🚍 *MWANAUME KAMA KICHWA* 🚍
*_Ev. Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
🚗Tafsiri hii imechukuliwa kwa upeo wa chini sana na pande zote wanaume kwa wanawake, hali ambayo imepelekea ndoa nyingi kuyumba
🚗Tafsiri ya Mwanaume ni kichwa, wengine wameitafsiri kuwa Mwanaume ni mbabe katika familia, aliye Alfa na Omega, Dictator, asiyestahili kuheshimiwa, kushaurika nk
🚗Wengine wameitafsiri kuwa Mwanaume ni kichwa cha Kuhudumia Familia, kutafuta pesa, kulisha familia nk
🚗🚗Lakini kwa mtazamo wa Biblia na tafsiri halisi ya Mungu, mpaka Mwanaume kuitwa mfano wa Kristo Yesu, SI jambo dogo Kuna maana kubwa
🚗🚗Na kama wana ndoa watatumia, wataiangalia tafsiri ya biblia ndoa yao itakuwa Paradiso ndogo
🚗🚗Kiuhalisia na mtazamo wa Biblia, Mwanaume ameitwa ni kichwa cha mkewe na familia kwa ujumla, kama Yesu alivyo kichwa cha kanisa, kwa kutazama umuhimu na kazi za sehemu 7 za kichwa
🏢 *SEHEMU 7 ZA KICHWA NA KAZI ZAKE* 🏢
👦🏼Kichwa hiki unachokiona (Mwanamke kwa Mwanaume) ni kiungo kikubwa na kina kazi kubwa sana 7,
👦🏼Mwanaume ukitambua ulivyo wa pekee, na ukitumia kwa umakini sehemu hizo 7 ndoa yako utaifurahia milele
👦🏼Mwanamke ukitambua nafasi na umuhimu wa Mume wako kama kichwa na unatengeneza mazingira mazuri ya Heshima, Adabu, Utii na Unyenyekevu kwa mmeo, ndipo hizi sehemu 7 zitakuletea furaha, upendo na amani katika ndoa yako
👦🏼👦🏼Popote ukiona kichwa jua kina sehemu zifuatazo;Akili, Macho, Masikio, Pua, Ulimi, Mdomo (lips),na Meno haya ni maeneo muhimu sana
👦🏼👦🏼Utakuja kujua kwa nini Mungu alimpa Mwanaume nafasi au sifa ya kichwa na kumfananisha na Yesu Kristo
🏫 *SIFA NA KAZI ZA KICHWA* 🏫
🏡🏡UBONGO (AKILI):Kichwa kina ubongo ambayo ni injini ya maamuzi, fikra, tafakari ya mwanadamu
🏡Kazi kuu ubongo ni kuchanganua mambo kabla ya kufanya maamuzi, ni kuzalisha hekima na njia mbadala katika mambo magumu
🏡Mwanaume kama kichwa, unahitaji kutumia akili sana kufanya maamuzi ya faida kwa familia yako kwa amani, Biblia inasema hata Kuishi na mkeo kama mwili (uliobeba Moyo) unahitaji Kutumia AKILI SANA(1Petro 3:7)
🏡🏡MACHO:Macho ni kiungo muhimu sana, yana kazi kuu mbili, Kutazama na Kuona
🏡Kutazama, ni kutambua jambo likivyo ktk sura yake na Kuona ni Kuchanganua sura ya kitu na kukitendea kazi, kubaini ubora na mapungufu yake
🏡Mwanaume kama kichwa chenye macho unahitaji Kutazama na kuona mambo kwa mkeo na familia kwa ujumla, kuyachanganua, kujua yapi ni bora uyaboreshe na yasiyo bora utumie Akili kuyadhibiti
🏡Mwanaume macho yako (ya tafsiri ya kichwa) yakiwa mbovu ndoa itayumba (Mathayo 6:22-23)
🏡Macho yako kama Mwanaume (ya tafsiri ya kichwa) yakiwa vizuri, mkeo ataenjoy na ndoa yenu itakuwa salama. 🌏🌏MASIKIO:Masikio yana kazi ya kusikia na kusikiliza, hizo ni kazi kubwa na ngumu, kwa kuwa ndizo zinazo tengeneza mawazo na maamuzi
🌏Kusikia ni kupata sauti yoyote masikioni, iwe inamaana au haina,
🌏Kusikiliza ni kuweka umakini na utulivu, juu ya sauti unayoisikia na kujua ina maanisha nini na kwa nini isikike katika hali hiyo
🌏Mwanaume kama kichwa chenye masikio, ili ndoa yake iwe makini anahitaji Kuwa na uwezo mkubwa wa kutambua sauti ya mke wake na watoto wake, kujua hii sauti ya mke wangu inamaana gani na aifanyie maamuzi ya busara
🌏Mwanamke, anahitaji kujua mme wake anapata sauti nyingi huko na huko akiwa nje ya nyumba, akirudi ndani inabidi ni mpe sauti itakayo mfanya atulie, atabasamu na kunipenda zaidi.
🌏🌏PUA:Pua ni kiungo muhimu katika kichwa, ina mawasiliano na ushirikiano mkubwa na moyo na mapafu
🌏Lakini kazi ya pua ni kunusa(to detect) harufu nzuri na harufu mbaya na kufanya maamuzi ya kupokea harufu nzuri tu
🌏Mwanaume kama kichwa, unahitaji kunusa na kubaini harufu ya mambo yatakayo hatarisha ndoa na familia yako na kuyadhibiti, kunusa harufu za mambo mazuri mkeo abakufanyia uyaboreshe na kumtia moyo ili kulinda ndoa yenu.
🌏🌏Hayo yakizingatiwa mtaona kila siku mnacheka na kufurahiana daima..
🌏🌏Lakin Mwanamke ajue hasiruhu kuwa njia ya kupitisha harufu mbaya(kero) utaondoa amani kwa utaondo 🎒🎒MENO:Miongoni mwa viungo muhimu ktk kichwa, na msaada kwa tumbo ni meno, kazi kuu yake ni kuhakikisha usalama wa tumbo kwa vitu vyote vipitavyo kinywani
🎒Meno kazi yake ni kuvunja vunja vitu vigumu nakuviweka katika ulaini ili tumbo lipokee vitu salama
🎒🎒Mwanaume kama kichwa chenye meno, unahitaji kushughulika na mambo magumu, hatar kabla ya kumpasia mkeo, Hakikisha yakifika kwa mkeo hayata leta madhara
🎒Kuna mambo mengine ktk maisha, vifua vya kukabiliana nayo, tunatifautiana kati ya Mwanaume na Mwanamke, usipo Anglia utamfanya mkeo kukata tamaa
🎒Mwanamke mweshimu sana mmeo isimuone hivyo unavyo muona ukahisi ndo alivyo, Kuna vitu anamalizana navyo, anapambana, anaumia Makusudi wewe uwe na amani, ufurahi, maisha yaende
🎒Lakini wanawake wengine wanaweza kumdharau mme wake na kumbana muona wa kawaida sana, unakosea sana, yeye kana kichwa chenye meno anaumia kutafuna mambo magumu, ili wewe uenjoy maisha. 🚆🚆ULIMI:ulimi ni kiungo kikali sana, kinafanya kazi na akili, umasikio na macho ili kuhakikisha maelekezo yanayo tolewa na ulimi yako kamili
🚆Mwanaume kama kichwa chenye ulimi, unahitaji, kuonya mambo yasiyo na faida ktk familia yako yasiendelee, kufundisha mambo mapya ili kuisaidia ndoa yako,
🚆Kwa kutumia ulimi jua, ulimi una nguvu ya kujeruhi, na kuganga, hivyo unapoongea na mkeo onyesha kumjali, kumpenda na kumhurumia ili amani idumu
🚆Mwanamke unahitaji kujiadhari na tabia, vitendo vinavyo hudhi, ibua hasira,vitendo vya dharau, usimwonyeshee mmeo, ukivifanya atatumia ulimi vibaya kama kichwa na ATAKUJERUHI, na huo ndo utakuwa mwanzo wa migogoro mizito katika ndoa yenu.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
Thursday, 26 January 2017
SEHEMU 7 ZA KICHWA(MWANAUME)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment