🥦🥦 *HUU NDIYO UZURI WA MUNGU WETU KWETU*🥦🥦
*_Imeandaliwa na Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
*NEW MONTH NOVEMBER 1.209*
................................................
*_Tafakari ya Leo_*
_Shalom wana wa Mungu aliye hai. Leo ni tarehe 1.11.2019 ni mwanzo wa mwezi katika siku ya kwanza,nakutafakarisha uzuri wa Bwana_
*(21)Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini.(22)Ni huruma za Bwana hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.(23)Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.Maombolezo 3:21-23*
🥦Katika andiko hili, mstari (21)... Kuna jambo la kujifunza na kupata nguvu ya kuendelea mbele katika safari ya kuelekea mwisho wa Mwaka. Hapa yako mambo makuu 2.
1⃣Anasema _Najikumbusha Neno hili....._ Nimuhimu sana katika maisha kuwa na tafakari juu ya *Uliko Toka* Kujikumbusha, kwa lugha nyingine ni *Kurejea nyuma uliko pita, au kurudisha kumbukumbu za kilicho semwa,onwa* Vipi mpendwa Ukirejea nyuma uliko toka tangu tarehe 1.1.2019,unaona nini? Kama mpaka sasa upo ila unataarifa za watu wengi ambao mpaka sasa hatunao duniani,wengine ni wapendwa wetu wa karibu.... Hii Haikupi kuona kwamba *Bado Bwana ana Haja nawe Duniani?* Pamoja na Changamoto ngumu ulizopitia na tunazopitia lakini Uhai bado upo ndani yetu na Uhai ndo Injini ya Mabadiriko ya Maisha.
👉Jikumbushe ulivyo ponywa na Ajali ile mbaya, jikumbushe ulivyo pita kwenye lile pito zito mpaka ukakata tamaa, Lakini Ulipita, *Huo ndo uzuri wa Bwana*
👉Jikumbushe neno hili, Bwana wetu alivyosema *Sitakuacha wala kukupungukia* jitie nguvu sasa katika mwanzo mpya wa mwezi huu.
🥦Katika Mstari huo huo wa 21b, anasema _Kwa hiyo Nitatumaini_ Ukijikumbusha wema wa Mungu kwako, hutakuwa na Sababu ya *Kukata tamaa* na kuona kama Mungu amekuacha, aliye tenda yale ndo atatenda na *Hili* kwahiyo NITATUMAINI.
2⃣Katika mstari wa (22), amesema..... _Ni huruma za Bwana Hatuangamii_, Hakika ukikaa ukatafakari utajua ni Huruma tu za Bwana, adui ibirisi,mawakala wake wana lenga kila siku *Tuangamie* na wakati mwingine wanataka watumie nafasi ya *Udhaifu wetu* kutuangamiza ila HURUMA ZA BWANA zina tukinga.
_Hali halisi kwenye ulimwengu wa Roho kwako ni hii_
*13 Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana akanisaidia. Zaburi 118:13*
👉Kila siku, kila saa,kila dakika wapo *Wakusukumao sana* ili uanguke,lakini kwa nini hata sasa umesimama(Kiuchumi,kiafya,kindoa,kimahusiano,kieleimu,Kikazi,kihuduma nk) Ni *Huruma za Bwana* wakitusukuma anatusaidia kusimama.
🥦Tunaweza kuendelea kufurahia maisha ya kila siku,ni kwasababu tu *_Rehema za Mungu Hazikomi_* Na huo ndo usalama wetu, Rehema ni kiwango cha juu cha Kusamehewa na kuhurumiwa wakati ulikuwa unastahili adhabu.
3⃣Katika Mstari wa (23).... _Amesema, Ni Mpya Kila Siku Asubuhi_, tunatembelea kwenye mambo mapya ya Mungu, kawaida ya Mungu kwetu siyo *Kutulisha Viporo vya Jana* anatuandalia mambo mapya kila siku asubuhi.
🥦Kwa lugha hiyo walio cheka jana yako wata shangaa leo yako na kesho yako.... Maana utakuja na *Mambo mapya* yanayo toka kwa Mungu wetu. ( _Huu ndo uzuri wa Mungu_)
🥦Halafu anasema, _Uaminifu wake Mungu ni mkuu_, Hapa ndo huwa mioyo yetu inatulia kwa Bwana, yeye ni mwaminifu akiahidi atatenda,kazi yetu ni kumwamini na kuvumilia.
👉Huna sababu ya kumwacha Bwana, kuacha kumtumikia, kukatishwa tamaa na watu au mazingira, Uaminifu wa Bwana ni Mkuu,kiwango chake cha Kutimiza alicho sema ni cha Juu na Uhakika ndo maana yake.
_Unajua nini? Tumeanza mwezi huu na Bwana nao utaisha, Usiogope wala usiogopeshwe, ni mwisho wa Mwaka Utasafiri utatoka nyumbani salama na utafika uendako salama, Kafara za waovu Hazikuhusu wewe, sisi tunalindwa na Nguvu za Mungu kwanjia ya Imani( *1Petro 1:5*), Ni kweli mwisho wa Mwaka kuna matukio mengi ya Mauti na Ajali,Sema Hazinihusu mimi,wewe umeahidiwa na Mungu kwamba Bwana atakulinda na Mabaya Yote, tena atakulinda Utokapo na atakulinda Uingiapo ( *Zaburi 121:7-8*) Huna haja ya Kuogopa Tena_
Hii ndiyo Tafakari yetu leo katika mwanzo wa Mwezi huu wa 11,kwa kuwa ni Neno la Bwana, Litakufaa Leo,mwezi kesho na mwakani kila siku litakuwa jipya.
*_Ulikuwa nami Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto( WhatsApp 0755444078, Facebook Elisha Kazimoto)_*
©2019
Thursday, 31 October 2019
UZURI WA MUNGU KWETU NEW MONTH
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment