Wednesday, 29 August 2018

MAHUSIANO NI INTIMACY I

❤❤ *RELATIONSHIP IS ALL ABOUT INTIMACY(MAHUSIANO UJUMLA WAKE NI UKARIBU)*❤❤
     *Sehemu ya I*
     By Ev Elisha Kazimoto
    Whatsapp 0755444078
   Facebook Elisha Kazimoto.
_Shalom wana mahusiano,kwa mara nyingine Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa  Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto,nakuletea Kipengele cha Kisaikolojia kinacho linda Mahusiano na Kuonyesha uhai,harufu nzuri katika mahusiano yoyote,yawe ya kiurafiki,kiuchumba,kindoa hata Kiroho,ukikosa haya umekosa vitu vikubwa mno,waweza jikaza kusafiri katika ulimwengu wa Mahusiano ila utafika umechoka au waweza usifike mwisho wa safari,au ukafika na makovu mengi na majeraha mengi_.
❣Ukweli ni kwamba wana mahusiano wengi,wanaendesha mahusiano yao *_Kiugumu ugumu_* na si kwamba wanafurahia,au hawaoni kuwa kuna mapungufu,ila hawana namna ya kufanya,wengine ni matokeo ya kimfumo,wengine ni matokeo ya Kihistoria,wengine ni matokeo ya Kutopenda kujifunza mambo mapya,wengine ni *Ujuaji wa Kutojua* haya yote yamefanya mahusiano mengi ya wana mahusiano Kuishi kiugumu ugumu( _Hapa si wana wa Giza wala wana wa Nuru_)wote wanapita katika ugumu ugumu.
❣Kisaikolojia, *Mahusiano yanajengwa na Ukaribu* na ndo maana ya mahusiano (Ukaribu/Intimacy )ndo uzaa neno Mahusiano kama hakuna Intimacy/ukaribu Kisaikolojia hakuna Mahusiano ila  kuna *Kushikiriana* Neno KUSHIKIRIANA halina Taste ya Love(maana yake kuna Conditions/Mazingira Hali zinazo wafanya Kuwa wote ila isingekuwa hizo hakuna sababu ya kubaki katika mahusiano hayo).
❣Kisaikolojia kuna mahusiano *Hai*, Mahusiano yaliyo *Poa* mahusiano yaliyo *Kufa* katika aina zote hizi watu wapo wanaoishi katika aina hizi zote, Aidha yaliyo Hai, au uwe kwa yaliyo Poa,au yaliyo Kufa.
❣Raha ya Mahusiano yoyote yawe na Intimacy/Ukaribu, ukaribu ukikosekana ndo unazaa Kupoa,kupoa kunazaa Kufa. *_Marafiki wengi wanaoelekea uchumba au uchumba umeyeyuka na wengine kuishi kwa Stress/Msongo wa Mawazo kwa namna ya mahusiano yalivyo,hawafurahii mahusiano(hamwelewi elewi mwenzake) ila wanaenda kwasababu Anatamani aolewe,au aoe,au kwakuwa ameisha lipa mahari,au kwakuwa amepita mahusiano mengi sasa anaona na haya nayo avunje atakuwa wa nani sasa,au umri umeenda ngoja ajikaze waende hivo hivo ila HANA RAHA NA MAHUSIANO HAYO_*
❣Ndoa nyingi zimebaki zikishikiriwa na WATOTO, KIAPO CHA MADHABAHUNI,KUOGOPA UPWEKE AKIAMUA KUACHANA NA MWENZAKE, BASI TU WOKOVU HAURUHUSU KUACHANA WALA KUCHEPUKA. Hayo ndo yameshikiria ndoa, ila SI INTIMACY/UKARIBU.
❣ *Wana Mahusiano yoyote, Intimacy Ndo inayoshikiria Mahusiano ya uchumba na Ndoa, hata Wokovu wetu unashikiriwa na Intimacy na Mungu wetu* ukipoteza Intimacy umepoteza Raha na Radha ya Mahusiano na Ndoa.
❣❣ *INTIMACY/UKARIBU UNAZAA MAMBO YAFUATAYO*❣❣
1⃣Intimacy inazaa Upendo kati ya wanao husiana kwa mahusaino yoyote. Ukaribu katika Fikra,katika Matendo usipo kuwepo mtakuwa hamna upendo ila mna KIFUNGO(Kinyume cha Upendo ni Kifungo )maana upendo ni Hisia Huru. Sasa kifungo ni Kulazimika Kukaa na huyo kwasababu hakuna namna nyingine(kwa waliookoka)wasiookoka hapo ndo Unapiga chini unatafuta mwingine.
2⃣Intimacy inazaa KUAMINIANA. Ukaribu ndo kunakupa kumjua mwenzako,madhaifu yake na kuyabeba,uwezo wake na kuupa nguvu na Kumwamini. *_Intimacy isipo kuwepo, Hakuna Kuaminiana_* Mahusaino mengi ndoa nyingi WANAISHI BILA KUAMINIANA, Hapo Hakuna pepo,wala uchawi Ni mtu Binafsi Uwezo wake wa Kujenga Ukaribu/Intimacy ni mdogo mno kutokana na Kuishi maisha ya Kimfumo(Kabila,familia,misimamo binafsi),Historia za maisha ya awali alikopita,Kutokubali mabadiliko ya Kujifunza, *Ujuaji wa Kutojua.*
👉Kuaminiana kuna kua kulingana na LEVELS za Mahusiano mliyopo na Time ya kukaa katika mahusiano.
👉Mahusiano ya urafiki yana kuaminiana kwa kawaida,uchumba kuaminiana kunaongezeka maana na Intimacy imeongezeka na muda ni mrefu kidogo, Ndoa ndo Kuaminiana kunaongezeka sana maana na Intimacy imekuwa kubwa kiasi cha Ku share Miili. _Ila maajabu ya Kisaikolojia ni kwamba, wan ndoa ndo Hawaaminiani kwa level ya juu sana_ Shida hapa ni Ugumu wa Fikra, Imani Potofu ya Misimamo iliyo Kufa.
3⃣Itimacy ina zaa Kumfurahia Mwenzako na Amani. Ni ukaribu wenu ndo unaopelekea kumfurahia mwenzako, awe karibu au mbali moyo unamfurahia, una Amani naye. Huu mdo ustawi wa mahusiano na ndoa.
👉Kama hakuna Ukaribu, mwenzako awe mbali au awe karibu unamuona wa kawaida,na uhisi chochote juu yake na haya ndo ( *Mahusiano yaliyo kufa*)
4⃣Intimacy inazaa *Mawasiliano hai* huu ni ugonjwa wa wana mahusiano na wana ndoa. (Problems in Communication )Mahusiano yoyote yaliyo hai yanadhihirika katika mawasiliano na katika mawasiliano tunaangalia ( *Purpose/Sababu ya kuwasiliana, State of Communication/Hali ya mawasiliano(lugha,sauti, na Awamu za mawasiliano/levels)*
👉Mawasiliano kwa wachumba na wana ndoa baadhi yamekuwa ni *Makavu,ni Viporo* kwa kisingizio cha Ubize, kuwa haya ni mambo ya kitoto,ya kujishaua,ya wale waliooana wenye mchecheto bado( *Hizi uwa ndo lugha za watu walioona wao Wamefeli kwenye kipengele hicho*) sawasawa na wanaosema HAKUMA MTAKATIFU DUNIANI, baada ya wao kufeli kuishi maisha matakatifu wanahisi na wengine wote wameshindwa.
👉Wana mahusiano wengi na wana ndoa wamebaki kuwasiliana kwa  *_Matatizo, Maagizo na kwa Dharula ikitokea_* (Purpose) Siyo kwa Caring
👉Na wengine wanawasiliana kwa Sauti isiyo Vutia,isiyoonyesha utaofauti wa Intimacy kati ya mwenzi wake(mpenzi wake)na mtu baki mwingine... na wengine kwa lugha ya Ukali na Kufoka(State of communication)
👉Wengine wanawasiliana baada ya kipindi Kirefu kuondoa LAWAMA(Level/Times)
👉Mfano,mwenzako mmeachana kwa muda kikazi au kimajukumu(hasa mlo kazini) yale masaa 12 ya kazi mpaka 14 _Unawasiliana na mwenzako mara ngapi kwa sms,au call?_ au Umesafiri kwa siku1 hadi mwaka nk, mara ngapi unawasiliana na mwenzako kwa siku nzima 24hrs? *_Hiyo inaonyesha Intimacy yenu au Distance yenu na aina ya mahusiano mliyo nayo_*
👉 Kuna wengine wanao wasiliana kwa *_Care & Love,(Purpose ),Kwa lugha ya kupenda,kuthamini,(State of communication)na mara kwa mara(Level/Times)_* hawa watu Mahusiano yao yatakauwa Imara, pamoja na changamoto nyingine kuwakumba lakini Mahusiano yao ni Imara, hawa si wa Kubeza wapo kwenye kona ya Kufanikiwa kwa lolote kiurahisi.
❣ *Mahusiano siyo kujivunia Kutoa Matumizi yote ya Familia(mama au baba),hiyo ni Sawa na Kujivunia kutoa sadaka na zaka kanisani lakini HUNA MPANGO NA IBADA* ibada ni Fellowship na Mungu(Intimacy)ndo lolote unalolifanya kwa Mungu lina maana. Hivyo hivyo, Mwenzako anahitaji INTIMACY kwanza ndo lolote utakalo fanya litakuwa na Maana Kwake.(Kuwa muda na mwenzako,time yo chat with people and with your Partner )Siyo mda wote umeinama kwa simu au laptop mpaka unakuwa kero kwa mwenzako unakuwa mtumwa wa Teknolojia ( _Haya ni mambo madogo ya kisaikolojia ila ndo uleta migogoro katika mahusiano na ndoa,ushusha thamani na upendo kati yenu_)
*_Hii ni sehemu ya Kwanza ya Lecture hii ya Mahusiano ujumla wake ni Ukaribu,usikose sehemu ya pili ya mwendelezo wake_*
Mchambuzi ni Mwanasaikolojia na mchambuzi wa masuala ya ndoa na Mahusiano Ev Elisha Kazimoto
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment