Tuesday, 15 August 2017

IMANI KATIKA MAHUSIANO

*Swali*: _Kuna mkanganyiko wa dini,dhehebu na Imani, nani nioe au niolewe naye, je madhebubu ya Kikristo yote ni sawa?au kunatofauti?_
*Mchambuzi Ev Elisha Kazimoto*
_Labda niseme kwa mtazamo wa jumla tu kuhusu mambo ya ya imani,kwa kujibu swali ila uchambuzi wa kina kuhusu dini na madhebu na historia yake ni mada kubwa mno yenye nasomo marefu mno,ila kwa Summarization naweza kusema kwa ufupi kama ifuatavyo,hata bila ya maandiko,somo maalumu lina maandiko yakutosha_
Kuna vitu hivi vya kutofautisha,na vinatofautiana
1.Dini
2.Dhehebu
3.Imani.
4.Taratibu
👉Dini ni njia inayobeba mlengo wa mtu/kiongozi mwanzilishi(mfano. Ukristo -Yesu Kristo, Uislamu-Muhamad)hivo hivo,budha,hindu nk
👉Dhehebu matabaka ndani ya dini, yanayoanzisha kwa mlengo wa imani katika maandiko kadhaa kama msingi wa imani yao. Pia madhebubu yanaanzishwa kulingana na ongezeko la watumishi wenye maono mbali, na malengo ya kupanua huduma.( kwa makadirio duniani,Ukristo unamadhebu karibu 14000,na uislamu una madhebubu 7000)
👉Imani,ni msinamo wa dhehebu husika(na hiki ndo kiiini cha wokovu,mapokeo,upagani, na Ushetani)ndani ya dini,dhehebu....
Sasa,mfano. Kuna madhebubu ya Kikristo, yenye imani ya Kipentekoste yanayo amini katika misingi 17 ya Imani ya Kipentekoste ya wokovu(baadhi ya misingi ni, 1.Anguko la mwanadamu(kutenda dhambi na kufukuzwa edeni, 2.Ukombozi wa mwanadamu kwa njia ya Yesu Kristo, 3.Kufa na kufufuka kwa Yesu,4.Ubatizo wa maji mengi,5.ujazo wa roho mtakatifu,6.Kuishi maisha matakatifu hapa duniani,7.unyakuo wa kanisa,na ujio wa Yesu kristo mara ya pili,8.Uwepo wa mbingu mpya na nchi mpya(maisha ya milele baada ya kufa),10.uwepo wa Jehanamu ya milele, 11.Uwepo wa Mungu mmoja aliye hai, 12. Utatu mtakatifu(Mungu baba,Mungu mwana na Mungu Roho mtakatifu )
Jamani hiyo ni kati ya misingi ya madhebubu ya Kipentekoste yote, kama TAG,EAGT,FPTC,CAG,FGBF(KAKOBE),.... Na baadhi Ministry
(Baadhi ya Ministry za Mitume na Manabii au Wachungaji zina imani ya kipentekoste ila wameingiza vitu vyao vyenye utata, kama mafuta,maji,vitambaa,kukanya watu,kuromance watu,deliverance kwa njia ya ngono, nk)
Baadhi ya madhebubu ya Kikristo, mfano Roman,Anglican,Lutheran Morovian,Sabato,Jesus only, Siloamu nk...misingi ya Imani yao imechanganyika, ya kimapokeo na ya kibiblia(mfano, ubatizo wa watoto, ibada ya sanamu, ibada ya wafu, kuimbea marehemu ahamishwe kutoka motoni kwenda mbinguni,kuokoka ni baada ya kufa,siyo duniani,tutaishi milele duniani hakuna kufa, Yesu alishindwa kazi Adamu Mnuo ndo kakamilisha kazi, hakuna utatu mtakatifu kuna Yesu tu),hakuna ujazo wa Roho mtakatifu,ubatizo hauna maana, kubatiza kuondoa dhambi ya asili,nk hizo ni imani zikizo nje ya Biblia, ni mapokeo ya ukengeufu na Upagani.
Sasa kila mmoja kwa dhehebu lake,imani yake ajipime je, Misingi ya Imani yake ipo katika Biblia au au ni mapokeo ya ubunifu wa wanadamu?
*_Kwa maelezo mafupi waweza tafakari mambo haya ya imani_*
   Ev Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment