Thursday, 24 May 2018

SEMINA YA SEHEMU YA 5

🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
  _By Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp  0755444078)_
.........................................
*_Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu._*
      *SEHEMU YA 5*
*Sifa 7 za Mtumishi wa Kweli wa Yesu Kristo*
......
......
_Shalom mtumishi wa Mungu unayezidi kufatilia somo hili muhimu katika utumishi wa Kristo,tuendelee kuchanganua hatua muhimu katika utumishi,katika sehemu ya 4, tumeangalia hatua ya kwanza ya *Utakatifu* na sasa twende hatua ya pili._
2⃣ *Kujifunza na Kusoma Neno la Mungu* Hii ni hatua muhimu sana kwa mtumishi yeyote wa  kweli wa Yesu Kristo. Hii ni kwa sababu *Huduma yoyote iliyo nje ya msingi wa ujuzi na ujazo wa Neno la Mungu ni Batili*
✈Neno ndilo kipimo pekee cha huduma zote,ndimo zilimo *Siri za Kimungu* za huduma zote.
(Wakolosai 3 )
------------
16Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
17Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
.........................................
✈Mtumishi yeyote wa Mungu asiyejikita katika Neno,kusoma au kunifunza basi huduma yake haiwezi kuwa na nguvu ya kupasua anga na kuwa na kibali.
✈Unahitaji uwe na uwezo mkubwa katika huduma yako,hata unapo simama kwa huduma popote katikati ya watu wa level zote za kiroho, *Jibidishe kusoma na kupata mafundisho ya neno la Mungu* neno ndani yake limebeba sauti ya Mungu,limebeba maelekezo,namna uwezavyo kumtumikia Mungu katika unyoofu.
"Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio."
(Methali 30:5 )
.....................................
✈Kusoma neno na kujifunza neno la Bwana,kuna kupa hazina ya maarifa ya kutosha,huduma yako isipwaye.Linakujengea ujasiri na uwezo wa kumjibu kila mtu kwa hekima kwa habari ya tumaini la wito wetu(wokovu).
3⃣ *Kuwa mtu wa Maombi ya Bidii* mtumishi yeyote anayeingia kwenye Tasnia ya Huduma ya kweli ya Yesu Kristo, *_Maombi kwake ni maji,ni dozi_* maombi kwako yasiwe na Likizo. ( _Kuna watumishi wengine,uanza kwa bidii ya maombi,ila wakianza kuona Mungu anatembea nao,miujiza au kibali kikubwa kwa watu,maombi ya kufunga na ya bidii wanaacha_) hiyo siyo kanuni ya kiroho, kanuni ya utumishi wa kweli inasema Omba bila kukoma.
*"ombeni bila kukoma;"*
(1 Wathesalonike 5:17 )
✈Siri hii kwako mtumishi wa Mungu, uliye katika huduma na unaye tamani kuingia, ni kwamba, *_Huduma yoyote,kipawa na karama yoyote unayoijua wewe ina muhusu Mungu aliye hai,basi jua inatunzwa,inatengenezwa kwa maombi ya bidii_* humo ndo utapata siri nyingi,upako wa pekee.
✈Ukiona watu wanatafuta madawa,nguvu za giza ili wapate mvuto,kibali,upako na miujiza jua yakuwa ndo walee wa kula kula,hawana ratiba na Mungu ya kufunga na kuomba.Wanahitaji vitu vya dezo,( *finished issues*)ukizipata na wewe utakuwa *Completely finished*.
✈Pasipo maombi hakuma mafunuo mapya juu yako,wala sura mpya na ya uwepo wa Kimungu. Ukisikia wahubiri au waimbaji wana nena vitu Adimu,mafunuo adimu nyimbo adimu jua wametulia magotini pa Bwana kuomba wanakuja na vitu vipya,vinavyo gusa maisha ya watu na kuwapa majibu.
*Wakolosai 4:2-3,Mathayo 26:41*
✈Kwenye maombi ya bidii ndo tunapata mamlaka ya kuamuru vitu na kuvitiisha chini yetu na vika tii.Fatilia huduma yote ya Yesu pote alipo fanya miujiza, juu yake alitangulia mlimani kuomba. ( *Luka 5:16-18*) Soma na andiko hili umuone binadamu kama wewe...
(Yakobo 5 )
------------
17Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
18Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.
✈Faida ya upako uliopatikana kwa njia ya maombi,kwanza hauchuji,pili autiliwi mashaka maana unafanya huduma ikiwa safii chini ya Roho mtakatifu watu hawajiulizi maswali juu ya unachofanya.
*Mfano maombezi ya saizi ya baadhi ya watumishi yanatuacha hoi,maswali kibao,ni uchafu mtupu wa ngono,wakiuganga,tunajiuliza haya mafunuo yametoka kwa nani?, deliverance ya romance mke wa mtu,mdada imetoka wapi,kushika wanawake maziwa nk nani kakuongoza,kumvua mmama chupi madhabahuni uiombee apate mtoto au mdada aolewe huu ufunuo mbona ni wa ngono tupu?* majibu utayapata huyu si mtu wa magotini niwa upande wa nyenzo za giza.
✈Mtu mwenye upako ORIGINAL raha sana vitu vyake ni nitofauti,muone huyu tu kwenye andiko hili....
(2 Wafalme 13 )
------------
20Elisha akafa, nao wakamzika. Basi vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi mwanzo wa mwaka.
21Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.
..............................................
4⃣ *Uvumilivu* Hii ni hatua ya nne ya Mtumishi wa Kweli wa Yesu Kristo. Huduma iliyo sahihi aihitaji haraka,kutaka kupanda haraka,ujulikane haraka,uwe mtu mkubwa,umiliki vitu vikubwa ghafla, *_Mambo yote ya Kiroho graph ya kukua kwako inaendana na kiwango cho ukuaji wa roho yako._* jiulize unapo patamani hapo na kutaka leo uonekane hivyo tishio je,roho yako umeifanyia hayo iwe kiwango hicho cha tamanio la moyo wako?
(3 Yohane 1 )
------------
1Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.
2Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
✈Mara nyingi watumishi wengi wamejikuta wanaangukia kwenye mikono ya utumiahi wa kishetani kwa sababu ya tamaa,kutaka kuwahi na kujulikana,heshima kubwa,mali nyingi haraka sana bila kufuata kanuni za kiroho. Hiyo ni baada ya kuona kama Mungu hawatimizii matakwa yao,amechelewa....Mungu anafanya vitu kwa wakati wake.
*"ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako."*
(Kumbukumbu la Sheria 11: 14), Waebrania 10:36.
.......................................
*_Leo niishie hapo,usikose kutufatilia katika sehemu ya 6 ya somo hili la utumishi_*
By Ev Elisha Kazimoto( Whatsapp 0755444078)

No comments:

Post a Comment