Monday, 10 September 2018

WADADA KUWA SINGLE MOTHER

*Swali: hili limeulizwa lina jibiwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa*
.kumekuwa na wimbi LA mabinti nawaskia wanasema wanataka kuwa single parents, kwba wazae tu watoto wao na wawalee na wasiwe na attachment yoyote ya mume na mke,

1. Je ni kwamba wadada hao hawataki kuolewa
2. Je ni kwamba wanapeda kuolew ila wanaume wanakataa kuwaoa
3. Je wamekosa wa kuwaoa?
4. Je km MTU anahiari kuzaa zao ni kwanini wasiishi pamoja?

Note: walio wengi ni wadada wanaofanya kazi za kuajiriwa au kujiajiri
........................................
*_Ev Elisha Kazimoto,Whatsapp 0755444078_*
*Kwanza hii lugha ya Single Mother ni ya Ushetani,upagani na Ukengeufu*
👉Huu ni uhuni,uasherati wa machukizo kwa Bwana.
👉Unaanzaje kuzaa bila ndoa?, unakusudia kulea mtoto peke yako hivi utamlea katika njia zipi?naye akuwe awe single mother au father? Mungu alikusudia malezi ya baba na mama(mithali 22:6).
👉Suala siyo sababu ya msingi ya kuhitaji kuwa Single mother, shida ni Vijitabia vinavyo chipuka baada ya kuanza kuona Nuru ya Uchumi mzuri na Umaarufu
1⃣Wadada wengi wakisha kuwa na elimu au pesa WANAOTA VIBURI na kujiona wanaweza endesha maisha,hawahitaji kuwa chini ya mtu,wanahitaji uhuru sana,hawahitaji kunyenyekea mtu,(hicho ndo kiburi cha wadada) *_Ndo maana hawataki kuolewa,maana ndoa kanuni yake lazima uwe chini ya mwenzako(mwanamke)_* hutaki kuww chini ya mwenzako Usiolewe.
*_16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Mwanzo 3:16_* wanawake baadhi waliosoma na kuwa na vijisenti hawataki kutawaliwa Wanahitaji watawale kwakuwa wamepata pesa au umaarufu.
👉Angalia wimbi kubwa la *Wadada/Wamama WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI,angalia niwangapi wapo kwenye ndoa,wangapi wanahitaji ndoa,wangapi WAMEWAACHA WAUME ZAO na kuwa Single mother na kujiita MADAM....,hawa watu hawajawahi kuokoka ila WALIOKOKESHWA na mazingira,ila ukija kufatilia kiundani, ni KIBURI kwa waume zao,hawahitaji kutawaliwa,kupangiwa ratiba, wanahitaji waende sawa sawa na umaarufu wao* Wengi waimbaji wanajiita Madam,Single mother, ila ni Vijitabia vyao ndo vimewapelekea kuachika,SIYO USUMBUFU WA WANAUME ila wao ndo wasumbufu. _Hivi wanaume wa waimbaji wote wa nyimbo za injili ndo wasumbufu tu_‼kama hawajaachika,wana mgogoro mkubwa wa ndoa. (Hapa kunahitajika tafakari kubwa siyo kurusha mpira kwa mtu)
👉 *_Ndoa niya watu wawili wenye Akili Timamu_* akisha patikana mmoja mwenye kichaa,inabidi mmoja aongeze uwezo zaidi mara mbili ya mwanzo ili kutuliza kichaa cha mmoja.
2⃣Si kwamba Wanaume wa kuwaoa hawapo wanaume wapo wengi, *Ila wanaume wa kuoa wadada wa type ya tabia zao hawapo* Labda kuwasaidia wadada,wanaume hawaoi Sura,wala shape,wala elimu yako na pesa, wanaoa Mke anayefaa kuishi naye wakatimiza ndoto zao za maisha. Sasa mtu wa kutimiza ndoto za mwenzake lazima awe amejipanga kwa NIDHAMU(Awe na akili timamu)ya kutotanguliza maslahi yake ila ya mwenzake.
3⃣Wanaokubali kuzaa nao hawawezi kuwa walezi, *Mnapaswa kujua kuna watu wanafaa kwa Sex ila si kwa Ndoa, na wengine wanafaa Kwa ndoa ila si sex* ( _Mpaka utafakari sana ndo uelewe sentensi hii ya kisaikolojia_). Kwa hiyo wanaume hawazai nao kwasababu wanahitaji kulea watoto nao ila kwasababu Wanaweza kutimiza Tamaa zao za sex za muda mfupi bure bila kuonga ila kuongwa.
*_Nihitimishe kuwa, wadada wenye mawazo haya na wale mlojichomoa kwa waume zenu mna Laana kubwa ya Matumbo yenu,hampaswi kuwaza kuzaa wala kulea watoto Hamna Maadili ya Kulea_* Msituharibie kizazi cha kesho Rudini kwa Mungu Mfuate neno la Mungu kama mmeamua Kuokoka, kama hamkuamua kuokoka basi jivueni hilo jina la ULOKOLE.
_By Ev Elisha Kazimoto(Mjumbe Mkali - Mithali 17:11)_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto.

No comments:

Post a Comment