*NI UTATA MTUPU*
(*_Ninaye Mpenda Hana Mpango na mimi, na Aliye na mpango na mimi Simpendi_*)
*_Ev. Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
❤Miongoni mwa changamoto ya Kisaikolojia vijana wanayokutana nayo katika mchakato wao wa kutafuta wenzi wa maisha ni huu *Utata Mtupu*_Unaye Mpenda ndo kwanza Hana Mpango na Wewe, lakini Usiye Mpenda Ndo anampango mkubwa na wewe_,Nitachambua Utata huu kwa Mitazamo miwili, Mtazamo wa Kibiblia na Mtazamo wa Kisaikolojia.
❤Siku zote ndoa, Mapenzi, huambatana na Tabia zifuatazo;,
💍 *_Hisia kali ya Kupenda Sura, Umbo_* 💍 *_Makadirio ya uzuri wa kitu usicho kiona kwa kutumia taswira ya sura unayoiona_*
💍 *_Matarajio ya hali ya baadaye ya mtu huyo_*
💍 *_Shahuku ya kuwa katika Imaya ya mfumo wa maisha ya mtu huyo unavyo mwona_*
❤Sasa, Utata wa Kisaikolojia unakuja wapi kwa matazamio ya vijana juu ya wenzi wanao wahitaji?
❤ _Saikolojia ina falsafa hii, (Philosophy)isemayo_ *_Beauty is not up on the object, but on ones Eyes_* (_Uzuri haupo katika kitu, ila katika macho ya mtu) ndiyo maana unayesema mzuri wenzako wanaona kawaida sana au Hana Uzuri.
❤Utata huu wa Kisaikolojia umewafanya watu kuchelewa kuoa/kuolewa, au kuoana na mtu ambaye hakutarajia na hakutaka.
❤_Hapa vijana wa kike na kiume muwe makini sana, kwa kuwa unaweza kujiumiza sana, halafu mwisho wa maumivu huwa ni maamuzi yasiyo kidhi mahitaji ya kisaikolojia.
❤ *_Vijana wengi wakianza mchakato wa kutafuta wenzi, huorodhesha vigezo vingi bya mtu anaye muhitaji, na wengi huenda mbali sana kwa kuwa na msimamo usio badirika, wakihitaji vigezo vyote vitimie_* Lakini wanacho sahau katika vigezo alivyo weka inaweza isiwe rahisi kumpata mtu mwenye vyote, au Vigezo alivyo viweka kuna upande mwingine tofauti na yeye na yeye hawahitaji kuwa na mtu mwenye vigezo hivyo, hivyo kwa kishikiria vigezo vyote hivyo ana kinzana na mtu wake sahihi anaye mtafuta.
❤ Kuweka vigezo si mbaya, nikuweka dira ya kufikia malengo yako, lakini unahakika gani kuwa na wewe unafiti katika vigezo flani vya anaye kutafuta ambaye humjui?
❤👉�Baadhi ya vigezo vinavyo sumbua vijana;
💍 *_Awe beautiful /handsome wa ukweli_*
💍👉� *_Awe vizuri kiuchumi_*
💍👉� *_Awe mrefu, mrefu kiasi, mfupi, mfupi kiasi_*
💍👉� *_Awe ananizidi au namzidi Elimu_*
💍👉� *_Asiwe mfanyakazi kada ya Ualimu, Nesi, Askari, nk_*
💍👉� *_Asiwe anatoka familia maskini au yenye watu wengi_*
💍👉� *_Awe na nyumba au usafiri_*
💍👉� *_Awe Mkristo, mchungaji, mwimbaji, TAG, EAGT, EFATA, FPTC nk_*
❤Haya yote ni mazuri, ila wewe umejiuliza unavigezo gani? Vyote ulivyo ainisha unavyo? *_Sasa kama wewe huna vyote, hivyo umemwekea nani?_*
❤ _Ushauri wa Kisaikolojia hapa kwa vjina wa kiume na wakike, usikurupuke kusema *HUYU NO*, Kama hujafanya cross checking ya vigezo vyako watu wakiviainisha kama unauwezo wa kukubalika_
❤ Laini pia angalia katika vigezo ulivyo ainisha, aliye kuja, au unaye mwendea kama hana vyote, inaweza athiriaisha yako ya ndoa, au unaweza kufanya vizuri ila itahitaji kuongeza umakini kuiweka ndoa katika malengo yako? Fanya maamuzi.
*MTAZAMO WA KIBIBLIA*
❤ _Biblia inaweza kutupa majibu ya Utata huu_ ila majibu ya Biblia yanahitaji kutumiwa na mtu aliye na sifa hizi, ndo Biblia inaweza kukupa majibu, ya _Mtu usiye mpenda ndo anakuhitaji, na unaye mpenda hakuhitaji, ikageuza, Yule unaye mpenda hakupendi Akakupenda_
*Ayubu 42 : 2 - Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.*
👉�👆Makusudi ya Mungu hayazuiliwi kwa hisia za mtu za kisaikolojia. Ila kuyatimiza mapenzi ya Mungu katika kuoa na kuolewa uwe upo katika kona hizi:
1⃣ _Uwe upo vizuri na Mungu_
2⃣ _Uwe ni mtu wa kujituma kwenye mambo ya Mungu kwa bidii_
3⃣ _Uwe na tabia ya kumtegemea kumwamini Mungu katika mambo yako yote_
4⃣ _Mtazamo wako kwa ndoa uwe ni kwa faida ya ufalme wa Mungu na kwako_
5⃣ _Uwe unamjua Mungu kweli na unaweza kuyakubali mapenzi ya Mungu_
*Warumi 9 : 11 - *_(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),_*
❤ _Katika kuhitimisha Utata huu, Sibkwamba huwezi kupata mtu wa vigezo vyako vyote, unaweza pata ila ni neema, lakini pia unapo kutana na Utata huu usiutolee Maamuzi ya haraka, inaweza kuwa unaye mpenda hakupendi si Wako, ndo maana Mungu haja mwekea Connection ya kuambatana na hisia zako, lakini huwenda unaye mpenda hakupendi, hawezi beba future yako ya ndoa unavyo tarajia, ndo maana Mungu hajaweka hali ya yeye akupende, lakini unaye mpenda hakupendo, ukilazimisha akupende kwa mbinu zako, ndani anaweza rudi katika hali yake ya mwanzo ya kutokupenda, utaumia zaidi ya ujana_
👉� *_Anaye kupenda humpendi, tafakari, ameona nini kwangu na yeye ana nini cha ziada, lakini nimi Mapenzi ya Mungu kwa huyu mtu_*
❤❤ Mwisho Lenga sana Kwanza kupata mtu aliye na Hofu ya Mungu❤❤
*_Ev. Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
Thursday, 31 August 2017
NAMPENDA-HANIPENDI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment