitenga ili afaidike yeye zaidi,kumbe anaelekea kupoteza mwelekeo wake kutokana na kwenda kinyume na kanuni ya Mungu ya Umoja.
*_"Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe; Hushindana na kila shauri jema."_*
(Methali 18:1 )
*_Kwa leo niishie hapa tutaendelea na shemu ya 8 wakati mwingine, by Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)_*
Thursday, 2 August 2018
SEMINA YA NENO SEHEMU 7
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment