Thursday, 26 November 2020

MAHUSIANO NI GHARAMA

NAULIZA HIVI,
          Baadhi ya watu  wanasema wanaogopa kuanzisha penz kwa sababu wanaogopa gharama ya penzi lakn pia wengina wanasema,
  Penzi la kweli halina gharama je ni kweli au wapendwa hiyo imekaaje hapo? Majb na maon tafadhali🙏🙏🙏
*Anajibu Msaikolojia Ev  Elisha Kazimoto*
*KILA KITU KINACHOLETA MATOKEO CHANYA,RAHA,FURAHA MCHAKATO WAKE LAZIMA UHUSISHE GHARAMA*
👉Ni muhimu kujua kuwa gharama ni mchakato ambao unakulazimisha kufanya jambo husika ili utoe matokeo chanya, kwa lugha nyepezi *Inakulazimu kufanya jambo hata kama unahisi ugumu au uwezo ni mchache,inakulazimu ufanye* ili kutimiza Azma ya furaha yako.
👉Sasa mahusiano ni sekta ambayo mwenye akili timamu unapoingia mchakato wa kuanzisha na kulinda mahusiano LAZIMA UINGIE GHARAMA KUBWA ili utoe matokeo unayoyahitaji na usipo ingia gharama basi utapokea matokeo au majibu tofauti na shauku yako.
*Baadhi ya Gharama ambazo unaziingia kwenye mahusiano*
1⃣MUDA: Ukianzisha mahusiano,uwe tayari kutoa muda wako kwaajili ya mwenzako,muda wowote ili kulinda furaha na upendo.
👉Wengi walioanzisha mahusiano na KUJIFANYA BUSY,mahusiano yao Yalivunjika,au walienda bila furaha.
👉Kuna wakati umebanwa,lakini inakulazimu uwe na muda wa kuwasiliana na kumsikiliza,kumwambia kitu mpenzi wako.
2⃣GHARAMA YA PESA. Ukianzisha mahusiano uwe mkaka au mdada USIWE MBAHIRI AU KUHURUMIA PESA, jua tu utaingia gharama ya kuhudumia mwenzako kwa PESA.
👉Usipo taka pesa ikitoke ukakwepa gharama mahusiano yata yumba au kuvunjika.
NB:Uwe makini hapa kuna watu wanaingia kwenye mahusiano wanalengo la kutengeneza KITEGA UCHUMI,wengine kwa sababu ya malezi au hali zao wana uhitaji mkubwa wa kutunzwa kipesa. Sasa usipo jipanga kwa gharama ya pesa UTAYAKIMBIA MAHUSIANO.( Ila ushauri usiwe mchwa kwenye mahusiano unatafuna tu, kuwa ng'ombe unalishwa nawe unanywesha maziwa)(yaani hudumiwa nawe hudumia kwa pesa)
3⃣Gharama ya KUUMIZA NA KUUMIZWA, kwenye safari ya mahusiano kuna wakati UTAMUHUMIZA MTU AU ATAKUUMIZA kwa makusudi au kwa bahati mbaya,ujipange kwa gharama hiyo kubeba maumivu ya muda na kuyatua kwa amani na mahusiano yanendelee.
4⃣Gharama ya WEWE KUTUMIA AKILI KUISHI MJINGA/KICHAA MZURI.
👉Wengi hawajui kwenye ndoa au mahusiano *Mmoja wapo ni Mjinga au Kichaa mrembo/handsome* ambaye ukiamua ujibizana naye au ku ACT kwa matendo yake juu yako NDOA AU MAHUSIANO yatavunjika au itakuwa kelele kila mara.
👉Dawa ya kukwepa kero na migogoro wewe ongeza uwezo wa akili timamu,ila mwenzako umuhesabu kama *Kichaa mrembo au handsome* kama haleti madhara makubwa hasa katika uchumba ila kwneye ndoa WEKA MUHURI kwamba ninaishi na mgonjwa,mimi ni mzima hapo mtazeeka pamoja.
👉Msiwe vichaa wote ndani,mmoja awe mwenye akili,APUUZIE Shari hizi,hapo mnaenda, sasa KUPUUZA KILICHOKUUMA NDO GHARAMA HIYO KUBWA EVER HAPPENED.
Niishie hapo zipo nyingi.
*By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*

1 comment: