Tuesday, 15 August 2017

KUSUA SUA KWA MAWASILIANO

*Swali la Mahusiano mtu ameuliza( Mdada)*
*_Hivi unaweza kukaa kwa muda gani bila kuchat na mpenzi wako(Mchumba wako)?_*
*_Mimi wa kwangu now yupo busy hakuna cha kuchat labda kameseji kamoja tu asubui na kengine usiku. Najisikia vibaya kwakweli, hii imekaaje naomba ushauri_* 😭😭
MAJIBU: NA MWANASAIKOLOJIA YA MAHUSIANO NA NDOA *_EV ELISHA KAZIMOTO_*
WhatsApp 0755444078
_Kuna mambo ambayo wana mahusiano mnahitaji kuyajua hasa mambo makuu mawili,nayo ntaya chambua hapa katika uchambuzi wangu, karibu tuanze sasa uchambuzi wetu_
1⃣ Siku zote wadada jueni ya kuwa love is two way traffic (ni njia mpeano)siyo kupokea tu. Na hiyo ni mpaka kwenye ndoa, ukishaona tayari tumependana au tumeoana anza kutoa na kupokea matendo ya upendo,kuwa mwanamke siyo kigezo cha kukaa na kusubiri utafutwe kwenye simu,utumiwe vocha,upewe zawadi,usifiwe.. Hapo unalazamisha kukaa stage 1 ya awali ya kutafutwa(hapa mmeisha ingia stage ya kupendana siyo kupendwa)na hili ndo kosa la kisaikolojia na kimantiki wadada na wanawake hukosea. Hata kwenye ndoa wanawake wengi wanasubiri waombwe sex, uliombwa honeymoon ukiwa mgeni,ukikaribishwa,basi saizi umeonja na wewe anza kuitaka upewe na yeye atake apewe ndo love hiyo ya watu wenye akili ya saikolojia ya mapenzi.
Sasa katika mahusiano,kijana alikuwa anajinyima,anawinda mpaka akakunasa,(yeye alikupenda)ila wewe hukumjua,hukumpenda ndo maana kila dakika,alikuwa akikuweka busy kimawasiliano,kizawadi, ili kujuleta karibu,ushibe matendo ya upendo na wewe umpende ili mpendane. Sasa mmeisha pendana wajibu wa kuwasiliana niwakila mmoja kumtafuta mwenzake muda wowote. Hata kijana anahitaji kuona hutu niliye mleta karibu kweli yupo karibu au bado yupo mbali? Usisubiri kutafutwa,mtafute,mpe maneno mazuri hata vocha na wewe mtumiepo mara moja moja(Love is Two Way Traffic )Mpeano. Ukisubiriwa mimi mdada nitafutwe tu,niambiwe maneno mazuri tu,asipi fanya unajiuliza eti mbona amebadilika? Jua amegundua pamoja na harakati za kukuleta karibu iki mfanane(mpendane hazijazaa matunda)bado anakupenda wewe imegoma kumpenda,kitakacho tokea ni KUKUACHA,atafute mwingine atakaye elewa Falsafa ya Mapenzi Kupeana siyo Kupokea tu.
_katika point ya kwanza nadhani wadada na wanawake mloolewa mmenielewa,usisubirie tu ufanyiwe(kama anaye tafutwa bado)kumbe ulisha kubaliana kuwa katika love naye au ndoa,peaneni matendo ya upendo,kama ni mawasiliano nawe mtafute kila ukimfikilia,akikuwahi sawa,ukimuwahi sawa_
*Ukipoteza wewe kwa ujinga na uzembe wanaokota wengine wenye njaa na akiki ya ziada ya kupet pet na hutompata tena,akiangukia mikononi mwa wajanja*
2⃣ Katika Point ya kuwa na mawasiliano hafifu katika mahusiano kwa kigezo cha UBIZE *_Nitoe Angalizo hapo_*
*_Ukiingia kwenye biashara ya Mahusiano(MAPENZI)Kumbuka simaanishi Ngono(Mapenzi ni Msamiati wa Kisaikolojia ulioshiba Hisia kali juu ya mwenza wako) ukiingia katika biashara ya mahusiano(Mapenzi)uwe una uhakika wa kulipa gharama ya ya vitu vifuatavyo._*
1.Gharama ya Muda, uwe unajua ya kuwa mwenzi wako anahitaji presence yako katika mawazo yake(hili ni janga la wana mahusiano) ( *_Mwenzako anahitaji Presence /Uwepo katika Akili yake muda mwingi_*) na hiyo ndo tafsiri ya upendo au mapenzi( ndo maana biblia inasema mpende Mungu wako kwa Akili yako yote, that means ndani ya akili yako iwepo presence ya Mungu. Huko ndo kumpenda Mungu.hivyo hivo hata katika mahusiano kama huna presence y mwenza wako akilini hakuna love hapo mnasindikizana muda wowote break up itatokea akipatikana wa kuweka presence yake sawasawa...
Na ni njia ya kuwasiliana mara kwa mara ndo inajenga presence yako kwenye akili yake. Kwa hiyo kwa vyovyote vile uwapo busy pata dakika chache iwe kwa sms,call,face to face za kuweka ku cement sura yako kwenye akili yake.
2.Gharama ya pesa, 3.gharama kuumizwa hizo sizielezei kwakuwa siyo topic yangu ya kujibu swali.
*NOTE* _Kama mtu anasema yuko busy hawezi hata kuku sms,call hata mara 3,4,5 kwa siku lakini mwanzo alikuwa ana call,sms hata mara 10,20 anza kumfatilia kwa umakini anaweza kuwa anajenga saikolojia yako ya kukuzoeza kuwa mbali naye iki siku atakapo kwambia Bye bye usiumie sana_  maana hakuna ubize saidi ya mwenzako. Love inatunzwa kwa mawasiliano ndo image yako inakaa kichwani mwake na kujenga nguvu ya uaminifu,furaha moyoni mwake juu yako.
*_So usidharau mabadiliko madogo madogo ya kisaikolojia katika mahusiano kama mawasiliano,zawadi,maneno mazuri yakianza kupungua_*
Mwisho, wana mahusiano lazima mfahamiane mazingira yenu ili kuepusha kuhisi tofauti( Psychological Confusion ) peaneni uhalisia wa ubize wenu ili muwe na muda maalumu wa kuongea,kuchati ambao ubize umeisha mpange mfano. Siku nzima mlo busy wote au mmoja yuko busy,basi saa 4-6 usiku,(mfano tu) tutaongea,chati tupeane ya kutwa nzima. Hiyo ndo akili ya mahusian. Siyo kusema upo busy tu, busy muda gani? 24hrs au? Labda hujapenda na kupendwa.
             *T  A  K  E  C  A  R  E*
*_Ulikuwa nami mchambuzi wa masuala ya mahusiano na ndoa Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
Fb Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment