Monday, 2 January 2017

NENO LA MWAKA 2017

✈✈ *MWAKA 2017 NI MWAKA WA KWENDA MBALI*✈✈
   *By Ev Elisha Kazimoto*
      *0755444078*
*_Bwana Yesu asifiwe sana wale wenye tumaini katika Bwana,huu ndio ujumbe alionisemesha Bwana tarehe 31/12/2016 mnamo majira ya saa 2 usiku,baada kumsihi Mungu nini Mungu anasema kwangu kuhusu mwaka 2017,kama ambavyo amekuwa akinisemesha kila mwisho wa mwaka akinipa neno la Mwaka mzima la kusimamia,mfano mwaka 2014 tarehe 30/12/2014 Mungu alinisemesha kuhusu 2015 kuwa utakuwa Mwaka wa Kicheko..AYUBU 8:20-21,na hakika kwa wote na mahali pote nilipo nena neno hili tangu kwangu hata kwa watu walio liamini neno la Bwana( 2Wafalme 7:1), lilitimia kwao.Tarehe 31/12/2015 nikapewa neno la mwaka 2016 kuwa utakuwa mwaka wa...Kupanua Mipaka yako(Isaya 54:2)..na sasa tarehe 31/12/2016 nimepewa neno la Mwaka 2017 kuwa utakuwa mwaka Wa kwenda Mbali_*    

  ( *KUTOKA 8:25-28*)
_25 Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu ndani ya nchi hii._ 

_26 Musa akasema, Haitupasi kufanya hivyo; kwa kuwa tutamchinjia sadaka Bwana, Mungu wetu, na hayo machukizo ya Wamisri; je! Tutachinja sadaka ya hayo machukizo ya Wamisri mbele ya macho yao, wasitupige kwa mawe?_ 

*_27 La, tutakwenda safari ya siku tatu jangwani, tumchinjie dhabihu Bwana, Mungu wetu, kama atakavyotuagiza._* 

_28 Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu Bwana, Mungu wenu, jangwani;_ 
*lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni.*
✈Wewe uliye okoka,unamwitaji Mungu na nguvu zake ili kwenda mbali mwaka huu, *_Ni lazima kwenda mbali,ila kuna ushindani mwingi sana katika ulimwengu wa roho,changamoto nyingi zinazo kusudia kuto enda mbali,kutopiga hatua,kurudisha nyuma_*  Ndiyo maana nakushauri mtu wa Mungu katika mwaka huu, *Kaa na Mungu sawasawa* watakao kuwa na uwezo wa kwenda mbali ni wale, *Walio wa Mungu kweli* wasio kubaliana na usemi wa adui, wasiokubaliana na changamoto za mazingira kuwakatisha tamaa, yaani *_Watu Ving'ang'anizi wa Imani hao 2017 Wataenda mbali kiroho na kimafanikio ya kimwili._*
✈ Ukisoma andiko letu pale la Farao na Musa na Haruni,uangalie mchuano wao,waruhusiwa watoe dhabihu lakini katika nchi ya Misri humo humo, na hawa lengo lao ni kutoka Misri, *Siku zote adui Hataki utoke mikononi mwake, anatamani aendelee kukuona katika vifungo alimo kuweka* Lakini na hawa watumishi wa Mungu hawakukubali changamoto ya mazingira hayo,wakasema *_Imetupasa kwenda mwendo wa siku tatu_* siyo hapa Misri,tunahitaji tutoke twende mbali.
✈ _Huwezi kufanikiwa,kupata heshima ukiwa bado ndani ya teso,huzuni,vita hiyo inayokuumiza ya tangu mwaka/miaka iliyo pita._ unahitaji kukataa ndo Mungu aingilie kati utoke uende mbali.
✈ *_Huu ni ujumbe mfupi,lakini ni mpana sana katika kuutafakari,Mungu akupe neema,2017 usijisahau,fanya maamuzi ya kuwa Rafiki wa Mungu na Mtu faida katika ufalme wa Mungu,utaenda mbali sana 2017, lakini pia wale waliozoea kudharau mambo ya Mungu,kuwa busy na mambo yao,mwaka huu unaweza kuwa mgumu kwao_*
  ✈✈ _Nikutakie safari njema ya siku 365 uende mbali katika jina la Yesu Amen_✈✈
   *By Ev Elisha Kazimoto*
          *0755444078*

No comments:

Post a Comment