*Swali:Hivi inakuwaje kijana anakuja kukuchumbia,hajishughulishi na chochote,kwa kifupi mvivu,anaanzisha mahusiano na wewe ila anamtegemea binti amtunze mwanzo mwisho, hapa kweli kuna uwezekano wa kuwepo ndoa?*
Majibu na Ev Elisha Kazimoto.
WhatsApp 0755444078.
Katika swali hili,kuna mambo ya msingi yakuyaangalia,:
*_Ndoa haijengwi kwenye vitu,ila kwenye upendo wa dhati ulogundua kitu cha ziada kwa mwenzako,chenye faida kwenye maisha yako, na hicho huwa kinawafanya watu wenye vision kukubali kumuoa huyo mtu,au kuolewa na huyo mtu_* kijana kuwa na pesa na kutokuwa na pesa,hakipimi uwezo wa kuwa na wewe. Anaweza kuwa hana kitu muda huo,ila mbele ya safari atakuwa navyo,au wewe ndo uliye lango la yeye kufikia ndoto zake.
2.Pili Tunapo anzisha mahusiano(au kabla ya kuanzisha mahusiano)au kusema yes tuanze safari lazima ujue *_mahusiano ni gharama, gharama ya pesa,muda,gharama ya kuumizwa,gharama ya kusamehe,na gharama ya kuonyesha mwelekeo wa maisha_* kijama wa kiume kama huna uwezo wa kujua gharama hizi lazima nizibebe,au kama unazikwepa,hupaswi kuoa,na unastahili kuachwa.
NB: *_Kwenye kitafuta na kuelekea ndoa,tunaishi kwa vision na plans, kwenye ndoa tunaishi kwa Imani na Uvumilivu, sasa usilete tabia za ndoa imani na uvumilivu kwenye mahusiano,tafsiri yake ni wewe hujielewi,na huna uwezo wa kuishi na mtu._*
Fanya kazi,pambana kwa namna yoyote uonyeshe vision na plan kwa unaye taka kumuoa,usimfanye kuvumilia na kuwa na imani kabla ya muda.
*MWISHO WA MADA*
No comments:
Post a Comment