Friday, 24 August 2018

KUMPATA MME

*KUPATA MME*
( _Anaandika Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto-0755444078_)
👉Suala la ndoa ni jambo jema na ni Ahadi ya Mungu kwa watu wake ni haki yao.
👉Ila ndoa inapingwa sana na ufalme wa giza kwa kuwa ndoa ndiyo ufunguo wa baraka za mtu. Kuna baraka za pekee ambazo ukiwa peke yako hata uwe na upako wa kufufua watu hutazipata kama haujaingia katika ndoa( _Unakumbuka Andiko la Apataye mke apata kitu chema naye Ajipatia Kibali kwa Bwana?_) Kibali kinakuja na baraka( *Ikiwemo baraka ya Uzao, baraka ya kuufurahia mwili wa mwingine kiuhalali*)nk... Uzao ndo unaotoa watumishi wa Mungu,na ndo unaotoa waganga wa kienyeji-watumishi wa shetani.
👉 Kuufurahia mwili wa mwenzako ndo tiba ya Saikolojia ya mwanadamu(stress nk) ndo enjoyment ya mwisho ya mwanadamu hapa duniani.
👉Kucheleweshwa kuingia katika ndoa, anachokitafuta shetani kwako dada *_Ni kukuchanganya kisaikolojia,uondoke mbele za Mungu(uachane na kumgoja Mungu)uvamie yoyote asiyetoka kwa Mungu,shetani akupigize tapeli wa kukuumiza maishani ili upoteze baraka,azalishe watu wa kumtumikia_* (Migogoro ya ndua, stress,michepuko na Divorce )kwa hiyo unapoona kucheleweshwa *_Kuingia kwenye ndoa_*, Usichanganyikiwe na kukata tamaa bali jipange vizuri,omba ongeza viwango vya kumpenda Mungu.
👉Kupata mme,hakuhitaji nguvu nyingi za kimwili,bali maarifa ya kiroho na kisaikolojia ili ukae vizuri *Site* kwenye nafasi ya kukutana na mtu wako kutoka kwa Bwana.
👉Muda wa Kuchelewa,ndo muda *_wa kujifunza na kupunguza changamoto zako na kuongeza uwezo kimwili na kiroho wa kumumiliki mume,ni muda wa kuonyesha upendo wako kwa Mungu kuwa uoendo wako kwa Mungu haufungwi na vitu au hali ila Uzuri wa Kristo wa Kukuumba kwa Kusudi lake_* kwa hiyo unahitaji kumwamini Mungu hata katika ukimya wa Mungu usioonyesha Dalili ya matokeo unayo yahitaji.Hiyo ndo Imani Kuu.
( _Haujachelewa kwakuwa we Mbaya,No,kila kitu alichokiumba Mungu alikiona ni Chema,nawe umeumbwa kwa uzuri wako pekee wa kushangaza yupo atakaye ugundua na kuutafuta_)
*Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,*
*Zaburi 139:14*
_Walio chelewa kuolewa wameisha kufa tayari,ila uliye hai bado,unangoja muda wa Kusudi la Mungu kwako kuwa katika ndoa_
Inuka iambie nafsi yako sijacheleweshwa, nimesubirishwa kwa kusudi kubwa la Kimungu nililo libeba.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078.

No comments:

Post a Comment