🎾SOMO: *UJENGE MOYO WAKO NA NAFSI YAKO KATIKA UWEZO WA KUTO YUMBISHWA NA TUFANI YOYOTE*🎾
_By Ev Elisha Kazimoto(whatsapp 0755444078)_
🎁 *_Utangulizi Wa Somo_*🎁
*28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Mathayo 11:28*
🥦Kwenye andiko hili kuna mambo ya kuzingatia kama 4,ambayo yatakusaidia kama mwamini wa Yesu Kristo Kuujenga Moyo wako na Nafsi yako.
🥦Hapa kuna mwito wa Yesu kwa watu wote( walio nje na walio ndani ya Kanisa)
🥦wanaoitwa na wale wenye kusumbuka,wenye masumbufu maishani mwao
🥦Kundi lingine ni wale waliolemewa na Mizigo(mizigo ya aina yote)
🥦Lakini pia kuna jibu la Yesu au Suluhisho la Yesu ni kuwapumzisha.
*_Sasa kwa mujibu wa andiko hili Mizigo siyo dhambi tu,au magonjwa tu, hapa mizigo ni Hali zote,zilizoongezwa kwenye maisha yako ambazo Hukuumbiwa na Mungu,chochote kinacho Athiri amani yako alokuumbia Mungu ni mzigo_*
🎁KUNA MAENEO MATATU YANAYO HUSIKA NA KUBEBA MIZIGO HIYO KATIKA MAISHA YA MWANADAMU🎁
1⃣ *MOYO* ni kiti cha mizigo yote ya Maamuzi mabaya. Matendo yote yasiyo ya haki,yaletayo hatia, matendo yote yanayolenga kuumiza mtu, matendo ya kutendewa kinyume na matarajio yako ni *Mzigo wa Moyo*.
20 ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.
1 Yohana 3:20
21 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;
1 Yohana 3:21
👉👆Kuna watu usema moyo unaniuma,mapigo ya moyo yanaenda kwa kasi,pressure,kifua kubana,kutenda mambo kwa Hasira,kuzira na kununa ni matokeo ya Moyo kubeba Mizigo Isiyo stahili.
2⃣ *AKILI/NAFSI* Hiki ni kiti cha kubeba mizigo yote inayotoka kwenye mazingira kwa kuona au kusikia mambo magumu yasiyo na majibu kwa muda huo unao hitaji majibu. *_Ni mawazo Makali yasiyoonyesha mlango wa kutokea_*
🎁👆 Kuna watu anasema kichwa kinauma bila ugonjwa,kichwa kizito,macho yanauka,machozi yanalengalenga,hasira kwenye uso,majibu makali naya mkato,kutukana na kizunguzungu, hayo ni matokeo ya *Akili/Nafsi kubeba jambo lisilo na Majibu wakati huo unaohitaji majibu*
20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.
Marko 10:20
21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Marko 10:21
22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Marko 10:22
🎁👆Akili ikikosa majibu inatoa picha nje haraka kwenye uso kuwa hapa majibu hakuna kwa muda huu,ni baada ya kusikia inapelekea mzigo wa akili.
3⃣ *MWILI* Hiki ni kiti cha mizigo itokanayo na hali ya hewa,vita ya kiroho,au changamoto za dunia.
🎁👆Kuna watu anasema Mwili wangu hauko vizuri,naumwa,hauko kawaida,sijui nimekuwaje,au anakuonyesha Jeraha la mwili,au anajiona mnyonge sana,wa chini,hafai kati ya watu, hayo yote ni matokeo ya Mizigo itokayo katika mazingira,adui kama wachawi na mapepo juu ya mwili wake.
3 Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu.
Ayubu 2:3
4 Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
Ayubu 2:4
5 Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.
Ayubu 2:5
🥦Kwa mtazamo wa hapo juu,utagundua *Kila mwanadamu aliye duniani,ana mizigo,awe kanisani au nje ya kanisa ila tunatofautiana aina ya mizigo, kuna mizigo inayokuumiza ila Haikuzuii uzima wa milele,japo yaweza kukukwamisha,na kuna mizigo ambayo inakuzuia moja kwa moja kumuona Mungu* Hapa ndo utaona umuhimu wa Kanisa na watumishi wa Mungu.
🥦Kanisa ni Mahali ambapo tunakuja Kutuliwa mizigo yetu yote, na Neno la Mungu ndilo nyenzo ya kutua mizigo ya watu.
🥦Kwa kadri unavyosikia au nenwa Neno la Kristo,katika uimbaji,kuabudu,kusifu mahubiri vikimnena YESU KRISTO automatically mizigo yako inashushwa, na kwa Kadri yakinenwa matatizo,watu mizigo inaongezeka.
🥦Na hapa ndo Mtihani na Huku kwa wasimamao madhabahuni pa Bwana,mwimbaji,mwombaji,muhubiri Yesu Asikike sana kuliko hali,vitu na maisha. Mizigo itatuliwa.
*_Msingi wa Somo_*
👉 _Maisha ya wokovu ni safari yenye mwanzo wa safari na mwisho wa safari._ *Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu; Wafilipi 1:6*
👉Na mfumo wa safari ya wokovu kuna vituo rasmi na vituo visivyo rasmi, kila kituo kina mchango wake katika safari yako. ( *_Vipo vituo vya kupumzika na kustarehe,vituo vya uchungu, vituo vya kujifunza, vituo vya kukatisha tamaa,na vituo vya kutiwa moyo na nguvu_* vyote vipo katika safari yako moja ya wokovu.)
*58 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana. 1 Wakorintho 15:58*
👉Uwezo wa kutambua utofauti wa vituo katika safari,ndiyo nguvu yako ya kufika mwisho wa safari yako salama.
20 Bwana akasema, Mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwa;
Hesabu-Numbers 14:20
21 lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa Bwana;
Hesabu-Numbers 14:21
22 kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu;
Hesabu-Numbers 14:22
23 hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona;
Hesabu-Numbers 14:23
24 lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na uzao wake wataimiliki.
Hesabu-Numbers 14:24
*KIINI CHA SOMO*
*_4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.Yakobo 3:4_*
👉 _Katika somo letu kuna mambo muhimu kama 5 unapaswa kuya fahamu vema ili somo hili liwe baraka na nguvu na ufunguo wa maisha yako ya kiroho na kimwili_
1⃣Kujenga moyo wako.
2⃣Kujenga Nafsi yako
3⃣Uwezo
4⃣Kuto yumbishwa
5⃣Tufani yoyote
👉 *Kujenga Moyo wako* ni kuuzoeza moyo wako ambao ni Kisima cha Maamuzi, Kujua kuwa Mfumo wa maisha yako Unaratibiwa na Mungu na si Mazingira wala Mtu yeyote na kwa maana hiyo *Hakuna mwenye uwezo wa kubadiri Hatima yako* iliyopangwa na Mungu.
*23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. Mithali 4:23*
👉 *Kujenga Nafsi yako* Ni Kuizoeza Akili yako ambayo ni Lango(barabara) ya Matukio yote yatokayo katika milango mitano ya fahamu kuupelekea moyo ufanye maamuzi,kujua yakuwa Si kila Tukio uonalo lina Maana, Si kila sauti(maneno)usikiayo yote yanakufaa wewe,sikila hisia zikujiazo ni sahihi bali Kila jambo lina maana yake kwa muda wake CHAMBUA LA KUKUFAA.
*3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo 2 Wakorintho 11:3*
👉 *Uwezo* ni Nguvu ya kubeba mazito yanayokulemea moyoni na akilini na ukaonekana hukubeba kitu,pia ni nguvu ya kufanikisha lengo lako katika vikwazo vingi, nguvu inayo kusaidia kunyamaza wakati unatakiwa kusema, na kusema wakati unatakiwa kunyamaza( *Huo ndio Uwezo*)
1 Mara kulipokuwa asubuhi wakuu wa makuhani walifanya shauri pamoja na wazee na waandishi na baraza nzima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta mbele ya Pilato.
Marko 15:1
2 Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu, akamwambia, Wewe wasema.
Marko 15:2
3 Nao wakuu wa makuhani walikuwa wakimshitaki mambo mengi.
Marko 15:3
4 Pilato akamwuliza tena akisema, Hujibu neno? Tazama ni mambo mangapi wanayokushitaki!
Marko 15:4
5 Wala Yesu hakujibu neno tena, hata Pilato akastaajabu.
Marko 15:5
👉 *Kutoyumbishwa* Ni namna unavyozidi kukaa katika Tumaini,Imani yako,lengo lako pindi inapotokea chamgamoto za kiroho au kimwili,au kimazingira za kukutoa katika Njia yako.( *To Stay Focused No Matter what circumstances come across*) huko ndo kutoyumbishwa.
👉 *Tufani yoyote* Tufani ni chamgamoto,vikwazo,hali ya kukatisha tamaa,hali ya kuleta uzuni, vitu vyote vinavyo tishia Hali yako ya uthabiti na kufanikiwa na kusonga mbele ni *Tufani* Usiyumbishwe.
31 Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua.
Luka 13:31
32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
Luka 13:32
👉 *_Kutoyumbishwa siyo kiburi,siyo dharau ni uwezo wa kupangua hoja dhaifu zinazo lenga kukudhahofisha utoke kwenye lengo la tumaini la wito wako_*
👉Sasa waweza kujua na kuona wapi tunaelekea katika somo letu na sasa utakuwa na hamu ya kusogea hatua nyingine ili uwe hodari katika maisha yako ya kiroho na kimwili. _Andiko letu kuu tulisome ili tuanze uchambuzi_
*4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.Yakobo 3:4*
👉Yakobo kuna kitu kikubwa hapa anajaribu kukifunua na kutupa ufunuo mpya kupitia chombo( *Merikebu, Usukani na Bahari na mawimbi yake na Nahodha*) hapa kuna siri kubwa ya maisha ya kiroho ukielewa itakusaidia sana.
👉 *Naodha* ndiye mwenye nia na lengo la safari yake inaanzia wapi na kuishia wapi. ( _Nahodha ni wewe mtu wa Mungu_)
👉 *Merikebu* ni chombo kinacho beba abiria(watu)ambao imewapasa kutoka eneo moja kwenda lingine( _Chombo ni Wokovu wako_) na abiria ni mfumo wako wa maisha kama( Ndoa,uchumi,afya,elimu,huduma,nk)ambayo vipo kwenye Merikebu kubwa ya wokovu inabidi vifike salama mwisho wa safari yako Nahodha.
👉 *Usukani* _Uwezo wako_ wa Kiroho na Kiakili wa kuratibu mambo,kusikiliza,kuona,kuhisi na Ukayatolea maamuzi kwa kadri ya Nia yako,imani yako mbele za Mungu bila Kubadirishwa na Mazingira,watu,hali ili ufike uliko kusudia,uishi sawa sawa na ulivyo kusudia.
👉 *Bahari* ni ulimwengu huu ambao tunaishi wenye *Mawimbi* maudhi,vikwazo,changamoto nyingi.... Laini *_Nahodha anakokusudia kwenda anakwenda_* pamoja na misukosuko yote ya mawimbi,merikebu haifuati mawimbi ila inafuata Usukani ulioshikiliwa na Nahodha mwenye lengo la Merikebu inaenda wapi.
👉Katika safari yoyote ya kimaisha,ili usiharishe safari au kwenda mwelekeo ambao *Hukukusudia kwenda* tambua kuwa *_Si kila anayekuona kwenye safari anajua ulianzaje safari,nia ya kusafiri ni ipi, unasafiri na nini(ulivyo beba)na unaelekea wapi mwisho wako_* hivyo huna haja ya kupambana na msafiri mwenzako,kudharau,au kumuona kawaida, unamjua ni msafiri kwenye gari moja ila hujui ni nani katika safari hiyo,umuhimu wake kwako na anaishia wapi.
👉 Abiria wengine *Ni wezi, wengine wana uwezo na taaluma ya Uokoaji pale chombo kinazama,wengine ni wabishi na wakorofi,wengine ni watu wema tu* hao wote ili ufike salama lazima ujue kucheza kwenye maeneo yao kulingana na hali zao.
👉 Kwa *Abiria wezi* tunza mizigo yako vizuri(na nena kwa habari ya mambo ya kiroho)
👉Kwa *Abiria wakorofi na wabishi* Kaa Kimya Usijibu hoja zao, utaharibu Radha ya safari yako na utaonekana nawe ni mpumbavu kama alivyo mpumbavu. ( *_Watu Dhaifu ujibu kila Neno, watu Hodari Unyamaza ili kupata hekima ya Kujibu sahihi_*) Kanuni hii usipo ijua kiroho utakuwa mtu wa Kurudi nyuma kiimani kila mara.
👉 Kwa *Abiria wenye uzoefu wa uokoaji* Huwezi kuwajua mpaka itokee dhoruba na upate matatizo ya kuzama na wakuokoe katika kuzama( _Kwa maana hiyo hapo Unahitaji kutengeneza sura ya amani kwa kila mmoja,usiwe Kero kwa abiria wenzako safarini,maana nani wa kukuokoa humjui_) wezi hawajulikani,na waokokaji hawajulikani ila wakorofi na wabishi hujionyesha kwa maneno yao ndani ya merikebu.
48 Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?
Luka 22:48
49 Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotukia, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga?
Luka 22:49
50 Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume.
Luka 22:50
51 Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya.
Luka 22:51
👉 Kwa *Abiria waungwana* kaa nao kwa sura ya uungwana maana hao ndiyo wanaoifanya safari yako Usiboreke.( *_hawa hawanaga muda na mambo ya watu,wao wanamuda na mambo yao,hata itokee nini wao kimyaa safari iende hadi mwisho_*
👉Unapaswa kujua anayejua *Thamani ya safari yako,na mizigo muhimu uloibeba ni wewe mwenyewe* wala si Abiria mwingine, ndo maana Abiria aweza kukanya mzigo wako,begi lako ili avuke apite atoke nje,maana hajui ukicho beba, yeye anaona ni gunia,au begi tu la kawaida, wewe huoni begi, *Unaona vitu vya thamani na muhimu ulivyo beba* Unaangaika kulikwepesha begi lisikanyagwe au kurushwa rushwa Ovyo.( *_Thamani ya wokovu wako na huduma yako, maisha yako unaijua wewe,kwepesha kwepesha wasiojali wasikanyage au kurusha rusha ovyo_*)
17 Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu.
2 Petro 3:17
18 Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
2 Petro 3:18
*ILI USIENDELEE KUYUMBISHWA KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU NA MAISHA JIULIZE MASWALI HAYA*
1⃣ Kwa nini nilianza safari hii?(huwezi ishia njiani au kupotezwa njia na wapuuzi kama unajua Lengo la kuanza safari hiyo na umuhimu wa kule uendako)
2⃣Nimeanza safari na nani? (hapa utajua safari inakuhusu wewe na si watu wengine) hii itakulinda usikatishwe tamaa na abiria waendao karibu hawafiki mwisho wa safari
3⃣Jiulize abiria wote ni kama mimi? (utajua kuwa abiria wanatofautiana sana pamoja nakuwa gari moja ila tabia ni tofauti) Hii itakusaidia usiangaike na abiria na kuumiza kichwa na tabia zao safarini angaika na uwezekano wako wa kufika salama(Vumilia maudhi niya muda, wengine wanaishia njiani,wengine wanapita kwenda kaa nyuma kabisa mbali nawe)
👉Jambo muhimu na la pekee ni muhimu kujua *Tumaini /lengo la wito wetu, halibadirishwi na mazingira,au kelele za watu tunaosafiri nao, bali tumaini letu linabatilika kwa maamuzi yetu wenyewe ya kukubali kukata tamaa na kurudi nyuma*
25 Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika.
Mithali 3:25
Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.
Mithali 3:26
Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika.
Mithali 23:18
👉Uongoze moyo wako( *wewe mwenyewe*) usiruhusu mazingira au mtu mwingine nje na Bwana na neno lako wauongoze watakavyo wao utaishia njiani.
19 Sikia, mwanangu, uwe na hekima, Na kuuongoza moyo wako katika njia njema.
Mithali 23:19
Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika.
Mithali 24:14.
*_Nimalize kwa kusema hivi, katika maisha ya kiroho au ya kimwili kuna vitu viwili au vitatu vikuu vyenye uwezo mkubwa wa Kuathiri Maisha yako yote mpaka unaondoka duniani_*
1⃣ *Adaptation*
2⃣ *Revolution*
3⃣ *Unique*
👉 *Adaptation* You lose your characters, Qualities then you absorb of other people( _Yaani unapoteza sifa zako na tabia zako unaanza kuishi za wengine_) Kuwa makini na adaptation inaweza kukugharimu pale itakapo hitajika uhalisia wako wewe kama wewe na si wa mazingira kutatua changamoto mbele yako.
👉 *Revolution* Ambition,and struggle to change the existing system to follow your perception /desires ( _Yaani unafanya harakati na unatamani ugeuze mazingira au watu wawe kama wewe au upendavyo_) Hii ni nzuri sana ila hakikisha ulivyo unafaa mazingira yote na rika zote na hali zote na wewe una vitu muhimu vya kusaidia wengine. Ila utatumia nguvu kubwa sana na unaweza umia na kupiteza baadhi ya vitu vyako muhimu.
👉 *Unique* To be distinguished from other people, to possess your own characters.( _Yaani maisha ya upekee sawa sawa na ulivyoumbwa,ulivyo chagua uwe sawa sawa na Nature yako_) Hii itakusaidia usigongane na watu,usiwe na stress utaenjoy maisha yako..
*_Imeandaliwa na Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078
No comments:
Post a Comment