✅ *NITAZIMA SHANGWE ZA ADUI ZANGU GHAFLA*✅
*_Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
_Shalom watu wa vita. Usiku huu wa mkesha ni usiku wa Operation ya Kuzima shangwe ya adui zangu ghafla_
*WAAMUZI 16:23-30*
23 Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.
24 Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.
25 Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.
26 Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea.
27 Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.
28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
29 Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto.
30 Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake.
👉👆Kupitia mistari hiyo,Roho wa Bwana akufundishe kitu tunapoenda kuanza maombi ya kuzima Shangwe ya hao maadui wanao shangilia shida yako.
👉Samsoni alilibeba kusudi la Mungu,na alitumika kwa nguvu zake zote kuhakikisha Mungu anainuliwa daima( _Hii ndiyo kazi tunayo fanyasiku zote,na kama unahitaji ushindi siku ya jaribu lako tumika kwa Mungu kwa nguvu zako zote_)
👉👆Utumishi wa Samsoni ulileta hasara kubwa kwa maadui wa taifa la Mungu (wafilisti),walimsagia meno,walimuwinda kumuua( _Ndicho kinacho endelea kwako na kwangu,tunapo omba,fanya kazi ya Mungu kwa nguvu,ni hasara kwa shetani,wachawi nk, wanaanza kutuwinda watuue_)
👉👆Samsoni alipita katika *kipindi cha kutoona, kutokuwa na tumaini,nywele hana,macho hana,na yupo katika kambi la adui zake* ( _Hiki ni kipindi cha wengi wanakipitia,adui amekushambulia,huoni njia,jaribu kali wala hujui na huoni pa kupenyea,lakini watu wanakudhihaki kwa jaribu lako,tatizo lako_)
👉👆Wafilisti walishangilia,walisifu miungu yao na mungu wao Dagoni wakisema mungu wao amemtia Samsoni adui yao mikoni mwao( _Unapo pita katika jaribu na wakati mambo yako magumu,ndoa ina shida,uchumi umeyumba,umri unaenda hujaoa au kuolewa,bado Uzao huna katika ndoa miaka inasonga,wapo wanao dhihaki,wanashangilia,wanadhani dawa zao,kafara zao,mganga wao amekushugulikia, *Hilo lisikuvunje moyo* hicho ni kipindi tu cha Nywele za Samsoni hazijaota_)
👉👆Nywele zako zokiwa bado fupi hazijaota,utatukanwa matusi yote,kila mmoja atakudharau,isikupe shida *Nywele zako zina rudi,utumishi wako mbele za Mungu hazijasahaulika,utazizima shangwe zao Ghafla*
👉👆Shangwe zilipo zidi za maadui wa Samsoni (wafilisti) waliitisha sherehe ili wamlete samsoni hadharani awachezee wafurahi(yaani wafurahie tatizo lake la kutokuwa na macho) ( _Siku zote adui zako huwa hawajui kipindi chao kupigwa na kuziba vinywa vyao,ili wewe utoke katika jaribu_) hawa wafilisti walimuita Samsoni wakasahau nywele zake zimeota tena( wakati wako unakuja,furaha yako inarudi tena)
👉👆Samsoni aliletwa haoni,ila kuna kijana alimshika mkono kumsaidia kwenda mwisho wa jaribu lake( _Nawe Mungu akuinulie mtu wa kukushika mkono akusaidie katika jaribu lako unapoelekea mwisho wake_)
👉👆Samsoni alipofika ukumbini maadui zake walishangilia kweli,shangwe ya dhiaka,ilimuuma sana(kama unavyoumia wewe unavyosimangwa), ila Samsoni akamwambia kijana yule aliye mleta *_Niache niziegemee nguzo hizi mbili ambazo jengo hili lote linazikalia_* (uuuuuuuh saa ya kichapo imefikaaa, shangwe yao inakwenda kuzima ghafla wao bila habari)
👉👆 *_Usiku wa leo tafuta nguzo mbili za jaribu lako,tatizo lako,maadui zako,twende kuzima shangwe ya wahuni waliotudhihaki muda mrefu_*
👉👆 Katika nguzo Samsoni aliomba maombi makali akiwa amezishikilia nguzo( *_Nawe sasa ukiwa umeshikilia nguzo za tatizo lako,za maadui omba maombi makali, mwambie Bwana nikumbuke leo nipate kuzizima shangwe za maadui zangu_*
👉👆 Kwa nguvu zote samsoni akazivuta nguzo,nyunva ikaanguka,na kuua watu wengi mno kuliko aliowaua kipindi cha uhai wake( _Maombi yetu leo tunavuta nguzo hizo za utasa,umaskini,magonjwa,kukataliwa na yote yanayo kusibu_) sikiliza, mwisho wa jaribu lako ni mkuu sana utukufu wake kuliko ulivyokuwa wakati unaanza tatizo.
_Sasa anza maombi ya kuita kwa nguvu, Ee Mungu unikumbuke sasa jengo hili la maadui liangushwe na shangwe zao zizimike_ Anza maombi.
*By Ev Elisha Kazimoto*
No comments:
Post a Comment