Tuesday, 14 August 2018

KESI YA KUACHANA NA KURUDIANA

🔥🔥🔥🔥Shalom mwalim natumaini ujambo
  Naomba ushauri nilikua nimeoa tukaja tukaachana na mke wangu akidai kachoka kukaa namimi skumpa taraka akaenda kwao baada ya miezi 3  akaolewa mi nilibaki na mtoto akiwa na miaka 4 sasa anamiaka 5 sasa kule aliko olewa kaachika tena anaomba arudiane nami sasa mimi siko tayar kurudiana nae koz atakule aliko olewa alikua ni mke wa pili
mimi sina mapenzi nae tena nisaidien🔥🔥🔥🔥
*_Nionavyo mimi kwa Kesi hii,ila wewe nawe usomaye una namna unaona_*
    Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp  0755444078)
........................................
*Hapa kunahitaji Operation ya Kiroho na Kisaikolojia*
_Nianze na Operation ya Kiroho kwa kumsaidia huyu mwanaume aujue mtazamo wa ndoa Kiroho kama anasema Mkristo,sijui ni Mkristo tu au aliyeokoka, kwa vyovyote maadamu amekuja Wodini ngoja Aingizwe Theatre_
👉Ndoa ni Agano ambalo linahitaji kulindwa kwa namna yoyote lisivunjike,ndiyo maana kabla ya mtu kuingia kwenye ndoa watumishi wa Mungu wa Kiroho wanafundisha na wanasaikolojia tunataadharisha, *_Usiingie kwenye ndoa na mtu kwa kumtamani tu,kwa hisia ambazo uchemka muda mfupi baadaye zinakata,ingia kwenye ndoa na mtu ambaye nafsi,moyo na mwili umemkubali kwa aina yoyote umejitathimini kuwa mpaka uzeeni na kifo sita mwacha_* kwakuwa agano la ndoa lina nguvu kubwa ya kuunganisha mioyo,miili na nafsi na linabeba hatima ya kesho yenu(likivunjwa inabindi livunjwe lisijengwe tena kiholela)
10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;
1 Wakorintho 7:10

11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
1 Wakorintho 7:11

15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
1 Wakorintho 7:15

👆Andiko hapo limesema, Mtu asimwache mwenzake,ila atakayethubutu kuacha,siyo kuachwa,...Ukiacha kama unapenda kukaa katika haki basi hesabu Biashara ya ndoa kwako mwisho kaa single mpaka kaburini, na yule uliyemwacha hapaswi kuoa au kuolewa kwakuwa mwenye agano naye bado yuko hai,hapo ndo Biblia imesema mkikaa mkaona usingo umewashinda RUDIANENI katika angano lenu maisha yaende.
👉Ila alieyondoka aliyeondoka AKIOA AU KUOLEWA(yule aliyeachwa AGANO LAKE LIMEVUNJIKA maana yule ameanzisha agano lingine,katika ulimwengu wa roho hatunaga maagano 2,kuna agano moja,kwahiyo aliyeachwa YUKO HURU KUOA AU KUOLEWA,au aliyeondoka Akifa uko huru kuoa au kuolewa huna aganao na mtu tena.
👉Huyu baba ayakue hayo,asiumize kuchwa,mwanamke alishajichanganya,na alisha vunja agano lake liko kwa mwingine,Temdo la kuolewa ndo alivunja agano la mme wa kwanza,so mume huyu ana haki ya kuoa au kukaa bila kuoa ila SI KURUDIANA NA MKE YULE.
👉Mpaka hapo yule mke wa kwanza hana sifa kiroho za kurudi kwa mme wake wa mwanzo,kwakuwa Alishaolewa( *_Huo ni udhalilishaji,dharau kwa mme wa kwanza_*)mpaka unaolewa inamaana Umefunga mafaili yoote ya mme wa kwanza moyoni mwako na kuyatia moto ili usajiri maifaili mapya,upendo,hisia zoote alishaondoa kwa mme wa kwanza,mpaka unaolewa tayari yule wa kwanza unamuona kama kaka yako,mahaba yanahamia kwa mwingine.
👉Kisaikolojia hana ukweli wowote wa anarudi kwakuwa anampenda mme wa kwanza,ila kwasbabu AMEACHIKA KULE, swali ni angekuta kule Raha mstarehe,ASINGE RUDI. Tendo la kutaka kurudi katika lugha ya Kisaikolojia ni, *_Wewe usiye na malengo nihifadhi,wewe usiye na hisia maalumu nitunze, wewe nahitaji kuoata mahitaji ya kutunzwa ila sina mapenzi na wewe_*)
Kuna lugha nyingi sana za dharau, ambacho baba huyo anapaswa kujua,asidhani mwanamke huyo anampenda kama kipindi wanaoana ajue anahitaji asikae wa kutanga tanga anatafuta hifadhi..
👉Niseme huyo mwanamke ni miongoni mwa wanawake ambao hawakutakiwa kuolewa mpaka wanaingia kabulini maana moja, *_Hawana sifa ya kuitwa wazazi, laiti wasingepewa uzao wakaishi wakiwa TASA,hawafikirii gharama ya mtoto kukosa malezi ya wazazi wote(hasa mama) akiwa mdogo miaka 4,unakuwa umemwathiri kisaikolojia maisha yake yote_* sasa kwanini usihesabu gharama ya mtoto asiye na hatia?unamwadhibu mmeo na mtoto?mwadhibu mmeo tu....4yrs mtoto is too young.
👉Kurudi kwa mmewe wa kwanza si kwamba anakuja kulea watoto ila ndoa anawapandikiza maroho machafu na tabia mbaya wanaweza wasimweshimu hata baba.
👉Lakini mpaka hapo huyu mwanamke ni Sumu, anaweza akaua muda wowote ndani yake anakisasi kujiliza na kurudi ni Lugha za Delila na kwa Samsoni,hakuwa anampenda ila alikuwa anatafuta one day akamilishe mission yake ya Kisasi.
👉Ogopa mtu ambaye umemuoa,akatoka akaolewa,halafu akataka akurudie Huyo kama ni chakula ni kipolo kilicho chacha,kama ni bidhaa badi tayari Expired date yake inamiaka mingi ndo zile bidhaa za kuchomwa hata kama zinaonekana mpya.
NB:ASINGEOLEWA BAADA YA KUACHIKA,TUNGEMWEKA MIONGONI MWA WANAWAKE WENYE BUSARA NA WANAOHITAJI KUHURUMIWA NA KUSAMEHEWA YAANI HAPA NINGEKUWA NATOA KAULI ZA KISAIKOLOJIA NA KIROHO ZA KURUDIANA KWA NAMNA YOYOTE.
Ila kwa huyu ndugu......  PIGA CHINI,MUWE MLIFUNGA NDOA KANISANI,MAHAKAMANI,MKEKA,MLIOKOTANA MWAMBIE MIMI SIYO mnyama (mbwa)alotolea mfano bible KURUDIA MATAPISHI..... Abaki ni mzazi mwenzako wa mbali,anq haki kuwaona watoto,watoto kumtembelea,kuwahudumia ila HANA HAKI YA KUWA MKE.
*_Ukipata ndoa,jua kuna watu wanaililia ndoa miaka inaenda, hawana wa kuwashika mkononi,bado wanavumilia,wanaadamu na wanaapa wakija kuolewa au kuoa watawapenda wenzao na kuwa tunza,wewe unapata ndoa, changamoto ndogo unamuona mwenzako hafai na unaamua kulianzisha,ukisha poteza ndo utajua thamani yake pamoja na usumbufu wake_*
👉Hii tabia si nzuri mpaka kwa walioko kwenye uchumba, yaani mtu anamnyanyasa mwenzake,anamuendesha,anatesa hisia zake mpaka mtu najuta kukupenda,kukupa moyo,kuingia kwenye mahusiano nawe.
👉Mtu akisha fanya maamuzi ya KUKUPIGA CHINI kwakuwa huvumiliki, au unaamua kumuacha mtu kwa ubabe,kwa kejeki,kwa kumuumiza,kwakuwa aidha umepata KIPYA, bado anamoto wa ku care,unaamua kumtupilia mbali mlotoka mbali naye,unamuona WASTE MATERIAL yakikushinda na kule ukaachwa ndo unamuona mtu anarudi kwa uso wa huruma na upole kama kondoo,ila aliondoka kwa uso wa Dubu na Nyati, aloo ogopa watu wa aina hiyo NEVER GIVE HIM/HER ANOTHER CHANCE( hiyo ni kisaikolojia) hakuoni kama una thamani ila wewe umekuwa ZIADA,BASI TU mweda bure si kama mkaa bure. Kwenye ndoa hatuna mahusiano ya aina hiyo.
👉Ndiyo maana huwa tunawashauri wana mahusiano, ku break na kurudiana ni jambo la kawaida ila *_Kuwa makini na breaking yako, tumia busara,tumia lugha nzuri,ondoka kwa amani maana waweza rudi dunia hii inazunguka,usije taka rudi kumbe ukisha pachoma moto utapata aibu_* kwa wana ndoa ukiondoka punguza maneno ya kutafuta haki yako na kumchafua mwenzako,tulia uombe neema ya kurejeana kwa amani.Na usii gie kwa mme au mke mwingine tukia ungoje muujiza wa kurudiana.Lakini hata ukikengeuka ukaoa au olewa LINDA SIFA,NA HESHIMA ya mzazi mwenzio. Huwezi jua siku moja mtakutana wapi na nani atakuwa anahitaji kubwa la kusaidiwa na mwenzake.
............................................
*_Mtu mwovu ataki kusikia Neno ila Kuasi tu,hivyo Mjumbe Mkali Atatumwa Kwake_*
(MITHALI 17:11)My Signature.
*Ev Elisha Kazimoto(WhatsApp 0755444078*)

No comments:

Post a Comment