🛢🛢 *FANYA KAZI KATIKA OFISI SALAMA NA BOSS MWAMINIFU* 🛢🛢
*_Ujumbe huu umeandaliwa na Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto(Mjenzi wa Maisha ya Kiroho)_*
🛢 _Shalom mtakatifu wa Mungu uliye katika ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo, Neema na rehema za Mungu wetu ziwe juu yako. Shahuku yangu leo ni kukufunulia Siri iliyo katika Ofisi ya Bwana Yesu ili unapoamua kufanya kazi katika ofisi hii uwe na Matumaini katika maisha yako kuwa Unafanya kazi katika Ofisi Salama na kwa boss Mwaminifu kwako._
*28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Warumi 8:28*
🛢Katika mstari huu,tunapata kuona *Mungu(boss mwenye ofisi) anatoa taarifa kuwa anafanya KAZI pamoja na watu wale wa mpendao* Lakini katika KAZI hiyo wanayoifanya Anawapatia Mema Yote(Mshahara) wale walioitwa Kwa Kusudi lake.
🛢Maisha ya kumtumikia Mungu yamebeba Hatima na Heshima ya maisha yako kama mwanadamu.
*26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.Yohana 12:26*
🛢Kuna siri kubwa katika kuyatoa maisha yako kwa Mungu Umtumikie, ndani yake kuna Neema yaziada asiyokuwa nayo mtu mwingine, hapa amesema BABA atakuheshimu. ( _Neno Heshima hapa linawakilisha maisha yenye Heri,ulinzi,kibali,mpenyo kwako_) Mungu akikuheshimu dharau za wanadamu zinakoma, waliokuhesabia siku za kutofanikiwa wanashangaa kuona zinapita, nawe upo unasonga mbele.
🛢Kila aliyejitia Nia ya kukaa katika Ofisi ya Mungu, maisha yake yalibadirishwa, maana Mungu si dhalimu Akiahidi Kukuheshimu,anakuheshimisha kweli kweli katikati ya mataifa.( Huo ndo uzuri wa Kumtumikia Mungu).
*10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. Kumbukumbu laTorati 28:10*
🛢Faida ya Kumtumikia Mungu katika Roho na Kweli,kwa uaminifu mkuu.... Bwana anaachilia Neema yake juu yako,katika ulimwengu wa Roho na katika ulimwengu wa mwili Utukufu wa Bwana,kibali cha Bwana,na Utisho dhidi ya maadui zako unawekwa juu yako.
🛢 *Katika Utumishi wako waweza kukutana na Changamoto nyingi za kukukatisha tamaa,kukurudisha nyuma*
👉Safari ya Utumishi inaweza kuwa na changamoto nyingi za *Usizimie moyo kwa mapito hayo* Unapaswa kujua Nani unamtumikia,nani Alikuita katika utumishi wako huo,huuo ndo wa kumwangalia,huyo ndo wakumsikiliza kila wakati.
👉Yawezekana wengine wakasema *Hukuitwa na Mungu, maneno mengi ya kejeli juu yako,kukudharau, wengine hata kukuwekea Vikwazo vikali ili Kuziba kibali chako,Kuficha Neema yako isionekane kwa watu* Uhitaji kupambana nao,Unahitaji kukaa katika Wito wako na Kumwomba Mungu Neema ya Kuvuka pito lako hilo. *Hakuna kitu kilichowekwa na Mungu ndani ya mtu kinaweza kuzuiliwa na Mwanadamu (Anakuwa anatafuta balaa katika maisha yake na Utumishi wake)*
👉Mtu wa kushindana nawe,pambana nawe katika kuzuia kusudi la Mungu lisitimizwe, Hashindani nawe,hazuii kazi yako, Anazuia kazi ya Mungu, Mungu Akiamua kuingilia kati Ataaibika aibu kuu wakati wewe ukipandishwa.
*_Ninachosema nawe ni Amina na kweli, jambo kubwa jihakikishe je,Umesimama na Mungu wa Kweli? Unatumika bila Hila?_* Tulia kanuni hii itatenda kazi...
*29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.Warumi 8:29*
*30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.Warumi 8:30*
👉Huna sababu ya kuumizwa kichwa,kulia na watu Wasiojua *Asili yako,ambao hawakukuchagua,wala hawana uwezo wa kukutukuza* Unahitaji kushikamana na Bwana Anayejua Asili yako, aliyekuchagua kabla haujazaliwa na huko huko akakutukuza.
🛢👉Habari njema kwako mtumishi wa Bwana,ni kwamba kilicho tukuzwa na Bwana hata ungefanya harakati zote za kukichafua,kukizima,kukiharibu Hakizimiki,hakichafuki,wala Hakipotei yeye aliyeanzisha KAZI ndiye anayeitimiza.
*Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;Wafilipi 1:6*
👉Nikutie moyo,kazi tuliyo nayo ni kubwa na Inachanua,na kwakawaida Mizabibu ikichanua Lazima Vimbweha vidogo vidogo viibuke kwaajili ya kupukutisha Maua yake yasilete matunda,... Hapo ndo Neno la Bwana linasema....
*15 Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua. Wimbo Ulio Bora 2:15*
👉Kwenye maombi yako, shika Mbweha hao wadogo wadogo,(kwanini wameitwa wadogo wadogo,kwakuwa hawana Uwezo wa Kubadiri Hatima yako) Wageuzie hayo yote wanayoyapanga juu yako,na mwambie Bwana lilinde kusudi lako ndani yangu nami nikae katika kusudi lako.
🛢👉Uzuri wa Ofisi ya Utumishi wa Kimungu chini ya Boss wetu Yesu Kristo ni Kulinda Haki za watumishi wake, siku zote ukikaa katika haki na kutenda haki Kusudi la Mungu kwako ndilo litakalo simama daima siyo makusudi ya wanadamu.
*Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.Mithali 19:21*
🛢👉Nimalize kwa kusema kuna faida kubwa kukaa na Mungu vizuri na kumtumikia yeye kwa Uaminifu, *No matter what you are facing, Breakthrough is there* Utapenya kwa Mkono wa Bwana .
*_Ulikuwa na mimi mtumishi wa Mungu, Ev Elisha Kazimoto(Mjumbe wa Matengenezo ya Kiroho)_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
Wednesday, 9 October 2019
FANYA KAZI NA MUNGU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment