Tuesday, 12 September 2017

TATIZO LA KITANDANI

*Swali: Utafanyaje ikitokea umefunga ndoa na kijana unaingia ndani siku ya kwanza,anashindwa kufanya kazi,wiki,mwezi...mnara hausomi.?*
_Anajibu Ev Elisha Kazimoto_
WhatsApp 0755444078
*_Kwanza kabisa,wapendwa suala la ndoa ni suala tata sana na jepesi sana,na ni la kiroho 50% na la kimwili 50%,kwasababu hiyo umakini u ahitajika sana_*
👉Nianze kwa kuwashauri vijana na kuwaondolea wasiwasi, Ndoa inahitaji uiendee ukiwa vizuri mbele za Mungu,uwe na uwezo wa kiroho wa kuweza kushughulika na changamoto mbakimbali kiroho na kimwili,.
👉Ukiiwndea ndoa ukiwa vizuri na Mungu atakupa mtu wa kufanana na wewe,atakuepushia balaa zingine kama hizo( _Lakini kama zitaruhusiwa na Mungu,ujue Mungu ameona uwezo wako wa kiroho unaliweza kulibeba,na litakuwa na jibu,maana biblia inasema Mungu hakupi jaribu zaidi yaimani yako_) kwa hiyo ukiwa na Mungu vzr utavuka kwa namna atakavyo kupa njia ya kutokea,jaribu halikai daima, adhabu ndo inakaa daima,na jaribu haliumizi na kujuondoa mstarini,ila linakuimarisha na kukupa hatua.
👉 Pia vijana ambao hamja oa,kuweni na maarifa ya kuombea ndo yako ijayo,ombea kila kitu acha kuwa na aibu mbele za Mungu, mfn. *_Ukiwauliza wachumba mlo humu,na wana ndoa,nani alikuwa akiomba Mungu ampe mme au mke wa kumtosheleza katika tendo la ndoa,ampe mtu wa size yake kimaumbile?_* utakuta katika 100 ni 5 tu au 2.tunakosa maarifa wakati mwingine, Ndoa ni taasisi inayo windwa mno,unaweza andaliwa stress kubwa na shetani ili uiache imani. Haya mambo yashugulikie mapema kuwa wazi kwa baba,au *Unatatizo mwambie Mungu ili tatizo mbona litamnyima furaha mwenzangu?* shugulikia
*Usipo kaa na Mungu vizuri na Mungu,ndo utajichanganya kufanya sex kabla ya ndoa ili kujua uzima wa mwenzako, ndugu yangu huja win ila ume fail, vp ukishaoana ukakatika kiuno? Au ukapoteza viungo muhimu vya kukusaidia kufanya sex kwa uhuru?utakaa kwenye ndoa au utatoka?* silaha kubwa kwako kijana si kuogoa changamoto bali kujiweka vzr na Mungu atakupa mtu sahihi na aliye vizuri.
👉Jambo lingine, *_watumishi wa Mungu tumezidi kuongea na vijana,wawe wawazi,kusema kama yuko fit au anamapungufu, lakini pia waaimamizi wa ndia ni watu wakaribu kwa hawa wana ndoa watarajiwa, wa kiume kwa wakiume,wakike kwa wakike,kuulizana ata kutazama kama minara inasoma. Huku wachungaji nikumwapisha kijana,hata kabla ya kufunga ndoa,tuhakikishie uimara wako,hatuitaji kesi baada ya ndoa_* nyakati hizi haya yanafanyika.
👉 Lakini kuna suala la kushambuliwa ki nguvu za giza,unaweza kuwa fit,kijana au binti,ila unaingia ndani tu, kijana unaona laini haisomi,wiki,mwezi nk,au mdada ile kubisha hodi mlangoni wala hata kuweka mguu ndani,binti kilio machozi kama maji,maumivu makali, utafanyaje ?ndo maana yangu ya kuwa na mngu vizuri. *Ntawaletea somo la maandalizi ya kiroho ya kuingia katika ndoa* kuna kina ameo rafiki yangu mwaka jana yuko fiti,ila kwenye harusi walichezewa game na wachawi,mambo ya zawadi mtu alimpa pipi akala wakati wa kutoa zawadi,na sabuni, kufika ndani walionja tu,network zika kata miezi karibu3,walipanda mlimani,network zikarudi, mwezi ulo pita wamepata mtoto. Sasa si kila network kukata ni ugonjwa kwamba kijana hakusema,kuna *Kushambuliwa*
👉Jambo lingine,watu mkiwa katika uchumba,nimambo ya kawaida, kumuuliza kitekiniki mfano, *_Ana ugonjwa gani,tatizo linalo msumbua, nk_,amezaa watoto,kuna ex wake anaye msumbua,* na wakati wa kuwa wazi ili kuepusha migogo ya ndoa baadaye.
*Kama mmepitia hatua zote tangu mwanzo,na mmewashirikisha watumishi wa Mungu (walezi)wenu tangu mnaanza mtaepusha mengi,wanajua mengi, shida ya vijana wanachumbiana kimya kimya wanawashirikisha watumishi yote walisha maliza,sasa ukiambiwa *huyo kijana ni Toashi mnara hausomi,utakubali,?au utaona wanakuonea wivu, au huyu binti ametoa mimba nyingi na kizazi hana,utaamini, au huyu kwao wachawi naye dada ni mpaaji balaa,utamuacha na mmeisha fika mbali?* shirikisha watumishi mpunguze matatizo.
👉Kama limekukuta kama huyo honeymoon *_Usipaniki,tulia,ongea na mwenzako kwa upendo na utaratibu,ujue ni tatizo la kuzaliwa,ukubwani,ndo wa kuathirika na kunichua,au ndo ameshambuliwa, kama lipo nje ya uwezo wenu,waone watumishi wawashauri,wawaombee,kama ni hospital mpate matibabu, maadamu mmependana,mmekubaliana kuoana,na kuapa kuishi wotw milele Mungu atatoa njia_*
NB: kwa watumishi wengine kama kijana ni Toashi,yaani hafanyi kazi,wanaifungua ndoa,maana ndoa inakamilika kwa tendo la ndoa.
*Ev Elisha Kazimoto*
0755444078

No comments:

Post a Comment