Wednesday, 9 May 2018

CHANGAMOTO ZA VIJANA KUELEKEA NDOA(PART I)

*CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO NA SULUHISHO LAKE KATIKA MAHUSIANO KUELEKEA NDOA*
    (SEHEMU YA I)
.........................................
_By Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto_
     *0755444078*
_Shalom wana wa Mungu wote mlio katika safari hii ya Mahusiano ya uchumba,au mnawaza kuanza safari hii,na wengine wameisha pita katika safari hii,sasa tumebaki kuwa walimu na washauri wa ndugu zetu wanaoianza safari hii. Leo nataka kusema katika nyanja mbili ya Kiroho na Kisaikolojia tunapo yasemea mahusiano kwa vijana. Kuna Changamoto nyingi vijana wanakumbana nazo na hawajapata majibu,jambo linalowapelekea kuendeleza foleni ya wana ndoa wabaya,wenye migogoro na kuachana(Divorce) nyingi kwa wana wa Mungu. Majibu hayo yanabidi yawe yamegawanyika katika pande mbili kiroho na kisaikolojia._
*Fuatana nami katika uchambuzi huu wa Changamoto na Suluhisho lake katika mchakato wa kuingia katika ndoa*
...................................
🔥 *CHANGAMOTO*🔥
✍ *Kuna changamoto ya Maamuzi yakuingia katika ndoa* Miongoni mwa vitu vikubwa vinavyo vuruga vichwa vya vijana sasa,ni namna ya kufanya maamuzi ya kuingia katika ndoa. Tuna vijana wengi wanaotamani kuoa au kuolewa ila wanashindwa kufanya maamuzi ya kuingia rasmi katika ndoa,na hii imetokana na *Hofu kubwa* ya kuogopa kuwa na ndoa mbaya,kwasababu maisha ya ndoa nyingi zinazowazunguka kanisani na mitaani kuwa na migogoro mingi hata kuwafanya vijana kupoteza hamu ya kuingia katika ndoa, *mioyo inatamani ndoa,ila Akili inagoma kwa vitu walivyo experience kwa watangulizi* kwa hiyo tuna vijana wengi makanisani,umri unaenda ila wanasita kuingia katika ndoa.(Moja ya Athari inayotokea ni kuwa na Vijana-wanaume,na Wadada -Mama yaani wanaoendelea kushiriki ngono kanisani ila hawajaoa na kuolewa)
✍ *Changamoto ya  Kushindwa kutofautisha Ndoa na Tendo la ndoa* Hii ni changamoto kubwa katika ukubwa wake inayosumbua karibu  85% ya vijana,katika utafiti wangu,na katika kufundisha makongamano ya vijana juu ya mahusiano na ndoa,vijana wengi wanaofikiria kuingia katika ndoa *_Hawajui kwa nini wanaamua kuingia katika ndoa_* wengi wanatamani kuingia katika ndoa *kutuliza tamaa za mwili(Sex)* jambo ambalo wengi kwanza limewafanya kuitafsiri ndoa kama Uwanja wa Sex(ngono) yaani ndoa ni sex, kulingana na tafsiri hii wengi wamejikuta wakishiriki sex kabla ya kufunga ndoa,wengine kulazimika kuoana kwa sababu ya mimba ilopatikana kwa bahati mbaya,au kufunga ndoa wakiwa wajawazito,na wengine kuolewa ndoa za mitara,au kuacha wokovu.( *Je,Ndoa ni Sex?*)swali linalochanganya wengi,tutalijibu kwenye suluhisho.
✍ *Changamoto ya Kimaisha hasa katika Uchumi* Tatizo lingine linalowapa vijana kigugumizi katika safari ya kuelekea ndoa ni Hali ya Kiuchumi,wapo vijana wanao amini *Ndoa ni Pesa,bila pesa ndoa itakushinda, wapo wanao amini Upendo unamechishwa na pesa,na wapo wanao amini Ndoa ni Upendo tu,uwe maskini au tajiri suala ni upendo. Utofauti wa mitazamo hii umewaathiri vijana katika safari yao ya kuelekea katika ndoa,ambapo ujikuta watu wawili waliopendana wanatofautiana katika mitazamo.* na hapo ndo safari ya hao wawili huwa ngumu.
✍ *Changamoto ya Kielimu* Tuliko toka katika miaka ya 1990 kurudi nyuma, Elimu haikuzingatiwa kama Kigezo cha Kumpata mtu wa kuoana naye,ila miaka ya 2000 mpaka sasa na tunako elekea,kumekuwa na mtazamo wa Kiwango cha Elimu kuwa ni Kigezo kikubwa cha Kumpata mtu wa kuoana naye. Changamoto ni watu waliopendana lakini wanajikuta wanatofautiana sana kiwango cha Elimu,jambo ambalo wengine uamua kuvunja mahusiano,na wengine kuwa na uchumba wa muda mrefu ili kutumiza kwanza kigezo cha Elimu.
✍ *Changamoto ya Kiimani*  Hapa kuna mambo mawili yanaumiza vichwa vijana makanisani na watumishi wa Mungu wanaochunga vijana hawa. Moja,Namna ya kumpata mke au mme *Mchaji wa Mungu* wengi wa vijana makanisani niwasanii,wanaigiza kuokoka,wengine wamejiingiza katika wokovu kupata mke au mme,au kupata sifa ya mlango wa kutokea kimaisha.Kwa misingi hii vijana wamejikuta wanaogopa kuoa au kuolewa maana kuna hati hati ya *kuangukia kwa Tapeli* kwa kuwa waigizaji ni wengi kuliko walio halisi.
_Pili,ni vijana kupendana watu wa imani,na mtazamo wa kiroho tofauti. Hii imeleta mkanganyiko wa kiimani,wengi wamerudi nyuma,na wengine wamelazimisha kuoana hatima yake imewapelekea kwenye migogoro ya ndoa na changamoto ya malezi ya watoto kiimani._
✍ *Changamoto ya Itikadi za Madhehebu(Kumbuka kuna tofauti ya Dini-Imani na Itikadi za Dhehebu)mfano wote ni makanisa ya kipentekoste ila kuna itikadi za dhehebu moja kutofautiana na lingine(hawa hawaruhusu hiki,hawa wana ruhusu,hawa usisuke hawa suka)* Hapa nazungumzia misimamo ya dhehebu moja hadi lingine,hii imeleta changammoto kwa vijana,dhehebu moja kuwa na misimamo ya kwao inayotofautiana na wengine,mfano.. *Kusuka,kujipamba,kufunga vilemba,kuvaa suruali nk* hii imewapa vijana kigugumizi pale wanapokutana kwenye maeneo kama vyuoni kwenye fellowship zinazowaunganisha pamoja,wakitoka vyuoni kurudi makanisani kwao,wanagawanywa kwa itikadi,wengi uchumba uvunjika.(na wengine wakiamua kuoana mmoja inabidi Asalimu amri kwa moyo wote ili alinde Amani ya ndoa yake,au aendeleze msimamo waishi kiubabe kwa falsafa ya "Kuamua Kukubaliana Kutokukubaliana"
✍ *Changamoto ya  Malezi* Kizazi tulicho nacho sasa,ni tofauti na kizazi kinachomalizikia, utofauti wa malezi katika familia,umetengeneza kizazi ambacho katika ndoa ni mzigo,hivyo vijana kuwa katika wakati mgumu wa kuchagua nani awe mke au mme wangu( *Shida tabia na makuzi*) ya vijana hawaandaliwi kuwa *Wake au Waume,wenye uwezo wa kuendesha ndoa katika majira ya aina zote,dhiki,raha na taabu hawawezi,wanapenda raha,wameandaliwa kuishi katika raha* wapo waliokuwa maishani mwao hawajui hata kupika,kupasua kuni,kuosha vyombo ,wamekulia chini ya House girl na House boy mpaka wanaoa na kuolewa hawajui kuwajibika,hii inawapa changamoto vijana katika ndoa.(hapa ndo utakuta familia za ajabu,mpangilio wa ajabu ndani ya nyumba nk)
✍ *Changamoto za  Kifamilia* Katika safari ya mahusiano kuelekea ndoa,vijana wanakumbana na vipingamizi vya kifamilia vya kuwekewa vikwazo,kutooa au kuolewa na kabila flani,mtu wa kada ya kazi hii,jambo ambalo limewafanya vijana kuoa au kuolewa na watu wasio katika matamanio yao,wanaoa au kuolewa kwa shinikizo la wazazi.( *Na wengine wamechelewa kuoa au kuolewa kwakuwa walio kuwa chaguo lao muda ule, WALIKATALIWA NA FAMILIA sasa wamekosa watu wa aina kama ileile ya wa sifa zinazotakiwa na familia*) mwisho wake ni nini...Wengi wameanguka katika dhambi,wengine wameishia kuwa na ndoa za ajabu Zisizo gusa Hisia zao.Wanaishi ili kutimiza wajibu na kuonekana nao wapo kwenye ndoa ila Hawana Partner wanaogusa maisha na hisia zao.
✍ *Changamoto ya Gharama za Mahari* Kigugumizi kingine kwa vijana wanapoanzisha mahusiano fikra inahamia kwenye gharama za kulipia mahari, ambapo familia zingine *zimegeuza ndoa mtaji wa kiuchumi,au kifuta jasho cha malezi,badala ya ndoa kuwa ni kupanua mahusiano ya kifamilia. Zoezi la Mahari limewafanya vijana kuchelewa kuoa na kuolewa,kuanguka katika zinaa,na kuishi maisha ya unyumba bila kufunga ndoa.
✍ *Changamoto ya  Gharama za Harusi* Kuna kitu kinapanuka katika vichwa vya vijana na kuwa Utamaduni, kitu hicho ni *Ushindani wa Ukubwa na Ubora wa Sherehe za Sendoff na Harusi* Siku hizi vijana hawako tayari kuoa au kuolewa kama harusi haitakuwa ya kifahari, *_Pete ziwe za Gold,Shera ya tausi,suti kali,kiatu,ukumbi,keki ngazi 12,kwa ujumla wanahitaji Harusi yake iwe Unique (pekee)* ndo waoane,kabla ya hayo yote hayajatimia ndoa isubiri.
✍ *Changamoto ya Maarifa ya husuyo mahusiano na ndoa* Ni hitimishe kwa Eneo hili ambalo ni bahari ya matatizo kwa vijana, ni Maarifa(Shule)juu ya mahusiano na ndoa. Huu ni ugonjwa wa vijana wengi makanisani,wataalamu,walimu na watumishi wa Mungu wa kukokotoa Uwanja huu wa mahusiano na ndoa *Kwa kina* bado hatuna,aidha hatujui umuhimu wa ndoa,au tumefeli katika ndoa, au tunarahisisha suala la ndoa, hivyo tunashidwa kufundisha katika ubora,au tujizamisha rohoni sana na kuiona ndoa ni kitu cha kimwili sana au rohoni sana,kumbe ndoa ni 50/50.Vijana hawana maarifa,wanafanya wanachoona kina faa,kwa kuendeshwa na taarifa za mitadao,hatima yake ni kuzalisha ndoa mbovu na dhaifu.( Na wengi wa wasemeaji wa ndoa makanisani WANAPENDA KUISEMEA KATIKA MTAZAMO HASI SANA KULIKO MTAZAMO CHANYA hii ni shida kubwa sana, misingi hii vijana wanapata tabu sana kufikia malengo yao na tunazalisha jamii Dhaifu sana katika kila sekta ya maisha.)
_Haya ndiyo baadhi matatizo makubwa yanayo watesa vijana wengi katika kizazi cha sasa. Ulikuwa nami_
*_Mtaalamu na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na ndoa, Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto_*
    Whatsapp 0755444078.
Facebook Elisha Kazimoto.
*Hii ni sehemu ya kwanza ya Somo,sehemu ya Pili inafuata,inayo Toa suluhisho la Changamoto hizi zote zinazo wakumba vijana katika kuelekea Ndoa*

No comments:

Post a Comment