💣💣 *UNAWEZA KUSHINDA VITA YA KIROHO ILA UKASHINDWA VITA YA KISAIKOLOJIA(ENVIRONMENTAL PRESSURE )*💣💣
*_Na Ev Elisha Kazimoto(WhatsApp 0755444078)_*
.......
.......
_Shalom mtumishi wa Bwana,wewe uliyeokoka ni mwana wa ufalme wa Mungu,na ni Askali wa kiroho katika jeshi la Bwana,nakusalimu katika jina la Bwana_
🔫Moyoni mwangu limewekwa neno hili kwa nguvu sana,niseme nawe uliye mtumishi wa Bwana na muhudumu wa Madhabahuni pa Bwana,kwanza wewe ni wa muhimu katika ufalme wa Mungu,pili wewe ni mtu hatari sana katika ufalme wa giza,tatu Vita yako na mawindo yako hayapangwi kireja reja yanakuwa *_Carefully,Systematic Organized_* sijui kama umeelewa, yaani yanakuwa yanaandaliwa kwa Umakini mkuu,na kwa mpangilio maalumu na balaza la kuzimu la shetani.
🔫Unajua kwa nini vita ya mtu wa Mungu,mtumishi wa Mungu aliyesogezwa katika daraja ka kuwa muhudumu wa madhahuni pa Bwana,vita yake inapangwa kimkakati na utulivu wa hali ya juu sana ili kumnasa? *_Ni kwa sababu, Level yako nirahisi Kumshtukia adui yeyote kwa njia zozote na ukamshinda_* kwa mitego yoote ya dhambi,na ukengeufu wowote ni rahisi kuushutukia ukiletwa kwako. _kwa hiyo wewe unaletewa vita ya Kisaikolojia(Environmental Pressure )ambayo inaambata zaidi na *Nature yako/Personality & Character /Mfumo wa mazingira yako* yaathiri saikolojia yako ili ikupelekee Kukosa_
💣Nisikilize nikupitishe kwa watu hawa ambao ilikuwa ni *Vigumu shetani kuwa kosesha,kulingana na viwango vyao vya kumjua Mungu na nafasi zao mbele sa Mungu* ila Adui alitumia Saikolojia (Environmental Pressure )kuwakosesha, si semi kukuvunja moyo,au kuhalalisha kushindwa,ila NAKUTAADHARISHA kama mtumishi wa Bwana,na mtu wa vita ujipange kushinda kote kote kiroho na kisaikolojia. Tuna watumishi wengi Kiroho wako vizuri sana na adui anajua hilo,ila Kisaikolojia ni wadhaifu,kwa hiyo muda wowote faulu inaweza chezwa maishani mwao kupitia saikolojia na mambo mengi yakaenda ndivyo sivyo,hawajatenda dhambi,bado wako na Mungu ila Wamepunguzwa kasi kisaikolojia.
1⃣ *Musa* ni miongoni mwa wanadamu wenye sifa pekee ya kuongea na Mungu *Uso kwa uso* mtu wa aina hii kumkosesha ni vigumu mpaka utumie NATURE( environmental pressure ). Katika upako wake ule ule, *_Aliambiwa na Mungu auambie mwamba utoe maji Israeli wanywe, yeye Akaupiga kwa fimbo mara 2_*
7 Bwana akasema na Musa, akinena,
Hesabu-Numbers 20:7
8 Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao.
Hesabu-Numbers 20:8
9 Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za Bwana kama alivyomwamuru.
Hesabu-Numbers 20:9
10 Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?
Hesabu-Numbers 20:10
11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia.
Hesabu-Numbers 20:11
12 Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa.
Hesabu-Numbers 20:12
👉👆Kosa la Kisaikolojia lilifanyika hapa ndo likapelekea kosa la Kiroho kuto mtii Mungu. Sababu ya Musa kupiga Mwamba mara 2 badala ya kuuambia mwamba ni( *Environmental Pressure*) Maudhi ya watu kwenye mazingira,kumbuka wako mwilini(upako wako haukuondoi mwilini,haukufanyi usisikie,usione, ila unaweza kukusaidia kukwepa matokeo yakusika,na kuona)sasa inategemea Unaijuaje saikolojia yako katika mazingira yenye changamoto ndo Uiombee isivurugwe. Kilichofanyika kwa Musa na Haruni ( *Walipata Stress kutoka kwa watu*)Matusi,dharau,kelele tunataka maji,tunataka maji, mmetuleta kutuua, wakati hawa wanaowaongoza wamejitoa muhanga kwa Farao kwaajili yao,wamefanya mambo mengi wakati wako jangwani,lakini bado *_People they are shouting to them as the useless leaders_* Sasa kutibu Stress yao Musa na Haruni ilibidi ifanyike powerful Reaction, Majibizano yakuonyesha how strong and important they are kwa watu ili Saikolojia zao zikae sawa ndo waendelee na safari. Wakapiga mwamba mara 2 na maji yakatoka,wakanywa, heshima yao ikarudi,wakaonekana katika sura waliyotaka wao waonekane wasidharauliwe,lakini kumbe wakawa wameharibu Destiny yao. _Kwenye maisha si kila mara utashambuliwa kiroho *Unaweza shambuliwa kisaikolojia ili ukosee kiroho* Kuwa makini na Nature yako ni ipi( Hasira,Kutokubali kushidwa,Mwongeaji sana,Mwoga,nk)vyaweza kukufanya ushambuliwe kisaikolojiana ukakosea kiroho._
2⃣Mtu mwingine ni *Eliya* huyu ni mtu hatari sana katika huduma yake,ni mmoja wa Manabii wenye nguvu aliye mkabili mfalme Ahabu,akafunga mvua isinyeshe kwa muda wa miaka 3.5 na akairuhusu ikanyesha,na akawachinja Manabii wa Bahali 450 mwenyewe. Mtu huyu ni vigumu kumtikisa kiroho, *_Nabii huyu alishambuliwa Kisaikolojia na Mwanamke mmoja, Yezebeli mke wa mfalme Ahabu,kwakumtumia ujumbe kuwa,kesho nakuchinja kama ulivyo chinja manabii wangu 450_* Taarifa hii tu,ilichanganya Eliya kisaikolojia( Hii ni *Environmental Prsussure*)akaamua kukimbia kwa hofu na kujiombea kifo kwa Mungu. Swali,Je, waweza amini mtu aliye mkabili mfalme,kufunga mvua na kuiruhusu,kuchinja manabii 450 peke yake anaweza leo letewa taarifa ya mwanamke kuwa kesho atamuua naye Akakimbia? *Jibu si kwamba hakuwa na Imani, alipata Psychological Attacks* kutoka kwenye mazingira,reaction ikawa ni kuponya roho yake.
1 Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga.
1 Wafalme 19:1
2 Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.
1 Wafalme 19:2
3 Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko.
1 Wafalme 19:3
4 Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.
1 Wafalme 19:4
5 Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule.
1 Wafalme 19:5
👉Shambulio la Kisaikolojia linakupata kama wanadamu wa kawaida, siyo kama mtumishi wa Mungu,likikupata tafakari kabla ya maamuzi yoyote,Tafuta connection kati ya saikolojia yako na Roho yako ndo ufanye maamuzi,ila ukijiona kwakuwa mimi nimeokoka,natumika,ni mtumishi mkubwa,siwezi kushambuliwa kiroho ni kweli we kiroho ni vigumu kushambiliwa, Kisaikolojia je? Maana wee bado ni binadamu kama wengine,unasikia,unaona,unasema,Unaumia,unapenda kama binadamu huko ndo unashambuliwa,fanya maamuzi yako yoyote kwa kutuliza saikolojia yako kwanza Utatenda kwa Busara sana,utashinda vita nyingi mno.
3⃣Mtu wa tatu na mwisho katika ujumbe huu(japo wapo wengi ) ni *YESU KRISTO* Hapa ndipo utaona Ukubwa wa Vita ya Kisaikolojia katika maisha ya watumishi wa Mungu(Tunao simama madhahuni) _Yesu alikuwa mwanadamu kwa asilimia kadhaa,(kwa kuwa aliuvaa mwili huu wetu,na kuishi duniani kama sisi miaka 33)na alikuwa Mungu asilimia kubwa kwa kuwa alikuwepo tangu milele,nakuzaliwa kwake hakukuwa kwa hatua za kibinadamu(Yohana 1:1-5),na Yesu alikuja duniani Akijua kabisa ninakuja kuokoa wanadamu kwa njia ya mateso na kufa msalabani,na kufufuka siku ya 3._ kwa hiyo Yesu kwa lugha nyingine alikuwa anaishi akijua mwanzo na mwisho wake,siyo kama sisi tunaoishi kwa imani tukitazamia mwisho wetu kwa imani,no.... yeye alijua kila hatua,anayopitia,nani atahusika na atakuwaje mpaka mwisho.
👉Yesu huyu huyu(Mwana wa Mungu/Mungu mwenyewe)katika mwili alikutana na *_Shambulio la kwanza la kiroho-akiwa kwenye maombi siku 40_* MATHAYO 4:1-10 Alilipiga kiurahisii kwakuwa lilikuja kiroho naye kiroho ni chuma.
👉Shsmbulio la pili kwa *_Yesu lilikuwa la Kisaikolojia(Hisia za uchungu na mateso)alipo enda kuomba wakati saa inakaribia ya kukamatwa na kuteswa ili atimize kusudi lake, aliogopa,akaomba maombi haya "Baba Ikiwezekana Kikombe hiki kiniepuke...."_* Hapa alikuwa anapambana na Environmental Pressure(Mwili ulikuwa una sense maumivu ya mateso yatakavyo kuwa)Akili ikaanza kusoma kukwepa dhoruba hiyo,....Ila *Yesu alitulia,aka connect Saikolojia yake akairudisha kiroho akapata jibu,papo hapo akabadiri maombi akasema, "Si kama ni takavyo mimi bali mapenzi yako yatimizwe"*
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.
Mathayo 26:39
hiyo ndo tofauti ya walioshindwa na akiye shinda.
_Nimalizie kwa kusema watumishi wa Mungu,tupo katika dunia yenye *Pressure kubwa* juu ya sakolojia zetu, katika mwili tulio nao Tumevaa saikolojia ya Hisia(hasira,furaha,uzuni,uchungu na kupenda) Tulia sana,sana katika kufanya maamuzi ya maisha yako popote pale(Ukiroho Hauondoi Nature yako,ila unaweza kukusaidia kufunika Nature yako ukitulia vizuri na kujitambua wewe una React vipi katika changamoto zinazo shambulia maisha yako,status yako,kazi yako,huduma yako,ndoa yako ndo uombe Mungu akusaidie kutulia kabla ya kufanya maamuzi,yawe ya vitendo au ya Maneno,waweza hisi adui anakuandama kumbe uwezo wako wa Ku Control Nature yako wakati wa shambulio la Kisaikolojia ni Mdogo_.
*Mungu akubariki,ukiyajua haya,nyumbani kwako,kwenye ndoa,kazini,kwenye huduma yako utakuwa mtu wa pekee sana.*
Imeandaliwa na Ev Elisha Kazimoto
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha kazimoto.
No comments:
Post a Comment