Tuesday, 4 September 2018

KULIPA MAHARI KUBWA AU NDOGO

💰💰 *TAFSIRI YA MAHARI KUBWA AU NDOGO KATIKA NDOA*💰💰
_Anajibu Mchambuzi wa Masuala ya Ndoa na Mahusiano Mwanasaikolojia_ *Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
.......
.......
*MADA YA MAHARI HII IKO KIJAMII ZAIDI NA KISAIKOLOJIA KWA SEHEMU*
_Labda niseme kwanza, *Kiwango Cha Mahari,Hakitafsiri Thamani ya mwanamke,Tabia yake,Ubora wake na Faida anayo kwenda kuizalisha kwenye Familia yake* Ni mfumo tu ambao familia(Mzazi)ameamua kuuchagua Kujiridhisha Husia zake na moyo wake na mazingira yake ya kiuchumi basi,na uwezo alio nao wa kuitafsiri ndoa ya mtoto wake_
🏓Mahari kubwa,haituonyeshi kuwa huyu binti amelewa kwa *Maadili pekee* ambayo mmewe ataenjoy tangu anamuoa mpaka wanazeeka. Badala yake waweza lioa hata mil 100,na Ng'ombe 100 hata msimalize mwaka mmeisha achana, na mwingine akaleta Kilo 50 za sukari kama shukrani wakaishi kwa amani mpaka uzee na wakawa baraka kwenu wazazi.
👆Unielewe sijasema Mahari ndogo mdo inakupa ndoa ya Amani, mimi nakuonyesha *_Hakuna mahusiano ya mahari kubwa na Ubora wa mwanamke_* Suala linabaki pale pale kuwa Ubora wa mtu unategemea na Yeye binafsi anavyo mjua Mungu.
🏓 *Vijana kuogopa mahari kubwa na kuchelewa kuoa* hizi nisababu Binafsi za Kiuchumi japo yaweza kuwa kichocheo ila siyo sababu ya kimsingi, maana wapo *_Vijana ambao hata akiambiwa Mahari mil 20 haimpi shida,ila nao wanachelewa kuoa_* Shida ni Kumpata mtu Sahii wa kuishi naye Milele mpaka kaburini na Usipoteze Ndoto zako(Hilo ndo linawapa watu shida na kusababisha kuchelewa)
👉Unajua kuna watu *Wanajipenda,wana Vision kubwa* hawahitaji kuvipoteza kirahisi na kujipa stress ya maisha,ukizingatia ndoa ni Mkataba wa Kudumu(wa milele).Uchague vizuri,au vibaya na Excuse.
🏓Lakini wazazi kazima tujiulize kabla ya kupiga mtu mahari, *_Nini tafsiri ya Mahari,je ni shukrani kwako mzazi,ni kifuta jasho,ni kodi,ni mshahara wa kazi uloifanta ya kulea?_* ukijiuliza haya maswali hutaoanga mahari kubwa,isitoshe watu hawajui, *_Mahari yoyote iwe ndogo au kubwa, ukimpiga kijana jua Umemuunganisha na mwanao_* oesa anatoa mme wa mwanao,Akiangaka popote akapata oesa ata akauza gari kale(kama analo)ili kulipa mahari Maisha magumu siyo ya wazazi wa kijana,au kijana peke yake ni ya kijana na mwanao(mke wake)na watoto wao ambao niwajukuu wako.
👉Mbaya zaidi umebana nafasi ya wewe kusaidiwa na wanao (hao familia mpya)kwa viwango vikubwa. Ambapo ungepata dharula ya gari mkwe akaja na binti yako wajakubeba ukaenda kama mfalme,watakoia pesa kukutumha uende kwa daladala au tax ya kukodi.(kwa hiyo *Maumivu ya Mahari kubwa,anaugulia kijana na wewe mzazi*) huna ulicho save.
🏓Binti ni Referee mkubwa awezaye kuweka mambo sawa kuhusu mahari na kijana akalipa kwa wakati bila maumivu.
👉Wadada mnapaswa kujua *_Kutolewa Mahari kubwa Siyo kuthaminiwa,wala kuishi maisha ya kutodharauliwa kwenye ndoa_* Maisha ya ndoa ni kitu kingine,mahari kitu kingine,elimu au uchumi mkubwa wa familia yenu ni kitu kingine. Havina mahusuano na maisha ya amani,furaha na upendo,badala yake anaweza Laaniwa baba yako na mama yako kwa kukuozesha kwa mahari kubwa kumbe ndani we ni USELESS(MITHALI 14:1).
🏓Wewe binti ndo unayeenda kuishi na huyo mme ambaye leo anakamuliwa hadi senti ya mwisho(mnaanza maisha mkiwa hoi,madeni kibao kika kona,na hamuwezi rudi kwa wazazi kuomba wawasaidie muendeshe maisha,utapata faida gani sasa)
👉Ilibidi binti *_Usimame kuwashawishi wazazi mpaka walegeze kwa kiasi ambacho mmeo ataweza kiurahisi_* halafu mkishaoana mnajipanga Kuwahudumia wazazi wenu pande zote kwa ukaribu mkuu.
*_Ni hitimishe hivi,Kupanga ni kuchagua na kuchagua ni kupanga, Lolote utakalo litamani litaleta majibu,hasi au chanya ila ujue, Mahari kubwa,au ndogo,sherehe kubwa au ndogo Haipimi Ubora na Uzuri wako,ila mwisho wa mzunguko wewe ndo Utaumia na Mwenzako wengine tutabaki na kumbukumbu ukilipiwa mahari mil 15,harusi mil 70,ila maisha ya Amani au Kilio ni yako na Mmeo_*
Mchambuzi wako wa Masuala ya Ndoa na Mahusiano Mwanasaikolojia *Ev Elisha Kazimoto.*
Whatsapp 0755444078

No comments:

Post a Comment