Sunday, 15 January 2017

KUOANA NA MTU WA IMANI TOFAUTI

*UKWELI KUHUSU KUTAKA KUOANA NA MTU WA IMANI NYINGINE*
👉Kwanza naomba ifahamike kuwa ndoa ni Taasisi nyeti sana isiyo hitaji kubumba bumba mambo,na hapa lazima kweli ya Mungu iwe dhahiri ili kama unafanya maamuzi ufanye maamuzi ukijua madhara au faida ya ndoa *MIXTURE* Maamuzi yako ya sasa ndo maisha yako ya baadaye.
_Ziko sababu nyingi za kwa nini Usioane na Mtu wa Imani Tofauti na wewe hasa kama wewe ni wa Imani ya Wokovu kwanjia ya Yesu Kristo na unayahishi maisha hayo ya wokovu_
2KORINTHO 6:14-17
14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 

15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 

16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 

17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. 
👉Mstari wa 15, Kuamini ni nguzo kubwa katika imani na ndicho hutofautisha imani moja na NYINGINE,dini moja na nyingine na hapa ndo kutofautiana katika mwelekeo.
👉Suala la wote ni Wakristo halina nguvu katika imani,maana humo humo kwa Kristo hutofautiana katika Imani(kuamini)
*_Kuna wanao amini maombi kwa wafu,wengine hapana,wengine wanaamini katika kuwa watakatifu ni baada ya kufa,wengine wanaamini utakatifu ni hapa duniani Zaburi 16:3,wengine wanaamini katika kuwaombea walio kufa waingizwe peponi,wengine mtu akifa amekufa ataenda sawasawa na alivyoishi duniani,wengine wanaamini ubatizo wa watoto,wengine watu wazima waliokiri kwa kinywa kumpokea Yesu,wengine wanaamini ujazo wa roho mtakatifu na kunena kwa lugha,wengine haina haja,wengine wamaamini ukifa imeishia hapo,wengine kuna maisha ya kufa,wengine tutakaa duniani milele,wengine kuna mbingu mpya na nchi mpya(mbinguni),_*
Haya ndo baadhi ya mambo yanayo tofautisha Ukristo,yako mengi ni muda tu umezuia,sasa ona athari hizi....
👉Hapa si zungumzii Uana Dini(yaani kuwa Mkristo) nazungumza Mtu aliyefanya maamuzi binafsi ya Kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako kwa kutubu na dhambi zako na kuziacha,si suala la kuabudu kwakuwa nimekuta wazazi wangu walokole...hiyo ni uana dini ndo huwa wanashika dini ya baba na mama na hawataki kuihasi,ila ​Si kwba w all ikuta na Injili ikachoma mioyo yao wakaamua kkimbilia Yesu na kuacha njia zao mbaya​ w an epokea imani kwa wazazi huo si wokovu wala haupo kwenye biblia( ​Hao wanaweza oana na mtu yoyote wa aina hiyo,haijalishi wa dhehebu gani au dini gani​)
👉Katika Imani ya Wokovu wa Yesu Kristo(Kuokoka) ina msingi huu katika kuoana...
*_Amosi 3 : 3 - Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?_*
Kama hampo imani moja,hamuamini katika imani moja(sawasawa *Waefeso 4:1-6* hamuwezi kuoana labda kama wote mna wokovu wa Kifafa,yaani anaye sema ameokoka wokovu wake ni kifafa huyo anaweza fanya maamuzi hayo)
👉Tatizo linalo wasumbua na kuwachanganya vijana wengi sasa, *Kwa sasa kila dhehebu wanasema na sisi tumeokoka* lakini kwa uhalisia *Hawajaokoka wala hawana mpango wakuishi maisha ya wokovu* ila lugha hii ya kuokoka imezuka miaka ya hivi karibuni 10 tu kutoka sasa,kabla ya hapo ilikuwepo lugha ya Mimi dini yangu ni hii,na hao ni dini ya walokole (walokole) sasa ona shida hii...
👉Kuna uongo na utapeli wa kujifichia nyuma ya *Mungu,Amani ya Kristo,Roho kasema,Kufunuliwa* ifahamike kabisaa hakuna hata chbe ya ukweli Mungu,Roho mtakatifu kusema na mtu wa Mungu kuoana na mtu Asiye Amini(Okoka),Mungu si maskini kiivo mpaka aazime mtu upande wa pili kpatia mtu wake mtu Asiye sawa kiimani,lakini Issue ya amani,kuna *Amani ya Nafsi,Amani ya Shetani,Amani ya Hisia,na Amani ya Roho wa Kristo* je unajua kuzotofautisha?au ndo kumpakizia Mungu?
👉 Kuoana na mtu wa imani tofauti(yaani mnaamini tofauti) mfano 1 nitumie... *Wewe waamini ubatizo wa mtuzima na maji mengi(mke),na mme anaamini ubatizo wa watoto na maji machache* saaa fikiria mkipata mtoto anaishi imani ipi,je,nani anakubali kuipoteza imani yake aifuate ya mwenzake? Na endapo unaamua kuipoteza imani yako kwaajili ya ndoa, *Inaama imani yako ilikuwa Batili na wewe ulikuwa batili* Ndo zile imani za kukuta baba na mama wanaabudu imani flani na wewe ukadaka hiyo(si zungumzii dhehebu...mfano EAGT,TAG,FPTC haya ni madhehebu ila imani ni moja)no peoblem au (RC na Karithematic)ni kitu kimoja.
Mtoto huyu mtampoteza,malezi yatakuwa feki,kuna mmoja aliye na nguvu atalazimisha afuate misingi yake,mtoto atakuwa kama yatima mwenye mzazi mmoja na andiko la Mithali 22:6 halita timia kwake. Kwanini mchome kizazi chenu watoto wasiyo na hatia kisa mahaba yenu yasiyotokana na Mungu? Oana na mtu wa IMANI MOJA kama ni wapagani wapagani,kama wana dini,wana dini,kama Mlio wateule wa Kristo muwe wote wateule wa Kristo.
*_By  Ev Elisha Kazimoto_*
     *0755444078*

No comments:

Post a Comment