Tuesday, 10 December 2019

HARUFU YA ZINAA KUWA MAKINI

🖤🖤  *HARUFU YA ZINAA MAHUSIANO MTANDAONI*🖤🖤
mada..!
Dada kapata mchumba kwenye magroup ya kanisani,wakaanza mahusiano ambapo dada yuko mkoa mwngn na kaka kwingne,mahusiano yameenda kama miezi minne iv,dada kamwambia mkaka ingefaa vizur waonane ili wafahamiane vizuri, kaka akasema hana nafac kaz zimebana,akamwambia mdada yeye ndo aende anakoishi mkaka.dada akamuuliza ni salama huko wacje wakaanguka dhambin kaka akamjibu hamna shida watalala tu pamoja wala hawatafanya chochote kwani dhambi ni tendo lenyewe watafanya romance tu sasa dada bado ana hofu afanyeje?
.............................................
_Anajibu Mtumishi wa Mungu na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Kiroho na Kisaikolojia *Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist )_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
...................
...................
*_Wewe Msomaji wangu naomba usome taratibu swali la dada huyu halafu ufatilie majibu yangu hapa chini....Uone kazi kubwa tuliyo nayo kama watumishi wa Mungu,na kanisa la siku za mwisho lakini zama hizi za sicial media katika kuelekea ndoa Takatifu, wadada kaa macho,vijaa kaa macho wale mnao mpenda Mungu na mnao tamani ndoa safi na takatifu_*(KARIBU UPATE MAARIFA)

*Asomaye na Afahamu...*
👉Kuna mambo hapa ni yaainishe ya kiroho na kisaikolojia tuweze kuwajua hawa watu 2 vizuri ili kumsaidia mdada aliyeomba msaada.
1.Kuna mambo wadada au wakaka wanahitaji kuongeza umakini sanaaa katika nyakati hizi za mwisho na za mitandao ya kijamii katika kutafuta wenzi. *Ongeza umakini sanaa*
2.Kwenye magroup haya yote ya watu wa kanisani na mchanganyiko Si wote narudia *Si wote wanaochati kipendwa,kiwokovu wanauishi Wokovu* kuna watu ukikatisha mbele yao tu,hata akija inbox ukamtega atatiririka lugha za ngono tupu.
👉Tuna wahuni wengi mitandaoni wanaoitwa Sex Hunter wanatafuta wasichana kwa ghara zozote za kujivika vazi la upendwa na kutumia lugha nzuri ya upendwa kwa mateso makubwa ila wakitafuta angalau anase 1...Vivyo hivyo na mabinti wapo wanaowinda wavulana. *Ongeza umakini sanaaa kwenye social media*
Sasa angalia sifa za kijana huyu binti aamue ila mimi namfungua macho kiroho na kisaikolojia.
1⃣Anataka achumbie mdada,anasema hana MUDA....Wa kwenda kuonana na binti ila binti aende kwa kijana( *_Sentensi hii kisaikolojia,inamaana kubwa ni kwamba kijana hajampenda binti kiviiile na hana mpango wa kumuoa ila anataka Amuonje tu waachane hiyo moja, mbili anataka atengeneze mazingira ya binti kujichumbia ila si kuchumbiwa, tatu anataka kujiondoa kwenye lawama kwa lolote litakalo tokea la kumuumiza binti aje aseme wala mimi sikukufuata ulinifuata mwenyewe,nne anahitaji amfanye mdada ndo awe mtumwa wa mahusiano na si kijana_*) Ila kiroho lugha hii inaonyesha kijana Hajawa na mzigo wa Kimungu wa kuchumbia. 
👉Jamani mtafutaji anatoaga masharti! Hana nafasi yeye ni Kofuri ya mlango wa kazini? Si asubiri akipata likizo haraka ya nini,yaani siku zote 7 per 30days za mwezi yupo kazini hawezi omba hata ruhusa ya dharula ya siku 2 jmos na j2. Huyu tapeli mkubwa anataka *Kutuharibia na kutuumizia binti yetu*
2⃣Ameulizwa sentensi Muhimu sana ya kiroho na kisaikolojia..... *Salama huko?* hii sentensi kwa muulizaji kama anaufahamu mkubwa wa kiroho na kisaikolojia inamtosha kabisa *KUJUA MUOAJI,TAPELI,MCHA MUNGU* Ahiitaji kujibu majibu rahisi ukishaulizwa sentensi hii.... Najua binti aliiuliza kawaida,ila Wanasaikolojia na Watumishi wa Mungu tunaitafsiri katika Level Ukomavu wa Kiroho na kisakkolojia.
👉Kwa lugha hii unataka kujua mambo ya fuatayo.
1.Kijana anamweshimuje Mungu( *Kwa huyu ni Zero*)
2.Kijana anajiheshimuje( *Huyu zero*)
3.Kijana anakweshimuje mchumba mtarajiwa( *huyu ni bellow 5%*)
4.Kijana anatabia gani kwenye mahusiano( *Huyu ni mpenda ngono sana na si mwaminifu*)
5.Kijana anaweza jizuia kihisia kama uko naye?( *Huyu anakurarua mara moja*)
Huyu dada alimuuliza swali gumu sna ila linasomeka kiwepesi..... *Sasa nikupeleke kwenye majibu ya kijana ndo utajua huyu ni Tapeli la mapenzi hasa na halijawahi Okoka,kama anahisi utani Akajaribu ila aende amejiandaa kumwacha Yesu mkoa ule,wilaya ile,chumba kile na ajiandaye kutoka kule akiwa mke wa mtu na mimba juu akienda kwenye simu za hatari na ajiandae Kusalitiwa*
👉Kijana anasema njoo tu.... *Hatutafanya chochote* (Kujibu hivyo tu inaonyesha ulivyo jiandaa kwa sex) *Mwenye akili angesema karibu,nilikuwa nawaza ufikie kwa dada flani mpendwa kanisani,au kwa mchungaji,au kwa mzee wa kanisa, ngoja nitafiti wapi patakuwa pazuri kiusalama zaidi)
👉Kijana anasema *Tutalala Pamoja* Dah hivi kama hujazoea ngono hii lugha unawezaje mwambia binti ambaye humfahamu,ndo mnataka mfahamiane,muanze mahusiano au msianze? Huu ni ujasiri wa MZINIFU TU. ( Hivi mtu aliye okoka,amelelewa kimaadili unaweza mwambia jinsia tofauti na yako TUTALALA PAMOJA!(mpaka hapo umeisha mpa taarifa ya nini Kitaendelea)
👉Kijana anasema *Tuta Romance tu* ( Hii ni lugha ya mtu aliyezoea kuchezea mabinti sana na amezoea ngono,anajua kazi ya Romance nikuamsha hisia za ngono,HUWEZI KU ROMANCE MDADA,NA RUDIA KUROMANCE MDADA MKO WAWILI,CHUMBANI,KITANDANI,MDADA HATA KAMA NI NABII,NI AMEOKOKA MPAKA KUCHA IKAOKOKA, ASIKUOMBE UMALIZIE NA SEX LABDA KAMA MALAIKA AMSHIKIE PANGA ALIONE NA AKAE KATIKATI YAO.
👉 Na kijana uwezi romance mdada ukamwacha,akigoma utalia machozi beseni zima mpaka dada atakuhurumia atakupa tu(kijana anatamani kwa macho,mdada kumgusa,romance ataitamani sex mpaka basi)
*_Hivi jaman tufike hatua tuwe na akili komavu,hivi unasema tutalala pamoja,hatutafanya chochote ila tuta romance tu,hivi mtalala kila mtu amevaa majinzi?au mnachojoa nguo? Hivi mnalala hamjawahi fahamiana ndo mmeitana muoanane live ili ikiwezekana mchumbiane au muishie hapo,sasa mnalala wote kwa sura ipi?mmependana au mmeamua kujiozesha_*
MWISHO: IKIMBIE ZINAA,SI MSHAURI DADA HUYU HATA KUENDELEA NA MAWASILIANO NA KIJANA HUYU ANAMPOTEZEA MUDA UNLESS OTHERWISE  NA BINTI AWE NI MIONGONI MWA MATAPELI hapo waendelee wapelekane jehanamu.
*Kuanzia leo futa mawasiliano* natuma lecture ya saikolojia ya zinaa isome uone mtego uliopo kwako mdada.
*Imeandaliwa na kujibiwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment