๐๐ *UFUNGUO WA 10: MAKOSA HAYASAHIISHWI KWA MAKOSA* ๐๐
_Hello Hello wana Ndoa, kwa mara nyingine Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto* Anakuletea ufunguo wa 10 wa Ndoa yenye Furaha,karibu ufuatane naye katika Hoja hii_
๐Imekuwa kawaida ya watu wengi,iwe katika Mahusiano au katika maisha ya kawaida,wengi wametengeneza *Chuki,migawanyiko,magomvi na Migogoro* Kwa kushindwa kujua Saikolojia ya Mahusiano Inakataza Kutatua Makosa kwa kutumia makosa.
๐Kikawaida katika uwanja wa Kisaikolojia (Ambapo ndo makao ya Hisia) Mwenzako akikosea,ukamjibu kwa kosa jua Unaimarisha Mgogoro,au Unapanua mgogoro kati yako na yeye.
๐Kuitirafiana katika maisha kama wanadamu ni kawaida,kukosea kama wanadamu ni kawaida, shida matabaka,magomvi,kuachana kusingekuwepo,au kungekuwa kudogo sana na watu wangeishi kwa furaha.
๐Tatizo kubwa kwa watu ni pale mmoja Anapokosea, Mwenzake Anamjibu mwenzake kwa Makosa(kumkomoa) hapo haumbadirishi ila unamuongezea usugu.
๐Kila kosa,linahitaji Akili ya ziada ambayo ndani yake ina huruma,inakujali,inakuthamini,ina kupenda.palee ndo utaona mtu anatumia njia sahihi za kumwambia mwenzake *Jambo hili mke wangu,mme wangu linaniletea shida,waweza kulibadiri,kuliacha ili moyo wangu uwe na amani?* Kama wote wana akili ya Kisaikolojia,wamejifunza funguo za ndoa yenye furaha, hapo Watakuwa na Faragha ya kuzungumza,kurekebishana,kusaidiana na kupena mwanga mpya wa kuishi watatoka huko na majibu ya furaha na kuendelea kuishi kwa upendo.
_Niishie hapo kwa leo katika ufunguo huu wa 10, ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
Saturday, 12 October 2019
UFUNGUO WA 10
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment