Wednesday, 9 May 2018

SULUHISHO LA CHANGAMOTO ZA SAFARI YA NDOA(Part II)

*CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO NA SULUHISHO LAKE KATIKA KUELEKEA NDOA*
.....................................
     (SEHEMU YA II)
     *_SULUHISHO LA CHANGAMOTO_*
  *By Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto*
...................................
       0755444078
_Tunaendelea na sehemu ya pili kutatua changamoto mbali mbali zinazo sumbua vichwa vya vijana wengi_.
🌈 *Kuhusu Maamuzi ya kuingia katika ndoa*, hapa Vijana wanahitaji Elimu ya kisaikolojia na ya Kiroho kuwasaidia katika kufanya maamuzi,wajue maisha hayajengwi kwa kuangalia waliopita,tena wale walio feli,wanapaswa kujua kila mtu anamapito yake na Neema yake ya Kimungu. Lakini kujipanga kurekebisha makosa wanayo yaona katika jamii,wajue hawa kwa nini walikosea,walikosea wapi na wao waboreshe wapi ili kuilinda ndoa yao.
Tatu vijana wanahitaji kufundishwa uzuri wa ndoa siyo matatizo ya ndoa tu, waonyeshwe Kusudi la Mungu katika ndoa ni nini, na wafundishwe changamoto za ndoa na uwezekano wa kuzitatua. Mungu hakuumba ndoa ili watu *Waishi ndani yake kwa Kujikaza na Kuvumilia,bali aliiumba watu waifurahie na wapendezwe nayo* Vijana wanahitaji kujengwa kiroho kujua kusudi la Mungu kuweka ndoa siyo kuwajeruhi watu mioyo yao,bali kuwafanya watu wafarijike siku kwa siku kwa uwepo wa mwenza wako maishani mwako. Mtu mwenye mtazamo hasi juu ya kitu chochote mara zote ukifanya kimakosa( *Mithali 23:7a*) kama vijana wataiona ndoa ni eneo la vita sehemu ya kuingia ukiwa unajihami kukabiliana na mwenzako hatuwezi zalisha ndoa za akina Sara na Ibrahimu,tutazalisha ndoa za Anania na Safila,Samsoni na Delila. Tulio kwenye ndoa Tusitumie makosa yetu KUWATISHA wanaojipanga kuingia,tutumie makosa yetu kuwaonyesha mwanga wa kufaulu wao wasipite njia iliyotukosesha.
👉Wanaozidi kukazana kurekebisha mapungufu katika ndoa zao nakuonekana wamefaulu tuendelee kuwafundisha vijana Ndoa yenye Amani,furaha na Upendo inawezekana,tusipindishe maandiko kwa kuangalia udhaifu wetu na kuwaogopesha vijana. Maarifa yanahitajika sana ili kulinda ndoa yako.
🌈 *Kuhusu kushindwa kutofautisha Ndoa na Tendo la Ndoa* Hapa kanisa na wataalamu wajikite katika kufafanua misingi ya ndoa na uwanja wake,wajibu na majukumu ya kila mwana ndoa katika ndoa tangu wakiwa vijana,wajue tendo la ndoa ni kajisehemu katika ndoa ambako hakapaswi kubeba dhana nzima ya ndoa, wajue ndoa ni zaidi ya sex,ndoa ni majukumu na wajibu mbele za mwenzako na mbele za Mungu. Vijana wajulishwe kuwa,Yule anaye letwa maishani mwako kama mwenzi wako anakuja Kutimiza Ndoto na Maono yako ya Kimaisha, sasa maono ya kimaisha siyo sex ni kusudi la Mungu la wewe kuumbwa(Kusudi la Kiroho na kusudi la kimwili la maendeleo). Ndiyo maana tumeona watu wakioa au kuolewa utumishi unakufa ndani yao,au mme anatumika peke yake au mke anatumika peke yake,ukiwalinganisha viwango vyao vya kiroho ni mbali sana,kwa nini tumeshindwa kujua Ajaye maishani mwangu anakuja kutimiza maono yangu,lazima awe sehemu ya maono yangu,na lazima ni pate mtu sahihi wa kubeba maono yangu. Tukiwafundisha hivo vijana hapo tutakuwa na vijana waliojipanga kuoa au kuolewa kutimiza kusudi la Mungu siyo walalamikaji katika ndoa na waenezaji wa matatizo ya ndoa badala ya uzuri wa ndoa.
🌈 *Kuhusu Changamoyo ya Kiuchumi* Hapa ni vizuri kuwaweka vijana wazi, *Wasiishi kwa Imani,na kuoa kwa imani* wahimizwe wafanye mambo kwa vitendo. Zama hizi kila mtu anayetafuta mtu wa kuingia naye katika ndoa,anawaza kwanza mtu *atakaye mpa uhakika wa kupata mahitaji muhimu,yaani chakula,mavazi,na malazi* pesa ndilo jawabu la mambo yote, vijana wapewe elimu ya ujasiriamali,wajishugulishe kutafuta pesa, wafanye kazi,wasibague kazi ila wajiingize katika kupambana kupata kitu cha kuwaingizia kipato hatakiwe kidogo,kuliko kukaa bila kazi wakingojea Muujiza wa Mungu wa kupewa pesa,kulipiwa mahari,kushonewa suti, hayo tumwachie Mungu lakini tuwe na fimbo mkononi ambayo kwayo twaweza gawanya bahari(Musa akaulizwa una nini mkononi?)wewe kijana una nini mkononi ubarikiwe? Na mabinti waepuke kutegemea kuwa *Mama wa Nyumbani* badala yake wajipange kuwa mama wa Maendeleo, wajiandae kuwa wamama wajenzi wa familia bora wenye uwezo wa kupambana,kushugulika kuingiza kipato sawa sawa na *Mithali 31:1-15* inavyosema.
🌈 *Kuhusu changamoto ya Elimu* Kanisa lijikite katika kuhamasisha vijana walio katika umri wa kwenda shule,vyuo wapambane kupata elimu,na wale waliovuka elimu za msingi na sekondari basi wahimizwe kupata elimu ya Ujuzi wa mambo mbalimbali.Wanaoweza kuongeza elimu waongeze ilikukabiliana na changamoto za maendeleo ya utandawazi. Tusifikie hatua tukaridhika,ziko fani nyingi za ujuzi awezazo mtu kusoma wa umri wowote na kujiweka katika nafasi nzuri,huwezi jua mambo ya mbele na mabadiriko ya tawala na nchi na matakwa ya upepo wa kisayansi duniani. (Kijana iweje uridhike? Elimu kubwa huna,Ajira huna,Pesa/biashara kubwa huna na Upako wa tofauti kiroho huna) unategemea kuoa na ukaishije kwenye dunia hii ya chagamoto kubwa za wasomi na matajiri?
NB: *_Wadada wafundishwe namna ya kuongeza elimu huku wakiongeza unyenyekevu na adabu_* Utafiti unaonyesha,kwa kadri wadada wanavyoongeza elimu ndivyo wanavyopoteza sifa ya kuolewa,na kuogopwa kwa sifa ya kuota kiburi na dharau kwa waume zao. Wadada wajifunze na kujua kuwa elimu,cheo na pesa Siyo tiketi ya kuwa na Sifa ya Kuolewa,bali ni tabia njema na moyo wa kumthamini mmeo. Unyenyekevu uonekane tangu ukiwa bado ujachumbiwa katika kuongea,katika kuwajibu wale wanaokutaka ila huwataki,jiombee sana ili uwe mtu anayefaa.
👉Wazazi mawazo yenu ni mema kwa kutaka watoto wenu wa kike waolewe na wasomi,matajiri ila msiwapande watoto wenu kiburi nakujiona wao hawawezi olewa na watu wa aina flani,ila wa level flani,maisha ni mzunguko mtoto wako akipitwa katika mzunguko umri ukaenda atakulaani wewe na atakuletea aibu nyumbani na utakuwa umezika ndoto zake utaona ni Heri mara elfu angeolewa na yule mlo mkataa.( Hekima ziongoze zaidi ya Hisia).
🌈 *Kuhusu changamoto ya Kiimani* Watumishi wa Mungu wajikite katika kufundisha zaidi ya kuhubiria vijana, Vijana wanahitaji kufundishwa,huu ni umri wenye Maswali kibao ya kimaisha,udadisi mwingi,usiri mwingi,majaribio mengi, sasa kama Makanisa hayatatumika kama Madarasa ya Kiroho na Kimwili kuwaandaa vijana kuwa Watumishi wazuri wa Mungu wenye imani thabiti ya Kimungu,wasioyumbishwa na upepo wa imani za ajabu ajabu,basi tutazalisha vijana ovyo makanisani,wakurupukaji na wasio faa kuwa baba/ mama wakesho.Vijana waandaliwe,wachongwe kiroho,wapokee sifa ya utumishi,wajisimamie kiimani,wawe na uwezo wa kiroho wa kupambanua imani feki na orijino,wawe na viwango vya kumpenda Mungu kutoka moyoni si kwa mazingira yako vizuri ndo anampenda Mungu,yuko na watumishi ndo ni mtakatifu,akiwa mbali na kanisa na famila basi ni majanga matupu. Hao vijana hawafai kupewa mabinti na vijana wetu wa kiume. Wafundishe wawe na uwezo wa kukabiliana na mazingira yote ya raha na ya dhoruba. Msingi mwema,uwekwe mapema tangu wanapookoka. Kanisa limekosa mafundisho,badala yake limejikita katika kuhubiri  miujiza na baraka zaidi ya kuwafundisha vijana kumjua Mungu na kumpenda Mungu kwa kina wakawa na uwezo binafsi wa kulifasiri neno la Mungu mioyoni mwao na kuliishi.
_Kijana mwenye misingi imara ya kiroho anapofika muda wa kuoa au kuolewa,anakuwa mtulivu na anamsikiliza Mungu katika kuingia katika ndoa,anajua ipi ni imani sahihi na ipi ni imani potofu. Pia vijana walioiva kiimani wanaouwezo wa kupambanua matapeli na  waliookoka kweli kweli._ Madarasa ya waongofu wapya yarudishwe upya makanisani,idara za vijana ziboreshwe sana, zijikite kuwaandaa vijana kuwa watumishi wazuri wa Kristo na wababa/wamama bora. Shida kubwa tuna vijana wakuabudu ibadani ila siyo walio na mzigo na kazi ya Mungu,ambao wanatambua mimi nimeokoka lakini Mungu amenipa neema hii iujenge mwili wa Kristo. Ndo maana siku hizi wainjilisti vijana wanapungua kwa kasi,wachungaji vijana,manabii na mitume na waimbaji tuna wakongwe na wasitaafu wa serikali walio wengi, vijana walioingia katika utumishi *_Niwahuni,wababaishaji,feki na wapiga madili_* hata kwa macho unaona huyu hakuna. Wenye mzigo,walio na mioyo na uchungu wa mji wa Bwana na Kuta zake kama akina NEHEMIA wanazidi kupotea. Kwanini? Kwasababu makanisa ya siku hizi mengi yanatafuta POPULARITY (Kujulikana)siyo Yesu kujulikana. Tangu mtu anaokoka kila siku anaambia Naona ukifanikiwa,naona ukiinuliwa,panda mbegu izae,haujui lingine,huyo unahisi kiroho chake kikoje.Tutapata mtumishi humo,madhabahu ni zinaa na uganga,kijana je alookokea humo huyo atakuwaje. KANISA LIJIPANGE UPYA.
👉Lakini ni muhimu vijana wakafundishwa nguvu ya imani katika ndoa,utofauti wa imani unaweza kuwapelekea kuwa na ndoa isiyo na mwelekeo maalumu na malezi mabaya ya watoto na kizazi kiovu.
🌈 *Kuhusu changamoto ya Itikadi za Madhehebu* hapa vijana wafundishwe neno vizuri,waijue misingi ya neno la Mungu na mapenzi ya Mungu,wasiendeshwe na mapokeo ya watu na interests za mtu mmoja na kujitia kinfungoni.Hapa viongozi wa makanisa kuna haja ya kutafakari,tunaandaa kizazi cha watu wanao hofu mapokeo ya kanisa au Mungu mwenyewe. Watu wafundishe Neno la Kristo wajazwe Roho mtakatifu,waongozwe na Roho wenyewe atawasaidia kupambanua mambo yoote yanayoleta ukakasi makanisani( mara kusuka,mara wigi,mara mapambo,mara masuruali)kanisa limejitahidi kuwatiisha watu chini ya sheria ila siyo chini ya neno la Mungu. *_Ndo maana waweza Ona maajabu ya Kiroho,mtu huyo alokuwa havai suruali,kujipamba akiwa kanisa flani,maala flani,akitoka akaenda kanisa lingine Utamkuta yooote aliyoelekezwa ni dhambi na akatii ndo yoote anayafanya_* Je, huyu alilitii neno la Bwana au alitii vitisho vya watu walombele yake. Je,hakuyafanya muda ule kwakuwa alikuwa akiongozwa na Roho au sheria,na sasa anafanya kwakuwa anaongozwa na Roho au mazingira. Hapa ndipo penye Hekima na Maarifa ya watakatifu, *"Tukiongozwa na Roho hatutakuwa Chini ya Sheria"* na tutafanya lolole popote kwa Amani kulingana na maelekezo ya Roho wa Bwana.
(Changamoto nyingine,kuna makanisa yamekata tamaa,mpaka sasa Hawaamini kama mtu anaweza kuongozwa na Roho,wala Roho aweza tembea na Mtu,wamekuwa na mtazamo Hasi juu ya Roho wa Bwana na Vipawa vyake na Madhihirisho yake kwa watu) Ila niwaambie ambao bado mnasikia Taa ya Bwana ndani yenu, hayo hayana budi kuwepo, *Yesu ni Yeye Yule Jana Leo na hata Milele habadiriki.* WAEBRANIA 13:8 endelea kuomba Roho wa Bwana aendelee kuwa nawe na mlinde mtunze,usimfiche kwa madhihirisho yake mwache afurike.
🌈 *Kuhusu Malezi* Hapa niseme na wazazi wa kimwili na wa kiroho,tusiwe na upendo kupita kiasi,au kuziba macho tusione umuhimu wa maisha ya vijana sasa na baadaye wanapoelekea katika ndoa. Tuwaingize watoto wetu,vijana wetu katika kuwajibika,kujishugulisha na kujua kufanya kazi za kila aina.Tuwapime uwezo wao kwa kuwapa kazi ili kuwaandaa kuwa wababa na wamama wawajibikaji kwa familia zao. Wazazi wa kimwili hakikisha mtoto katika umri wake kuna vitu anaweza vifanya kwa ubora,mzoeze maisha ya aina zote ili aweze kukabiliana na changamoto za ulimwengu.Huku wazazi wa kiroho tuwaingize vijana katika utumishi,tuwajaribu katika kona nyingi za utumishi kuona wanafaa wapi katika mwili wa Kristo.Tunapo wapa majukumu ya Kiroho makubwa na kuwaonyesha njia ya kuyatekeleza ndipo tunapo WAZOEZA KUONGEA NA MUNGU NA KUWA NA MAISHA YA UKARIBU NA MUNGU. Ikumbukwe hawa ni vijana wapo katika muda Timing and Error(Muda wa kubahatisha kwa kufanya vizuri na kukosea)wanahitaji kusaidiwa kufuta makosa yao siyo kuishi katika makosa yao.Katika kutafuta uhalisia wa kitu LAZIMA KUKOSEA KUPO makosa siyo Matatizo,ila tusipo wakosoa na kuwaelekeza tutazalisha MATATIZO kwao. *"Every one Learn from his or her Mistakes"*  Errors are not  Mistakes,and mistakes are not Problems (Errors comes from Trying, Mistakes comes from Challenges,but Problems are the results of failure to Try,and failure to solve challenges in a good way)That's my Philosophy you may take it.
🌈 *Kuhusu Familia* Familia lazima ijue mipaka yake katika mchakato wa kihisia wa kijana kuingia katika ndoa,familia ishauri,ilee na ielekeze,ila maamuzi yaachwe mikononi mwa vijana,ili kuepusha lawama katika ndoa za vijana wao.Wazazi wengine wamekuwa ndo waamuzi wa nani aoe au aolewe na yupi,uwe una taka au hutaki,vikao vya kifamilia vinakaa kwa lengo la kupinga maamuzi ya binti,kwaajili ya maslahi tu,(mara kabila,mara elimu,mara kiwango cha uchumi)hawajielekezi kumsaidia mtoto wao,ndugu yao,kulitafuta kusudi la Mungu katika maamuzi yake,ila kutafuta sifa na heshima na uwezo wa kifedha na mali kwaajili ya manufaa ya familia. Wazazi tumewafanya watoto waingie katika Ndoa ambazo hawakuzikusudia na wala hisia zao ziko nje kabisa na huyo mlomchagua. Kumbuka Love is all about  Emotional (kama hana hisia juu yake kumpenda ni vigumu)huu ndo umekuwa mwanzo wa wanandoa kuendeleza mahusiano yao na *Ma Ex Girl/Boyfriend wao huku wakiwa katika ndoa na kuibua migogoro ya ndoa,mwili upo ndani hisia ziko nje* Tumezalisha lawama kwa watoto kuwa maisha haya ni kwasababu wazazi walinilazimisha,badala ya kuwa baraka kwa ndoa za watoto wetu tunakuwa msiba.(STOP THAT BEHAVIOR )
🌈 *Kuhusu Gharama za Mahari* Hii ni kona ya wazazi na kijana wa kiume, kwanza wazazi wa binti wajue ndoa siyo biashara,wajikite katika kutazama namna ya kuwaandalia watoto wao familia mpya,bora na yenye uwezo wa kiuchumi,badala ya kujipanga kutaja Mahari kubwa,wajipange kumuwekea mtoto wao msingi mzuri wa maisha. *Usisubiri Pesa ya Mahari ndo umfanyie binti vitu vya kumuaga,hiyo ni sawa na kuamisha pesa kutoka mfuko mmoja wa suruali na kuweka mwingine na kushukuru kwa zawadi,ni sawa na kujikopa mwenyewe* Tukibadirisha mtazamo wa Mahari ya Ndoa,tutawaokoa vijana wengi na stress za ndoa. Pia vijana wahimizwe kufanya kazi kwa bidii wawe na uwezo wa kulipa mahari na kumaliza *Siyo Kukopa Mke kama unakopa nyanya kibandani.* Makanisani vijana wabanwe vizuri waonyeshe miradi yao ya kiuchumi Mapemaa.
🌈 *Kuhusu gharama za Harusi*,Hapa tufikie hatua vijana,binti na kijana wa kiume,mjue uwezo wenu,msipende kuigiza maisha ya mitandaoni na kwenye ma TV,wakati uwezo wako wakawaida sana. *Fanyeni yaliyo kwenye uwezo wenu kwa furaha* siyo mnamaliza sherehe una madeni yakulipa mwaka mzima.Kumbukeni hao watu unaotafuta wakupe Credit mnakuwa nao siku 1,baada ya hapo unabaki wewe na mwenzako na maisha yenu. *Jiandae kufurahisha nafsi zetu na si za watu* ukitaka maisha ya kushindana na kuiga utaishia kujilaumu na kuona wewe ni mtu wa kutofanikiwa.
............................................................
_Masuala ya mahusiano na ndoa yanahitaji kila siku ujifunze na ukubali kupokea mambo mapya,huu ni uwanja mpya kila siku usiwe mgumu kubadirika na kupokea mawazo mapya,kwa nini uishi kiugumu ugumu wakati maisha haya hitaji Stress? Mtangulize Mungu,ongeza maarifa jaribu kubadirika utaona ndoa ilivyo ya ushindi_.
*_Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na ndoa Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment