💊💊 *MATAPELI WAEPUKE KATIKA MAHUSIANO*💊💊
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
_Shalom vijana wote mlio kwenye urafiki na mlio kwenye uchumba,dawa ya kuganga majeraha yasiyo na sababu hii hapa_
💉 Mara nyingi watu wakiingia katika mahusiano wanapenda mpaka wanakuwa vipofu,hawaoni hatari☠☠☠,wanajiachia kwa kila lugha,kila tendo,kila eneo,mwisho wa siku wanaishia kulia😭😭😭.
💉Unapaswa kujua mambo haya katika unapoanza urafiki au uchumba,ndo utawakwepa *Matepeli na Wahuni wanao Jeruhi mioyo*
1⃣ *_Si kila mmoja anahitaji urafiki,au Uchumba ana Akili timamu_* Nikama lugha ngumu ila ndo ukweli,kuna watu unaanza nao urafiki,uchumba akili zao siyo sawa,hawawezi kujua gharama ya moyo wako ikoje katika mahusiano hayo,hawajui umempa moyo kiasi gani,aulindeje asikujeruhi,ila wao wana *Maamuzi ya kukurupuka yasiyo jali Hisia zako* huyo hana akili timamu,usipo kuwa makini atakufanya maisha yako yote ya urafiki,uchumba au ndoa kujeruhika na kulia mara kwa mara.( *_Kumtambua, Angalia anavyo kuchukulia kila siku,maamuzi yake kwako,na ikitokea mkatofautiana maamuzi yake yakoje_*
Usijiue bure,epuka tapeli huyo.
2⃣ *_Si kila anaye anzisha mahusiano na wewe Amedhamilia kukuoa,kuolewa na wewe(kuingia katika ndoa)_* Ndivyo ilivyo,watu wana sababu nyingi za kuja kwako kwa lugha ya kuchumbia au kuchumbiwa, _wengine wameachwa wana majeraha yao,wanahitaji wakutumie upoze majeraha yao ili wale wawapendao wakute wana mioyo iliyo tulia,imekauka damu_ *kwa hiyo wewe unatumika kama Transformer Pozo🙄🙄🙄* wengine hawahitaji upweke,wanatafuta watu wakuwaondolea upweke ilavsi kuingia nao kwenye ndoa,...Ukijiachia kwa watu hawa utalizwa sana,utangoja sana. ( _Kumtambua mtu huyu, hana mtazamo wa future,hapendi kuzungumzia hatima ya mahusiano yenu,ni mdadisi sana juu ya habari zako,ila za kwake anaficha sana, ana maigizo mengi kuliko uhalisia katika mahusiano,hapendi kuingia gharama sana kwaajili yako(gharama ya muda,upendo,kujali,kutoa nk) yeye anahitaji atimiziwe mambo yake ila ya kwako anaya ruka)_* Ukizubaa unapigwa mimba,au unapiga mimba mtu halafu hakuna ndoa,au unavuliwa👉👙na kuachwa.
3⃣ *_Si kila anayeanzisha mahusiano na wewe,wewe ndo mtu wake wa kwanza,huwenda wewe wa 20_*
Kama hukujua kanuni hii,utaumia sana,unahitaji kuwa mtu wa kutafakari,kila anaye anzisha mahusiano na wewe ya uchumba au ya urafiki hajaanza na wewe, *_Kuna mwingine ametoka kuvua👉👙wadada kama 10 na wote alikuwa akiahidi kuwaoa lakini kwanza aonje tunda😋mwisho anawapiga chini, na kuna walio vuliwa👉👙karibu na watu 25 wee wa 26,ameisha ona na kuzoea utamaduni huu wa kuvuliwa na kila mchumba,rafiki,sasa ukikausha bila kumvua👙,moja utapigwa chini, mbili Utashawishiwa na kutegwa mpaka uingie mtegoni._ Kuwa tambua watu hawa,ni *Wepesi kuomba ngono kabla ya ndoa,wanahimiza,na kusisitiza ngono ndo muoane,au ndo atafurahi au kukuamini,kukupenda*, Luga zao za mitego mitego, wanaomba sana picha za utupu zako,hawawezi kuthibiti hisia zao,waongo. Kuwa makini na hao ukimwamini atakuchezea na kukuacha.
4⃣ *_Si Kila anaye kuja kuanzisha mahusiano na wewe yupo peke yake,ameachana na mtu wake wa kwanza_* Msaikolojia mtaalamu wa mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto* Nakujuza haya uyajue Usiumizwe ovyo na Matapeli,.... _Kuna watu wanaanzisha mahusiano huku wakiwa na watu wao,yaani anatafuta *Spare Partner* wewe unayeingia naye katika mahusiano unakuwa *Stabilizer* ya mahusiano yake,ukibahatika unaweza chukuliwa wewe akaachwa kabisa wa kwanza,au mkaachwa wote_ (Kumtambua mtu huyu, mara nyingi wanakuwaga busy sana,kila ukimwambia mbona mawasiliano yetu yana dolola,utaambiwa niko busy sana,mambo mengi,mbona huniamini,kama vipi tafuta mtu mwingine asiye na ubize, wana majibu ya shortcut, hawana lugha za kubembeleza,ni wakali...wanapenda ngono,wasichana wanapenda kuchuma cash sana,ukiwa mbaili kwao wanaingia mitini🌴🌴🌴.) Kuwa makini nao ukimpa mwili wako anapotea.
💉 *Mchumba Makini,mwaminifu utamjua tu kwa haya hapa* Wala hakuna haja ya kutafuta tochi ni wazi wazi utamuona...
*_Kijana au binti kwanza,anaheshimu lile agano la neno lake la nakupenda uwe mke au mme wangu wa ndoa,anajali,anaheshimu mwili wake na wa kwako,anahofu ya Mungu hayuko tayari kumkosea Mungu, Pili hataki kuumiza wala kumuuzimizwa na mtu wake,anajitahidi kutatua changamoto za mahusiano kwa amani, anaimarisha mawasiliano hata kama yupo busy sana na shuguli na kazi,lakini muda wa mawasiliano na mwenzake lazima upatikane,Tatu anawaza na kupangilia harakati za ndoa na maisha na kumshirikisha mwenzake kila hatua,hataki kuchelewa sana kuingia katika ndoa, hutasikia kuomba ngono wala mambo yote machafu,lakini nimshirikishaji sana wa mambo ya Mungu na ratiba za Kimungu,kama ibada,kusoma neno,kumtumikia Mungu,maombi na kufunga na kuvumilia katika yote mpaka mfike ndoa._ Mtu huyu ukimpata umepata tunu,zawadi,na upendeleo kwa Bwana.
💉💉 *_Mpaka hapo binti/kijana umejua nani wa kuoana naye,nani wa kupiga chini haraka sana ili usiumie_*💉💉
By Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)
0755444078
( _Mtaalamu wa Saikolojia ya Mahusiano na Ndoa_)
Sunday, 25 December 2016
MATAPELI WA MAHUSIANO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment