*UCHUMBA NA MUDA WAKE KISAIKOLOJIA NA KIROHO*
_Ev Elisha Kazimoto_
WhatsApp 0755444078
_Shalom vijana wote mnao taka kuingia katika mahusiano na mlio kwenye mahusiano, karibu tuchambue Uchumba na makando kando yake kisaikolojia na kiroho_
👉 Kuna mkanganyiko kati ya uchumba na urafiki(mahusiano) kwanza nivitofautishe hivi vitu viwili ili tujue muda unao faa wa uchumba,na muda wa kutambulishana kwa wazazi na marafiki nk.
1⃣ *Mahusiano ya kirafiki* ni mahusiano yaliyojengeka baina ya watu wawili,yenye msingi wa *_Mrandano,kupatana,na kuona umuhimu wa Huyo mtu katika kufikia malengo flani_* mahusiano ya kirafiki ndani yake hayana kauli ya agano la kuoana,na mara nyingi urafiki auna siku maalumu ya kuunda,ila unatokea Autonatic kutokana na kuona vitu flani muhimu juu ya mtu mwingine vinavyo kufaa wewe,ndipo ukaribu uanza kujengeka na kugubdua mnaelewana sana.
👉Urafiki hauna mtu mmoja,unaweza kuwa na marafiki hata zaidi ya 10,20 ila marafiki hutofautiana ukaribu kulingana na vitu kila mmoja alivyo navyo vinavyo kuvutia.
👉Katika urafiki wa kijana na binti hauna habari za ndani za kiba,wala hakuna makubaliano yoyote(wala hakuna zuio la huyo rafiki,kumnyima uhuru wa kuwa na maamuzi mbadala ya kuwa na marafiki wengine wengi)
👉Lakini katika urafiki haishauriki ufunue siri zako zote kwa hao/huyo rafiki maana hauna afano naye, na pamoja na kuwa naurafiki wa kina kuna mipaka mikubwa ya kufanya vitu(sex no,mazawadi ukiyatoa hakuna ujira wake,wala tegemeo maana hakuna agano)
👉 *Uchumba* Ni hatua nyingine kubwa inayo husisha maamuzi ya watu wawili,wanaoona waweza kuishi pamoja kama mke na mme,walio tayari kupeleka taarifa zilizo rasmi kwa watu wanaohusika katika pande zote mbili,ili kurasmisha nia yenu ya kuoana,hatua hizi zifuatazo zikifanyika ndo watu uitwa Wachumba:-
1⃣ Wawili walopendana kukubaliana kuwa twaweza kuoana.
2⃣Walezi wa kiroho wenu kupewa taarifa(hapa ziko aina 2 za taarifa,moja _Kuna taarifa ya kuna mtu nimemuoana anahitaji kunichumbia/kumchumbia vipi maisha yake ya kiroho na ya kimwili kwa ujumla_) sasa mlezi wa kiroho atakacho kwambia ndo kina kupa kuendelea mbele au kusitisha safari. Taarifa ya pili ni, _Baba nina mtu niliyempata tayari,tumeongea,tumekubaliana kuoana,sasa tunalileta mbele yako ili liwe rasmi na taratibu zote zianze za kuelekea ndoa_
3⃣ Kupeleka barua ya posa kwa wazazi wa binti,ukikubaliwa mnaendelea mbele. Ikigoma basi hekima zingne utafutwa.
4⃣Kupima afya zenu kama mna maambukizi au la, kama kuna maambukizi,safari imeishia hapo,au mpaka kwa maridhiano mengine.
5⃣Taratibu za kutambukishana kifamilia hufuata.
_Baada ya hatua hizo muhimu ndipo wengibe hupeleka mahari ya kwanza,ili wazazi waruhusu hatua ya kuvikana pete💍💍 ndipo sasa Hasa watu uitwa wachumba,na kanisani utangaza Rasmi flani na flani ni Wachumba_ *Na hiyi ndo hatua rasmi ya hatua watu kuitwa Wachumba* kabla ya hapo ninyi ni *_Marafiki tu kwa lolote la kutokea,break up,kutapeliwa pesa,mali nk usimlaumu mtu yeyote ukubali kuumia peke yako_*
👉Sasa suala la *Kutambulishana kwa marafiki na ndugu* nimerleza hapo juu hatua hizo zikifuatwa automatic kuna watu watakuwa wamejua kulingana na hatua mnazoingia na ukaribu na umuhimu wa watu kwenu. Ila kwa marafiki wengine mnajitambulisja kulingana na umuhimu wa rafiki yako kwako.
*Ushauri wa kisaikolojia na kiroho,usifanye biashara ya kutambulisha mahusiano yako kwa kila mtu,maana kuna Athari kuu 2,ya kiroho na kisaikolojia :*
1⃣ Kisaikolojia, kwakadiri watu wanavyoongezeka wanaojua mahusiano yako,utapata changamoto ya mahusiano yako kuchambuliwa,kuibuliwa madhaifu ya mwenzako,kuzushiwa mambo mabaya,jambo ambalo linaweza athiri mahusiano yenu,upendo,kuaminiana nk.hata kurumbana kwasababu ya maneno ya watu
2⃣ Kwa kadiri mnavyo ongeza idadi ya watu kufahamu mahusiano yenu,ndivyo *Mnavyoongeza uwanja wa mashambulizi ya kiroho juu ya safari yenu ya ndoa* hivyo mjipange, mishale kutoka kwa watu 5,kuikwepa ni rahisi kuliko itoke kwa watu 100.
👉 *Muda wa kukaa katika uchumba* unategemea na maandalizi na uwezo wenu juu ya harusi. Japo inashauriwa isipungue miezi 6,na isizidi miaka 1.5 hadi 2 kuepusha uchumba kuvunjika,kuchokana na kuanguka katika dhambi ya zina.( na muda maana yake unahesabika tangu mlipoitwa wachumba kwa mujibu wa hatua nilizoeleza juu) wengi mna hesabu na muda wa urafiki ambao unakuta miaka 3,4...jambo ambalo si kweli.
NB: _Uchumba si ndoa,ni ruksa kuvunja hata siku mnakula kiapo ukakataa,ndoa haifungwi,na hakuna dhambi,maadamu kuna the shocking information,isiyo vumilika. Ndiyo maana pia,kisheria kabla ya siku ya kufunga ndoa,uchunba unatangazwa siku 21,na fomu zibabandikwa makanisani,akitokea mtu anasababu ya kusitisha,anaruhusiwa. Japo,omba sana lisikutokee maishani ni kovu la kisaikolojia la kukugharimu kimawazo._
*Ulikuwa nami mchambuzi wa masuala ya mahusiamo na ndoa Ev Elisha Kazimoto*
WhatsApp 0755444078
Saturday, 9 September 2017
UCHUMBA,MUDA WAKE KISAIKOLOJIA NA KIROHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment