*CHANGAMOTO YA UMRI KATIKA KUOA/KUOLEWA*
*_Ev Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
_Shalom watu wa Mungu,vijana na wazazi wenye vijana umri ya ujana,niwakaribishe katika uchambuzi huu wa *Presha ya Umri kwa Vijana katika kuelelea kwenye NDOA* Upo na mimi Mtaalamu wa Saikolojiana Mchambuzi wa Masuala ya Saikolojia *Ev Elisha(Baba Eve)* karibu sana_
🌹Kwanza niseme,Suala la kuoa na kuolewa ni suala la Kiroho(Kimungu) na ni suala la Kihisia(Kisaikolojia) kwa hiyo unapo anza kuhisi unaweza kuingia,kuhitaji ndoa unahitaji kujipanga sana Kiroho na Kisaikolojia,kwani Kujisahau katika haya mawili kunaweza *_Kusogeza Mbali Muda wako wa kuoa/kuolewa nje ya muda ulo tamani kuingia katika ndoa_*mfano ulitamani kuingia katika ndoa below 30 years,ukaja kuingia above 30years.
🌹 _Kisaikolojia,ufahamu wa kijana wa kike au wa kiume huanza kutamani mahusiano ya jinsia nyingine sana kati ya umri wa miaka *15-19*( siyo kutamani ndoa,ni kutamani mahusiano ya kimapenzi na jinsia nyingine) na Kutamani Ndoa kwa hisia za chini huanza kati ya miaka *20-25*, na kati ya miaka *26-29* kiwango cha kutamani ndoa huwa cha juu,na kati ya miaka *30-35*Hofu utanda na wasiwasi mkubwa uingia wa kupata mtu wa kuingia naye katika ndoa, na kati ya *35-40*Matumaini huanza kupotea wa kuoa au kuolewa,japo mtu hakati tamaa kabisa ya kutokuwa na mwenzi,na kati ya miaka *45-55*mtazamo huanza kuwa wakuwa na maisha binafsi na ndoa huwa suala la bahati na sibu_
*NINI TABIA ZA KILA MUHULA NA CHANGAMOTO ZAKE*
_Hapa naomba uwe makini na utazame kwa makini katika vipindi hivi vilivyo ainishwa pale juu,Tabia hizo zinaweza kuusogeza muda wako wa kuingia katika ndoa, *Baadaye ntaongea kuhusu muda wa Mungu,unavyo weza sogeza muda wako wa kuingia katika ndoa,hapa naanza na Tabia za Kisaikolojia*_ karibu upo na mimi Mtaalamu wa Saikolojia Ev Elisha(Baba Eve)
✍ Katika ule muda wa kutaka mahusiano ya kimapenzi na si ndoa( *15-19*) huu muda wengi wanasukumo wa *_Kijiachia katika mapenzi kwa kila anaye mtamani,aliye na pesa,au vitu vya kushawishi, mzuri wa sura,muda wa kufanya mapenzi na kila mtu atakaye taka kufanya mapenzi,hajali Promise ya ndoa anajali kutimiza tamaa za mwili_* kwa sababu hiyo wengi hasa (Wadada)huchezewa sana na kujeruhiwa mioyo na vijana wa kiume. *_Mbaya zaidi katika kipindi hiki hakuna Anaye waza au kufikiria Thamani ya ndoa,au kufikiria kuwa maisha yake hayo anavyo jiachia yanaweza athiri mpango mzima wa yeye kupata mtu sahihi wa kuingia naye kwenye ndoa_* Athari ya Tabia za kipindi hiki;
1⃣Ni kueneza sifa yako mbaya ya kutothamini mwili wako.
2⃣Kueneza Uchi wako kwa kila mtu(upo vizuri au vibaya,una mapungufu kitandani au uko vizuri)kumbuka _uzuri wako kitandani katika kipindi hiki hakukupi tiketi ya kuingia katika ndoa,bali kukushusha thamani na kuonyesha wewe kahaba_ na ubovu kitandani ndo unakuzika kabisa na kukimbiwa.
3⃣Kupata Alama ya kupoteza kibali cha kuwahi kuolewa( _mfano kupata mtoto kipindi hiki,utapata shida sana kumpata mtu wa kuoana naye ukiwa na mtoto_)
✍ Katika kipindi cha kutamani ndoa kwa hisia za chini Miaka 20-25,( *Hapa wengi ndo huvuruga mambo na muda wao halisi wa kuolewa au kuoa,kwani ni muda wa Uzuri huongezeka,kujitambua huongezeka,shape hukaa sawasawa,Elimu uanza kuonekana,pesa kidokidogo huanza kuonekana,Ajila hupatikana,* _Kwa sababu hizi kufukuzia wadada,au kuwindwa na vijana huwa kiwango cha juu,Foleni ya Requests huwa kali, na wengine vijana ndo hupanga wadada 5,7,10.....kuwaweka sawa kuwaoa,kwa kisingizio wanaangalia the best kati ya hao wote,mwusho huishia kuto pata hata mmoja,maana kisaikolojia huwezi kuwamiliki watu zaidi ya 2 vizuri kiasaiklojia kwenye mapenzi mpaka ukaonekana unafaa kuwa mme wake_
_Na kwa upande wa Wadada hapa ndipo *Hujipoteza kabisa na kujipa sifa ya kutoolewa* ambapo huanza Kujiona,kuchagua kijana wa kumuoa,hupanga vigezo visivyo wezekana katika mazingira yake,hupanga vigezo bavyo jata yeye hana,huwatimua vijana wanao kuja kuwachumbia kwa GIA ISIYO YA USTAARABU, dharau huongezeka,hutegemea kuolewa na watu wazito,well off ,walofanikiwa sana,huwakwepa vijana wasio na kazi ya kuingiza pesa mwisho wa mwezi(Ajila),huwauliza wanao kuja kuwachumbia swali la Una nini cha ziada,nyumba,usafiri,unaishi kijijini au mjini,familia yenu mko wengi au wachache,kama mpo wengi na una wadogo zako wengi kama 4 na kuendelea,hata ukiacha kumsumbua,wanaogopa kusomesha ndugu huku ana watoto wake, *Lakini nao huwapanga vijana kama 3-5 na kutazama nani ana mwelekeo mzuri wa kimaisha* shida yao huwa hawapendi kuwa wawazi sana kwa kijana, ANAMTAKA-HAMTAKI,hali hii ya kuzungushwa vijana huwafanya kumfutikia mbali na kutafuta mwingine,na kujikuta wote wamemwacha kimya kimya au kuvunja mahusiano naye._
Pia kwa kipindi hiki vijana wote wa kike na kiume *Huwa na Misimamo isiyo na tija* mfano aina ya mavazi,urembo,mwili (huna six park,huendi gym umekosa mtu tayari)kabila,Carrier flan kama wewe si mfanyakazi wa carrier flan hutakimbiwa na kila mtu.
✍Katika kipindi cha kuitamani ndoa kwa hisia za juu yaani miaka 26-29( *Kwa kijana wa kiume ni mzuri sana kwa kuwa yeye ni mtafutaji,ila kwa wadada ni muda wa heartbeat kwenda speed,hofu inaanza kui gia hasa kama hayupo kwenye mahusiano imara(serious ) wanapata shida sana* Lists ya watu wa kuulizia au kuuliza huanza kupungua, taarifa za Awali huanza kuhukumu maisha yako ya sasa na ya baadaye( _yaani ulivyo tumia vipindi viwili vilivyo pita huanza kuathiri uhitaji wako wa sasa na baadaye_),Watu huanza kujitia wale walio wakwepa,au kuwapiga vibuti, huanza kuwa wapole,waelewa,wastaarabu,wasikivu wa kila ombi na kujibu kwa Adabu,hukirudia kipindi cha kwanza,hutamani mahusiano na kila mtu,hutafuta mawasiliano ya watu,marafiki wote wazamani na wapya,na hutega sikio kwa walio bado single kama anaweza pata mtu wa kumkubali au kumwambia neno la kumuoa. (Si kipindi kizuri sana kisaikolojia kwani kinakutaka ujipendekeze kwa kila mtu)
✍ Katika kipindi cha hofu na wasiwasi, miaka 30-35( *Kipindi hiki hofu kwa muhusika na familia yake huanza kuingia juu ya uwezekano wa kupata mtu,Mvuto wa ujana huanza kufifia,utu uzima huanza kutokezea,kwa mabinti ni kipindi ambacho kama ni kufanya mahusiano au kiliki no za simu, ANA DELETE VIJANA WOTE WALO CHINI YA UMRI WAKE, si rahisi kuolewa na kijana unaye mzidi miaka 2,3,4,5....huanza kuwafikilia walio juu yake kiumri,kichagua hupungua,vigezo hupungua,kutojiamini huanza,kwa upande wa vijana wasicha wadogo huanza kuwakimbia kwa kuogopa umri mkubwa*) na Wengi hapa vijana kwa wadada huwa na *_Kigugumizi cha kutaja Umri wake_*
✍Katika kipindi cha Matumaini kupotea miaka 35-40( _Hali huwa tete,lawama nyingi hutupwa juu ya muhusika kutoka kwa familia na watu walo mfahamu kwa rika ya ujana mbichi,kujilaumu huongezeka,wengine huamua kutoolewa tena au kutooa tena,wengine huamua kutafuta mtoto angalau mmoja kwa njia zisizo rasmi,wadada huanza kuwaganda wanaume akimtania_.
*_Katika mambo yote,muda wako wa kuingia katika ndoa unaweza kusogezwa mbele kwa kusudi la Mungu,si kweli kuwa kila anaye chelewa kuingia katika ndoa amefanya uzembe,ila kusudi la Mungu_* Haya yanaweza kuwa mambo muhimu ya kusogezwa mbele kwa ndoa yako.
👉 Bado mtu wako,au wewe katila ulimwengu wa roho haja kaa katika Position (nafasi) ya kuibeba ndoa na kukufanya uendelee kumpendeza Mungu.
👉Bado hujakamilisha vema utumishi wako wa ujana ukiwa huru,ndoa itakunyima uhuru na kushindwa kulitimiza kusudi la Mungu
👉Muda wako wa kuingia katika ndoa katika ulimwengu wa roho bado
👉Ni jaribu lako unaloliweza,lakini utafanyika ushuhuda mkubwa kwa wengine
👉Mkuu wa Uajemi(Anga)amepingana nawe sana na kumzuilia mwenzako usimuone.
NB: _Usiingie kwenye ndoa kwa kuwa umri wako umeenda utaumia,utapata mwiba mbingu utaikosa kisa ndoa,Usiingie katika ndoa kisa marafiki zako wote wameoa na kuolewa,we sikama hao utapoteza mwelekeo waaisha. Tulia na mtegemee Mungu ndoa ipo tu,punguza na kuondoa makosa kwenye maisha yako ya kiroho na kimwili
*_Nini ukifanye kama kijana ili kukabiliana na changamoto hizi zote za miroho na kisaikolojia, moja kuwa mtu wa kumpenda Mungu nyakati zote na tumika kwa moyo na bidii sana kwa Mungu,kuwa mtu wa maombi na kushughulikia vikwazo vyote katika ulimwengu wa roho, Jivue vazi la kuto kubalika na kataa roho ya kukataliwa na kukosa kibali kwa watu, Pili,kusa makini na tabia zako,lugha zako,presentation yako kwa watu,usiruhusu hali yako mfn,elimu,pesa,status yako na familia yako iwe na sauti kubwa kuliko utu wako_*
_Ulikuwa na mimi Mtaalamu wa Saikolojia na Mchambuzi wa Mahusianl na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve ) 0755 444078_ ✍Facebook Elisha Kazimoto
✍Blog Material Adimu University
✍Whatsapp (Gropu Material Adimu University-Chuo cha Mahusiano na ndoa)
✍Whatsapp no. 0755444078
*_Huko kote utakutana na Mafundisho ya kina_*
Thursday, 12 January 2017
UTATA WA UMRI NA NDOA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment