Thursday, 14 September 2017

WALOKOLE NA WAPAGANI

*SWALI KUHUSU WALOKOLE NA MAHUSIANO NA WATU WA MATAIFA*
      _______
Ninaswali kiongozi.
Linanitatiza sana napenda nijibiwe kwa fikra zaidi moja.

1) _Hivi kwanini walokole wengi huwa hawana upendo na watu wasio walokole.. Yaani hujitenga sana kiasi cha kuweka mipaka._

2.) _Nimeliona hili nilipokuwa sekondari mpaka chuoni.Hasa wale wa makanisa wanaoita ya kiroho_

3.) _Lakini matendo yao wengi ni Wachoyo Wasengenyaji,Wachochezi,Viburi_

4.) _Na hawana uhusiano mzuri na watu anaolala nao kwa kujiona wao ni watakatifu sana hawatakiwi kuwa karibu na mataifa hata kwa jambo la jumuia kama kusoma na michezo (mpira wa miguu na pete)_

5.) *Naomba unisaidie.*
_Chanzo ni nini..Nini kifanyike kuwasaidia walokole wa namna hii maana kila taasisi wapo tena wengi tu._


*Mchambuzi wa Swali hili ni Ev Elisha  Kazimoto*
WhatsApp 0755444078.
_Ndugu na rafiki yangu uliye uliza swali,swali lako ni moja,ila *nimelitenga katika vipengele 5 ili Nikupe ufafanuzi kwa kuzingatia vipengele hivyo* naamini kufikia mwisho utajua Walokole ni watu gani na kwa nini wanaishi maisha hayo unayoyaona na kuyatafsiri hivyo ulivyo uliza swali lako_
👉Swali lako majibu yake yapo kimaandiko zaidi kuliko kifikira,na kwakuwa umeuliza vizuri kuwa *_.....Hasa walokole wa Makanisa ya Kiroho....._* tayari tunatafuta Itikadi yao,katiba yao inawaelekeza vipi ndipo tujue namna ya kuelezea tabia zao. ( _Kwanza tuanze na Ufunguo wa Kwanza wa Msitari wa biblia unaotuonyesha Chanzo cha watu 2 kutofautiana tabia na matendo_)👇👇👇👇
*Amosi 3 : 3 - Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?*
👉Hapa Biblia inaongelea watu wawili walio eneo moja(Duniani) ila wanasafiri kwenda maeneo 2 tofauti( Mbinguni na Jehanamu) _Safari ya watu hawa,ina mahitaji mawili tofauti,kila njia ina kanuni zake,mizigo yake ya kusafiri nayo,maadili yake, kila mmoja anaenda kulingana na kanuni za aendapo, ndo akasema *hawa watu, hawawezi kwenda pamoja sambamba,kushikamana,mpaka kwanza wapatane, aidha wakubaliane njia moja iwekwe pembeni,watumie njia moja, yaani mmoja wapo,aamue kuachana na njia yake,afuatane na mwenzake,hapo watatembea pamoja,wata panga moja,watashirikiana katika kila jambo maana wamepatana kutembea njia moja*_ 👉Sasa Watu waliookoka,(walokole) huonekana tofauti na wapagani kutokana na kutofautiana *katika kile wanacho kiamini,maadili ya safari yao, tumainilao* aliyeokoka Anaambiwa,na anaamini Kuishi maisha matakatifu hapa duniani,ambaye hajaokoka,au mwana dini anasema huwezi kuishi maisha matakatifu hapa duniani, tunaokoka baada ya kufa. (Kwa hilo tu,watatofautiana mahitaji ya kuishi,kukaa,kufanya mambo yao) anaye amini katika utakatifu *Atajilinda na mambo mengi,* asiye amini katika utakatifu,hana kizuizi,atafanya lolote,na kuishi vyoyote.👇👇👇👇👇
*_Waebrania 12 : 14 - Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;_*
👆👆👆👆Aliyeokoka ameambiwa atafute utakatifu,maana hakuna mtu atakaye mwona Mungu asipokuwa nao. Ambaye hajaokoka hana sharti hilo.
*_1 Petro 1:15 - 16 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 16. Kwakuwa imeandikwa mtakuwa watakatifu,kama mimi ni mtakatifu_*
👆👆👆hii ndo sababu ya walokole kuwa makini na nazingira yanayoweza kuwaondolea sifa ya utakatifu.
*Sasa nianze namba moja hadi nyingine katika swali lako moja la msingi, kwa nini walokole wanaonekana hawana upendo lwa mataifa*
_Kwanza hapa niweke sawa,tunatofautiana katika kutafsiri neno upendo, kunaanaye tafsiri upendo,mwingine Anaamini upendo ni mtu kuambatana na mimi katika kila jambo nitakalo mwambia,liwe zuri au baya akikubaliana nami huyo anamipenda(huu ni mtazamo wa mtu asiye sahihi)_👇👇👇
*_Waamuzi 16 : 15 - Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi._*
👆👆👆kama wewe ni Mkristo utaijua habari hii ya Samsoni na Delila, Delila aliutafsiri upendo ni Samsoni amwambie siri ya nguvu zale,lakini lengo la Delila lilikuwa kumuuza Samsoni kwa adui zake.
👉Upendo wa kuuana,kupotezeana mwelekeo wa tumaini langu siyo upendo,ila ni Sumu iliyopakwa asali. ( _Upendo wa walokole ni mwingi sana kwa watu ambao hawajaokoka,maana hufunga na kuomba kuwaombea wale wenye shida,wasiomjua Mungu watoke mikononi mwa shetani,hulipa gharama ya kiuchumi,kuandaa mikutano,safari kwenda kuwahubiria neno la Mungu,kuombea watu wenye vifungo vijakali mpaka wafunguliwe wawe huru, huu ni upendo mkubwa,ambao mpagani hawezi kufanya,gharama kuilipa,ya kufunga siku 3,7,10,14 huli chakula,hunywi maji,na unatoa pesa laki 1,5,mil 1,2 ili muite muhubiri awaletee sulihisho hawa wapagani wanao teswa na mapepo na wachawi, huu ndo upendo mkuu_  upendo wa kwenda kilabuni kupiga bia,kufanya zinaa,na vijiwe vya story za kihuni,huo siyo upendo sahihi.
*Kwa nini walokole kujitenga na wamataifa?*
👉Tumeishaanza kuona majibu,wanajitenga kwakuwa hawafanani matarakio yao na matendo yao,kipa mmoja anajiadhari mwenzake asimuondoe katika lengo lake. Mbali na hiyo Neno la Mungu limeonya mahusiano yasiyo zaa jambo jema kati ya walokole na wapagani yasowepo.
*2Wakorintho 6:15-17*
14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 

15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 

16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 

17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. 

18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,
*_Msitari wa15,na 17 ina majibuya wazi,ni katika kulinda kitu kinachoitwa Utakatifu_*  Kujitenga huku si kama wanavyokusema wale wasiookoka, kujitenga huku kunalenga kutoambatana katika mambo yawezayo kuchafua vazi lako la wokovu la usafi( ila mtu akianza harakati hizo,uhesabika kuwa anajitenga kwa mambo yoote)
_Aliye okoka hapaswi kuafuatisha kila kitu wanachokifanya wapagani,maana lengo letu siyo moja_👇👇👇👇
*Warumi 12 : 2 - Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.*
👉Pointi ya tatu ya walokole wengi wachoyo,waongo,wenye viburi nk.... Hii inategemea aliyeona haya matabia ni wa mlengo gani,anatasiri wokovu katika sura ipi,aliomba nini mpaka akaona ni wachoyo,alisikia wanasema nini mpaka akasema niwasengenyaji( huwenda walikuwa wakisema tabia zake mbaya,zinawaumiza,waongea ili wamwonbee atoke huko, nk) mfno, vijana wengi wakiume wasiookoka huwasema vibaya wasicgana wakilokole kwamba wana viburi,wanajiona,wachoyo, kisa alimtongoza akakataa,alimshiti,alimpa kauli ya usirudi tena. _lakini biblia inasemaje kwa mtazamo wa watu wa mataifa kwa walokole? Huyu ni Yesu mwenyewe anasema haya maneno_👇👇👇
*_Yohana 15 : 19 - Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia._*
👆👆Sasa siku zote mtu anaye kuchukia hata ungetenda jema analiona baya,hatakusena vizuri kwa lolote. Ila mzizi wachuki umetokana na kutofautiana na njia.
*_Pointi ya nne ya wao kutokuwa na mahusiano na watu wanao lala nao au kaa nao_* Hii inarudi katika tafsiri ya mwanzo ya watu wenye mahusiano mazuri lazima wawe na lengo moja,wanafanya mambo yanayo fanana, mfano chuoni, *_Mpo hostel  wanafunzi wa4, mmoja ameokoja watatu hawajaokoka, au vice versa, huyu anakuja na demu wake,au boyfriend wake kufanya uchafu humo,huyu hana hayo mambo,au hawa wanakuja na bia huyu hanywi,twende disco hutu hawezi kwenda njia yake na katiba yake hairuhusu, automatically watamwona hafai,anajitenga anajifanya mtakatifu,siyo anajifanya ndivyo ilivyo ni mtakatifu,hapaswi kushiriki matendo ya giza_*
👉Kwa lugha fupi ni kwamba wanatimiza kilichoandikwa na kusemwa na Mungu kupitia neno lake.
*_Waefeso 5 : 11 - Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;_*
👆Ukiyakemea matendo yao hayo,ya ulevi,ngono,ukahaba,disco,nk ndo utaonekana wewe unajifanya mtakatifu sana,na ndipo utaanza kuambiwa wewe nawe unadhambi,unakufuru kujiita mtakatifu. Hii kwa walokole si jambo la kushangaza *Hata Yesu mwenyewe walimsema hivyo,aliposema mimi ni mwana wa mungu* kwa hiyo ni mwendelezo wa kile kilichoanzishwa na mwasisi wa imani ya Kikristo.👇👇👇
*Mathayo 26:59-67*
59 Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua; 

60 wasiuone wangawa walitokea mashahidi wa uongo wengi. 

61 Hata baadaye wawili wakatokea, wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na kulijenga kwa siku tatu. 

62 Kisha Kuhani Mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini? 

63 Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu. 

64 Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni. 

65 Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake; 

66 mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema, Imempasa kuuawa. 

67 Ndipo wakamtemea mate ya uso, wakampiga makonde; wengine wakampiga makofi, 
Pointi ya 5, Nini kifanyike kuwasaidia watu wa aina hiyo, ni hii.... *_Jambo la ili usione tatizo lao KUOKOKA kuamua kuambatana nao hilo ndo jibu la msingi,utakuja kuona mpo kitu kimoja,mnashirikiana,mnapendana na hautaona utofauti ulokuwa ukiuona kwanza. Ukiokoka unakuja kwe ye familia ya Mungu,kwa hiyo mnakuwa na upendo wa kindugu_* kama watoto wa familia moja ya Kimungu.
*Yohana 1:12*
_Bali wote wakiompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu ndoyo wale waliaminio jina lake_
*NDUGU MPENDWA KARIBU KWA YESU*
_Imeandaliwa na Ev Elisha Kazimoto_
WhatsApp 0755444078

No comments:

Post a Comment