💈💈 *UKABILA KATIKA NDOA*💈💈
*Swali* _Kuna watu,vijana au familia kukataa kuolewa au kuoa kabila flani na kutaka kabila flani hili lina maana gani na umuhimu gani katika ndoa?_
*Anajibu Mwanasaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
.......
.......
.......
_Hii ni mtazamo wa Kijamii,ambao ni mapokeo ya wazee wetu yaliyo lenga kujenga Koo na tamaduni moja za watu wanaoelewana katika Mila na Desturi_
👉Tangu enzi hizo za mababu zetu ndoa haikuwa haki ya mtu binafsi anayeoa au kuolewa,ila ilikuwa ni haki ya Kifamilia(wazazi),ndiyo maana Wazazi ndo walio husika na kumtafutia Kijana wao mke kutoka katika familia waliyoipenda na waliyo hisi inatabia njema,marafiki,na malezi mazuri ya binti au kijana lakini wanaendana kitamaduni/kimila,na kijana au binti hakuruhusiwa kubisha,kukataa mchumba huyo,na wazazi pia walihusika na Kumlipia kijana Mahari.
👉Mfumo huu ulilenga kulinda (Family Species ) mfumo huu umetoka katika BIBLIA ambapo Mungu aliagiza watu waoane ndani ya kabila lao,ndo maana unamuona Rebecca anamwagiza Yakobo ujombani ndo aende akachukue mke kule kwa Labani, Isaka pia, na wana wote wa Israeli waliagizwa Wasioe nje ya Kabila lao.(Taifa lao)
👉Utofauti wa Kabila ulitafsiriwa utaleta utofauti wa mila na desturi jambo litakalo pelekea Kuingiza mambo mapya kama Kuabudu miungu mingine na kutoa kafara kama za watoto,kupitisha watoto kwenye moto ambayo ni machukizo kwa Mungu wa Israeli. Ili kulinda mahusiano yao na Mungu iliwabidi waoane wao kwa wao..
👉Tabia hii imeendelea mpaka tamaduni zote za dunia wanapenda kuoana wao kwa wao ili kukinda mila na Desturi zao.
.....
.....
....
*Uchambuzi unae delea angalia zama hizi kiroho na kimwili kwa nini kuna mwingiliano wa makabila* Uko na Ev Elisha Kazimoto
👉Kijamii kwa sasa mambo yamebadirika sana na miiko ya mababu imefutika aidha kwasababu mbalimbali ikiwemo...
1.Maendeleo ya kijamii(Utandawazi)ambapo kumekuwa na mwingiliano wa jamii,kabila,taifa kila kona kiasi kwamba mipaka ya kiutamaduni imefutika,kulingana na watu kuwa pamoja katika kazi,shule,biashara na nyumba za ibada hii imeleta utamaduni sawa wa pamoja na watu kuanza kutamaniana na kuelewana na kuona waweza ishi pamoja.
2.Wazee wa zamani wamepungua walioshika mila na desturi na kuwaridhisha watoto wao,kwa sasa watu wanaendesha familia kulingana na mchakato na kasi ya nchi,na elimu walizopata.
3.Suala la Utumwa(Colonization )kwa jamii za Kiafrika limeathiri mifumo mingi ya kijamii na tamaduni zetu.
4.Mwingiliano wa jamii na watu unaoletwa na biashara,elimu,siasa na dini umeondoa mipaka ya kulimda tamaduni husika. Ndiyo maana ndoa sasa haifuati kabila inafuata level ya mwimgilianao na kuelewana baina ya watu wawili(ndo utamaduni wao)
👉 *_Kibiblia Kabila linamaanisha nini kwa sasa na linazingatiwaje katika ndoa?_* _Hili ni swali la msingi kwa sasa, Kwa watu waliookoka Bado Maadili ya Ndoa kwa mujibu wa Kuzingatia Kabila Upo palepale..Wooote waliokoka Tumezaliwa katika Familia ya Kristo kwa Neno na kwa Roho wa MUNGU kupitia Damu ya Yesu Kristo tuna share Common blood group ya Yesu(Ufunuo 5:9-10, Yohana 1:11-12, 1Yohana 5:1-10, 1Petro 2:9-10) kwa kutaja machache baada ya kuwa katika Kristo sasa tunakuwa na sifa zifuatazo._
1.Kabila la Watakatifu
2.Taifa la wana wa Mungu walioitwa kwa jina la Bwana.
👉Sisi tunaagizwa Kuoana watu wa Kabila moja ili kulinda utamaduni wetu wa(Ibada mbele za Mungu wetu, utakatifu wa maisha ya mwili na roho,utumishi wa madhabahuni pa Bwana)
👉Kuoana na mtu asiyeookoka ni Kuoa nje ya Kabila lako ambapo utaingiza mambo mageni katika kabila la watakatifu wa Mungu jambo ambalo hakimpendezi Mungu(utavuruga utamaduni wa ibada,utumishi na utakatifu).
👉Kwa kijana aliyeokoka yeyote awe binti au kijana wa kiume.... *_Anacho zingatia Ni Kuoana na Kabila la Watakatifu kutoka Taifa la Wana wa Mungu_* siyo makabila ya kijamii haya kwetu hayana nguvu,ndo maana tunapo okoka Utu wetu wa Kale unabadirishwa ikiwemo mila na desturi zisizo faa,ukorofi, vyote vinamezwa tunakuwa wapya watu wenye Utamaduni mmoja wa Utakatifu.
👉Wengi wanaogopa kabila flani wanatelekeza wake, wanaua waume,wana ukahaba,hawa wakorofi,wagomvi,nk....Jambo ambalo kwa waliookoka Hayo yote ni Marufuku na tumeyaacha tumegeuzwa na kuvikwa utu mpya tabia mpya,biblia inasema sisi tuwe Wanana(wapole),magomvi,uasherati na uchafu wote tumeambiwa visitajwe kwetu na mambo mengi yakumfanya mtu kuwa mwema, sasa utaogopa nini tena? *_Sisi tunachoogopa ni Kuoana na mtu ambaye utu wake wa ndani haujageuzwa hapo ndo majanga tabia zote za Asili anazo na zinamwendesha hapo ndo utakoma kama umeoana naye_*
Kwa kuhitimisha niseme Suala la Ukabila katika ndoa,watu wasio na viwango vizuri vya Kiroho ndo vinawapa shida,kuogopa kabila hili au lile...Ukweli ni kwamba Makabila Yoote yana Ubovu wake na Uzuri wake,hakuna kabila la kusimama likajisifu kuwa hilo ni kabila Perfect,ila tunatofautiana matatizo basi...Kabila liliokamilika ni la Watakatifu kutoka Taifa la wana wa Mungu basi.
👉Watu wenye uwezo,vijana waliookoka vizuri suala la kabila,elimu,uchumi siyo kipaumbele kwao maana hivi ni nyongeza katika CV kubwa inayo hitajika kwa mme au mke na vinatolewa na Mungu mda wowote. Ndiyo maana Binti yule uliye mkataa kuwa hana pesa wala kazi nzuri unamkuta ndo ana Bonge la ndoa na maisha SUPER,na wewe ulotafuta Pesa kabla ya mapenzi ya Mungu unalia na pesa zako wala huzifaidi nazo zimeisha,ulitafuta Elimu nzuri huifuarahii,ulitafuta kabila zuri ukasahau Kabila la Watakatifu,ndo sasa unachanganyikiwa mwenzako haeleweki,wengine wanatafuta wazungu au waafrika wa nchi flani yaani hataki aoane na Mtanzania au mkenya mwenzake, umeacha kutafuta Taifabla Wana wa Mungu sasa unataka Talaka ukae peke yako hizo ndo athari za Kuwa Shallow kiroho,ila walio na uwezo kiroho wanajua mambo yote ya Mwilini mafanikio yanatoka kwa Baba wa mbinguni aliye Yote katika Yote wanjua muda wowote maisha yao yaweza badirishwa kikubwa wakae CONNECTED NA MUNGU hilo ndo jambo kubwa.
*_NB: Unajua Adamu alikuwa kabila gani na Hawa alikuwa kabila gani,unatafuta wa kufanana nawe katika kusudi la Mungu_*
By Ev Elisha Kazimoto(whatsapp 0755444078)
No comments:
Post a Comment