Thursday, 1 December 2016

NAMNA YA KULINDA UCHUMBA WAKO

*UKIPATA MCHUMBA JIPANGE VIZURI*
   *_By Ev. Elisha Kazimoto_*
         *0755444078*
*_SIRAHA ZA KULINDA UCHUMBA WAKO._*
🌟Maombi, usiwe mvivu kuombea uchumba wako kila siku, kumfunika mwenzako kwa damu ya Yesu mwenzako, macho yake, hisia zake, na moyo wake, ukuwaze wewe tu. Mlinde dhidi ya mashambulizi, kataa roho za breakup, kuchokana n.k.
🌟Mawasiliano ya karibu. Msiruhusu kuweka interval kubwa ya muda bila kujuliana hali hata kwa sms. Ukisha tangaza kuingia ktk vita ya mahusiano, usikwepe Gharama ya pesa na muda, hiyo ni kwa usalama wa uchumba wenu.
🌟Epuka ku test hisia za wasichana /wavulana wengine mbali na mwenzako, utalowea huko au utajiumiza kisaikolojia. Wapo watu wana wachumba lakini wana wajaribu watu wengine kudate nao, kama kuwatania, hiyo ni sumu kubwa.
🌟Ridhika na chaguo lako, usimlinganishe mwenzako na wasichana /wavulana wengine, may be ulo wahi kudate nao itakusumbua kiakili na kuleta breakup,.
🌟Usithubutu kuzungumzia zungumzia your past partners inamuumiza mwenzako, inaweza tengeneza sumu ya mahusiano yenu.
🌟Kuwa muwazi kwa mwenzako. Mtafika mbali kwa amani.
🌟Usiwaamini marafiki zako hata kama wameokoka ambao hawajaoa au kuolewa, ukawaunganisha unganisha na mchumba wako, watakuliza 😪😪😪, watakuzunguka, mtaachana halafu unasikia kesho wameoana.
🔥🔥🔥🔥mimi 👐🏻🙅🏻kukuunganisha na 👉🏻💁🏼wangu, ujue umepata kibali, mbele za Mungu na mimi na hapo dk za mwisho, sikupi no, hutaongea naye mara kwa mara, KULINDA UCHUMBA WAKO KAZI 👮🏽🔫🔫💣🔪 *_YAJUE MAMBO HAYA KABLA YA KUINGIA KATIKA NDOA._*
Kuna mambo itabidi uyafanyie utafiti na uyajue kabla ya Kuingia katika ndoa.
💥Nikiingia katika ndoa, sitaishi kwa maamuzi yangu binafsi, lazima nijue mwenzangu anasemaje ktk maamuzi yangu. (Hapo jifunze kumshirikisha mchumba wako mambo yako)
💥Ninawajibika baada ya kuoana, kuwajibika kwa familia mbili na si moja tena, bila upendeleo.
💥Itanilazimu kumlinda mwenzangu kihisia, kijamii na kiafya,.
💥Itanilazimu kumpendeza mwenzangu kuliko mtu mwingine yeyote.   *_JIPANGE KUSHUGHU LIKIA VYANZO VYA MIGOGORO KATIKA NDOA._*
🌟Kabla ya Kuingia katika ndoa jipange kisaikolojia kushughulika na vyanzo vya migogoro katika ndoa vifuatavyo.
💢Kuto tambua nafasi yako na ya mwenzako. Ukishindwa kujua kuwa mimi ni baba au mama mwenye nyumba, na kujua huyu ni mke wangu au mme wangu na kumpa nafasi yake na kuiheshimu, fahamu unatengeneza jehanamu yako ya ndoa.
💢Kupendelea upande mmoja wa familia katika kutoa huduma, au kukaribisha wanafamilia. Wekeni mikakati namna ya kuzihudumia familia zenu kama wana ndoa na si kama mtoto wa familia.
💢Kutowekana wazi vipato vyenu, na matumizi yenu. Ukitaka amani itawale ktk ndoa, weka wazi mapato na matumizi yako, ninyi si ni mwili mmoja?
💢Kuto wajibika ktk nafasi yako ktk familia.
💢Kuwapa uhuru mkubwa ndugu na wazazi kuwa waamuzi ktk mambo ya ndoa yenu.
💢Kuto tunza siri za ndoa yenu, kutaipasua ndoa
💢Kuto kuwa na moyo wa kusamehe na kuachilia.
Kubishana na kushindana na mwenzako, Kutopenda kushuka mbele za mwenzako.
💢Kuwa mtu wa kujihesabia haki hata katika makosa, na kuwa mzito wa kuomba msamaha.
💢Kuwa mtu wa kumlaumu mwenzako kila wakati.
💢Kujisahau kuwa umeoa au umeolewa, yaani kuendeleza mfumo wa maisha ya ubachela, kujiachia na watu wa jinsia tofauti yako kupitiliza
🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟
    *_By. Ev. Elisha Kazimoto_*
     *0755444078*

No comments:

Post a Comment