π§π§ *HUWEZI KUPATA MCHUMBA KAMA HUJIPENDI*π§π§
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
_Hello ππ»♂ππ»♂ vijana na mabinti,hii zamu yenu kumeza dawa ya kuzuia ubachela na shangazi usio na sababu kwako_ vijana wa kike na wakiume wamefikia hatua ya kutafuta dawa za kuleta mvuto wa kimapenzi,wengine kusaka maombezi kila kona ili wapate wachumba,lakini bado hali ni tete,no mchumba ila kuharibiwa maisha na kuishia zinaa tu,hakuna anayekubali kuishi na mtu ndani. *_Sasa unajua sababu yake? Mtaalamu wa saikolojia ya mahusiano na ndoa, Ev Elisha Kazimoto nakuletea uchambuzi huo_* Fuata nami:
_Ukiwa kijana,ishi maisha ya kujipenda,kujikubali,yanayo vutia,yanayo kuvitia wewe hata watu wengine,kuwa na maisha ya kujiamini,yenye mpangilio,yenye ushawishi,mwanamke/mwanaume ahiitaji sana sura anahitaji umakini wako wa maisha_
π§Lazima kwanza kijana ujue, Mahusiano ni ushawishi wa Hisia za mtu ziambatane nawe,kumiliki na kuteka Hisia za mtu mwingine,kumfanya ahisi uwepo wako maishani mwake ni ukamilifu wa mapungufu yake lakini ni faida kwake.
π§ Sasa kwa lugha hiyo ya kisaikolojia,nimuhimu tuanze kujiuliza hivi ninapo taka kuanzisha mahusiano ya uchumba ili niishi na mtu huyu,KWELI nina uwezo na nguvu ya Kumiliki Hisia zake,na yeye akajiona yuko salama na amefika? *_Hapa ndipo watu hupoteza wachumba au kukataliwa_*
π§Hisia hubatana na mtazamo wa Physical Appearance ya mtu,personality ya mtu na Prsentation ya mtu kwa watu ndivyo huvuta au hufunga hisia za mtu juu ya mtu.
π§ *Kuna vitu unahitaji kuwa Makini Kama hujapata Mchumba,na wakati ukiwa na mchumba*π§
⚓ Kuwa makini kauli zako, _Unapo kuwa kijana upo katika nyakati za kuoa au kuolewa bado unatafuta,chunga kauri zako,_ Kuna vijana kwa mabinti kabla ya uhitaji mkubwa wanakuwa na kauli za kibabe,za kujiona,za dharau,za kuonyesha hana uhitaji mkubwa na mambo ya mahusiano, *_Unacho paswa kujua kisaikolojia Kauli zako zinaishi,zinatangaza akili yako na maisha yako,kauli hujenga ngome inayo yeyusha hisia za mtu_* Kuna watu hupenda kusema,mimi _siwezi oa/olewa na kabila flani,kimo flani,rangi flani, kada ya kazi flani,hizo kauli zina nguvu ya kufuta hisia za mtu ambaye ange vutiwa na wewe_ Lakini pia kauli zina sifa ya kusbaa haraka kwa watu,zikisambaa wakati huna uhitaji wa kuoa/kuolewa huwezi kuona shida,ila ukifika wakati wa uhitaji utatamani upite kila kona kwa kila mtu unatengua kauli but it is too late.
π§Kuwa makini na Uvaaji wako, hiki ni kitu kinacho wakilisha Personality yako,mpangilio wa maisha yako,kwa hiyo kama hujali namna ya uvaaji wako inawakilisha namna usivyo makini katika kupangilia maisha au mambo katika maisha yako( *Unaishi Rough*),unahitaji kujua kwamba hisia zinaenda na mvuto wa mwonekano wa mtu(Hapa si zungumzii kumiliki nguo nyingi),uwezo wa kujiweka vizuri kwa nguo hizo ulizo nazo, kumechisha. Kila mtu anapenda mtu *Presentable* kwa watu,ndoa haiishii chumbani,ni pamoja na mwingiliano na watu,sasa kila mtu hapendi *Kumili Kituko* mtu asiye jijali. Je,umepoteza wachumba?jiulize uvaaji wako ukoje.
π§Kuwa makini na kampani ya Marafiki zako; Marafiki ni watu wanao share(milikishana tabia),kama marafiki zako tabia zao ni mbaya,una hati hati ya kutopata mme/mke, ukishaambatana na mtu flani watu wanajua na wewe niwa hivyo, *_Usije jifariji kwamba mimi huyo ni rafiki yangu tu,ila mambo yake simo_* hiyo unaamini wewe,walio nje wanajua na wewe niwa hivyo. Sasa hiyo inaweza kukugharimu kupata mtu wa kuoa/kuolewa naye.
*_Leo nimesema na wewe vitu hivyo vichache, kwa Masomo mengi ya mahusiano,ndoa na Saikolojia katiks maisha ya mahusiano kutana na Mchambuzi Mtaalamu wa Saikolojia ya mahusiano na ndoa Ev Elisha Kazimoto, Katika Blog ya Material Adimu, na Group la WhatsApp (Material Adimu University)kujiunga ni kwa Interview, lakini pia muda si mrefu madara maalumu ya Uponyaji wa Kisaikolojia katika Mahusiano na Ndoa yataanza,Mawasiliano ni 0755444078*
_By Ev Elisha Kazimoto_
Thursday, 1 December 2016
JIPENDE NDO UPENDWE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment