πππ *UNAMPANGO WA KUOANA NA MAREHEMU UNATEGEMEA NINI?*πππ
*Na Ev Elisha Kazimoto*( _Mjumbe Mkali. Mithali 17:11_)
WhatsApp 0755444078
*_Mhubiri 9 : 4 - Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa);_*
_Shalom watu wote mlio makanisani na hasa wale waaminio mwito( *Wokovu*) na tumaini la wito wetu katika Kristo Yesu Bwana wetu. Kuna jambo hili ambalo limekuwa likisumbua vichwa vya vijana wakiume na wakike muda wa *Kuoa na Kuolewa* mpaka kufikia hatua ya kuibadiri kweli ya kristo kuwa uongo( *Warumi 1:25 )ili mradi kutimiza nia zao na tamaa zao za kuingia katika ndoa, jambo hili ni Ushetani wa mtu anayesema ameokoka(sina uhakika)Kuchumbiana na Mpagani(Marehemu anayetembea) na kujipa haki kuwa Mungu atambadirisha tukifika ndani*_ Naomba unitegee sikio uone Misukule ya ndoa iliyo tengenezwa makanisani, na kuwasumbua watumishi wa Mungu makanisani, mitandaoni kushauri watu na kuombea watu wenye misukule ya ndoa,misukule walio itengeneza wao kwa tamaa zao ,na kuziba masikioπππ yao wasisikie kweli,na kuziba machoπππ wasione ukweli wa neno la Mungu.
_Ninaye kuletea uchambuzi huu dawa ππ ya wagonjwa wa mapenzi walio vitandani ni *Ev Elisha Kazimoto* Mchambuzi na Mshauri wa masuala ya Mahusiano na Ndoa_
ππ Kijana wa kiume na wakike,soma mstari huu tena,unaobeba ujumbe huu na uelewe ndo ndoa yako iwe paradiso ndogo.πππ
*_Mhubiri 9 : 4 - Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa);_* vijana wanapoingia moto wa kuoa na kuolewa na kuanza kuona π
kalenda inasoma miaka mingi na bado hajapata mtu wa uhakika wa kuoa au kumuoa,anaamua kubadili kanuni za kibiblia ziende sambamba na hisia zake.( *Anaanza Kumtafuta Aliye Hai katika wafu* π *_Luka 24 : 5 - nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?_* )
ππ Kijana ameokoka,ni mwimbaji,ni mpiga vyombo kanisani, wakati wakuoa na kuolewa, anaangaza macho,( *Anatafuta six packs, mwenye pesa, elimu kubwa,mwenye mshahara mzuri,mwenye usafiri hata kama ni mwanadini tu,mpagani,ili mradi anakidhi baadhi ya vigezo vya kimwili alivyo jiwekea* Sikiliza hajaokoka,ila ili mradi anakidhi baadhi ya vigezo vyake vya kimwili( hujui *Unabeba Simba aliye Kufa,(Mpagani) unaacha Mbwa aliye Hai(mtu aliyeokoka)mwenye tumaini kwa Mungu kuwa muda wowote atabarikiwa na kufanikiwa.
ππ Mtu aliye okoka ni Hai amehuishwa,Anaona,anasikia,anahisi,anaongea,anapenda,anachukia,anapumua,ana akili timamu ya kufanya maamuzi sahihi, ila mtu yeyote ambaye Hajaokoka( *_hajampokea Yesu maishani mwake,na kutembea katika Neno la Kristo huyo ni Marehemu anayetembea_* haijalishi amefanikiwa au ni msomi huyo ni *Marehemu* ukiamua kuoana naye jua umeoana na Marehemu anayetembea.ππ
*_Waefeso 2 : 1 - Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;_*huyo ndo mchumba wako ambaye hajaokoka.
*SIFA NA TABIA ZA MAREHEMU*
_Ukiamua kuchumbiana na mpagani,usiwasumbue watumishi wa Mungu na niombeeni,ninapita katika wakati mgumu, uliyataka mwenyewe kuoana na marehemu mwenye sifa hizi_
π *Marehemu Haoni* marehemu siyo kipofu,ni kwamba hana macho, kwahiyo jua unaoana na mtu asiyeona thamani ya Mungu,moyo wako,lipi baya na lipi zuri(utakapo ona anafanya vitu ambavyo ni kero kwako katika ndoa,usimlaumu *Haoni*chochote,na hatuwezi mwombea kuona huyo si mtu kipofu, ni marehemu asiye na macho.
π *Marehemu Hasikii* vijana wanafunga ndoa na marehemu,muda mfupi miezi kadhaa,mwaka 1,2...ngumi,kesi lawama,hasikii,hasikii,yaani nimesemaa,hasikii anaendelea na tabia yake, hivi tangu lini umewahi ongea na marehemu kabulini au Mochwali ujamwambia sogea hapo tuweke marehemu mwingine akasogea? Unapoteza muda kuongea na Marehemu hasikii leo hata kesho,uliyataka mwenyewe.
π *Marehemu Hajitambui* Vyovyote marehemu anakaa,uchi sawa,mvishe nguo sawa,chima moto sawa, sasa kijana unafanya maamuzi na kuoana na mpagani,jua unaoana na marehemu asoye jitambua, waliookoka kinacho tufanya tujitambue,ni Yesu Kristo chanzo cha Maarifa ( *Mithali 1:7* kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa) na *Maarifa ni uwezo wa kufanya jambo sahihi,muda sahihi ,mahali sahihi kwa kusudi sahihi* nikuulize anaye chepuka anamaarifa,anayetelekeza familia ana maarifa,anaye mpiga myoshe mme wake ana maarifa.?Anaye kuomba sex hamjafunga ndoa nawe ukampa ninyi mna maarifa.?πππ
*_Mithali 6 : 32 - Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake._*
πππNdo maana nikasema umeoana na Marehemu asiye jitambua(hana akili kabisa) kwa hiyo usimlaumu. *_Marehemu hakukutafuta wewe,ila wewe ndo umemtafuta, wewe uliona ni marehemu ukaenda kwake,yeye hajitambui kama ni marehemu,_* jiulize watu wakikuta mtu nafanya sex na marehemu,analaumiwa nani na kutukanwa nani?marehemu au mwenye uhai? Ukioana na mpagani mpagani halaumiwi,wala hapati laana kutoka kwa Mungu wewe uliye hai ndo moto utakuwakia.
π *Marehemu ana nuka* Ndoa yako inanuka siyo inanukia,na ndoa yako itanuka siyo kunukia kwasababu umeoana na marehemu,utaoana na marehemu. Hiyo ni sifa ya marehemu, saizi Hanuki ndo maana upo karivu naye,uba mahaba naye,akianza kutoa harufu utarudi kwenu au utamfukuza. *_Wengi walioana na marehemu kabla hawajaanza kutoa harufu,wachungaji wakaonya wee,mitandaoni tukafundisha wee masomo yote muhimu,ila mtu kang'ang'ana na kuoana na marehemu kisa hanuki,walipooana marehemu kaanza kutoa harufu,ndo _Mlokole Msukule anaanza kusema,"huyu hakuwa chaguo la Mungu,hayakuwa mapenzi ya Mungu,kwanza hatukufungia ndoa kanisani"_* wee ni Msukule wa kiroho, ukifanya maamuzi ukijua,umeambiwa ila umelazimisha,sasa usitegemee kutoka kwenye ndoa hiyo upate mtu sahihi tena,utapata msukule mwingine wa kiroho.
ππHivi hii sela ya *_Nimeona kijana/binti anasifa zote za kuwa mke/mme wangu ila hajaokoka mliipata kitabu gani cha Biblia,......... ?_* hivi sifa zote unazijua ndo hayoo nimeona mtu kabisa amekamilika na viungo vyote *Ila Ni Marehemu Amekufa* hivi unaakili? Huyo aliye kufa hata kama ana viungo vyote atatufaa nini? Ndo maana *Leo vijana ndoa zenu za ovyo, haziwafai,na hazilifai kanisa,wala haziifai familia yenu* mmebeba marehemu hana faida popote.
ππ Shida vijana mnabeba marehemu kwakuwa mnajitafutia wake na waume kwa tamaa zenu siyo Mungu anakupa. _Ona Adamu anamwita mke wake alopewa na Mungu,anamwita HAWA,maana yake mama wa walio hai wote.πππππ
*_Mwanzo 3 : 20 - Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai._*
ππwee mke wako ni mama wa wawatu gani, Mmeo ni baba wa watu gani, unaweza ukawa Hawa ila una baba wa marehemu ( hii inamaana uzao wenu,sizungumzii watoto tu mfumo wote wa maisha ni mfu)una mama/baba wa waliokufa. Chochote kitokanacho na nyinyi kimekufa.
*Mimi Mtumishi wa Mungu na Mchambuzi wa Masuala ya ndoa na Mahusiano Ev Elisha Kazimoto, kupitia uchambuzi huu na kushauri kijana Oa/Olewa na Mtu aliyesimama Kweli kweli Kwa Yesu*
_Sababu kubwa ni kwa sababu aliyeokoka ni Hai,hata akijikwaa,akiumia,akiugua kiroho,kisaikolojia anauwezo wakutibiwa siyo kama marehemu.πππ
*_Mhubiri 9 : 5 - kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa._*
ππAliyeokoka ana moyo wa kujishtukia akifanya ndivyo sivyo kwake,asiye okoka hajishtukii. Kwanza aliyeokoka anagopa kufa( kutengana na Mungu )anaweza badirishwa na neno la Mungu kanisani,sasa marehemu unambadirisha na nini. *Eti atabadirikia ndani tukioana nitamuhimiza mambo ya Mungu* πππ lakini wewee waulize wachawi Maiti akisha zikwa kaburini wakifukua wanakuta marehemu anapumua. Au ndo nakuoza kunaanza.
ππUkioana na aliyeokoka (aliye hai)unakuwa na tumaini la kuibadirisha ndoa muda wowote kwa namna yoyote kupitia maombi.(ujiwa na aliye hai hata kama ni mgonjwa una matumaini ya kupona)siyo marehemu.
*_Mhubiri 9 : 4 - Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa);_*
_Endelea kutafuta simba waliokufa huko nje upaganini kisa alikuwa boyfriend /girlfriend wako chuoni,amekusaidia sana chuoni,amekutafutia kazi,amesema ukimkubali ataokoka, tafuta na ubebe huyo simba mfu,unaacha mbwa walio hai,wanao bweka,unawadharau kisa hawana manyoya na meno marefu, wezi watakuja nyumbani kwako hakuna mbwa wa kubweka kwa Bwana awaamshe majirani waje kukusaidia dhidi ya wezi,unalisimba marehemu ukishaibiwa Akili zitakurudia,ndo utatafuta mbwa woote,watakuwa wameisha chukuliwa,utalia na simba wako mfu daima.._
Mwenye sikio na asikie neno Roho aliambia kanisa la vijana.
*_Imeandaliwa na Mchambuzi na Mshauri wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto (Baba Eve)_*
Fb Elisha Kazimoto
WhatsApp 0755444078
Call: 0657557570
*Muhubiri wa Injili isiyo Chakachuliwa*
No comments:
Post a Comment