Sunday, 4 December 2016

KUOA BINTI MSOMI/MWENYE ELIMU NI MWIBA?

🏆🏆 *HOFU YA VIJANA KUOA MKE ALO NA ELIMU KUBWA AU KIPATO KUKUZIDI*🏆🏆
   *_By Ev Elisha Kazimoto_*
      *0755444078*
_Shalom,vijana,mabinti na wale ambao mmeisha ingia ndoa,nitegee sikio la ufahamu na uelewa,mwana saikolojia na mchambuzi wa masuala ya Ndoa *Ev Elisha(Baba Eve)* nikupe Maarifa ya Changamoto hii ilo na shida kweli hata katika ndoa_
✍Kumekuwa na kigugumizi kwa baadhi ya vijana cha *_Hivi nioe kweli huyu dada msomi,mwenye mshahara kunizidi,mwenye uchumi,anayetoka familia Matawi ya juu,si ntapoteza heshima ya uanaume?Ataniheshimu kweli?_* Lakini imeenda mpaka kwenye ndoa wapo wanao juta kwa mke kuwa na uwezo wa kifedha au Elimu,vimegeuka fimbo kwa mwanaume ndani.
✍Hapa kuna shida pande zote mbili,kijana huu ni mtazamo potofu,usitumie makosa ya wengine kujipa jibu kwa maisha yako,unapaswa kujua kila mtu ana Neema yake na mfumo wake wa ndoa,inategemea umejipangaje kuingia kimaarifa na kiroho na kisaikolojia.
✍Kwa wamama na mabinti hii nichangamoto kwenu,ambayo inaweza kukufanya,uchelewe kuolewa,au uchezewe tu na wajanja,na mama katika ndoa,uishi maisha yote ya ndoa bila kuifurahia.
_Sasa ambatana nami katika uchambuzi huu katika point 9_
1.Tunapo oa au kuolewa,hatuoi au kuolewa na Elimu,Cheo,Pesa wala Utajiri wala Kabila, tunaoa au kuolewa na mtu ambaye anaweza kutufanya tufikie vision zetu,anaye toka kwa Bwana,wakunisaidia,kufika mbinguni na duniani kutimiza ndoto zangu.
_Haijalishi ni mtoto wa waziri,wanapesa chafu,ana masters mimi ni form 6 au 4 au STD 7,kinacho matter tumependana kwa dhati ili tuwe pamoja_au tumependana kwa sababu flani
2.Vijana mnahitaji kufahamu jambo moja,msiwe na fikra potofu,hatutengenezi unyenyekevu/utii wa mke,au hatupati heshima kutoka kwa wake zetu kwa kuwanyima fursa,au akiwa hana elimu,au hana pesa,kila kitu ananitegemea basi hapo atanitii,atakuwa mnyenyekevu na heshima kwangu, huo ni ufinyu wa akili ya mwanaume,hofu,kutojiamini na hufai kuwa kwenye orodha ya wanaume wa ukweli.
Ukitengeneza ndoa ya namna hiyo,huo ni utii feki,heshima feki,na akija kuzipata pesa,au maarifa utaumia.
3.Ni uzembe wa akili na wakimaisha kutaka kuoa mwanamke asiye kupa changamoto,ambaye kila kitu ni ndiyo,ndiyo....hana mawazo ya challenge,hamuwezi fika mbali hata kiroho,kimaendeleo,lakini mwanaume utakuwa na mzigo mkubwa wa kubeba familia....Nini maana ya msaidizi?mtu wa kuishughulisha akili yako,ikilala anaiamsha,usije kujisahau kama kichwa cha familia.
4.Unapooa oa mtu wa kukufaa,awe na pesa,elimu maadamu umempenda,anauwezo wa ku make future na wewe, Elimu,au Pesa siyo maisha ya ndoa,maisha ya ndoa nizaidi ya pesa,inahitajika akili na upendo wa dhati,japo Elimu na pesa vina mchango flani katika maisha ila siyo kigezo cha ndoa ya furaha.Wapo maprofesa,masters,degree, pesa chafu na utajiri lakini ndoa ni moto. Ndoa ni zaidi ya vitu hivi vionekanavyo
5.Kati ya Mwenye Elimu au Maarifa nioe yupi,lazima tujue Terms hizi mbili.. *Elimu* _Ni nyenzo inayo fungua ufahamu wa mtu na kumpa mwanga(maarifa)namna ya kuendesha maisha, ipo Elimu rasmi ya darasani na isiyo rasmi itokanayo na jamii na maisha ya kila siku._
*Maarifa*  _Ni ujuzi unao msaidia mtu kufanya jambo sahii,muda sahii,Eneo sahii kwa Lengo sahii_  Kwa tafsiri hizo mpaka hapo unaweza kujua uoe yupi.
*My comments, Kuishi na mtu asiye na maarifa hamtaenda mbali wala ndoa haiwezi kuwa ya furaha*
6.Wadada,na Wanawake mloolewa ndo mmewajengea vijana na wanaume wenu mtazamo wa *Kiubabe,na Kujiami na Hofu*  _binti kwa kadri unavyoongeza madarasa unaongeza Jeuri,Kujiona,Dharau kwa namna hiyo hujitengenezei mazingira ya kuheshimiwa,kupendwa,ila unatengeneza mazingira ya *Kusugua benchi la Ushangazi(Ubachela) miaka 28,30,34,37*  hata 40_ wakati walo maliza la 7, form 4, form 6 wakafeli wanaolewa na wanaenjoy maisha ya ndoa kwa furaha, sare utawashonea,michango utatoa na harusi utaudhuria nyingi na *Kwaito utacheza sana* utarudi nyumbani wavulana wanakuogopa kama Ukoma.(Vidato vyako ulivyo vitukuza havita kuvika pete 💍ya uchumba,wala kukufanya uitwe Mrs.
_Pata saikolojia hii wewe dada kwa mwana Saikolijia (Ev Elisha Kazimoto) kwakadri Unavyoongeza vidato au uchumi,jishushe,thamini watu wote,aliye soma,asiye soma,aliye na pesa na asiye na pesa, *Ongea na Watu wa Rika zote,fani zote za kazi* dharau fani flani ya kazi,ujipachike kwa mtu wa fani maarufu,usipo mpata huko wa kukuoa,utatamani hata Kondakta awe mme wako wewe mwenye Masters_
7.Mama uliyeolewa,Elimu yako,miradi,pesa,biashara yako pesa za familia uliko toka na kuwa na ndugu wakubwa serikalini,haviwezi jenga ndoa yako,wala havina mchango wowote,unamdharau mmeo au ndugu,wazazi wa mmeo,hujielewi wewe,ungekuwa wee wathamani ungekaa kwenu,ukaolewa na Elimu au pesa yako,au kwenye ukoo wenu ungeolewa huko ili ukae na kiburi cha pesa na elimu yako na umaarufu wa familia yenu, *_Ila kwakuwa ulikubali kutoka kwenu,na pesa zako na elimu yako, mimi mwalimu wa Mahusiano na ndoa nataka ni kwambie, Wewe na Familia yako Ni Maskini wa Hali ya Juu_*  Eeh....naona unaishangaa lugha hiyo, narudia kwa mkazo,  *Wewe na Familia yako Nimaskini wa Hali ya juu* maana yake ni nini?👇👇
_Kama kwenye familia nzima,na pesa zenu,umaarufu wenu,vyeo vyenu,na elimu yako na mshahara mkubwa, *Amekosekana wa Kukuoa* Mpaka ukaolewa na mtu mwingine,tena wa maisha ya kawaida, basi *Kuwa Mpole* huyo ndo BOSS wako na familia yako._
Weka vitu vyote chini,nyenyekea,tii mmeo linda ndoa yako acha ukorofi na dharau,penda familia ya mmeo na wathamini, *Zaidi ya yote Mweshimu mmeo kuliko mtu yeyote*
8.Lakini wanaume niwa taadharishe,mmesababisha shida ya ndoa zenu,mmeolea familia?yaani mmekuwa dhaifu kuzisimamia ndoa zenu,ndo maana vita ,ugomvi wa mkeo na mawifi,mashemeji,mama yako hauishi,shida ni nini,mke wako ume waachia wengine,kila mtu ana uhuru wa kuzungumza,kuonya,kulaumu,kusuta,upo kimya tu!Weka mipaka mkeo ni wako siyo wafamilia kurusha rusha,yaani kila mtu anaweza kuamua mkeo aweje,huu ni ufinyu wa maarifa,hujui yeye ni mgeni,na yuko mmoja kwenye familia ninyi mpo 12,kila mmoja akimshambulia afanyeje lazima Ajihami...ndo maana watakuja wa nyumbani kwenu anaenda kutembea,au analala na yeye anatafuta usalama,ninyi mpo 12 yeye 1,sasa Jeuri ndo mtu wake wa 2.
_Mwanaume muwekee mkeo mazingira ya usalama na kuheshimiwa na ndugu na wazazi na watu wote wanao kuhusu_
9.Wana ndoa,kuweni na muda wa kuzungumza,kuangalia kero,shida na madhaifu yenu na mwambizane ukweli kwa upendo na amani,mjenge ndoa yenu, *_Kuzira,kununa,kiburi,ukalip havijengi,na havita wasaidia,baladala yake inaingizwa kwa rekodi ya ndoa za migogoro na kipumbavu_* Rekebisheni mapungufu yenu ninyi ni wanadamu mpo duniani siyo mbinguni. Jenga heshima ya ndoa mlee watoto wenu kwenye maadili mema hawa watoto wasio na hatia.
*_Mwisho ndoa inahitaji akili na uvumilivu kwa mwenzako,mtaishi miaka yote mpaka uzee kwa furaha na upendo_*
     _@By Ev Elisha Kazimoto_
        *0755444078*

No comments:

Post a Comment