✍✍ *NGUVU YA KALAMU YA MWANDISHI*✍✍
Na Ev Elisha Kazimoto
WhatsApp 0755444078
_Shalom mwana maombi,mtu ukiyejiweka tayari katika nafasi ya kushinda, leo katika mkesha wetu wa maombi,nakuletea ujumbe mfupi lakini wenye nguvu ya kubadiri mwelekeo wa maisha yako hadi uzeeni,na ndiyo operation yetu usiku wa leo, *Operation ya Kufuta maandishi dhaifu na kuandika upya Maandishi ya nguvu*_ utanielewa ninacho kwambia.
*_Zaburi 45 : 1 - Moyo wangu umefurika kwa neno jema, Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi._*
✍Umewahi kusikia,na kujiukiza kwa nini watawala hulia,au upigia kelele waandishi wa habari?
✍Umewahi kujiuliza hivi kwa nini watawala (Rais)wanapo teua mtu au kutengua watu,wanaita waandishi wa habari, au inatolewa barua yenye kichwa, *"Kwa Vyombo vya Habari* wanajua nguvu ya kalamu ya mwandishi.
✍Ndiyo maana kwa mtawala au mwanasiasa ukimnyima nguvu na nafasi katija Vyombo vya habari ni adhabu kubwa kwake,kuliko kumpuguzia mshahara.
✍Namaanisha wewe mtu wa Mungu ni mtawala( *Mwanzo 1:26-27, Ufunuo 5:9-10*) ila unahitaji nguvu ya Kalamu(Mamlaka ya Kristo katika ulimi)
✍Usiku wa leo,unapaswa kujua wako waandishi uchwara,kalamu za mtaani(wachawi,mapepo,watu wenye hila)waliandija na wanazidi kuandika mabaya katika maisha yako.
✍Na katika maisha yako,waloandika wameweka kichwa cha habari kikuubwa cha kuuzia gazeti la maisha yako,kwa mapepo,wanadamu nk,kichwa kisemacho, *Hawezi Kuolewa, Hata fanikiwa, Ni wa magonjwa, Ni wa migogoro katika ndoa au kazini, nk* vichwa vya habari vya maisha yako vimewavutia wachawi,watu,mapepo hata wewe kuendelea kuandika madhaifu katika maisha yalo.
✍Usiku wa leo katika operation yetu,tuna tumia mfuto wa Damu ya Yesu,tunafuta kauli zote,vichwa vya habari vyote viovu,vya kushindwa,kutofanikiwa,kutapata kazi,mme,mke nk na tunatumia Kalamu zetu,na kwa ustadi mkubwa tukiopewa na Bwana wa kuumba,yakaumbika.( *Mithali 18:21*),Futa maandishi ya wachawi,mapepo na watu wenye hila na andija Upya, na Upige Title kubwa, kama hii *WACHAWI HAMNIWEZI TENA, UMASKINI KWISHA, USHINDI LAZIMA,SIRUDI NYUMA NG'O* na zingine na zingine kwa kadri ya upako na ufunuo unao kushukia.
✍Halafu anza kuandika mema yote unayoishi,inabidi yasomeke katika maisha yako,kama mke,mmw,nyumba,usafiri,huduma kuu,kufauru masomo,andika,hayo uyaandikayo ndo yatakufanya uwe na level nyingine.
✍Kwenye maombi kawambie maadui,mliandika shida hizi kwangu,mkahisi hakuna wa kuzifuta?sasa Damu ya Yesu imefuta leo na sasa naanza kuandika upya kwa ustadi mafanikio yangu.
*_Kutoka 17 : 14 - Bwana akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu._*
✍Mara baada ya ujumbe huu wewe unaandika nini? Musa aliambiwa andika andika habari hii iwe ukumbusho jinsi maadui walivyokomeshwa mbele ya wana wa Mungu,ili maadui wafadhaike na wana wa Mungu watiwe nguvu.
_Mimi naanza kuandika sura mpya ya huduma,uchumi,ndoa ,kazi,maisha mengine, naamini nawewe unanafasi ya kuandika ili kila asomaye ajue kuna nguvu imewekezwa na haiporwi kirahisi._
WhatsApp 0755444078
*Ev Elisha Kazimoto*
Friday, 25 August 2017
KALAMU YA MWANDISHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment