💣💣 *ỦS̉ỈJ̉Ỉ̉T̉ẺN̉G̉ẺN̉ẺZ̉ẺẺ M̉ẢT̉ẢT̉ỈZ̉Ỏ T̉ẺN̉Ả*💣💣
*_B̉ỷ Ẻv̉ Ẻl̉ỉs̉h̉ả K̉ảz̉ỉm̉ỏt̉ỏ@2017_*
*0755444078*
_S̉h̉ảl̉ỏm̉ w̉ảt̉ủ m̉l̉ỏp̉ảt̉ả ̉n̉ẻẻm̉ả k̉w̉ả M̉ủn̉g̉ủ k̉ủv̉ủk̉ả m̉w̉ảk̉ả 2016 n̉ả k̉ủỉn̉g̉ỉả 2017 k̉w̉ả ủs̉h̉ỉn̉d̉ỉ,h̉ảỉj̉ảl̉ỉs̉h̉ỉ ủm̉ẻỉn̉g̉ỉả 2017 ủk̉ỉw̉ả k̉ỉt̉ản̉d̉ản̉ỉ,g̉ẻr̉ẻz̉ản̉ỉ,ủn̉ảl̉ỉả ảủ ủn̉ảc̉h̉ẻk̉ả,h̉ảỷỏ ỷỏt̉ẻ n̉ỉ s̉ẻh̉ẻm̉ủ ỷả m̉ảỉs̉h̉ả,b̉ảd̉ỏ ủn̉ả n̉ảf̉ảs̉ỉ k̉ủb̉w̉ả ỷả k̉ủb̉ảd̉ỉr̉ỉs̉h̉ả m̉ảỉs̉g̉ả ỷảk̉ỏ k̉ủl̉ỉk̉ỏ ỷủl̉ẻ ảl̉ỉỷẻ ̉k̉ảt̉ả r̉ỏh̉ỏ 2016 k̉ảt̉ỉk̉ả s̉h̉ỉd̉ả h̉ỉz̉ỏ,d̉h̉ảm̉b̉ỉ h̉ỉz̉ỏ,m̉ảt̉ẻs̉ỏ h̉ảỷỏ n̉k̉,w̉ẻw̉ẻ ủn̉ả n̉ảf̉ảs̉ỉ k̉ủb̉w̉ả k̉ủf̉ản̉ỷả m̉ảp̉ỉn̉d̉ủz̉ỉ_
Ndo maana mtaalamu wako wa Saikolojia na mchambuzi wa masuala ya Mahusiano na ndoa *_Ev Elisha Kazimoto @2017_* mwanzoni kabisa mwa mwaka nakuletea Miwani👓 ya kukusaidia kuchungulia maisha yako ya mahusiano yako na Mungu,na Mchumba wako,na Mme/mke wako ili usiingie kwenye Matatizo na Stess zilizo kukumba 2016. *_sasa fuatana nami katika uchambuzi huu_*
*_Yohana 5 : 14 - Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi._*
✈ Nianze kwa kukutafakarisha, unakumbuka nini na nini 2016? Ukifumba macho🙈unaona nini, ukitafakari🙇🏻🙇🏻♀ unakumbuka nini?, Katika yale unayo yakumbuka yanakupa kufurahi😃😃😃au yanakupa kusikitika na kulia☹☹😭😭? Je,hayo yanayo kuhuzunisha yalikuja kama majaribu au uliyasababisha mwenyewe? Yanayo kupa furaha na kucheka yalikuangukia bila kutegemea au uliyatengenezea mazingira? *_Mpaka hapo najua umetafakari_*, Lengo langu ni uvae miwani👓 utazame vizuri siku 362 zilizo mbele yako ili *Usijitengenezee Matatizo Tena* Safiri nami
💎💎 *KIJANA/BINTI ULIYE KWENYE MAHUSIANO*💎💎
✍ Binti ulipewa promises nyingi na zawadi na kuahidiwa kuolewa 2016,umeishia kutumiwa tu kama chombo cha starehe,kwa sasa unalaumu na kulalamika na kulaani wavulana, Acha Kulalamika *_Acha kugawa mwili wako ovyo kama bigijii_* 2017 jiheshimu utaheshimika.
✍Kijana wa kiume, 2016 umepanga wadada wa watu foleni zaidi ya 7,wana hamu ya kuingia katika ndoa,mwaka umeisha hawajui hatima yao ni ipi, *Mbaya zaidi Umewatumia,umewavua nguo,mpaka huna hamu na hata mmoja huna mpango wa kumuoa* hiyo laana itakutafuna, 2017 Usiongeze laana,futa laana yasije yakakukumba mabaya zaidi.
✍Wewe mdada,ambaye 2016 kila aliye kuomba urafiki ulikubali,aliyekuahidi kukuchumbia ulimvulia nguo👙,2016 imeisha kwa kuvua nguo tu hujavalishwa hata pete ya urembo💍,unahisi kisaikolojia huko timamu? _Kisaikolojia umevurugwa wa kukuoa anakazi kubwa ya kukurudisha katika hali ya ubinadamu_. *2017 Usivue nguo kujiletea matatizo ya kisaikolojia yatakayo kufanya uchukie wanaume wote duniani*
✍Wewe Kijana, Umekwepa mimba ngapi ulizo wapa wa dada wa watu 2016,walikuamini kwa udanganyifu wako,umewaondolea sifa za kuitwa wadada,na sasa wanaitwa wamama wasio na waume. Uchungu huo ulo usababisha kwao usiuendeleze 2017, *_usijitengenezee matatizo makubwa ukawa na mwaka mbaya._*
*Mlio kwenye mahusiano*
✍Usiendelee na mahusiano ya kuvuana nguo👙kabla ya ndoa utajiletea laana ya kuto pata mtu sahii.
✍Msitende unyama wa kutoa mimba kwa sababu ya zinaa yenu kabla ndoa,kisa mnakwepa aibu,..Mtapewa aibu kubwa na Mungu baada ya kuua kiumbe hicho.
✍Acha mchezo wa kupotezeana muda wa tutaoana,kumbe unamuenjoy mwenzako huna mpango naye, hiyo itakugharimu huwezi kuwa na ndoa nzuri.
*WEWE MWANA NDOA WA 2017*
✍Usijitengenezee stress kwenye ndoa kwa kutotimiza wajibu wako kama mama kwa mme wako au kwa mke wako.
✍Acha kujitengenezea matatizo ya kukosa amani kwenye ndoa kwa kusikiliza majungu ya vijiweni,wenzako wanapigana busu vyumbani mwao wewe na mwenzako mnalala mzungu wa nne. linda mwenzako daima.
✍Unahisi ukiwa mbabe kwa mwenzako ndo unamkomoa ili wewe uenjoy au na wewe ndo walewale wenye akili fupi ya kukuta tawi alolikalia yeye na mwenzake.!.Usijiletee matatizo 2017,tulia ufurahie mwaka.
*Wewe Msimama Madhabahuni*
✍Wewe uloaminiwa na Mungu na kanisa,acha udanganyifu wa kuimba kwenye praise team,kwaya huku wewe ni mzinifu wa hali ya juu,acha kuichafua Madhabahu ya Bwana,2017 yanaweza kukuta makubwa,aibu ya mwaka. 2016 umefanya zinaa kwa kujificha sana na umefanikiwa,kuopoa vibinti vya praise team,kwaya..vijana wengi umewaangusha hata mchungaji wako umemwangusha, *STOP* usijiletee matatizo makubwa.
✍Enyi Makuhani wa Mungu mloibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, *_Mwahubiri mafanikio tu na miujiza,dhambi hamuzioni?Mbona mmegeuza wadada wanao hudumu ofisini kwenu na nyumbani kwenu mmewageuza Wake zenu wa pembeni? Wana kwaya na Praise team unao zunguka nao kwenye huduma mbona wawavua nguo?Mmewatelekeza Mama wachungaji nakuwaona hawafai mnaruka na vidada vidogo🤔🤔._* Acha 2017 inakuja kama moto usije pata aibu ya mwaka.
*NI HITIMISHE HIVI*
_Mungu amekuhurumia 2016,umevuka lakini pia amekuvumilia sana kwa maovu mengi,kwa nini mwaka huu usibadirike? Umekuwa na mwaka mgumu 2016,umeumizwa,umelia,umeachiwa jeraha na kovu la kudumu katika hisia na mahusiano yako,lakini wewe mwenyewe umekuwa mchangiaji mkubwa wa matatizo yako hayo,sasa Ushauri wangu kwa mwaka 2017_ 👇👇👇
*_Yohana 5 : 14 - Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi._*
*By Ev Elisha Kazimoto @2017*
*0755444078*
Monday, 2 January 2017
USIJITENGENEZEE MATATIZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment