🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
_By Ev Elisha Kazimoto_
WhatsApp 0755444078
...................................
*_Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu_*
*SEHEMU YA 3*
*"Namna ya Kukabiliana na Nguvu ya Wito"*
...
...
_Karibu tena katika sehemu ya tatu,taratibu tunaanza kuingia ndani ya somo letu linalo itwa, *"Utumishi wa Kweli Katika Kristo Yesu"* maana yake nini,mtu yeyote anayejipanga kumtumikia Mungu,au yupo katika Tasnia ya Huduma Takatifu ya Madhabahuni lazima tutamuona katika misingi hii nitakayoielezea hapa. Labda kwanza nikupe chimbuko la Somo hili_.
....
....
🌈 _Mnamo mwaka wa 2007 ndani yangu kulikuwa na fukuto kubwa sana la kutumika,lililoanza mwaka 2006 mwezi December 29 katika mkesha mkubwa wa Vijana wa wilaya Dar es Salaam TAG Magomeni kwa kuitwa na Bwana akimtumia mtumishi wake kwa neno la kinabii,nikatoka mbele nakuwekewa mikono kwa machozi mengi,tangu siku hiyo ndani yangu kulianza kuwaka moto wa kutumika katika huduma ya *Uinjilisti na Ualimu wa Neno la Mungu*,lakini moyoni mwangu kulikuwa na maswali mengi sana ya nitafanyaje,nitasimamaje,nani atanishika mkono kunikuza huduma yangu,nitatembeaje na Mungu kwa viwango ninavyo vitamani,maswali hayo yalinitesa sana zaidi ya *Miezi 10*,ndipo mnamo tarehe 3/11/2007 usiku saa 7 nimetoka uwanja wa mpira *Kuomba pale Pugu Boys Sekondari wakati nasoma pale,kufika kitandani Bwenini(Azimio-Bweni langu) Sauti ikaniita,ikaniambia Andika, "Utumishi wa Kweli Katika Kristo Yesu"* nikaandika,nikalala,dakika chache nikaamshwa,nikaabiwa, andika tena, *Jinsi ya Kukabiliana na Nguvu ya wito* nikaandika, nikalala,dakika chache nikaamshwa,nikaambiwa andika tena, *Hatua 7 za Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu*,nikaandika, tena,nikaambiwa andika *Sifa 7 za Mtumishi wa Kweli wa Yesu Kristo*, nikaandika, nikaambiwa tena,andika, *Nguvu kubwa 3 zinazopambana na Huduma ya mtumishi wa Kristo* nikaandika,mambo yote hayo yalifanyika katika usiku mmoja wa tarehe 3/11/2007_.
🌈 Baada ya hapo ndipo nilikuwa na safari ya siku 26 yakuandika *Mafunuo* hayo kwa mkono wangu(tangu tarehe 3-29/11/2007.)haya mambo ndiyo yaliyo ijenga huduma yangu,na kunipa kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu,na mpka sasa natembea kwayo na kuzidi kumuomba Mungu nifikie huko juu zaidi aliko kusudia kunifikisha. Ndiyo maana *_Nakuletea mtiririko wa masomo haya yaliyo badirisha wengi na kuinua wengi,wote walio pata nakala ya somo hili au semina nilikofundisha somo hili wamezaliwa watumishi wakubwa wa Kristo katika huduma._* Nikuombe sasa fuatana nami katika semina hii nawe waweza kuwa miongoni mwa watu watakao inuliwa na Bwana nakuwa watumishi wakubwa katika kizazi hiki cha mwisho,tunapohitimisha safari ya maisha ya dunia, uwe miongoni mwa *_Masazo ya Bwana yanayotumika katika misingi ya Kimungu bila kuchakachua wala kuchakachuliwa kiroho_* kama tunavyoona sasa hali ya makanisa na utumishi inakuwa mbaya siku kwa siku, *Utata ni mwingi,maigizo na vituko kwa wasimama madhabahuni ni vingi* Wewe Uwe Sazo La Bwana la Utumishi Wa Kweli Katika Kristo Yesu.
.....................................
🍇 *Utumishi na Nguvu ya Wito*🍇
🌈 _Sasa nikurudishe katika Kichwa chetu,leo katika sehemu ya 3 tunapoiangalia Nguvu ya wito,namna ya kukabiliana nayo,ili usiishie kupotea,au kujiingiza katika utumishi wa utata. Wengi waliitwa na Mungu ila hawakutulia kujifunza na kuelekezwa, *Moto* ule uchemkao ndani ulipoanza wakalipuka nao,wakaishia kuwa Watumishi feki,wa uganga,ovyo,kila kitu chao kinamaswali ndani yake,waliitwa vizuri na Mungu wakashindwa kujua namna ya kukabiliana na nguvu ya wito,wakaishia kuwa watumishi wa shetani_
🌈 Utumishi ni *Kipawa* cha Mungu ndani ya mtu kinachotumika kutimiza *Mapenzi ya Mungu* siyo matakwa yake(shika neno hilo) KUTIMIZA MAPENZI YA MUNGU.( *Mithali 17:8, 1Wakorintho 15:10*). _Mtume Paulo anasema, kwa Neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo.........._ *Unaweza kuona tunakuwa hivi watumishi wakubwa wa Yesu Kristo kwa Neema ya Mungu* ili tutimize kusudi lake siyo letu. Ndiyo maana hatupaswi kujisifu,na kuuacha unyoofu wa Bwana uliotuweka na kututambulisha kwa watu na kuyaendea matakwa yetu na tamaa zetu.
🌈 *Nguvu ya Wito* ni Mlipuko,msukumo mkubwa wa Kimungu wenye shahuku kubwa mno ya Kutimiza kusudi flani la Kimungu linaloonekana ni kama mzigo ndani ya mtu. *Msukumo huu wa Kufanya kazi* ndiyo huwa chanzo cha watu kuinuliwa wakitembea vizuri na Mungu na hapa ndo wetu *uharibikiwa* maisha yao ya kiroho na utumishi uzikwa hapahapa.
🌈 Wewe mtumishi wa Bwana unayeuendea utumishi wa Bwana, kwanza kabisa LAZIMA ujue kutofautisha mambo haya mawili, *"Kuitwa na Kutumwa"* Mungu hufanya mambo kwa hatua ili azalishe watumishi *Hodari watakao kidhi mahitaji ya kwenye mazingira wanakotumwa* kufanya kazi ya Mungu.
🌈 Sasa basi, Hatua ya kwanza katika utumishi ni *Kuitwa* pale katika kuitwa ndipo palipo na *Interview* baada ya kushinda vipimo katika wito ndipo Mungu uingia hatua ya pili ya *Kumtuma* mtumishi wake.
*_Ni vizuri sasa twende kwa ushahidi wa Maandiko,watumishi kadha wa kadha watusaidie kujifunza safari ya Utumishi,kuitwa na kutumwa_*
🌈 Maandalizi ya kuitwa na kutumwa kwa mtumishi wa Mungu *Musa* ( *Kutoka 2:1-3, 5-6*) maandalizi ya kuitwa kwa Musa katika utumishi yalikuwa magumu sana,lakini tunaona alivuka mpaka akifika hatua ya pili ya kutumwa.
🌈 _Ni dhahiri wengi wetu tunapea msukumo ndani wa kazi ila mazingira yanakuwa changamoto, hapo ndipo inakubidi uwe makini usipoteze kitu hicho kilicho ndani., Unaweza tazama ( *Kutoka 2:11-14*) Musa alitaka kupotelea kwenye wito kabla ya kutumwa,ule moto ulipo chemka ndani akaona nduguze wanateswa na Wamisri akataka kujipa majukumu ya kuwakomboa nduguze,kumbe muda bado, Musa akafanya maamuzi ya *Kuua* ili akomboe nduguze, maamuzi yale yalimgharimu Musa kiasi cha kuwa *Mkimbizi* akatorokea Midiani akiogopa kukamatwa na Farao Misri alikokuwa anaishi._
🌈 Baadhi ya watu kwa kutotulia katika muda wa *Wito* wamejikuta wakiua vipawa vyao,karama zao,huduma zao,vibali vyao walivyo kuwa navyo wengine hata kuacha wokovu au kuanguka dhambini na kupoteza Neema iliyowekwa ndani yao. *_Sasa ni vizuri ufuatane nami katika maono haya aliyo nisemesha Bwana ili ufunguliwe ufahamu wako_* uweze kutumika kwa viwango.
🌈 NB: Ninapo hitimisha sehemu ya 3,niseme hivi, _Ni vizuri kutulia katika wito ili Mungu akupitishe katika ngazi zote za utumishi ili ufikie hatua ya kutumwa na Mungu,endelea kufanya kazi hizo zote nyumbani mwa Bwana ambazo watu wanaziita ndogo ndogo zisizo na heshima,kufagia uwanja wa kanisa,kudeki,kupamba,kusafisha vyoo vya kanisa,kufanya kazi kwa mchunganji nk,hivyo ndovyo vinavyo kujengea Experience(uzoefu)wa Kumsikiliza Mungu na kumpenda Mungu_.
*Ni mimi Mtumishi wa Mungu, Ev Elisha Kazimoto*
Huduma hii na nyingine zinapatikana katika Magroup ya Whatsap kwa no 0755444078.
👉Group la Kuza Huduma Yako
👉Group la Be Strong Spiritually
👉Group la Material Adimu University
👉Group la Psychologicla Healing
👉Group la Bwana nipe Ubavu wangu(wasichana)
Kwa Facebook Elisha Kazimoto na page zake kama tatu.
Hizo ni baadhi ya site nazisimamia na kufundisha.
*_Usikose mwendelezo wa somo hili sehemu ya 4_*
...............................................
*0755444078*
Friday, 18 May 2018
SEMINA - SEHEMU YA 3
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment