🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
_By Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)_
......................................
*_Utumishi wa Kweli katika Yesu Kristo_*
*SEHEMU YA 6*
*_Hatua 7 za Mtumishi wa Kweli wa Yesu Kristo_*
....
....
_Shalom kuhani wa Bwana na mtumishi wa Yesu Kristo,uliye madhabahuni na uliye na wito mkuu wa kuingia katika madhabahu ya Bwana kutumika,leo tuiangalie sehemu ya 6,katika hatua muhimu ambazo lazima uzipitie unapoelekea kutimiza ndoto zako,maono yako ya kutumika_
🍇5⃣ *Kuwa na shahuku ya kukutana na Yesu Kristo katika Huduma yako*, Mtumishi yeyote unayemuona yuko juu,na anendelea kupanda juu kihuduma,jua yakuwa ndani yake Alitengeneza *Shahuku kuu* ya namna huduma yake anatamani iwe,anatamani Yesu Kristo ajidhihirishe kwenye huduma kwa namna ya pekee,anatamani Mungu atukuzwe mno kupitia huduma yake, tofauti na watumishi waliopitia uchochoroni na kuibuka na nguvu kubwa za giza hao,shahuku yao ni *_Ajulikane,awe na heshima kuu,amiliki pesa na vitu vingi,aabudiwe nk_* hao ndo ambao hii hatua hawakuipitia walilipuka na uovu.
🍇Siri kuu ya huduma yoyote kuwa na nguvu na kibali kikubwa,ni *Shahuku ya ndani yako ikoje*,kiwango cha shahuku yako juu ya huduma yako,ndicho kiwango cha Harakati zako za kumtafuta Mungu na ndicho kiwango cha huduma yako itakavyo fanya kazi katikati ya watu.
*_"Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe."_*
(Methali 23:7 )Yohana 7:34-38,
🍇Hii ni dhahiri kuwa huduma yako haitakuwa kubwa kuliko nguvu iliyoko ndani yako. Watu wengi wanatamani huduma kubwa,yenye nguvu,ila shahuku yao ni ndogo ya kutamani Yesu atembee na wewe kwa viwango vikubwa,jitihada na mikakati ya kutembea na Mungu hana,ila anataka huduma kubwa.
NB: *_Tutaiona shahuku uliyo nayo ndani yako kwa kutazama,harakati unazofanya katika huduma yako kuifanya huduma yako itembee na uwepo wa Mungu_* lakini vitu unavyo fanya ili kujijingea uwezo na nguvu ya kutumika.
*_"Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;"_*
(Waefeso 3:20 )
🍇 Bidii yako ndo kwa Mungu,ndo kiwango cha Mungu kujidhihirisha kwenye huduma yako.
(Methali 8 )
------------
17 *_Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona._*
18Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia.
*1Samweli 2:30, 1Mambo ya Nyakati 15:2, Zaburi 18:20*
🍇 6⃣ *Kuwa na Unyenyekevu*, Hii ni hatua muhinu sana mtumishi yeyote anayetaka kutumika chini ya uongozi wa Roho mtakatifu na na kuwa na huduma kubwa na yenye kibali. *_Kuinuliwa kwako kunategemea na kiwango chako cha Unyenyekevu mbele za Mungu na mbele za watu_*
🍇Watumishi wengi wanaoingia katika huduma na walio katika huduma hatua hii imewashinda,ndiyo maana wengi huduma zao zimekufa,wengine wamebaki wakawaida mno shida ni kutokuwa na unyenyekevu.
🍇Wewe unayetamani kumtumikia Mungu kwa viwango, *_Jiombee sana,na jitahidi kuwa mnyenyekevu_* hapo mdipo utaona huduma yako inaanza kushika kasi,ikipanda.
(1 Petro 5 )
------------
6 *_Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;_*
7huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
🍇Mungu anatukuza kwa wakati wake,wengi akiwa na *Kibali kidogo tu, Mwimbaji CD yake ikapigwa sana tu ikapendwa(single),muhubiri wagonjwa 10 wakapona,basi* kila mtu anamuona hana upakao,anaanza kuunda majina ya kuitwa na watu( *Senior,Mashuhuli,Wa kimataifa,......Mkuu nk*) ndugu yangu usipende kujitambulisha sanaa kwa maneno mengii,wacha Bwana akutambulishe kwa Kazi yake atakapoiwekea mkono.( *Mathayo 23:12,Waefeso 5:21*)
🍇7⃣ *Kuwa na Imani Timilifu* Hii ni hatua ya mwisho,katika yale,au katika zile hatua alizonipa Bwana kuhusu huduma. Huduma ya Kiroho inaendeshwa kwa Imani,kuamini juu ya Nguvu na uweza wa Mungu ( *_Yaani leo uoni kitu,ila unanena kitu kikubwa_*) watu wote waliokwisha kuwa na huduma kubwa ukiwauliza watakwambia jinsi walivyo mwamini Mungu katika uwezo wa kuwafikisha pale walipo.
🍇Imani haitoki hewani inatoka katika *kusikia*,unapoanza huduma yoyote kuwa makini na watu unaowasikiliza, *_Si kila mtu wa kumsikiliza,si kila mtumishi wa kumsikiliza_* wemgine ni watumishi mawakala wa adui ukiwasikiliza wanakuvunja moyo kabisa na huduma unaacha. Chagua watu wakusikiliza,wanaoamini katika *Positive*, hapa ni muhimu kuangalia watu wanaoendana na maono yako,na hapa si kila mtu *Umwambie maono yako* wengine wanaweza kukukatisha tamaa mpaka ukaona kana kwamba unacheza kuwaza hivyo unavyoiwazia huduma yako.
🍇Jikite kusikiliza Neno la Kristo na watumishi Hodari katika huduma wasio dhaifu wa imani.
*_"Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo."_*
(Waroma 10:17 )
🍇Uwezo wa kuifanya huduma yako iwe ya pekee ni kuamini katika kile unachokiona ndani yako,ambacho kwa akili ya kibinadamu si rahisi kukitarajia,hao ndiyo watumishi Mugu anapenda kufanya nao kazi na kuwajibu
(Waroma 4 )
------------
18Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
19 *Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani*, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
🍇Mtu mwenye imani katika utumishi wake,utaona ni mtu aliye na imani(anamwamini)Mungu wake sana na hana mashaka naye kwa yale anayomwomba.
*_"Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao."_*
(Waebrania 11:6 )
Soma *Waebrania 10:35,Marko 9:17-22,* ondoa mashaka ndani yao kwa kuangalia mazingira magumu ya utunishi wako,angalia kusudi la wito wa Bwana ndiye awezaye kujenga sura mpya ya ushindi na utukufu.
🍇Unapojipanga katika kuingia kwenye utumishi huu wa Yesu Kristo,jiulize,hivi nimefikia viwango vya kumwangalia Mungu kama Mungu au bado na mwangalia Mungu kama Mungu mtu?
*_"Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa."_*
(2 Wakorintho 13: 5)
_Kufikia hapo niishie hapa katika sehemu ya 6 na katika hatua 7, sehemu inayofuta tutaangalia sifa 7 alizo nazo Mtumishi aliyekatika utumishi wa Kweli wa Yesu Kristo,ili uwe na maombi ya kujiombea umiliki sifa hizo ufae katika *Utumishi wa Madhabahuni pa Bwana aliye hai*_
By Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)
Thursday, 24 May 2018
SEMINA SEHEMU YA 6
SEMINA YA SEHEMU YA 5
🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
_By Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)_
.........................................
*_Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu._*
*SEHEMU YA 5*
*Sifa 7 za Mtumishi wa Kweli wa Yesu Kristo*
......
......
_Shalom mtumishi wa Mungu unayezidi kufatilia somo hili muhimu katika utumishi wa Kristo,tuendelee kuchanganua hatua muhimu katika utumishi,katika sehemu ya 4, tumeangalia hatua ya kwanza ya *Utakatifu* na sasa twende hatua ya pili._
2⃣ *Kujifunza na Kusoma Neno la Mungu* Hii ni hatua muhimu sana kwa mtumishi yeyote wa kweli wa Yesu Kristo. Hii ni kwa sababu *Huduma yoyote iliyo nje ya msingi wa ujuzi na ujazo wa Neno la Mungu ni Batili*
✈Neno ndilo kipimo pekee cha huduma zote,ndimo zilimo *Siri za Kimungu* za huduma zote.
(Wakolosai 3 )
------------
16Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
17Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
.........................................
✈Mtumishi yeyote wa Mungu asiyejikita katika Neno,kusoma au kunifunza basi huduma yake haiwezi kuwa na nguvu ya kupasua anga na kuwa na kibali.
✈Unahitaji uwe na uwezo mkubwa katika huduma yako,hata unapo simama kwa huduma popote katikati ya watu wa level zote za kiroho, *Jibidishe kusoma na kupata mafundisho ya neno la Mungu* neno ndani yake limebeba sauti ya Mungu,limebeba maelekezo,namna uwezavyo kumtumikia Mungu katika unyoofu.
"Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio."
(Methali 30:5 )
.....................................
✈Kusoma neno na kujifunza neno la Bwana,kuna kupa hazina ya maarifa ya kutosha,huduma yako isipwaye.Linakujengea ujasiri na uwezo wa kumjibu kila mtu kwa hekima kwa habari ya tumaini la wito wetu(wokovu).
3⃣ *Kuwa mtu wa Maombi ya Bidii* mtumishi yeyote anayeingia kwenye Tasnia ya Huduma ya kweli ya Yesu Kristo, *_Maombi kwake ni maji,ni dozi_* maombi kwako yasiwe na Likizo. ( _Kuna watumishi wengine,uanza kwa bidii ya maombi,ila wakianza kuona Mungu anatembea nao,miujiza au kibali kikubwa kwa watu,maombi ya kufunga na ya bidii wanaacha_) hiyo siyo kanuni ya kiroho, kanuni ya utumishi wa kweli inasema Omba bila kukoma.
*"ombeni bila kukoma;"*
(1 Wathesalonike 5:17 )
✈Siri hii kwako mtumishi wa Mungu, uliye katika huduma na unaye tamani kuingia, ni kwamba, *_Huduma yoyote,kipawa na karama yoyote unayoijua wewe ina muhusu Mungu aliye hai,basi jua inatunzwa,inatengenezwa kwa maombi ya bidii_* humo ndo utapata siri nyingi,upako wa pekee.
✈Ukiona watu wanatafuta madawa,nguvu za giza ili wapate mvuto,kibali,upako na miujiza jua yakuwa ndo walee wa kula kula,hawana ratiba na Mungu ya kufunga na kuomba.Wanahitaji vitu vya dezo,( *finished issues*)ukizipata na wewe utakuwa *Completely finished*.
✈Pasipo maombi hakuma mafunuo mapya juu yako,wala sura mpya na ya uwepo wa Kimungu. Ukisikia wahubiri au waimbaji wana nena vitu Adimu,mafunuo adimu nyimbo adimu jua wametulia magotini pa Bwana kuomba wanakuja na vitu vipya,vinavyo gusa maisha ya watu na kuwapa majibu.
*Wakolosai 4:2-3,Mathayo 26:41*
✈Kwenye maombi ya bidii ndo tunapata mamlaka ya kuamuru vitu na kuvitiisha chini yetu na vika tii.Fatilia huduma yote ya Yesu pote alipo fanya miujiza, juu yake alitangulia mlimani kuomba. ( *Luka 5:16-18*) Soma na andiko hili umuone binadamu kama wewe...
(Yakobo 5 )
------------
17Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
18Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.
✈Faida ya upako uliopatikana kwa njia ya maombi,kwanza hauchuji,pili autiliwi mashaka maana unafanya huduma ikiwa safii chini ya Roho mtakatifu watu hawajiulizi maswali juu ya unachofanya.
*Mfano maombezi ya saizi ya baadhi ya watumishi yanatuacha hoi,maswali kibao,ni uchafu mtupu wa ngono,wakiuganga,tunajiuliza haya mafunuo yametoka kwa nani?, deliverance ya romance mke wa mtu,mdada imetoka wapi,kushika wanawake maziwa nk nani kakuongoza,kumvua mmama chupi madhabahuni uiombee apate mtoto au mdada aolewe huu ufunuo mbona ni wa ngono tupu?* majibu utayapata huyu si mtu wa magotini niwa upande wa nyenzo za giza.
✈Mtu mwenye upako ORIGINAL raha sana vitu vyake ni nitofauti,muone huyu tu kwenye andiko hili....
(2 Wafalme 13 )
------------
20Elisha akafa, nao wakamzika. Basi vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi mwanzo wa mwaka.
21Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.
..............................................
4⃣ *Uvumilivu* Hii ni hatua ya nne ya Mtumishi wa Kweli wa Yesu Kristo. Huduma iliyo sahihi aihitaji haraka,kutaka kupanda haraka,ujulikane haraka,uwe mtu mkubwa,umiliki vitu vikubwa ghafla, *_Mambo yote ya Kiroho graph ya kukua kwako inaendana na kiwango cho ukuaji wa roho yako._* jiulize unapo patamani hapo na kutaka leo uonekane hivyo tishio je,roho yako umeifanyia hayo iwe kiwango hicho cha tamanio la moyo wako?
(3 Yohane 1 )
------------
1Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.
2Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
✈Mara nyingi watumishi wengi wamejikuta wanaangukia kwenye mikono ya utumiahi wa kishetani kwa sababu ya tamaa,kutaka kuwahi na kujulikana,heshima kubwa,mali nyingi haraka sana bila kufuata kanuni za kiroho. Hiyo ni baada ya kuona kama Mungu hawatimizii matakwa yao,amechelewa....Mungu anafanya vitu kwa wakati wake.
*"ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako."*
(Kumbukumbu la Sheria 11: 14), Waebrania 10:36.
.......................................
*_Leo niishie hapo,usikose kutufatilia katika sehemu ya 6 ya somo hili la utumishi_*
By Ev Elisha Kazimoto( Whatsapp 0755444078)
Friday, 18 May 2018
SEMINA -SEHEMU YA 4
🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
_By Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)_
.......................................
*_Utumishi wa Kweli Katika Kristo Yesu_*
*SEHEMU YA 4:*
*"Hatua 7 za Utumishi wa Kweli Katika Yesu Kristo"*
....
....
....
_Shalom mtumishi wa Mungu uliye shambani mwa Bwana,leo nikusogeze hatua nyingine muhimu sana katika utumishi wa kweli katika Yesu Kristo. Hapa tutaziona *Hatua Muhimu 7 ambazo kila mtumishi unaye muona anatumika katika ofisi yoyote ya Kimungu(Mungu aliye hai) amezipitia. Lakini kwanza kabla ya kuiangalia hatua mojamoja nikurejeshe katika Sehemu ya mwisho ya Nguvu ya wito inavyo unganika na hatua za utumishi_
🌲 *Wito wa Mungu* uambatana na nguvu za Mungu ili kuuandaa moyo wa mtu kuweza kumtafuta Mungu na kutembea na Mungu ili afanye kazi alopewa.
*"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."*
(Matendo 1: 8)
🌲Na nguvu ya Mungu katika wito huleta shahuku ndani ya mtu ya kutaka kufanya kazi. Na hapa ndipo mtu ua za harakati kubwa za Kumtafuta BWANA kwa maombi ya kufunga kwa kasi.( *_Hapa katika kumtafuta Mungu kwa kasi inabidi uwe makini sana_*) wengine wameishia kuzungumza na Shetani na wala siyo Mungu( Nina shuhuda na mifano ya watu wengi).
🌲 Jambo la kujua hapa katika kumtafuta Mungu kwa kasi,ndipo *_Unausogelea ulimwengu wa Roho wenye wafalme wawili Mungu na Shetani_* wote wanafanya kazi katika ulimwengu wa roho,na ukisha fika kule *kila mmoja atataka kusema nawe* changamoto ya wengi hapa ni *Kupambanua sauti* nani anasema naye,kati ya Mungu na shetani.
(1 Yohane 4 )
------------
1Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
2Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
3Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
.........................................
🌲Kwenye eneo hili la kupambanua roho(sauti)unapoanza huduma,ukiwa katika mchakato wa wito unapo mtafuta Mugu kwa kasi, LAZIMA UWE NA MENTOR( Mzazi wa Kiroho aliye makini katika huduma), wengi waliokosea katika Eneo la Kumtafuta Mungu kwa kasi, wameishia *Kuja na Mafunuo feki,machafu,ya uongo,ya ngono,ya utapeli,ya kiuganga,maigizo* lakini ni kweli alifunuliwa,aliongea na Mungu,malaika,akamwelekeza la kufanya katika huduma yake,hiyo siyo shida kufunuliwa, *_Shida ni nani kakufunulia?_*
(2 Wakorintho 11 )
------------
12Lakini nifanyalo nitalifanya, ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi; ili kwamba katika neno hilo wajisifialo waonekane kuwa kama sisi.
13Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
14Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
...........................................
🌲 Ndiyo maana utasikia watu wanasema, *_(Hapana,mtumishi huyu hapana,huyu siye Mungu,haya ni mafunuo ya kuzimu)_* shida imetoka kule hakupata mtu wakumsaidia kutafsiri sauti ile.
(1 Samueli 3 )
------------
4basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.
5Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena.
6Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena.
7Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.
8Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa Bwana ndiye aliyemwita yule mtoto.
...........
...........
*HATUA 7 MUHIMU ZA KIROHO KUZIPITIA*
......................................
1⃣ *Utakatifu* Hii ni sifa ya kwanza kabisa kwa mtu yeyote anayetaka kumtumikia Mungu wa kweli aliye hai, lazima awe *Mtakatifu*,maana hapa unaenda kufanya kazi na Mungu mtakatifu na Roho wake mtakatifu. Sasa huwezi enda kufanya kazi ofisi usiyo kuwa na sifa zake.( *Zaburi 14:2,16:3*)
👉Mungu akipo taka kusema na mtumishi wake au kumtumia kwanza ni kumuagiza *Kuvua viatu/uchafu,tabia zisizo faa ndo amsogelee* Mungu hawasiliani na *mtu mchafu* (Yohana 9:31),ila anaweza toa maelekezo kwa mtu mchafu atafute kutakasika.
(Kutoka 3 )
------------
4Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
5Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
👉Hautaweza mumtumikia Mungu kama huja vua tabia zako za asili na matendo yako yasiyo faa,hata yale unayo yachukulia poa,vua kwanza ndo utumiwe na Mungu.
"Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo."
(Yoshua 5: 15)
👉Kumbuka kwenye huduma,au utumishi madhabahuni pa Bwana,hatupokei tu Maagizo ya Mungu bali tunaongea na Mungu,sasa usipokuwa mtakatifu sawa na Mungu alivyo mtakatifu,hutapata *kuzungumza na Mungu,* ila utapokea maagizo ya Mugu ya kukuonya.
(1 Petro 1 )
------------
15bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
👉Unahitaji kumuona Bwana katika huduma yako? Pigania *Kuvaa vazi la Utakatifu* viwango vyako vya utakatifu,ndo viwango vyako vya kumsogelea Mungu,na unapomsogelea Mungu zaidi ndo unapata *wepesi wa kusikia* haraka pale tu anapo nong'ona nawe,na ndo madhihirisho ya nguvu zake yanatokea.
"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;"
(Waebrania 12: 14)
...............................................
*_Nihitimishe sehemu ya nne,tukutane sehemu ya 5,mafundisho haya na mengine mengi katika nyanja mbali mbali yanapatikana kwenye magroup yangu ya Whatsapp na facebook kwa no.0755444078_*
SEMINA - SEHEMU YA 3
🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
_By Ev Elisha Kazimoto_
WhatsApp 0755444078
...................................
*_Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu_*
*SEHEMU YA 3*
*"Namna ya Kukabiliana na Nguvu ya Wito"*
...
...
_Karibu tena katika sehemu ya tatu,taratibu tunaanza kuingia ndani ya somo letu linalo itwa, *"Utumishi wa Kweli Katika Kristo Yesu"* maana yake nini,mtu yeyote anayejipanga kumtumikia Mungu,au yupo katika Tasnia ya Huduma Takatifu ya Madhabahuni lazima tutamuona katika misingi hii nitakayoielezea hapa. Labda kwanza nikupe chimbuko la Somo hili_.
....
....
🌈 _Mnamo mwaka wa 2007 ndani yangu kulikuwa na fukuto kubwa sana la kutumika,lililoanza mwaka 2006 mwezi December 29 katika mkesha mkubwa wa Vijana wa wilaya Dar es Salaam TAG Magomeni kwa kuitwa na Bwana akimtumia mtumishi wake kwa neno la kinabii,nikatoka mbele nakuwekewa mikono kwa machozi mengi,tangu siku hiyo ndani yangu kulianza kuwaka moto wa kutumika katika huduma ya *Uinjilisti na Ualimu wa Neno la Mungu*,lakini moyoni mwangu kulikuwa na maswali mengi sana ya nitafanyaje,nitasimamaje,nani atanishika mkono kunikuza huduma yangu,nitatembeaje na Mungu kwa viwango ninavyo vitamani,maswali hayo yalinitesa sana zaidi ya *Miezi 10*,ndipo mnamo tarehe 3/11/2007 usiku saa 7 nimetoka uwanja wa mpira *Kuomba pale Pugu Boys Sekondari wakati nasoma pale,kufika kitandani Bwenini(Azimio-Bweni langu) Sauti ikaniita,ikaniambia Andika, "Utumishi wa Kweli Katika Kristo Yesu"* nikaandika,nikalala,dakika chache nikaamshwa,nikaabiwa, andika tena, *Jinsi ya Kukabiliana na Nguvu ya wito* nikaandika, nikalala,dakika chache nikaamshwa,nikaambiwa andika tena, *Hatua 7 za Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu*,nikaandika, tena,nikaambiwa andika *Sifa 7 za Mtumishi wa Kweli wa Yesu Kristo*, nikaandika, nikaambiwa tena,andika, *Nguvu kubwa 3 zinazopambana na Huduma ya mtumishi wa Kristo* nikaandika,mambo yote hayo yalifanyika katika usiku mmoja wa tarehe 3/11/2007_.
🌈 Baada ya hapo ndipo nilikuwa na safari ya siku 26 yakuandika *Mafunuo* hayo kwa mkono wangu(tangu tarehe 3-29/11/2007.)haya mambo ndiyo yaliyo ijenga huduma yangu,na kunipa kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu,na mpka sasa natembea kwayo na kuzidi kumuomba Mungu nifikie huko juu zaidi aliko kusudia kunifikisha. Ndiyo maana *_Nakuletea mtiririko wa masomo haya yaliyo badirisha wengi na kuinua wengi,wote walio pata nakala ya somo hili au semina nilikofundisha somo hili wamezaliwa watumishi wakubwa wa Kristo katika huduma._* Nikuombe sasa fuatana nami katika semina hii nawe waweza kuwa miongoni mwa watu watakao inuliwa na Bwana nakuwa watumishi wakubwa katika kizazi hiki cha mwisho,tunapohitimisha safari ya maisha ya dunia, uwe miongoni mwa *_Masazo ya Bwana yanayotumika katika misingi ya Kimungu bila kuchakachua wala kuchakachuliwa kiroho_* kama tunavyoona sasa hali ya makanisa na utumishi inakuwa mbaya siku kwa siku, *Utata ni mwingi,maigizo na vituko kwa wasimama madhabahuni ni vingi* Wewe Uwe Sazo La Bwana la Utumishi Wa Kweli Katika Kristo Yesu.
.....................................
🍇 *Utumishi na Nguvu ya Wito*🍇
🌈 _Sasa nikurudishe katika Kichwa chetu,leo katika sehemu ya 3 tunapoiangalia Nguvu ya wito,namna ya kukabiliana nayo,ili usiishie kupotea,au kujiingiza katika utumishi wa utata. Wengi waliitwa na Mungu ila hawakutulia kujifunza na kuelekezwa, *Moto* ule uchemkao ndani ulipoanza wakalipuka nao,wakaishia kuwa Watumishi feki,wa uganga,ovyo,kila kitu chao kinamaswali ndani yake,waliitwa vizuri na Mungu wakashindwa kujua namna ya kukabiliana na nguvu ya wito,wakaishia kuwa watumishi wa shetani_
🌈 Utumishi ni *Kipawa* cha Mungu ndani ya mtu kinachotumika kutimiza *Mapenzi ya Mungu* siyo matakwa yake(shika neno hilo) KUTIMIZA MAPENZI YA MUNGU.( *Mithali 17:8, 1Wakorintho 15:10*). _Mtume Paulo anasema, kwa Neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo.........._ *Unaweza kuona tunakuwa hivi watumishi wakubwa wa Yesu Kristo kwa Neema ya Mungu* ili tutimize kusudi lake siyo letu. Ndiyo maana hatupaswi kujisifu,na kuuacha unyoofu wa Bwana uliotuweka na kututambulisha kwa watu na kuyaendea matakwa yetu na tamaa zetu.
🌈 *Nguvu ya Wito* ni Mlipuko,msukumo mkubwa wa Kimungu wenye shahuku kubwa mno ya Kutimiza kusudi flani la Kimungu linaloonekana ni kama mzigo ndani ya mtu. *Msukumo huu wa Kufanya kazi* ndiyo huwa chanzo cha watu kuinuliwa wakitembea vizuri na Mungu na hapa ndo wetu *uharibikiwa* maisha yao ya kiroho na utumishi uzikwa hapahapa.
🌈 Wewe mtumishi wa Bwana unayeuendea utumishi wa Bwana, kwanza kabisa LAZIMA ujue kutofautisha mambo haya mawili, *"Kuitwa na Kutumwa"* Mungu hufanya mambo kwa hatua ili azalishe watumishi *Hodari watakao kidhi mahitaji ya kwenye mazingira wanakotumwa* kufanya kazi ya Mungu.
🌈 Sasa basi, Hatua ya kwanza katika utumishi ni *Kuitwa* pale katika kuitwa ndipo palipo na *Interview* baada ya kushinda vipimo katika wito ndipo Mungu uingia hatua ya pili ya *Kumtuma* mtumishi wake.
*_Ni vizuri sasa twende kwa ushahidi wa Maandiko,watumishi kadha wa kadha watusaidie kujifunza safari ya Utumishi,kuitwa na kutumwa_*
🌈 Maandalizi ya kuitwa na kutumwa kwa mtumishi wa Mungu *Musa* ( *Kutoka 2:1-3, 5-6*) maandalizi ya kuitwa kwa Musa katika utumishi yalikuwa magumu sana,lakini tunaona alivuka mpaka akifika hatua ya pili ya kutumwa.
🌈 _Ni dhahiri wengi wetu tunapea msukumo ndani wa kazi ila mazingira yanakuwa changamoto, hapo ndipo inakubidi uwe makini usipoteze kitu hicho kilicho ndani., Unaweza tazama ( *Kutoka 2:11-14*) Musa alitaka kupotelea kwenye wito kabla ya kutumwa,ule moto ulipo chemka ndani akaona nduguze wanateswa na Wamisri akataka kujipa majukumu ya kuwakomboa nduguze,kumbe muda bado, Musa akafanya maamuzi ya *Kuua* ili akomboe nduguze, maamuzi yale yalimgharimu Musa kiasi cha kuwa *Mkimbizi* akatorokea Midiani akiogopa kukamatwa na Farao Misri alikokuwa anaishi._
🌈 Baadhi ya watu kwa kutotulia katika muda wa *Wito* wamejikuta wakiua vipawa vyao,karama zao,huduma zao,vibali vyao walivyo kuwa navyo wengine hata kuacha wokovu au kuanguka dhambini na kupoteza Neema iliyowekwa ndani yao. *_Sasa ni vizuri ufuatane nami katika maono haya aliyo nisemesha Bwana ili ufunguliwe ufahamu wako_* uweze kutumika kwa viwango.
🌈 NB: Ninapo hitimisha sehemu ya 3,niseme hivi, _Ni vizuri kutulia katika wito ili Mungu akupitishe katika ngazi zote za utumishi ili ufikie hatua ya kutumwa na Mungu,endelea kufanya kazi hizo zote nyumbani mwa Bwana ambazo watu wanaziita ndogo ndogo zisizo na heshima,kufagia uwanja wa kanisa,kudeki,kupamba,kusafisha vyoo vya kanisa,kufanya kazi kwa mchunganji nk,hivyo ndovyo vinavyo kujengea Experience(uzoefu)wa Kumsikiliza Mungu na kumpenda Mungu_.
*Ni mimi Mtumishi wa Mungu, Ev Elisha Kazimoto*
Huduma hii na nyingine zinapatikana katika Magroup ya Whatsap kwa no 0755444078.
👉Group la Kuza Huduma Yako
👉Group la Be Strong Spiritually
👉Group la Material Adimu University
👉Group la Psychologicla Healing
👉Group la Bwana nipe Ubavu wangu(wasichana)
Kwa Facebook Elisha Kazimoto na page zake kama tatu.
Hizo ni baadhi ya site nazisimamia na kufundisha.
*_Usikose mwendelezo wa somo hili sehemu ya 4_*
...............................................
*0755444078*
Wednesday, 16 May 2018
UNAMCHUMBA MPAGANI NA UMEOKOKA
🔥 *MADA INAYOWAPA KIZUNGUZUNGU WATU WALI HAI NUSU NA MAREHEMU NUSU*🔥
..............................................
Yupo kwenye mahusiano ya muda mrefu na mwenzake ila wametofautiana kwenye dhehebu. Yeye ni mlutheri(na ameokoka), mwanaume ni mkatoliki (na hajaokoka). Binti hayupo teyar kumfuata mwanaume na mwanaume vivyo hivyo. Kadir siku zinavyoenda na mwanaume anaona kuwa binti kasimamia misimamo wake, akamwambia binti hivi, akubali wafunge ndoa ya kikatoliki, then wakiwa ndani ya ndoa yeye atabadilika na kuwa mlutheri. Sasa hapo, ndio pamemuacha binti, njia panda. Haelewi afanye nini, haelew akubaliane nae au akatae...
Uhusiano wao una miaka 6 sasa, na tatizo liko hapo tu. Wanapendana na wanaelewana vizuri
..............................................
*_Anajibu Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)_*
Hii mada inahitaji,utulivu katika kuichambua,ni mada ngumu isiyo hitaji ushauri au majibu mepesi. Vitu vya kisaikolojia au kiroho ni vitu vigumu kweli inapokuja kuvifanyia maamuzi.. *.kwanza mada hii Muhusika ni mtu mmpja tu,ndo anastahili kujadiliwa naye ni Binti*
👉Kwa maneno yake haya, *"Nipo kwenye mahusiano na kijana mimi ni Mlutheri(na nimeokoka),kijana Romani(Hajaokoka) mpka hapo tu,* _Inaonyesha mambo kama 3/4 kwa binti._
1.Binti hajui maana ya wokovu na hajawai kuokoka,ila amejipa jina la kuokoka kama FASHION.
2.Binti hajui maana ya ndoa na ndoa ya baraka na amani i atoka kwa nani.
3.Hakuzingatia kigezo chochote cha kiroho kumpata mme ila amempata kwa tamaa za mwili ikiwemo ngono,pesa,elimu,au uzuri.
4.Kiroho yuko 0% hawezi kutofautisha mapenzi ya Mungu na ya shetani, haki na dhambi,uchafu na utakatifu.
👉Pili kwa sentensi ya*Binti hayuko tayari kumfuata mme na mme hayuko tayari kumfuata binti* ni ishara kwamba binti Ni miongoni mwa waumini matapeli wa kiroho wanao shawishi watu wawafuate kwaajili ya kutimiza matakwa yao.
"Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,"
(1 Wakorintho 2: 4)
Msingi wa wokovu haufungamani na kuwaleta watu kwa Yesu kwa njia ya ushawishi,yaani kutumia pesa,vitu au mifump kama ya ndoa au ajira. Binti anadhihirisha wazi,kama kijana atasema *NAHAMIA* huko binti atakuwa tayari kuolewa. Swali la msingi,ni kijana amevutwa na injili ya Kristo au na mapenzi, kijana hataki kuukosa uzima wa milele au hataki kumkosa mdada mwenye shape hiyo..
3.Binti anasema, *kadri siku zinavyoenda kila mtu anamsimamo wake,hapo ndo panamuacha hoi hajui afanyeje* kwa sentensi hii Binti ndani yake ni marehemu wa Kiroho,yaani hana hata Alarm ya mbali ya Roho mtakatifu wa kumshauri lipi ni mapenzi ya MUNGU (Ndo maana nikasema Hawa wote *Niwapagani,ila MPAGANI SENIOR ni dada, Huyu kaka ni Mpagani JUNIOR*)
(Waroma 8 )
------------
9Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
...
14Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
...
16Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
Kwa lugha nyingine huyu dada ni msanii mwigizaji wa wokovu ila hana maisha ya UCHAJI MBELE ZA MUNGU. ( *SI MUHUKUMU ILA NASEMA NIKIONACHO KWA MUJIBU WA BIBLIA*) Maana wale wajifanyao wako Rohoni zaidi ya YESU hawachelewi kusema _USIHUKUMU_.
👉Hakuna mtu yeypte DUNIANI aliye okoka,ana Roho wa Mungu ndani yake,akafanya maamuzi ya kijinga na kishetani,bayo mpaka mtu aliyeokoka leo au mpagani anasema si sahihi.... Hayupo,ukimuona huyo jua ni BANDIA WA WOKOVU.
*MASWALI YA KUMUULIZA HUYO DADA*
1.Amempataje huyo kwa Mungu au kwa mtaani?
2.Miaka 6 anaombea uchumba au anaendesha uchumba kwa pesa na mapenzi?
3.Miaka 6 kwa mru asiyeokoka wawezaje kumzuia asifanye ngono( *je, ni kweli hajawahi kulala naye huyo kijana hata mara 1?) si jambo la hajabu ngono kwa mtu ambaye hajaokoka mwana dini ni BREAKFAST* si shida,si dhambi,hakuna hukumu,hakuna kujuta, ndiyo life style ya watu wa ufalme huo na wanajisifu kwa zinaa.
*NITARUDI KUHITIMISHA KWA LECTURE*
Kijana huyu hana kosa,wala shida,maana yeyote aweza oa atakaye jiingiza ndani ya 18 zake,hana limit ila tulio okoka tuna limit.
*"Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote."*
(1 Wakorintho 6: 12)
.
.
*_HIVI HIKI KIZAZI MBONA KINAPENDA KURAHISISHA SANA MAMBO HAYA YAHUSUYO IMANI KATIKA WOKOVU_*???!
Mtume Paulo akifufuka sasa ataliongoza kanisa la sasa,kama zamani zile alitaka kutia watu fimbo leo ingekuwaje watu wanavyo rahisisha mambo ya Mungu.
(1 Wakorintho 4 )
------------
20Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.
21Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole?
*_Inapofikia suala la kuizungumzia imani ya Wokovu,hatutamungunya maneno,japo wengi Wakristo feki wanaichukia kweli,wanahitaji utumie Hekima kuuubwa sana uovu uupe sura ya changamoto,Injili hiyo Mungu na aniepushie mbali katika utumishi wangu_*
WhatsApp 0755444078
KUOANA NA MPAGANI
*UKWELI KUHUSU KUTAKA KUOANA NA MTU WA IMANI NYINGINE*
👉Kwanza naomba ifahamike kuwa ndoa ni Taasisi nyeti sana isiyo hitaji kubumba bumba mambo,na hapa lazima kweli ya Mungu iwe dhahiri ili kama unafanya maamuzi ufanye maamuzi ukijua madhara au faida ya ndoa *MIXTURE* Maamuzi yako ya sasa ndo maisha yako ya baadaye.
_Ziko sababu nyingi za kwa nini Usioane na Mtu wa Imani Tofauti na wewe hasa kama wewe ni wa Imani ya Wokovu kwanjia ya Yesu Kristo na unayahishi maisha hayo ya wokovu_
2KORINTHO 6:14-17
14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
👉Mstari wa 15, Kuamini ni nguzo kubwa katika imani na ndicho hutofautisha imani moja na NYINGINE,dini moja na nyingine na hapa ndo kutofautiana katika mwelekeo.
👉Suala la wote ni Wakristo halina nguvu katika imani,maana humo humo kwa Kristo hutofautiana katika Imani(kuamini)
*_Kuna wanao amini maombi kwa wafu,wengine hapana,wengine wanaamini katika kuwa watakatifu ni baada ya kufa,wengine wanaamini utakatifu ni hapa duniani Zaburi 16:3,wengine wanaamini katika kuwaombea walio kufa waingizwe peponi,wengine mtu akifa amekufa ataenda sawasawa na alivyoishi duniani,wengine wanaamini ubatizo wa watoto,wengine watu wazima waliokiri kwa kinywa kumpokea Yesu,wengine wanaamini ujazo wa roho mtakatifu na kunena kwa lugha,wengine haina haja,wengine wamaamini ukifa imeishia hapo,wengine kuna maisha ya kufa,wengine tutakaa duniani milele,wengine kuna mbingu mpya na nchi mpya(mbinguni),_*
Haya ndo baadhi ya mambo yanayo tofautisha Ukristo,yako mengi ni muda tu umezuia,sasa ona athari hizi....
👉Hapa si zungumzii Uana Dini(yaani kuwa Mkristo) nazungumza Mtu aliyefanya maamuzi binafsi ya Kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako kwa kutubu na dhambi zako na kuziacha,si suala la kuabudu kwakuwa nimekuta wazazi wangu walokole...hiyo ni uana dini ndo huwa wanashika dini ya baba na mama na hawataki kuhiasi,ila Si kwamba walikutana na Injili ikachoma mioyo yao wakaamua kukimbilia Yesu na kuacha njia zao mbaya wamepokea imani kwa wazazi huo si wokovu wala haupo kwenye biblia( Hao wanaweza oana na mtu yoyote wa aina hiyo,haijalishi wa dhehebu gani au dini gani)
👉Katika Imani ya Wokovu wa Yesu Kristo(Kuokoka) ina msingi huu katika kuoana...
*_Amosi 3 : 3 - Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?_*
Kama hampo imani moja,hamuamini katika imani moja(sawasawa *Waefeso 4:1-6* hamuwezi kuoana labda kama wote mna wokovu wa Kifafa,yaani anaye sema ameokoka wokovu wake ni kifafa huyo anaweza fanya maamuzi hayo)
👉Tatizo linalo wasumbua na kuwachanganya vijana wengi sasa, *Kwa sasa kila dhehebu wanasema na sisi tumeokoka* lakini kwa uhalisia *Hawajaokoka wala hawana mpango wakuishi maisha ya wokovu* ila lugha hii ya kuokoka imezuka miaka ya hivi karibuni 10 tu kutoka sasa,kabla ya hapo ilikuwepo lugha ya Mimi dini yangu ni hii,na hao ni dini ya walokole (walokole) sasa ona shida hii...
👉Kuna uongo na utapeli wa kujifichia nyuma ya *Mungu,Amani ya Kristo,Roho kasema,Kufunuliwa* ifahamike kabisaa hakuna hata chbe ya ukweli Mungu,Roho mtakatifu kusema na mtu wa Mungu kuoana na mtu Asiye Amini(Okoka),Mungu si maskini kiivo mpaka aazime mtu upande wa pili kpatia mtu wake mtu Asiye sawa kiimani,lakini Issue ya amani,kuna *Amani ya Nafsi,Amani ya Shetani,Amani ya Hisia,na Amani ya Roho wa Kristo* je unajua kuzotofautisha?au ndo kumpakizia Mungu?
👉 Kuoana na mtu wa imani tofauti(yaani mnaamini tofauti) mfano 1 nitumie... *Wewe waamini ubatizo wa mtuzima na maji mengi(mke),na mme anaamini ubatizo wa watoto na maji machache* saaa fikiria mkipata mtoto anaishi imani ipi,je,nani anakubali kuipoteza imani yake aifuate ya mwenzake? Na endapo unaamua kuipoteza imani yako kwaajili ya ndoa, *Inaama imani yako ilikuwa Batili na wewe ulikuwa batili* Ndo zile imani za kukuta baba na mama wanaabudu imani flani na wewe ukadaka hiyo(si zungumzii dhehebu...mfano EAGT,TAG,FPTC haya ni madhehebu ila imani ni moja)no peoblem au (RC na Karithematic)ni kitu kimoja.
Mtoto huyu mtampoteza,malezi yatakuwa feki,kuna mmoja aliye na nguvu atalazimisha afuate misingi yake,mtoto atakuwa kama yatima mwenye mzazi mmoja na andiko la Mithali 22:6 halita timia kwake. Kwanini mchome kizazi chenu watoto wasiyo na hatia kisa mahaba yenu yasiyotokana na Mungu? Oana na mtu wa IMANI MOJA kama ni wapagani wapagani,kama wana dini,wana dini,kama Mlio wateule wa Kristo muwe wote wateule wa Kristo.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
SEMINA-SEHEMU YA 2
🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
_By Ev Elisha Kazimoto._
Whatsapp 0755444078
.................................................
*SEHEMU YA 2*
_Haleluya mtumishi wa Mungu nakukaribisha tena katika Meza ya Maarifa ili upate hazina za kukuongoza katika utumishi ulio ndani yako_.
..
..
*_"Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu."_*
(Isaya 60: 7)
...............................................
👉Unapojiandaa kwa utumishi,ni muhimu kujua kuwa, *Hatuipandi madhabahu ya Bwana kwa Mazoea,au tunapo jisikia,tunaipanda KWA KIBALI CHA BWANA* na wote walioipanda madhabahu ya Bwana kwa Kibali cha Bwana huduma zao zimekuwa na Impacts(Matokeo chanya).
👉Tuna huduma nyingi za watu wanafanya kama desturi,hazina mguso wa ndani,zina mguso wa hisia,hazina mlipuko wa nguvu za Mungu bali zina mlipuko kelele za ushabiki. Lakini Huduma yoyote ya Bwana Yesu ililenga ilete Mageuzi katika mioyo ya watu,mazingira na kumletea Kristo utukufu. Lakini huduma nyingi sasa zinepoteza *Harufu ya Uwepo wa Mungu* ndiyo maana tuna waigizaji,tuna watumia Nguvubza Giza ili kuwashawishi watu waone Matokeo ya Injili.
*_"Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe."_*
(Waebrania 2: 4)
...................................................
👉Unaweza kuona,tangu mwanzo enzi za mitume Yesu Kristo aliambatana nao katika huduma walizofanya mitume kila walipo kanyaga.
👉Je, unajipanga kufanya huduma *_Kawaida au Huduma ya Tofauti yenye Impacts katika maisha ya watu na ufalme wa Kristo_*? Wewe ambaye ndani yako kuna mzigo wa kufanya huduma, *Tulia Magotimi pa Bwana* uamze huduma yenye Mguso wa Kimungu.
👉Tatizo kubwa la Injili *Feki,na mafundisho feki,uimbaji feki* tulio nao sasa ni watu Kukurupuka na kuingia kwenye huduma bila kutulia magotini mwa Bwana,wanajikuta wamepwaya katika tasnia hiyo,uwezo wa kuonyesha matokeo ya Kimungu hawana,ushindani ni mwingi kwenye mazingira, *_Ndo chanzo cha kutafuta njia mbadala za upako wa kishetani na kufanya ujanja ujanja tu wa kihuni_* tofauti na Misingi ya Neno la Mungu na Maadili ya wokovu.
👉Inawezekana kabisa kutembea na huduma yenye upako,kibali na mguso wa Kimungu bila ujanja wowote,uhuni wowote,wala nguvu mbadala yoyote ya kipepo, lakini lazima upate Maarifa ya Msingi ya kukuongoza katika kuifikia huduma yenye Ukweli na Usafi,maana zama hizi,unaingia kwenye huduma kama mwana kondoo katikati ya mbwa mwitu.
*_"Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua."_*
(Mathayo 10:16 )
...............................................................
👉 Mtumishi wa Mungu unayeingia kwenye huduma shika sana sentensi hiyo ya Yesu, *_"Nawatuma kama kondoo,kati ya mbwa mwitu"_* unayeanza huduma shika sentensi hii ili uwe salama katika huduma yako.
👉 Kuna mbwa mwitu kwenye huduma, *_Mbwa mwitu zinazotunia viambata na kuvitukuza(mafuta,chumvi,maji,sabuni,nk) kila maombezi bila jina la Yesu,mbwa mwitu wanaotunga nyimbo Zisizo mtaja Yesu mwanzo hadi mwisho(jiulize wana mtukuza nani,au biashara?),mbwa mwitu wanaoendesha deliverance kwa ngono,romance nk,mbwa mwitu wanao pachika maneno ya Kimungu kwenye biti ya msanii wa bongo fleva,mbwa mwitu wanao fanya futuring kuimba gospel(nyimbo za kumsifu na kumwabudu Mungu akiwa na mwana muziki wa bongo fleva,mbwa mwitu,anaye toa unabii feki,mbwa mwitu aneye jitukuza yeye katika kufanya miujiza bila kumtukuza Mungu,mbwa mwitu wanaofundisha mafundisho potofu ya kutukuza mtu,dini na kuudharau wokovu_* hao ndiyo unaoenda kufanya nao kazi. Swali: *Wewe umejipangaje*? Utafuata mkumbo wa hao mbwa mwitu au uanjipanga kumdhihirisha Yesu Kristo kama alivyo.
👉Huduma ya Yesu Kristo inaenda kwa kanuni,hatua kwa hatua,ila huduma feki zinaota kama uyoga,zina michanganyo nyingi na ushawishi mwingi usiotokana na Mungu.
👉 Huduma sahihi ya kweli ya Yesu Kristo,ndani yake haina ushawishi,imebeba nguvu(pumzi ya Mungu)ya kuponya,kubariki na kuinua,lakini injili (huduma)zilizovamiwa zina ushawishi mwingi ndani yake zinapofanyika wa kuvuna pesa,heshima na uovu(zinaa). *swali,ni je wewe unajipanga kuwa na huduma gani?*
_"Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,"_
(1 Wakorintho 2: 4)
................................................
👉Kumbuka Huduma ya Kimungu iliyo ya kweli, *Aihitaji nguvu sana za kimwili na kujipambania ili ujulikane,uwe na heshima au nguvu,inakuhitaji kutulia,kujifunza,kufufuata kanuni za kiroho utapanda,utaheshimika na utabarikiwa na Mungu mwenyewe* hii ndo huduma ya kweli unayoiendea kama wewe si mbwa mwitu.
*_"Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu."_*
(Yohane 12: 26)
_Basi kufikia hapo ni hitimishe sehemu ya pili ya Somo hili la Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu, Usikose sehemu ya 3 ya Namna ya Kukabiliana na Nguvu ya Wito katika hudum yako uanyoiendea_.
*By Ev Elisha Kazimoto(WhatsApp 0755444078)*
Tuesday, 15 May 2018
SEMINA-SHEHEMU YA 1.UTANGULIZI
🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
_By Ev Elisha Kazimoto_
Whatsapp 0755444078
......................................
*UTANGULIZI*
_UJUE UTUMISHI WA MADHABAHU YA BWANA ALIYE HAI_
...
...
_Shalom watu wa Mungu alie hai,nikuombe sasa ukae mkao wa kupokea kitu kutoka kwa Bwan wewe uliye katika hema hii ya Bwana,uliye na mzigo na kazi ya Mungu,kuna vitu Mungu atasema nawe,na utajengwa na kuwa mtumishi wa viwango vinavyo takikana mbele za Mungu na Mbele za watu( *Mithali 3:4-5*).Fuatilia mfululizo wa masomo haya soku kwa siku ujipange kumtumikia Mungu aliye hai. Somo langu kuu ni :UTUMISHI WA KWELI KATIKA KRISTO YESU,hilo ndo somo tutalichambua kwa kina,ila kwa sasa mwanzo wa semina hii kuna vitu nataka nikuwekee kama msingi,hasa wewe ambaye *Bado unachipuki katika utumishi na unatamani kwenda mbali* kuna misingi Roho mtakatifu anahitaji akuwekee_.
✍Kwanza utumishi huu unaouendea, na ulio nao siyo *_Deal la mwanadamu,eneo la kutokea kimaisha,au kujiegesha baada ya kustaafu,au kupotezeapo muda baada ya kukosa ajira au la kufanya,siyo eneo la kujichomeka,ni eneo Takatifu,Ni Kipawa unapewa na Mungu aliye juu kwaajili ya Kuujenga mwili wa Kristo,na siyo kujenga maisha yako_* (Waefeso 4:11-12). Yaani Mungu anapokupa Hudum,Kipawa(Karama yoyote)analenga isaidie kuujenga mwili wake yaani Kanisa ili kukamilisha Kusudi la Ukombozi wa mwanadamu pale msalabani.
*_"Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa." (Methali 17: 8)_*
✍Mungu anapoweka mzigo wowote ndani yako,anakuwa ameuwekea vipimo vya kutosha kukuhakikishia kila eneo,kona,mahali utakapo Simama kuhudumia watu wa Mungu kwa huduma yoyote ile watu wanabarikiwa,Matokeo yanaonekana ya Kipawa chako(Gift)alichokupa Mungu) *_Kazi yako ni kutambua kipawa ukichopewa na Mungu na kukikuza kwa kanuni za Kimungu,utaona kinavyo fanya kazi kwa viwango vikubwa popote pale_* kipawa cha Mungu kina cover dunia yote( _Kila kigeukapo ufanikiwa_).
✍Changamoto kubwa ya huduma nyingi hasa katika zama hizi,ni *_Huduma za kujipa,kujipachika,kutafuta sifa,kupata eneo la kutokea kimaisha,mahali pa kujipatia mahitaji ya tamaa zako,mahali pa kushindana na mwenzako,ni za kuangalizia(kuiga ili mrafi upate watu wa kukuunga mko)_* tumeacha Huduma za KUITWA NA MUNGU,kusikia Mzigo mkubwa wa kufanya kazi ya Mungu na unapozembea au kutoifanya unakosa AMANI kabisa na unataabika moyoni. Huma hizo zimekuwa Adimu.
✍Changamoto nyinginw tumekuwa na wimbi la Wahuni tu wa kidunia wapagani ambao hana neno la Mungu lolote ndani,wamekimbilia kanisani siyo kuokoka na kumtumikia Mungu,ila kupiga madili na kujinufaisha wao na familia zao, ndiyo maana tuna watu wanao *Tumika chini ya nguvu za giza,ushirikina,madawa,kafara na waabudu shetani huku wakitumia kivuli cha Wokovu* ndani yao hawana mzigo na kondoo wa Bwana na utukufu wa Mungu,wao wana mzigo na kupata mahitaji yao waliyoyakusudia na heshima yao.
✍ Sasa ndugu mtumishi wa Mungu unaye jiandaa kuingia katika utumishi huu wa Kristo ni vizuri ukajipima kuwa *Shahuku yako,Mzigo wako upo wapi:*
1.Kupata fedha
2.Heshima
3.Kushindana
4.Uonekane na watu
5.Na wewe upo na kazi ya kukuweka busy
6. _Kuujenga mwili wa Kristo na kumzalia Yesu Matunda,na kuiandaa taji yako ya uzima._
Tafakari na uendelee kufuatana nami katika semina hii upate kitu cha kukusaidia kutimiza shahuku yako.
✍ Huduma ni kama mbegu,inapandwa,inaota,inakuwa mpaka kutoa matunda mengi,huwenda huduma yako ilo kama mbegu moyoni mwako,mwingine imeanza kuota,mwingine imeisha weka majani na matawi,mwingine maua yamechanua,mwingine matunda yaeweka hayajaiva,mwingine tayari watu wanachuma kwa kasi matunda, hivo usiwe na haraka au wivu,au kutafuta njia za mkato za kuivisha matunda wakaati bado ndo mche unaota majani,tulia fuata kanuni za kiutumishi, *Uivishe kwa wakati* hapo ndo utafurahia utumishi wako wenye faida.
........................................................
*_Hii ni sehemu ya kwanza ya semina,katika somo letu la utumishi wa wa Kweli katika Kristo,usiache kufatilia somo hili mpaka mwisho. Ni mimi Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078
UNIOE HARAKA NISIKOSE MTOTO
*MADA YENYE UTATA KISAIKOLOJIA NA KIROHO*
_Soma chini ya mada ufafanuzi wa Msaikolojia Mtaalamu wa Mahusiano na ndoa Ev Elisha Kazimoto_
Whatsapp 0755444078
*MADA*
Wote tumeokoka Mimi na huyu mdada, tumekuwa kwenye mahusiano muda mrefu sana almost miaka mi2 bila matatizo.
Juzi mdada kaenda hospitali kupima kaambiwa ana matatizo kwenye mfumo wa uzazi ambayo kama hatozaa hivi karibuni basi anaweza asipate mtoto kabisa. Kaja kaniambia nimuoe haraka sana ili azae asije kufa bila mtoto na Mimi nikiangalia mambo yangu mambo sijajipanga kuoa mwaka huu. Amekuwa mwaminifu sana kwangu Nani nimekuwa mwaminifu kwake muda wote ila kasema kama nikikataa kumuoa atatafuta MTU yeyote amuoe ili wazae nae mtoto na Mimi aniache. Wazazi wake wamemkubakia kufanya chochote ikiwa hata kuacha na Mimi na nikiangalia naona kweli kadhamiria kuolewa. Mimi nna miaka 29 yeye ana miaka 26.
Nifanyeje doctor Nioe ivoivo bila kujipanga au nimwache aende tuu.?
.................................................
*Hii mada Inahitaji utulivu mkubwa maana ina HOLD Effects za pande mbili kiroho na kisaikolojia.*
👉Kwanza niweke sawa mambo kadhaa kuhusu mahusiano ya kiuchumba kuelekea ndoa ili pasiwepo mtu wa kulamiwa katika pande hizi zote mbili ya msichana na mvulana.
👉Kwanza,Mahusiano ya uchumba ni jambo la makubaliano baina ya pande mbili,nini kifanyike na kifanyikeje na kwa muda gani,ni suala la makubaliano ya watu wawili kulingana na malengo yao.(Kwa mantiki hiyo,hawa watu nigekuwa nawafanyia Pdychological Counseling ofisini swali langu la msingi lingekuwa, Je,Mpango wa uchumba wenu mlikusudia myoane lini?baada ya mazingira gani kuwepo?).
*_Kwa maana kama mliweka makubaliano ya kuoana baada ya muda flani na vigezo vya muda huo mliona vina faa,basi kisaikolojia Kubadirisha muda inategemeana na jambo lililowafanya mbadiri muda lina nguvu kiasi gani KULIKO mambo yale yaliyowafanya mpange muda huo_*)
👉PiliSuala la kiroho Kama watu hawa wameanza mahusiano na Bwana,wamkabidhi Bwana suala hili na waingie katika ndoa muda wowote kiutakatifu,si lazima sherehe kubwa,ili mradi taratibu zimefuatwa ili kulinda maadili ya wokovu na kulinda uwepo wa Mungu katika ndoa yao.
*Ila niwatazamishe vitu kama 2 hapa vya kutulia kuwashauri watu hawa kulingana na lugha zao walizozitumia katika kuomba ushauri,kisaikolojia nazichambua hivi:*
🌈Lugha ya binti, *Nioe Haraka nipate Kuzaa,na kama hutofanya hivyo nitatafuta mtu yeyote mwingine wa kuzaa naye ili nisife bila kuzaa* Lugha hii ni dhaifu,kisaikolojia katika ndoa huyu mtu hafai kuwa mke,upendo wake upo kwa mtoto siyo mume( _Kumbuka tunapendana wawili bila watoto,tunafunga Agano la kuishi pamoja mpaka kaburini sisi wawili bila watot_ ila watoto ni zawadi ya Mungu,ndo maana wengine wanazaa walemavu,vipofu,viziwi,na wengine wanakufa,hatuachani na wengine wanakuwa wagumba mpaka uzee,inabaki ndoa ya waliopendana). Sasa mtu anapokuja na Hoja ya Kubadiri Utaratibu,mipango,ya namna yakuingia katika ndoa kwa utaratibu mzuri tuliokubaliana kisa eti,nimichelewa hatozaa na yuko tayari kutafuta mtu mwingine wa kuzaa naye,ninampa majibu yafuatayo.
1.Hakunipenda,anatafuta kigezo cha kuniacha,maana anajua sijajipanga na siwezi kuoa muda huu,hivyo anatafuta nafasi ya kunitoroka.
2.Huyu mtu kunakitu anahofu nacho,aodha anahitaji kunibambikizia mimba aseme niya kwangu kumbe kuna sehemu alipuyanga sasa anabumbabumba taarifa za daktari ili nimuoe haraka,au nifanye ngono naye haraka,kuficha uovu wake.
3.Huyu mtu anayeona mbadara wa mwanume mwingine mimi aliyenipenda bafo nipo, Ni hatari,hana mapenzi ya dhati na mimi.(Kama mtu anaweza kusema nitatafuta mtu mwingine wa kuzaa naye, that means *Anaye mtu,atampataj haraka hivo,watachumbiana muda gani,mpaka waoane,kwa lugha nyine atafanya Ngono na mtu mwingine,nani sasa,na wee ni binti siyo kijana kusema utongoze tongoze,kwa lugha nyepesi anauzoefu wa kutongoza wakaka na akawanasa kiulaini na hraka sana*)
*_Kwa mimi,huyu mtu NI HATARI SANA KUINGIA NAYE KWENYE NDOA_*.
.........................
Niseme kwa upande wa kijana. 🌈Ni jambo gani gumu kwake kimaandalizi hata asiweze kuoa mwaka huu?
_Lakini kwakuwa yeye ndo kichwa,na ukioa unatazamwa wewe kama kichwa kuendesha familia kiroho,kimwili na kijamii,hakikisha UNAOA KWA MUDA ULIOKUSUDIA KUWA HAPA NITAKUWA NIMEWEKA MAMBO SAWA,ili hata ukikutana na changamoto,usijilaumu kwa kuwahi kuoa,bali upambane kama kawida ya changamoto zote za maisha. *Kama unahisi hauko tayari kuoa mwaka huu,usilazimishe itakugharimu kisaikolojia mbeleni,mwache aende atafute mtu asiyeishi kwa mipango na malengo,wee tulia ufanye mambo kwa mipango na malengo utapata mtu wako kwa wakati._
*By Ev Elisha Kazimoto: 0755444078*
Thursday, 10 May 2018
KUOMBA RUHUSA/KUTOA TAARIFA KWA CHUMBA
🌈🌈 *SWALI; JE, NI SAHII KUOMBA RUHUSA AU KUTOA TAARIFA KWA MTU MLO KATIKA MAHUSIANO KATIKA MAAMUZI FLANI UNATAKA KUFANYA AU KWENDA SAFARI?*🌈🌈
Anajibu: Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto.
.............................................
Whatsapp *0755444078*
Facebook Elisha Kazimoto.
*NI HITIMISHE MADA HII KWA MITAZAMO KAMA 2/3*
_Kwanza ni muhimu kujua,kuna vitu 2 hapa ndani ya kitu kimoja, kwanza kuna kitu kinaitwa *Utu/Ubinadamu,na Pili kuna Kiwango cha Mahusiano* muuliza swali amesema (Nivibaya kuaga au kuomba ruhusa kwa mtu mlokwenye mahusiano?)_ swali liko hapa👈.
.
.
Sasa ni vizuri kujua kwanza,kwa watu mnao fahamiana,aidha majirani,au rafiki mnaunganishwa na kutu kinaitwa Utu,ubinadamu kwa maana hiyo kushirikishana taarifa mbali mbali,safari,dharula si mbaya ni sehemu ya utu,undugu,si kama wanyama.
👉Lakini pia tujue kuna tofauti kati ya *Kutoa taarifa/Kuaga na Kuomba Ruhusa.* Anaye Toa taarifa( _Anaashiria na kumaanisha kuthamini uwepo wa mwenzake,regardless mpo kwenye mahusiano ya uchumba au ndoa,au rafiki,au jirani. Lakini pia anadhihirisha ni mtu mwenye mahusiano mema na wanaomzunguka(utu na ubinadamu)pia anamaanisha katika safari yangu lolote laweza tokea,jema au baya,wewe ndo mtu wangu wa karibu kujua niko wapi na wakunipa msaada,lakini wakujua nini kimeendelea kama binadamu mwenzangu._
👉 Anaye omba Ruhusa,ana anamaanisha na kuashiria kuwa _Yuko chini ya mamlaka nyingine ambayo inabidi ibariki maamuzi yake,pia anaashiria kuheshimu nafasi ya mtu aliye juu yake,pia anatambua kuwa hataki kufanya maamuzi yanayoweza athiri mahusiano yake,na mwisho anakuwa anaashiria,anayemwomba ruhusa apime,maamuzi hayo,safari hiyo,yaweza kuwa na athari,ubaya kwa muhusika au mahusiano_ hizo ndizo maana za kuomba ruhusa. Na ndizo tofauti kati ya kutoa taarifa popote au kuomba ruhusa.
.
.
.........................................
*Sasa Tujibu Hoja ya Kutoa taarifa au kuomba ruhusa ya safari,au kufanya jambo,kwa mtu mliye katika mahusiano*
✍Kwanza ni muhimu kujua upo level gani ya mahusiano( _Urafiki,Urafiki wenye matarajio ya kuchumbiana,au Uchumba kamilifu_),kwa level zpte hizo 3 *_Kutoa taarifa kwa mwenzako kwa vitu au baadhi ya vitu SI MBAYA_* na taarifa inaweza kuwa kabla ya kwenda au baada ya kurudi,inatokana na jambo lenyewe unalofanya,na umuhimu wa jambo ukoje kwako binafsi na huyo mwenzako.(Kwa hiyo Si vibaya).
✍Ila katika mahusiano ya uchumba Kamilifu( vigezo na masharti kuzingatiwa)yaani *_Ni uchumba Rasmi,utambulisho kwa wazazi wa kiroho na kimwili,posa,au Mahari kutolewa,au pete ya uchumba hivi ndivyo vinavyo Ashiria UMILIKI/KUMILIKIWA kwa mtu_* hapa ndipo NENO KUOMBA RUHUSA NA KUTOA TAARIFA uenda pamoja. Maana si kila jambo utaomba ruhusa,na si kila jambo utatoa taarifa,kuna vitu na vitu na mazingira.
👉Sababu za kutoa taarifa na kuomba ruhusa nimeeleza. Ni muda wako wewe binafsi kujitafakari mahusiano yako yakoj.
NB: *_Kutoa taarifa na kuomba ruhusa ni matokeo ya vitu kama 2,(hapa ni kuanzia utoto,ujana,mahusiano hata kwenye ndoa) Moja,Malezi na Makuzi,kuna watu niwagumu kutoa taarifa au kuomba ruhusa,nitangu utoto walivyo lelewa,na walivyokuwa(grown up),Pili,inategemea umuhimu wa mtu huyo maishani mwako,ukiwa very cheep(unathamani kidogo kwake)haoni haja ya kufanya hivyo.(wanaoagwa,ombwa ruhusa wanakuwa na Impact kubwa kwa mtu),na Tatu inategemea mnahusianaje,kama mahusiano ni dhaifu usitegemee kuombaau kutoa taarifa,kama mahusiano ni mazuri,hot love,aisee HATA KWENDA UWANI,KUOGA UTAPEWA TAARIFA NA KUOMBWA RUHUSA YA SAA NGAPI NILE CHAKULA_*
.
.
.
...........................................
By Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto.
Whatsapp 0755444078.
Wednesday, 9 May 2018
SULUHISHO LA CHANGAMOTO ZA SAFARI YA NDOA(Part II)
*CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO NA SULUHISHO LAKE KATIKA KUELEKEA NDOA*
.....................................
(SEHEMU YA II)
*_SULUHISHO LA CHANGAMOTO_*
*By Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto*
...................................
0755444078
_Tunaendelea na sehemu ya pili kutatua changamoto mbali mbali zinazo sumbua vichwa vya vijana wengi_.
🌈 *Kuhusu Maamuzi ya kuingia katika ndoa*, hapa Vijana wanahitaji Elimu ya kisaikolojia na ya Kiroho kuwasaidia katika kufanya maamuzi,wajue maisha hayajengwi kwa kuangalia waliopita,tena wale walio feli,wanapaswa kujua kila mtu anamapito yake na Neema yake ya Kimungu. Lakini kujipanga kurekebisha makosa wanayo yaona katika jamii,wajue hawa kwa nini walikosea,walikosea wapi na wao waboreshe wapi ili kuilinda ndoa yao.
Tatu vijana wanahitaji kufundishwa uzuri wa ndoa siyo matatizo ya ndoa tu, waonyeshwe Kusudi la Mungu katika ndoa ni nini, na wafundishwe changamoto za ndoa na uwezekano wa kuzitatua. Mungu hakuumba ndoa ili watu *Waishi ndani yake kwa Kujikaza na Kuvumilia,bali aliiumba watu waifurahie na wapendezwe nayo* Vijana wanahitaji kujengwa kiroho kujua kusudi la Mungu kuweka ndoa siyo kuwajeruhi watu mioyo yao,bali kuwafanya watu wafarijike siku kwa siku kwa uwepo wa mwenza wako maishani mwako. Mtu mwenye mtazamo hasi juu ya kitu chochote mara zote ukifanya kimakosa( *Mithali 23:7a*) kama vijana wataiona ndoa ni eneo la vita sehemu ya kuingia ukiwa unajihami kukabiliana na mwenzako hatuwezi zalisha ndoa za akina Sara na Ibrahimu,tutazalisha ndoa za Anania na Safila,Samsoni na Delila. Tulio kwenye ndoa Tusitumie makosa yetu KUWATISHA wanaojipanga kuingia,tutumie makosa yetu kuwaonyesha mwanga wa kufaulu wao wasipite njia iliyotukosesha.
👉Wanaozidi kukazana kurekebisha mapungufu katika ndoa zao nakuonekana wamefaulu tuendelee kuwafundisha vijana Ndoa yenye Amani,furaha na Upendo inawezekana,tusipindishe maandiko kwa kuangalia udhaifu wetu na kuwaogopesha vijana. Maarifa yanahitajika sana ili kulinda ndoa yako.
🌈 *Kuhusu kushindwa kutofautisha Ndoa na Tendo la Ndoa* Hapa kanisa na wataalamu wajikite katika kufafanua misingi ya ndoa na uwanja wake,wajibu na majukumu ya kila mwana ndoa katika ndoa tangu wakiwa vijana,wajue tendo la ndoa ni kajisehemu katika ndoa ambako hakapaswi kubeba dhana nzima ya ndoa, wajue ndoa ni zaidi ya sex,ndoa ni majukumu na wajibu mbele za mwenzako na mbele za Mungu. Vijana wajulishwe kuwa,Yule anaye letwa maishani mwako kama mwenzi wako anakuja Kutimiza Ndoto na Maono yako ya Kimaisha, sasa maono ya kimaisha siyo sex ni kusudi la Mungu la wewe kuumbwa(Kusudi la Kiroho na kusudi la kimwili la maendeleo). Ndiyo maana tumeona watu wakioa au kuolewa utumishi unakufa ndani yao,au mme anatumika peke yake au mke anatumika peke yake,ukiwalinganisha viwango vyao vya kiroho ni mbali sana,kwa nini tumeshindwa kujua Ajaye maishani mwangu anakuja kutimiza maono yangu,lazima awe sehemu ya maono yangu,na lazima ni pate mtu sahihi wa kubeba maono yangu. Tukiwafundisha hivo vijana hapo tutakuwa na vijana waliojipanga kuoa au kuolewa kutimiza kusudi la Mungu siyo walalamikaji katika ndoa na waenezaji wa matatizo ya ndoa badala ya uzuri wa ndoa.
🌈 *Kuhusu Changamoyo ya Kiuchumi* Hapa ni vizuri kuwaweka vijana wazi, *Wasiishi kwa Imani,na kuoa kwa imani* wahimizwe wafanye mambo kwa vitendo. Zama hizi kila mtu anayetafuta mtu wa kuingia naye katika ndoa,anawaza kwanza mtu *atakaye mpa uhakika wa kupata mahitaji muhimu,yaani chakula,mavazi,na malazi* pesa ndilo jawabu la mambo yote, vijana wapewe elimu ya ujasiriamali,wajishugulishe kutafuta pesa, wafanye kazi,wasibague kazi ila wajiingize katika kupambana kupata kitu cha kuwaingizia kipato hatakiwe kidogo,kuliko kukaa bila kazi wakingojea Muujiza wa Mungu wa kupewa pesa,kulipiwa mahari,kushonewa suti, hayo tumwachie Mungu lakini tuwe na fimbo mkononi ambayo kwayo twaweza gawanya bahari(Musa akaulizwa una nini mkononi?)wewe kijana una nini mkononi ubarikiwe? Na mabinti waepuke kutegemea kuwa *Mama wa Nyumbani* badala yake wajipange kuwa mama wa Maendeleo, wajiandae kuwa wamama wajenzi wa familia bora wenye uwezo wa kupambana,kushugulika kuingiza kipato sawa sawa na *Mithali 31:1-15* inavyosema.
🌈 *Kuhusu changamoto ya Elimu* Kanisa lijikite katika kuhamasisha vijana walio katika umri wa kwenda shule,vyuo wapambane kupata elimu,na wale waliovuka elimu za msingi na sekondari basi wahimizwe kupata elimu ya Ujuzi wa mambo mbalimbali.Wanaoweza kuongeza elimu waongeze ilikukabiliana na changamoto za maendeleo ya utandawazi. Tusifikie hatua tukaridhika,ziko fani nyingi za ujuzi awezazo mtu kusoma wa umri wowote na kujiweka katika nafasi nzuri,huwezi jua mambo ya mbele na mabadiriko ya tawala na nchi na matakwa ya upepo wa kisayansi duniani. (Kijana iweje uridhike? Elimu kubwa huna,Ajira huna,Pesa/biashara kubwa huna na Upako wa tofauti kiroho huna) unategemea kuoa na ukaishije kwenye dunia hii ya chagamoto kubwa za wasomi na matajiri?
NB: *_Wadada wafundishwe namna ya kuongeza elimu huku wakiongeza unyenyekevu na adabu_* Utafiti unaonyesha,kwa kadri wadada wanavyoongeza elimu ndivyo wanavyopoteza sifa ya kuolewa,na kuogopwa kwa sifa ya kuota kiburi na dharau kwa waume zao. Wadada wajifunze na kujua kuwa elimu,cheo na pesa Siyo tiketi ya kuwa na Sifa ya Kuolewa,bali ni tabia njema na moyo wa kumthamini mmeo. Unyenyekevu uonekane tangu ukiwa bado ujachumbiwa katika kuongea,katika kuwajibu wale wanaokutaka ila huwataki,jiombee sana ili uwe mtu anayefaa.
👉Wazazi mawazo yenu ni mema kwa kutaka watoto wenu wa kike waolewe na wasomi,matajiri ila msiwapande watoto wenu kiburi nakujiona wao hawawezi olewa na watu wa aina flani,ila wa level flani,maisha ni mzunguko mtoto wako akipitwa katika mzunguko umri ukaenda atakulaani wewe na atakuletea aibu nyumbani na utakuwa umezika ndoto zake utaona ni Heri mara elfu angeolewa na yule mlo mkataa.( Hekima ziongoze zaidi ya Hisia).
🌈 *Kuhusu changamoto ya Kiimani* Watumishi wa Mungu wajikite katika kufundisha zaidi ya kuhubiria vijana, Vijana wanahitaji kufundishwa,huu ni umri wenye Maswali kibao ya kimaisha,udadisi mwingi,usiri mwingi,majaribio mengi, sasa kama Makanisa hayatatumika kama Madarasa ya Kiroho na Kimwili kuwaandaa vijana kuwa Watumishi wazuri wa Mungu wenye imani thabiti ya Kimungu,wasioyumbishwa na upepo wa imani za ajabu ajabu,basi tutazalisha vijana ovyo makanisani,wakurupukaji na wasio faa kuwa baba/ mama wakesho.Vijana waandaliwe,wachongwe kiroho,wapokee sifa ya utumishi,wajisimamie kiimani,wawe na uwezo wa kiroho wa kupambanua imani feki na orijino,wawe na viwango vya kumpenda Mungu kutoka moyoni si kwa mazingira yako vizuri ndo anampenda Mungu,yuko na watumishi ndo ni mtakatifu,akiwa mbali na kanisa na famila basi ni majanga matupu. Hao vijana hawafai kupewa mabinti na vijana wetu wa kiume. Wafundishe wawe na uwezo wa kukabiliana na mazingira yote ya raha na ya dhoruba. Msingi mwema,uwekwe mapema tangu wanapookoka. Kanisa limekosa mafundisho,badala yake limejikita katika kuhubiri miujiza na baraka zaidi ya kuwafundisha vijana kumjua Mungu na kumpenda Mungu kwa kina wakawa na uwezo binafsi wa kulifasiri neno la Mungu mioyoni mwao na kuliishi.
_Kijana mwenye misingi imara ya kiroho anapofika muda wa kuoa au kuolewa,anakuwa mtulivu na anamsikiliza Mungu katika kuingia katika ndoa,anajua ipi ni imani sahihi na ipi ni imani potofu. Pia vijana walioiva kiimani wanaouwezo wa kupambanua matapeli na waliookoka kweli kweli._ Madarasa ya waongofu wapya yarudishwe upya makanisani,idara za vijana ziboreshwe sana, zijikite kuwaandaa vijana kuwa watumishi wazuri wa Kristo na wababa/wamama bora. Shida kubwa tuna vijana wakuabudu ibadani ila siyo walio na mzigo na kazi ya Mungu,ambao wanatambua mimi nimeokoka lakini Mungu amenipa neema hii iujenge mwili wa Kristo. Ndo maana siku hizi wainjilisti vijana wanapungua kwa kasi,wachungaji vijana,manabii na mitume na waimbaji tuna wakongwe na wasitaafu wa serikali walio wengi, vijana walioingia katika utumishi *_Niwahuni,wababaishaji,feki na wapiga madili_* hata kwa macho unaona huyu hakuna. Wenye mzigo,walio na mioyo na uchungu wa mji wa Bwana na Kuta zake kama akina NEHEMIA wanazidi kupotea. Kwanini? Kwasababu makanisa ya siku hizi mengi yanatafuta POPULARITY (Kujulikana)siyo Yesu kujulikana. Tangu mtu anaokoka kila siku anaambia Naona ukifanikiwa,naona ukiinuliwa,panda mbegu izae,haujui lingine,huyo unahisi kiroho chake kikoje.Tutapata mtumishi humo,madhabahu ni zinaa na uganga,kijana je alookokea humo huyo atakuwaje. KANISA LIJIPANGE UPYA.
👉Lakini ni muhimu vijana wakafundishwa nguvu ya imani katika ndoa,utofauti wa imani unaweza kuwapelekea kuwa na ndoa isiyo na mwelekeo maalumu na malezi mabaya ya watoto na kizazi kiovu.
🌈 *Kuhusu changamoto ya Itikadi za Madhehebu* hapa vijana wafundishwe neno vizuri,waijue misingi ya neno la Mungu na mapenzi ya Mungu,wasiendeshwe na mapokeo ya watu na interests za mtu mmoja na kujitia kinfungoni.Hapa viongozi wa makanisa kuna haja ya kutafakari,tunaandaa kizazi cha watu wanao hofu mapokeo ya kanisa au Mungu mwenyewe. Watu wafundishe Neno la Kristo wajazwe Roho mtakatifu,waongozwe na Roho wenyewe atawasaidia kupambanua mambo yoote yanayoleta ukakasi makanisani( mara kusuka,mara wigi,mara mapambo,mara masuruali)kanisa limejitahidi kuwatiisha watu chini ya sheria ila siyo chini ya neno la Mungu. *_Ndo maana waweza Ona maajabu ya Kiroho,mtu huyo alokuwa havai suruali,kujipamba akiwa kanisa flani,maala flani,akitoka akaenda kanisa lingine Utamkuta yooote aliyoelekezwa ni dhambi na akatii ndo yoote anayafanya_* Je, huyu alilitii neno la Bwana au alitii vitisho vya watu walombele yake. Je,hakuyafanya muda ule kwakuwa alikuwa akiongozwa na Roho au sheria,na sasa anafanya kwakuwa anaongozwa na Roho au mazingira. Hapa ndipo penye Hekima na Maarifa ya watakatifu, *"Tukiongozwa na Roho hatutakuwa Chini ya Sheria"* na tutafanya lolole popote kwa Amani kulingana na maelekezo ya Roho wa Bwana.
(Changamoto nyingine,kuna makanisa yamekata tamaa,mpaka sasa Hawaamini kama mtu anaweza kuongozwa na Roho,wala Roho aweza tembea na Mtu,wamekuwa na mtazamo Hasi juu ya Roho wa Bwana na Vipawa vyake na Madhihirisho yake kwa watu) Ila niwaambie ambao bado mnasikia Taa ya Bwana ndani yenu, hayo hayana budi kuwepo, *Yesu ni Yeye Yule Jana Leo na hata Milele habadiriki.* WAEBRANIA 13:8 endelea kuomba Roho wa Bwana aendelee kuwa nawe na mlinde mtunze,usimfiche kwa madhihirisho yake mwache afurike.
🌈 *Kuhusu Malezi* Hapa niseme na wazazi wa kimwili na wa kiroho,tusiwe na upendo kupita kiasi,au kuziba macho tusione umuhimu wa maisha ya vijana sasa na baadaye wanapoelekea katika ndoa. Tuwaingize watoto wetu,vijana wetu katika kuwajibika,kujishugulisha na kujua kufanya kazi za kila aina.Tuwapime uwezo wao kwa kuwapa kazi ili kuwaandaa kuwa wababa na wamama wawajibikaji kwa familia zao. Wazazi wa kimwili hakikisha mtoto katika umri wake kuna vitu anaweza vifanya kwa ubora,mzoeze maisha ya aina zote ili aweze kukabiliana na changamoto za ulimwengu.Huku wazazi wa kiroho tuwaingize vijana katika utumishi,tuwajaribu katika kona nyingi za utumishi kuona wanafaa wapi katika mwili wa Kristo.Tunapo wapa majukumu ya Kiroho makubwa na kuwaonyesha njia ya kuyatekeleza ndipo tunapo WAZOEZA KUONGEA NA MUNGU NA KUWA NA MAISHA YA UKARIBU NA MUNGU. Ikumbukwe hawa ni vijana wapo katika muda Timing and Error(Muda wa kubahatisha kwa kufanya vizuri na kukosea)wanahitaji kusaidiwa kufuta makosa yao siyo kuishi katika makosa yao.Katika kutafuta uhalisia wa kitu LAZIMA KUKOSEA KUPO makosa siyo Matatizo,ila tusipo wakosoa na kuwaelekeza tutazalisha MATATIZO kwao. *"Every one Learn from his or her Mistakes"* Errors are not Mistakes,and mistakes are not Problems (Errors comes from Trying, Mistakes comes from Challenges,but Problems are the results of failure to Try,and failure to solve challenges in a good way)That's my Philosophy you may take it.
🌈 *Kuhusu Familia* Familia lazima ijue mipaka yake katika mchakato wa kihisia wa kijana kuingia katika ndoa,familia ishauri,ilee na ielekeze,ila maamuzi yaachwe mikononi mwa vijana,ili kuepusha lawama katika ndoa za vijana wao.Wazazi wengine wamekuwa ndo waamuzi wa nani aoe au aolewe na yupi,uwe una taka au hutaki,vikao vya kifamilia vinakaa kwa lengo la kupinga maamuzi ya binti,kwaajili ya maslahi tu,(mara kabila,mara elimu,mara kiwango cha uchumi)hawajielekezi kumsaidia mtoto wao,ndugu yao,kulitafuta kusudi la Mungu katika maamuzi yake,ila kutafuta sifa na heshima na uwezo wa kifedha na mali kwaajili ya manufaa ya familia. Wazazi tumewafanya watoto waingie katika Ndoa ambazo hawakuzikusudia na wala hisia zao ziko nje kabisa na huyo mlomchagua. Kumbuka Love is all about Emotional (kama hana hisia juu yake kumpenda ni vigumu)huu ndo umekuwa mwanzo wa wanandoa kuendeleza mahusiano yao na *Ma Ex Girl/Boyfriend wao huku wakiwa katika ndoa na kuibua migogoro ya ndoa,mwili upo ndani hisia ziko nje* Tumezalisha lawama kwa watoto kuwa maisha haya ni kwasababu wazazi walinilazimisha,badala ya kuwa baraka kwa ndoa za watoto wetu tunakuwa msiba.(STOP THAT BEHAVIOR )
🌈 *Kuhusu Gharama za Mahari* Hii ni kona ya wazazi na kijana wa kiume, kwanza wazazi wa binti wajue ndoa siyo biashara,wajikite katika kutazama namna ya kuwaandalia watoto wao familia mpya,bora na yenye uwezo wa kiuchumi,badala ya kujipanga kutaja Mahari kubwa,wajipange kumuwekea mtoto wao msingi mzuri wa maisha. *Usisubiri Pesa ya Mahari ndo umfanyie binti vitu vya kumuaga,hiyo ni sawa na kuamisha pesa kutoka mfuko mmoja wa suruali na kuweka mwingine na kushukuru kwa zawadi,ni sawa na kujikopa mwenyewe* Tukibadirisha mtazamo wa Mahari ya Ndoa,tutawaokoa vijana wengi na stress za ndoa. Pia vijana wahimizwe kufanya kazi kwa bidii wawe na uwezo wa kulipa mahari na kumaliza *Siyo Kukopa Mke kama unakopa nyanya kibandani.* Makanisani vijana wabanwe vizuri waonyeshe miradi yao ya kiuchumi Mapemaa.
🌈 *Kuhusu gharama za Harusi*,Hapa tufikie hatua vijana,binti na kijana wa kiume,mjue uwezo wenu,msipende kuigiza maisha ya mitandaoni na kwenye ma TV,wakati uwezo wako wakawaida sana. *Fanyeni yaliyo kwenye uwezo wenu kwa furaha* siyo mnamaliza sherehe una madeni yakulipa mwaka mzima.Kumbukeni hao watu unaotafuta wakupe Credit mnakuwa nao siku 1,baada ya hapo unabaki wewe na mwenzako na maisha yenu. *Jiandae kufurahisha nafsi zetu na si za watu* ukitaka maisha ya kushindana na kuiga utaishia kujilaumu na kuona wewe ni mtu wa kutofanikiwa.
............................................................
_Masuala ya mahusiano na ndoa yanahitaji kila siku ujifunze na ukubali kupokea mambo mapya,huu ni uwanja mpya kila siku usiwe mgumu kubadirika na kupokea mawazo mapya,kwa nini uishi kiugumu ugumu wakati maisha haya hitaji Stress? Mtangulize Mungu,ongeza maarifa jaribu kubadirika utaona ndoa ilivyo ya ushindi_.
*_Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na ndoa Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
CHANGAMOTO ZA VIJANA KUELEKEA NDOA(PART I)
*CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO NA SULUHISHO LAKE KATIKA MAHUSIANO KUELEKEA NDOA*
(SEHEMU YA I)
.........................................
_By Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto_
*0755444078*
_Shalom wana wa Mungu wote mlio katika safari hii ya Mahusiano ya uchumba,au mnawaza kuanza safari hii,na wengine wameisha pita katika safari hii,sasa tumebaki kuwa walimu na washauri wa ndugu zetu wanaoianza safari hii. Leo nataka kusema katika nyanja mbili ya Kiroho na Kisaikolojia tunapo yasemea mahusiano kwa vijana. Kuna Changamoto nyingi vijana wanakumbana nazo na hawajapata majibu,jambo linalowapelekea kuendeleza foleni ya wana ndoa wabaya,wenye migogoro na kuachana(Divorce) nyingi kwa wana wa Mungu. Majibu hayo yanabidi yawe yamegawanyika katika pande mbili kiroho na kisaikolojia._
*Fuatana nami katika uchambuzi huu wa Changamoto na Suluhisho lake katika mchakato wa kuingia katika ndoa*
...................................
🔥 *CHANGAMOTO*🔥
✍ *Kuna changamoto ya Maamuzi yakuingia katika ndoa* Miongoni mwa vitu vikubwa vinavyo vuruga vichwa vya vijana sasa,ni namna ya kufanya maamuzi ya kuingia katika ndoa. Tuna vijana wengi wanaotamani kuoa au kuolewa ila wanashindwa kufanya maamuzi ya kuingia rasmi katika ndoa,na hii imetokana na *Hofu kubwa* ya kuogopa kuwa na ndoa mbaya,kwasababu maisha ya ndoa nyingi zinazowazunguka kanisani na mitaani kuwa na migogoro mingi hata kuwafanya vijana kupoteza hamu ya kuingia katika ndoa, *mioyo inatamani ndoa,ila Akili inagoma kwa vitu walivyo experience kwa watangulizi* kwa hiyo tuna vijana wengi makanisani,umri unaenda ila wanasita kuingia katika ndoa.(Moja ya Athari inayotokea ni kuwa na Vijana-wanaume,na Wadada -Mama yaani wanaoendelea kushiriki ngono kanisani ila hawajaoa na kuolewa)
✍ *Changamoto ya Kushindwa kutofautisha Ndoa na Tendo la ndoa* Hii ni changamoto kubwa katika ukubwa wake inayosumbua karibu 85% ya vijana,katika utafiti wangu,na katika kufundisha makongamano ya vijana juu ya mahusiano na ndoa,vijana wengi wanaofikiria kuingia katika ndoa *_Hawajui kwa nini wanaamua kuingia katika ndoa_* wengi wanatamani kuingia katika ndoa *kutuliza tamaa za mwili(Sex)* jambo ambalo wengi kwanza limewafanya kuitafsiri ndoa kama Uwanja wa Sex(ngono) yaani ndoa ni sex, kulingana na tafsiri hii wengi wamejikuta wakishiriki sex kabla ya kufunga ndoa,wengine kulazimika kuoana kwa sababu ya mimba ilopatikana kwa bahati mbaya,au kufunga ndoa wakiwa wajawazito,na wengine kuolewa ndoa za mitara,au kuacha wokovu.( *Je,Ndoa ni Sex?*)swali linalochanganya wengi,tutalijibu kwenye suluhisho.
✍ *Changamoto ya Kimaisha hasa katika Uchumi* Tatizo lingine linalowapa vijana kigugumizi katika safari ya kuelekea ndoa ni Hali ya Kiuchumi,wapo vijana wanao amini *Ndoa ni Pesa,bila pesa ndoa itakushinda, wapo wanao amini Upendo unamechishwa na pesa,na wapo wanao amini Ndoa ni Upendo tu,uwe maskini au tajiri suala ni upendo. Utofauti wa mitazamo hii umewaathiri vijana katika safari yao ya kuelekea katika ndoa,ambapo ujikuta watu wawili waliopendana wanatofautiana katika mitazamo.* na hapo ndo safari ya hao wawili huwa ngumu.
✍ *Changamoto ya Kielimu* Tuliko toka katika miaka ya 1990 kurudi nyuma, Elimu haikuzingatiwa kama Kigezo cha Kumpata mtu wa kuoana naye,ila miaka ya 2000 mpaka sasa na tunako elekea,kumekuwa na mtazamo wa Kiwango cha Elimu kuwa ni Kigezo kikubwa cha Kumpata mtu wa kuoana naye. Changamoto ni watu waliopendana lakini wanajikuta wanatofautiana sana kiwango cha Elimu,jambo ambalo wengine uamua kuvunja mahusiano,na wengine kuwa na uchumba wa muda mrefu ili kutumiza kwanza kigezo cha Elimu.
✍ *Changamoto ya Kiimani* Hapa kuna mambo mawili yanaumiza vichwa vijana makanisani na watumishi wa Mungu wanaochunga vijana hawa. Moja,Namna ya kumpata mke au mme *Mchaji wa Mungu* wengi wa vijana makanisani niwasanii,wanaigiza kuokoka,wengine wamejiingiza katika wokovu kupata mke au mme,au kupata sifa ya mlango wa kutokea kimaisha.Kwa misingi hii vijana wamejikuta wanaogopa kuoa au kuolewa maana kuna hati hati ya *kuangukia kwa Tapeli* kwa kuwa waigizaji ni wengi kuliko walio halisi.
_Pili,ni vijana kupendana watu wa imani,na mtazamo wa kiroho tofauti. Hii imeleta mkanganyiko wa kiimani,wengi wamerudi nyuma,na wengine wamelazimisha kuoana hatima yake imewapelekea kwenye migogoro ya ndoa na changamoto ya malezi ya watoto kiimani._
✍ *Changamoto ya Itikadi za Madhehebu(Kumbuka kuna tofauti ya Dini-Imani na Itikadi za Dhehebu)mfano wote ni makanisa ya kipentekoste ila kuna itikadi za dhehebu moja kutofautiana na lingine(hawa hawaruhusu hiki,hawa wana ruhusu,hawa usisuke hawa suka)* Hapa nazungumzia misimamo ya dhehebu moja hadi lingine,hii imeleta changammoto kwa vijana,dhehebu moja kuwa na misimamo ya kwao inayotofautiana na wengine,mfano.. *Kusuka,kujipamba,kufunga vilemba,kuvaa suruali nk* hii imewapa vijana kigugumizi pale wanapokutana kwenye maeneo kama vyuoni kwenye fellowship zinazowaunganisha pamoja,wakitoka vyuoni kurudi makanisani kwao,wanagawanywa kwa itikadi,wengi uchumba uvunjika.(na wengine wakiamua kuoana mmoja inabidi Asalimu amri kwa moyo wote ili alinde Amani ya ndoa yake,au aendeleze msimamo waishi kiubabe kwa falsafa ya "Kuamua Kukubaliana Kutokukubaliana"
✍ *Changamoto ya Malezi* Kizazi tulicho nacho sasa,ni tofauti na kizazi kinachomalizikia, utofauti wa malezi katika familia,umetengeneza kizazi ambacho katika ndoa ni mzigo,hivyo vijana kuwa katika wakati mgumu wa kuchagua nani awe mke au mme wangu( *Shida tabia na makuzi*) ya vijana hawaandaliwi kuwa *Wake au Waume,wenye uwezo wa kuendesha ndoa katika majira ya aina zote,dhiki,raha na taabu hawawezi,wanapenda raha,wameandaliwa kuishi katika raha* wapo waliokuwa maishani mwao hawajui hata kupika,kupasua kuni,kuosha vyombo ,wamekulia chini ya House girl na House boy mpaka wanaoa na kuolewa hawajui kuwajibika,hii inawapa changamoto vijana katika ndoa.(hapa ndo utakuta familia za ajabu,mpangilio wa ajabu ndani ya nyumba nk)
✍ *Changamoto za Kifamilia* Katika safari ya mahusiano kuelekea ndoa,vijana wanakumbana na vipingamizi vya kifamilia vya kuwekewa vikwazo,kutooa au kuolewa na kabila flani,mtu wa kada ya kazi hii,jambo ambalo limewafanya vijana kuoa au kuolewa na watu wasio katika matamanio yao,wanaoa au kuolewa kwa shinikizo la wazazi.( *Na wengine wamechelewa kuoa au kuolewa kwakuwa walio kuwa chaguo lao muda ule, WALIKATALIWA NA FAMILIA sasa wamekosa watu wa aina kama ileile ya wa sifa zinazotakiwa na familia*) mwisho wake ni nini...Wengi wameanguka katika dhambi,wengine wameishia kuwa na ndoa za ajabu Zisizo gusa Hisia zao.Wanaishi ili kutimiza wajibu na kuonekana nao wapo kwenye ndoa ila Hawana Partner wanaogusa maisha na hisia zao.
✍ *Changamoto ya Gharama za Mahari* Kigugumizi kingine kwa vijana wanapoanzisha mahusiano fikra inahamia kwenye gharama za kulipia mahari, ambapo familia zingine *zimegeuza ndoa mtaji wa kiuchumi,au kifuta jasho cha malezi,badala ya ndoa kuwa ni kupanua mahusiano ya kifamilia. Zoezi la Mahari limewafanya vijana kuchelewa kuoa na kuolewa,kuanguka katika zinaa,na kuishi maisha ya unyumba bila kufunga ndoa.
✍ *Changamoto ya Gharama za Harusi* Kuna kitu kinapanuka katika vichwa vya vijana na kuwa Utamaduni, kitu hicho ni *Ushindani wa Ukubwa na Ubora wa Sherehe za Sendoff na Harusi* Siku hizi vijana hawako tayari kuoa au kuolewa kama harusi haitakuwa ya kifahari, *_Pete ziwe za Gold,Shera ya tausi,suti kali,kiatu,ukumbi,keki ngazi 12,kwa ujumla wanahitaji Harusi yake iwe Unique (pekee)* ndo waoane,kabla ya hayo yote hayajatimia ndoa isubiri.
✍ *Changamoto ya Maarifa ya husuyo mahusiano na ndoa* Ni hitimishe kwa Eneo hili ambalo ni bahari ya matatizo kwa vijana, ni Maarifa(Shule)juu ya mahusiano na ndoa. Huu ni ugonjwa wa vijana wengi makanisani,wataalamu,walimu na watumishi wa Mungu wa kukokotoa Uwanja huu wa mahusiano na ndoa *Kwa kina* bado hatuna,aidha hatujui umuhimu wa ndoa,au tumefeli katika ndoa, au tunarahisisha suala la ndoa, hivyo tunashidwa kufundisha katika ubora,au tujizamisha rohoni sana na kuiona ndoa ni kitu cha kimwili sana au rohoni sana,kumbe ndoa ni 50/50.Vijana hawana maarifa,wanafanya wanachoona kina faa,kwa kuendeshwa na taarifa za mitadao,hatima yake ni kuzalisha ndoa mbovu na dhaifu.( Na wengi wa wasemeaji wa ndoa makanisani WANAPENDA KUISEMEA KATIKA MTAZAMO HASI SANA KULIKO MTAZAMO CHANYA hii ni shida kubwa sana, misingi hii vijana wanapata tabu sana kufikia malengo yao na tunazalisha jamii Dhaifu sana katika kila sekta ya maisha.)
_Haya ndiyo baadhi matatizo makubwa yanayo watesa vijana wengi katika kizazi cha sasa. Ulikuwa nami_
*_Mtaalamu na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na ndoa, Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078.
Facebook Elisha Kazimoto.
*Hii ni sehemu ya kwanza ya Somo,sehemu ya Pili inafuata,inayo Toa suluhisho la Changamoto hizi zote zinazo wakumba vijana katika kuelekea Ndoa*