*_Tunafunga mada hii kwa namna hii_*
_Ifike hatua,vijana wa kike na wakiume,mjue jambo moja kuwa, ndoa siyo biashara,kwamba nisipo pata wateja soko hili napeleka pengine na nikipata hasara ntafanya biashara nyingine. Ndoa ni maisha,unapo amua kuoa au kuolewa,unatengeneza mkataba wa maisha ya Amani,au wa majuto mpaka kaburini(kwa ndoa za wana wa Mungu )hivyo usifanye mambo ya RISK(kujihatarisha)ndo maana vijana wengi wanasema siku hizi hakuna waoaji,na wakaka wanasema hakuna wanawake waolewaji,ndoa hazidumu ila migogoro ni mingi, shida vijana MNA RAHISISHA SANA NDOA kama kumtuma mtoto kwa MANGI DUKANI ANUNUE CHUMVI, ndoa inahitaji;_
👉 *Maandalizi ya kisaikolojia ,kimwili na kiroho*
👉 *Ndoa inahitaji Uhakika wa kujiridhisha kuwa chaguo hili litanifaa kiroho,kimwili*
👉 Ndoa ahitaji kudhania(to predict) mbeleya safari atabadirika
👉 *Ndoa inahitaji uingie na mtu unaye mfahamu vizuri,ndo maana inashauriwa,usimtamkie mtu kumuoa/kukubali akuoe bila kumfahamu kwa kina*
_Sasa jambo la hatari na kushangaza,unaanzishaje mahusiano online mtu humjui(hamjawahi kumeet face to face),huu si niuongo wa Phd,ukiulizwa,umenipendea nini,unajibu( utasema sura?),anavyo type haraka? Voice note zake au,tabia?umeiona wapi........ Kwa namna hii wengi wameoa majini_
*Unaachiaje moyo kwa mtu,moyo wa upendo wa ndoa kwa mtu usiye jua kwao,hujui ndugu zake,wazazi,historia yake na familia, ndo maana wengi wanapigwa mimba na kuachwa,wengine wanaolewa kwa wachawi balaa,watoto wako wote wanaliwa wakiwa wadogo*
Vijana msiseme siku hizi ndoa mbovu,sema ninyi ndo wabovu,mke/mme unempataje?yaani *_Eti unavyoona watu wanachangia humu,fasta unafata mtu inbox,nimekupenda tuanze mahusiano yakuelekea ndoa, wee Jambazi mkubwa,unependa au umetamani na hujui unalofanya,_*
Ndiyo maana wachumba wote mnaowapata mitandaoni wanawapiga kibuti humo humo mitandaoni.
*KAA ULIMPENDA MTU ONLINE SASA AMANI INATOWEKA JUU YAKE,UNATAKA NINI,URUDISHIWE AMANI FEKI YA KISHETANI ILI UFE? HUTAKI MUNGU AKUSAIDIE KUKUEPUSHA MABAYA?*
Ev Elisha-Counselor
Monday, 11 September 2017
MAHUSIANO MTANDAONI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment