Friday, 7 September 2018

WAIMBAJI NA NDOA

💔💔 *CHANGAMOTO YA WAIMBAJI KATIKA NDOA*💔💔
*_Swali linaulizwa,na linajibiwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto(Mjumbe Mkali- Mithali 17:11)_*
...........
...........
salaam mwalim wa class

Kabla sjaokoka nilioa baadae nikapata neema ya wokovu mimi na mke wangu
tuumeenda na kuzaa watoto wa 3
maisha yalikua poa tu
teacher kilicho tokea mpaka tumetengana na mke wangu ni hiki

mke wangu ali record albam ya nyimbo 9 tumekua begakwa bega nae
mpaka siku yauzinduzi wa albam yake
ugomvi ulianzia kat yangu na baba mkwe kunitaka nitoe laki7
akidai yeye anagalimia shorting na matangazo kwenye Radio
nika mwambia mzee iyo pesa sina ila ninalak 3 tu akakasilika na kuonda kwa mchungaji wangu nakunisemea nina kibuli simsikilizi
mbaya zaidi anamwambia mchungaj mimi sio type ya kumuoa mtoto wake
mi nimka vumilia mpaka siku ya uzinduz
sasa baada ya uzinduz mke akagomewa kuja kwangu baba mkwe akidai kwa binti kua anakuja kuitajilisha familia yangu
baada ya mwezi mke aliludi akakaa kidogo akarudi tena kwao mpaka leo ajarudi

binti anadai misiwezi kuja kwako wewe umskilizi baba yangu na ulinioa bahat mbaya tu
mi si type yakuolewa nawe

teacher nambie nifanyaje

je pana wokovu kweli apo
maana anaendelea kuimba makanisa mbalimbali

naomba ushauri wako mwalimu wangu

kazi njema😭😭
..................................
..................................
*Anajibu Ev Elisha(Whatsapp 0755444078)*
...................................
*HUYU NI MGONJWA MAHUTUTI, TUFUNGE MADA KWA KUMSAIDIA KIROHO NA KISAIKOLOJIA*
_Kwanza kijana nampa polee kwa changamoto hiyo ya ndoa,Lakini pia nampa polee kwani alikuwa mpagani akaokoka akitegemea akiokoka anatua mizigo,bahati mbaya mke,na mkwe wake wakamtwika nyingine ila Asikate tamaa Bado Liko Tumaini kwa Bwana_
👉Ni seme na mke, kwanza mwanamke huyu amegeuka kuwa miongoni mwa WANAWAKE WAPUMBAVU(MITHALI 14:1) yaani ni miongoni mwa wadada ambao HAWAKUSTAHILI KUOLEWA na mtu yeyote maana,hawajui Thamani ya mume,thamani ya Ndoa,thamani ya Malezi ya watoto(unaachaje watoto walelewe na mzazi mmoja kisa pesa za uzinduzi) na thamani ya Wokovu(Kwa lugha nyingine Huyu mmama ALISHAACHA WOKOVU,NI MPAGANI,HAJUI MAANDIKO,HAJUI MAANA YA HUDUMA ya Madhabahuni.(Tafuta google Semina yangu ya masomo 11,shemu 1 hadi ya 11 kuhusu Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu, Huduma ya Madhabahuni)-By Ev Elisha Kazimoto)andika MATERIAL ADIMU
👉Tendo la kuruhusu moyo wako ufanye maamuzi ya kutoka kwa mme wako bila kufukuzwa,bila ugomvi, kisa ni PESA ZA UZINDUZI WA ALBUM(Huduma)huu siyo Uchanga kiroho ila ni UKENGEUFU WA MOYO.
👉Huduma unayopigania kuifanya,hiyo ni huduma ya 2 kwako, HUDUMA YA KWANZA NI NDOA YAKO(Huyu ni mpagani kabisaa)si kwamba na MUHUKUMU ila ndivyo barua ya Matendo yake inasomwa
*_Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote;_*
*2 Wakorintho 3:2*
(Yesu alitwambia tutawatambua kwa Matunda yao)ntawaoa vigezo vya matunda yake.
👉Nimesema huyu mwanamke anamtumikia Mungu gani? Huduma gani anayofanya? Huduma ya kwanza SI UIMBAJI,huduma ya kwanza ni NDOA YAKE.👇👇👇👇
*_34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe._*
*1 Wakorintho 7:34*
👉Mpaka hapo amekwenda kinyume na Neno la Mungu,amekengeuka, Kwa tabia hii anakazi kubwa ya kupenya katika utumishi, ila nikimtafakari kiroho nakuta ameisha Vamiwa na Maroho yanayowashambulia waimbaji( *_Roho za  Kiburi,Roho ya Tamaa ya Pesa,Roho ya Zinaa_) Mpaka hapo viashiria vya hizi roho zote 3 anazo.(NTALETA SOMO LAKE BY EV ELISHA KAZIMOTO)
1⃣ *Kiburi* Tayari anakiburi kikuu biblia imekiita cha Uzima.Yaani kumgomea mmeo na kurudi nyumbani kwenu,kumshtaki kwa mchungaji kisa pesa hazikukamilika laki 7,yeye amepata 3,ni dharau,ni jeuri ni Kiburi kikuu(hapa hakuna unyenyekevu wowote inaousema Biblia wa mke kuwa nao kwa mmewe.

*_Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;_*
*1 Petro 3:1*
👉👆Huyu mwanamke anaweza kumfundisha nini mwanamke mwenye changamoto ya ndoa ambaye mme wake hajaokoka? _Kwanza nachelea kama kati ya hao watoto 3 walozaa kuna wa kike, Anahitaji kuombewa sana maana mama yake amemuharibia SOKO LA KUOLEWA tangu kwenye ulimwengu wa mwili mpaka wa roho.
2⃣ *Tamaa ya Pesa* Hii roho imeisha mvaa tayari,unaweza ona lugha za baba yake ndo za mtoto,baba anasema ukirudi unaenda kuitajirisha familia(yaani wamefanya uimbaji wa huduma kuwa mradi wa biashara)hapo utasema anamtumikia Mungu au anatafuta ugali? na mwanae anakaa HARUDI KWA MMEWE( *Hivi wee mwanamke Umeolewa na Baba yako?*)au ndo tambiko la kuzimu ili utoke kimziki uachane na mme wako ukae na baba yako ndo nyota yako itoke.( _Natamani ujumbe huu umfikie unapozunguka kwenye magroup halafu anitafute ni msaidie, Mauti inamtafuta tena mauti zote ya kiroho tayari alishaanguka bado ya kimwili_) Ndoa ni zaidi ya pesa hizo( *Ka albamu kwanza ni kamoja,anahisi yeye amekuja na upako awafunike watu wenye mafuta ya uimbaji moaka ukitazama sura zao unaona utukufu wa Mungu? Huyu mafuta ni ya magomvi na mafarakano*) Si hitaji kuwa Nabii kwake ila nisemalo ni hili kwa mwendo wake huu,asipo tubu Ataishia ALBUM 1 nayo itakosa soko,kabda ATOE KAFARA KUZIMU WA MWEZESHE ila kwa Mungu ninaye mjua anaye tumia Roho wake mtakatifu kuinua huduma asahau kusonga mbele.
*_Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu._*
*1 Wakorintho 14:33*
👉Kwa hiyo aimbe ila ajue anaimba chini ya uongozi wa *Roho Chafu/roho Mtakafujo siyo Roho Mtakatifu.* wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndiyo wana wa Mungu.(Warumi 8:14)
3⃣ *Roho ya Zinaa* mpaka sasa roho ya zinaa inamwendesha,aidha inamwandaa vema aitumikie au mpaka hivi ninavyoongea NI MZINIFU WA KUTOSHA.( _Sababu ni kwamba,unatoka kwa mme,tendo la ndoa unashiriki wapi,waweza kutoliona lina umuhimu sasa,ila shetani yupo,washawishi wapo,wengineunaowaita mabosi wako,waimbaji wenzako roho ya zinaa inatembea. Ukikutana mwimbaji mwenye pepo kama lako amemuacha mke wake kisa hawaendani wote mtaanza zinaa chafu_)
👉Wewe mwanamke haya maneno ya kwanza Alikuoa kwa bahati mbaya( *yawe yanasemwa nawe au baba yako*)wote wewe na baba yako mnawokovu wa kifafa, Kama ni kwa bahati mbaya jua wewe mke NDO BAHATI MBAYA(TENA MKOSI) na mwanaume alifumbwa macho kuja kwenye Familia ya watu Wanaoolewa kwa Bahati mbaya si kwa mapenzi ya Mungu,kwa lugha nyingine familia yenu mnahitaji maombi ya ukombozi kuwavua huo ubahati mbaya.
👉Nikuulize imekuwaje Umezaa na mmeo watoto 3 Kwa bahati mbaya? Najua SEX YOYOTE UWA INAFANYWA NA WATU WANAOFURAHIA NA KUPANGA ISIPO KUWA YA KUBAKWA.(nina somo langu la sex siya bahati mbaya niya makusudi kabisa masna ina hatua 11,tafuta google somo hilo by Ev Elisha Kazimoto) ilikuwaje hao watoto 3 mkawazaa kwa bahati mbaya?
👉Kabla ya kuanza kuimba hamkuoana kwa bahati mbaya baada ya uzinduzi ukaanza kujiona kwenye screen na mwenzako haonekani ndo ukahisi alikuoa kwa bahati mbaya.‼
👉Aisee na baba yako hakustahili kupewa uzao,ilibidi Mungu afunge tumbo Lake awe tasa *Maana hana uwezo wa Kulea* baada ya kuzalisha watumishi wa Mungu anazalisha vibaraka wa shetani tena kwa makusudi si bahati mbaya.
*_6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee._*
*Mithali 22:6*
👉👆 _Haya maneno yaweza kuwa magumu kwa watu wenye roho nyesi,ila kwa watu wa rohoni hii no tiba,kuna watu wanahitaji Kukaripiwa na kuonywa_

*_Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote._*
*Tito 2:15*

👉Kuna watu wanatuchafulia wokovu inatia uchungu. *WAIMBAJI MNATUPELEKA WAPI MNA NINI LAKINI*
1⃣Single mothers wengi ni waimbaji,si kwamba waume wao wamekufa ila WAMEACHIKA(ninyi mna laana ya Lusifa ila hamjui kuikimbia)
2⃣ Wanaoongoza kwa uzinzi na uasherati waimbaji wenye vi Cd na vi DVD(shida ni nini?)
3⃣Wenye kiburi ni waimbaji(mmemuiga Role model  wenu ibirisi eeh) naye alikuwa mwimbaji hatari.
4⃣Wasiofanya kazi za kuwaingizia vipato ila wanazunguka kanisa hadi kanisa kuimba,kuuuza CD,DVD na kuomba pesa baada ya kuimba eti ya nauli na kutegemezwa ni WAIMBAJI, kwa hiyo huduma imekuwa kitega uchumi? Kafanye kazi za kuwaingizia vipato ndo mtatumika bila kutolea macho kikapu cha sadaka.
👉 *_Ndo maana wengi mnatunga nyimbo za ajabu ajabu,siyo za mwongozo wa Roho mtakatifu,mnatunga za mashabiki_*) Badirika.
👉Nije kwa baba wa huyu mwanamke,sijui kama yeye bado yupo kwenye ndoa,ana mkewe bado au walishaachana,au amekufa,maana hata si msikii mama akitoa kauli kwa mwanae kwamba Rudi kwa mmeo. *_Umri mlio nao kama wazazi hata mpka mkaozesha,mnawajukuu huu ni Umri wa Busara_* yaani ilibidi umfukuze mwanao mwambie karudi kwa mmeo.
👉Eti unamsemelea mkweo kwa mchumgaji eti mkweo HAKUHESHIMU kwa pesa tu ndo hakuheshimu,hujui ndoa ni TAASISI INAYOJITEGEMEA, huna Mamlaka YOYOTE ya kunyoosha mkono wala mdomo kwa Ndoa ya mwanao HATA KIDOGO, sijui imani ya dhehebu lako ni ipi...Biblia imesema MTU ATAMWACHA BABA NA MAMA ATAAMBATANA NA MME WAKE/MME WAKE sasa wee unataka mwanao aambatane nawe?kwani wee ndo mmewe na mme wake ndo mzazi?
👉Umejitafutia Laana baba,maana kinachotenganisha ndoa NI KIFO TU(BIBLIA IMESEMA) sasa wewe ni KIFO?
👉Wazazi ni washauri katika ndoa ya mtoto wao SIYO WAAMUZI, waamuzi ni hao wawili waliooana,nimekerwa na lugha ya (UKIMUOA KWA BAHATI MBAYA),hukupokea Mahari,hukufanya harusi,hata kama walibenana hawakuja kujitambulisha walipokuwa bado wapagani?mzee mbona unaaibisha rika yako na wokovu wako..
👉Unataka mkwe wako Akusikilize,akutii....Maandiko ya wapi,yaani umenyosha mkono umegusa ndoa yake akutii na kukuheshimu TENA AMEKUSTAHI NA AMEOKOKA KWELI ungekutana na Wainjilisti ilibidi Uongozwe sala ya Toba upya na kufundishwa neno la Mungu.
👉Pesa unapanga laki 7 atoe,wee unajua kipato chake,hata ungejua kwani hazina matumizi mengine? Na mwenye jukumu la kuhakikisha pesa inapatikana siyo wewe baba ni ULIMI WA MKE WAKE,kama mke amekuwa Jehuri kisa ka album 1,hata hiyo laki 3 ametoa basi tu kwakuwa ameokoka ila ilibidi hata sh 10 asitoe.Maana huduma inayo bomoa ndoa haipaswi kusapotiwa na watu hata mbingu.
👉Mwisho ni mshauri huyo baba, *_Amwambie mke wake aseme kauli ya mwisho anarudi au harudi,na amuulize baba mkwe wake umeamua kunivunjia ndoa yangu?au unamrudisha mke wangu jibu watakalo toa akubaliane nalo atulie amshukuru Mungu,asimame na Yesu wake huyo mke amemwacha mwenyewe soon huyo mwimbaji mtasikia kaolewa, au ndo walee wanaojiita MADAM( nina somo la Unajiita Madam kumbe kahaba umeshimdwa ndoa tafuta google by Ev Elisha Kazimoto). Wakati ukifika Mungu atakuondolea kikombe hicho mbele huko waweza pewa mke mwingine,ila siyo sasa tulia lea watoto wako_
*_Ukikuwa nami mchambuzi wa masuala ya ndoa na mahusiano, Ev Elisha Kazimoto(MJUMBE MKALI -MITHALI 17:11)_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment