❣❣ *NJIA YA KUJIBIWA MCHUMBA*❣❣
*_Swali limeulizwa hapa chini,na Anajibu Mwanasaikolojia na mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078
......
......
*Kuna swali lilitaka kujua njia zipi Mungu anaweza tumia kumjibu mtu aliyeomba mke au mme*
👉Kwanza,hapa tuwekane sawa watu wote vijana kwa mabinti. *_Vijana wengi wanapenda kujibiwa na Mungu wakati wakitafuta mchumba,labda niwape Experience ya kiroho, Suala la Mungu kutumia njia yoyote kumjibu mtu Linategemea Mahusiano ya Kiroho aliyo nayo yeye na Mungu_* si kwa sababu umeamua kufunga na kuomba siku 21 eti unamshawishi Mungu akujibu unaweza ukaenda hata 40 na Usijibiwe au usijue kama umejibiwa na Mungu.
👉Shida ni kwamba vijana wengi wakati wa maisha yao ya kawaida kabla ya kuingia katika uhitaji mkubwa wa ndoa wanakuwa hawana mpango na Mungu,hawana maombi,hawana utakatifu,hawafanyi kazi ya Mungu kwa bidii, ila uhitaji ukiingia ndo wanaanza kubadiri gia ya kumshawishi Mungu,sasa mara nyingi Mungu Hafanyiwi maigizo kama wanadamu inabidi kama ni maombi yawe ndo maisha yako,utakatifu uwe ndo maisha yako,kutumika iwe ndo maisha yako.
*_Biblia imeweka wazi Nature ya Mungu,ukiwa na maisha ya kumpotezea Mungu wakati hauna shida,ukifika wakati wa shida yako naye atakupotezea_* Hujawai kufunga kuombea kanisa,kazi ya Mungu,maisha yako ya kiroho na kujua namna gani Mungu anajibu unasubiri *Kufunga wakati wa Kutafuta mke au mme* Unahisi utajibiwaje?
24 Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;
Mithali 1:24
25 Bali mmebatilisha shauri langu, Wala hamkutaka maonyo yangu;
Mithali 1:25
26 Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;
Mithali 1:26
27 Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.
Mithali 1:27
28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione.
Mithali 1:28
👆Kijana unahitaji kujipanga mapema sana kuwa na tabia ya kuwasiliana na Mungu ili kujua *_Wewe kama wewe Mungu anapendelea kukujibu kwa njia gani?_* kila mmoja ana njia kubwa,lango la kuongelea na Mungu,kupokea taarifa za Mungu.
👉 Ila vijana wengi wamekalili kuwa njia ya *_Kuonyeshwa mke au mme ni NDOTO/MAONO_* ndo lugha za vijana karibu wote Utasikia NIKAOTA,NIMEONYESHWA hii njia shetani ameisha wachungulia wengi amewapiga kwa wake bandia na waume bandia kwa KUITA NDOTO.
👉Mungu anazo njia nyingi za kusema na watu wake kuwajulisha,kuwapa taarifa ya kinachoendelea au kujibu maombi yako, JAMBO KUBWA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU YAKOJE mpaka Akuheshimu na Kukujibu? Mungu hatumii njia moja ziko nyingi.
14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
Ayubu 33:14
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
Ayubu 33:15
16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
Ayubu 33:16
17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;
Ayubu 33:17
👆Usikalili jiweke katika Position ya kumsikia Mungu kwa njia nyingi ila Ukimzoea Mungu atakupa YOUR CHANNEL (Njia yako maalumu)yakumsikia.
1⃣Mungu anaweza tumia watu kukupa jibu lako(watu wakawaida)unahutaji kuwa na maarifa ya kiroho na macho na masikio ya kiroho kujua huyu mtu katumiwa na Mungu kunijibu ombi langu hata yeye bila kujua.
2⃣Mungu anaweza tumia Watumishi wake(Wahudumu wa Madhabahuni)wakapewa jibu lako wazi au wakatumiwa bila kujua.
3⃣Mungu anaweza tumia Amani ya Moyo juu ya mtu au jambo(kuiruhusu amani au kuifunga amani)uwe makini kuielewa amani ya Mungu na amani ya nafsi yako(Amani ya Mungu haina conditions za matamanio)
4⃣Mungu anaweza tumia Neno lake kukupa mwanga sifa,na njia ya majibu yako.
5⃣Mungu anaweza tumia Maono kukujibu(maono huwa wazi na clear)
6⃣Mungu anaweza kutumia Ndoto kukujibu(ndoto zinakuwa na mafumbo flani unaitaji kuomba zaidi kujua tafsiri yake.
_Hizo ni baadhi ya njia unazoweza pewa jibu lako,njia zote zinahitaji uwe vizuri na Mungu na ujizoeze kumsikiliza Mungu_
*Ulikuwa nami katika uchambuzi Mwanasaikolojia na mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
No comments:
Post a Comment