Friday, 2 December 2016

LAZIMA ADUI YANGU AFUTILIWE MBALI

🚧🚧 *LAZIMA ADUI ZANGU NIWAFUTILIE MBALI*🚧🚧
     *_By Ev Elisha Kazimoto_*
        *0755444078*
_Shalom makamanda wa Bwana,watu wa vita,nakuletea ujumbe huu ili uwe hodari na moyo wa ushujaa Adui zako zamu yao imefika ya Kufutiliwa Mbali kwa mkono wa Mungu wenye nguvu_
🚧 Ujumbe wetu leo, *_Nikuwafutilia mbali na Kuwakatilia mbali maadui zetu_*  Kwa nini kufutilia mbali adui zako,ni kwasababu uovu wao wanao utenda katika maisha yetu ni mwingi mno,hauvumiliki,Lazima wafutiliwe mbali.👇👇👇👇
*_Mwanzo 6 : 7 - Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya._*
🚧👆🏻Mpaka Mungu anatoa maamuzi ya kumfutilia mbali mwanadamu na kila kiumbe,ni uovu,matendo mabaya yalikuwa yameuchukiza moyo wa Mungu.
🚧Kazi wanayo ifanya maadui katika maisha ya watu ni *Uovu mkubwa usiovumikika*,hebu tafakari mfumo wa maisha yako ulivyo vurugwa na wachawi,haki yako ilivyo porwa na maadui zako,ndoa yako ilivyo vurugwa,Elimu yako ilivyo shambuliwa,uchumi wako ulivyo tawanywa na Maadui, uovu huu ni mbaya sana hauvumiliki, *_Lazima Adui Akatiliwe mbali_*👇👇👇👇
*_Zaburi 118 : 12 - Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali._*
🚧Kukatilia mbali,kufutilia mbali ni kuondoa,kupoteza alama,sura za Adui katika mazingira yako tunapoelekea mwisho wa Mwaka,yako matatizo mengi ulokutana nayo maishani,ukiwa ni mpango na mchezo wa maadui zako,sasa zamu yao kufutiliwa mbali. _Mungu alitumia  Gharika kufutilia mbali mwanadamu mwovu na viumbe vyote, Gharika hiyo hiyo,ipo ya ulimwengu wa roho kuwafutilia mbali watesi wetu_👇👇👇👇
*_Mwanzo 7 : 4 - Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali._*
Siku hizi zilizobaki 29 kuhitimisha mwaka, *Ni siku za kushusha Gharika ya Moto kwa Wachawi,waganga wa kienyeji,Viongozi wanao pora haki za wanyonge* mpaka watakapo kuwa Wamekatiliwa mbali,tuingie mwaka  2017 kwa Ushindi na uzina wetu.
🚧Katika mwisho wa Mwaka,miezi kama hizo,wapo maadui na wana wa giza *_Wanazitumia Safari za watu kupata Damu ya Kafara kwa kusababisha Ajali,Pokea Neno la Kinabii leo katika mkesha huu wa OPERATION futilia mbali maadui, Hakuna Damu yako,wala ya jamaa yako itakayo kwenda na Kafara za Wana wa Giza katika jina la Yesu_* Bwana atatuma malaika katija safari zako zote,za mwendo wa miguu,kwa vyombo vya moto utakuwa salama, *Na kila adui atakaye jisogeza kupora Uhai wako,Atakatiliwa mbali,yeye ndo Atakuwa kafara ya Wenzake kwa jina la Yesu* Yesu tulie naye ni moto ulao👇👇👇
*_2 Samweli 7 : 9 - nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani._*
🚧Inuka kwa uhodari na ushujaa,tuombe Maombi ya vita,ya kiwakatilia mbali adui zetu,piga wachawi,piga waganga wa kienyeji,piga maadui wanao otea uhai wako,ndoa yako,elimu yako,kazi yako,upo uweza wa Mungu wa kuwakatilia mbali, *_Lazima adui zetu watupe visogo na si vifua,watakimbia huku tukiwakatilia mbali kwa jina la Yesu,mahali ulipo Sema Nitavuka Mwaka kwa Ushindi,Adui zangu Mmekatiliwa Mbali_*
_Ujumbe huu ni Mahususi kwa wana wa Mungu,watu wa vita,watu walio na uchungu na kazi ya Mungu watu wanaotamani kuishi ili wamtumikie Mungu_
*Mungu Akuhifadhi Umalize mwezi huu wa December salama uingie 2017 kwa Ushindi, Ameni*
    _BY EV ELISHA KAZIMOTO_
     *0755444078*

No comments:

Post a Comment