Thursday, 1 December 2016

KIJANA NA MCHUNGAJI WAKE KATIKA KUPATA MWENZI

🏁🏁  *KIJANA NA MCHUNGAJI WAKATI WA KUOA/KUOLEWA*🏁🏁
   *_By Ev Elisha Kazimoto_*
      *0755444078*
_Shalom, shalom vijana mlio na safari ya kuelekea kwenye ndoa takatifu, ndoa ya baraka ndoa ya kukusaidia ufike mbinguni, leo nakutana na wewe katika uchambuzi huu muhimu, wa Nafasi ya mchungaji wako katika kuindea ndoa yako_
🏁 Kuna vijana ambao maisha yao kanisani huwa hayaeleweki, na wala hawana muda na mpango na mchungaji, miaka yao yote awapo kanisani, *_Ila ukifika muda wa kuoa au kuolewa ndipo wanaanza kujisogeza kwa mchungaji_*  ndo ruti za kufanya kazi kwa mchungaji zinaanza, kushugulika kanisani kunaanza, ni muda tu uhitaji wa kuoa/kuolewa unapo fika sasa hapa upo jatika hatari kubwa na uhuni.
🏁 Vijana wengi hawajui umuhimu wa mchungaji wake mpaka muda wa kuoa,/kuolewa maana utafanya yooote, ila lazima upite kwa mchungaji wako kwaajili ya kuiandaa ndoa yako, sasa hapa huwa ndo vijana wanachemka. *Angalia umuhimu wa mchungaji wako*👇�👇
� *_Malaki 2 : 7 - Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa Bwana wa majeshi._*
✍� Kijana unaenda kuoa, kuolewa, mnakubaliana kuoana, unaenda kwa mchungaji *_Anakwambia Huyu kijana/binti hakufai, maisha yake siyo mazuri, mchawi huyu, ametoa mimba huyu 3, kijana huyu atakuwa mzigo kwako mvivu kweli_* mnafanya maamuzi gani baada ya maneno hayo ya mchungaji?
✍� Vijana, wengine huamua kuto washirikisha wachungaji mambo yao ili wasije wakawaharibia dili lao, _Hivi kweli ungekuwa kijana unaye mpenda Mungu, unajituma kanisani na upo karibu na mchungaji wako, kweli unaweza kunuwazia mchungaji wako kwamba ukimuhusisha mahusiano yako atakiharibia dili?!_  *Hapo wewe ni muhuni ndo maana una wasiwasi wa kuto mwambia mambo yako mchungaji wako*
✍�Hivi, unaamini mchungaji wako anamfahamu sana huyo mchumba unaye taka kuoana naye kuliko wewe? Je, madhaifu ya kiroho na kimwili ya huyo unaye taka kuchumbia unayajua, unahisi nani wa kukusaidia kama si mchungaji wa huyo mtu wako?
✍�Lakini vijana wamewatupilia mbali wachungaji, wanaanza mahusiano, Uchumba mpaka ndoa, bila kumuhusisha mchungaji kwa kika hatua, baada ya kuoana ndoa inaanza kuyumba ndo umuhimu wa mchungaji unaanza kuonekana, mnampa ratiba za maombi ya kufunga sikuu 7.awaombee huu ni upuuzi.
✍�Kuna vijana muda wa kuoa /kuolewa, _wanawaona wachungaji hawapo kiroho, wanaweza kutumiwa na shetani kuharibu uchumba wao, hivyo hawawahusishi,_  hata wakiwahusisha kidogo, mchungaji akishauri, wanagoma hii imepelekea ndoa nyingi kuwa na majanga, kuvunjika, kukosa amani.
✍� Kijana pamoja na kuwa upo kiroho zaidi au umepoa, mchungaji ana nafasi ya pekee kukushauri katika safari ya ndoa unayo iendea,  *_Si semi mchungaji kukuchagulia mke/mme wa kuoana naye japo anaweza kukushauri_* 👇�👇�
*1-Samweli 3:1-9*
1   *_Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri._* 

2 Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona), 

3  _na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu;_

4 basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa. 

5 Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena. 

6 Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena. 

7  *_Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake_*.

8 Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa Bwana ndiye aliyemwita yule mtoto. 

9  *_Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake._*
✍�👆�Kuna vitu wewe huvijui, lakini mchungaji anaweza kukutatulia mambo hayo, na ukapata mtu sahihi.
✍�Wapo wachungaji feki, lakini wapo wachungaji original, lakini kama kijana utakuwa uko vizuri na Mungu utamjua mchungaji feki na original mapemaa wala si muda wa kuchumbia au kuchumbiwa, na kama unajua mchungaji wako ni feki kwa nini kuendelea kukaa chini yake? Lakini vijana muda wa kuoa na kuolewa ndo huwa wanawaona wachungaji wao kuwa ni feki, hapo utazoa bomu.
✍� Kijana anaye weza fanikiwa katika hatua ya ndoa yake, mi yule ambaye yupo karibu na mchungaji wake hata kabla ya kuanza harakati za kuchumbia/kuchumbiwa, huyu kijana atafaulu saba.
✍� wachungaji wengi, kijana ukisha zama kwenye mahusiano ndo unaenda kumshirikisha mchungaji, huwa wana nyamaza kimya ili kuepusha shari, _Ushauri wangu kwako kijana, jenga mahusiano mazuri na mchungaji wako, mchungaji awe kama mzazi wako, ili kwa hatua hii muhimu akusaidie usije oana na mtu ambaye ni Bomu kwenye ndoa_
✍�  *_Mfanye mchungaji rafiki yako, ili Upate kumfahamu vizuri kama ni feki au original, na ndipo katika hatua za uchumba akikushauri hutakuwa na wasiwasi naye_*
_Kwa leo niishie hapa, ila jifunze kws Samweli na Eli, usijiaminishe sana, mchungaji ana nafasi yake muhimu kwako_
  *_By Ev. Elisha Kazimoto_*
     *0755444078*

No comments:

Post a Comment