Friday, 18 August 2017

TAA YAKO ISIZIMWE

🌳 *MAISHA YAKO YA KIROHO NA KIMWILI YANAHITAJI ULINZI MKUU NDO UFANIKIWE*🌳
               *_By Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
_Shalom watu wapendwao na Bwana,leo Bwana amenipa kitu cha kukuongezea katika maisha yako ya kivita katika ulimwengu wa roho. Watu wengi mambo yao yameshindikana,ndoa zimevurugika,wachumba wamekuacha kizembe,elimu imegoma,biashara imeingia hasara,kazini na mtaani unahisi upweke,kuchukiwa na kutengwa,kumbe kuna mchezo mchafu wachawi,maadui zako wanaufanya katika ulimwengu wa roho wa *Kuzima Taa zako* na katika ujumbe huu nakupakulia aina ya taa 4 inabidi uwe nazo makini zisizimwe ndo malengo yako yatatimia_
*_Kulinda Taa Yako Isizimwe na Wahuni_*
*Mathayo 6:22-23*

22 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. 

23 Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo! 
✍Taa ni chanzo cha mwanga,unao saidia kuona pa kwenda au kukaa.
✍Maisha uliyo nayo,ni sawa na idadi ya taa zinazo waka au zilizo zimwa.
*2Samweli 21:15-17*
15 Basi kulikuwa na vita tena kati ya Wafilisti na Israeli; Daudi akashuka mpaka Gobu, na watumishi wake pamoja naye, akapigana na Wafilisti; naye Daudi akaishiwa na nguvu. 

16 Naye Ishi-benobu, aliyekuwa mmojawapo wa Warefai, ambaye uzito wa mkuki wake ulikuwa shekeli mia tatu za shaba kwa uzani ,naye amejifungia upanga mpya,alijaribu kumwua Daudi. 

17 Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti, akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli. 
✍Adui anajua taa ikizimwa na uharibifu unaingia.
✍Adui anajua taa yako ikizimwa,uwezo wako wa kukwepa mishale yake ni mdogo na atakuweza.
✍Adui anajua taa yako ikizimwa,Malengo yako hayatimia na ndo kusudi la mchawi.
*Baadhi ya Taa za Mwanadamu*
*1.Kibali(Mithali 3:4-5)*
👉Kibali ni nguvu ya kukubalika(Mvuto kwa watu)/kwa Mungu
👉Mtu akikosa kibali mbele za Mungu na mbele za watu,hupelekea ukomo wa furaha yake na uwezo wa kufanikisha malengo yake.
*2.Heshima(Mithali 8:17-18,Yohana 12:26),*
👉Heshima ni Kustahilishwa, kuwa na nafasi ya upendeleo katikati ya wengine wanao mzunguka.
👉Mtu akiondolewa heshima na maadui,anadharauliwa na kuwekwa katika nafasi ya kupokea,kusikia na kuona mabaya.
*3.Utisho(Kutoka 23:27)*
👉Utisho ni nguvu ya kumdhohofisha aliye mbele yako,aidha akupishe,aachilie mbele yako alo navyo,au atende kwa hofu na unyenyekevu mbele yako.
👉Utisho unaambatana na Mamlaka ya kutoa amri na jambo likafanyika bila kupingwa.
👉Taa ya Utisho ikizimwa mtu anapoteza nguvu ya kutoa amri na ikatekelezwa, lakini hutopishwa na adui yiyote mbele yako,au kuachia vitu vyako
*4.Utofauti/Upekee (Waamuzi 16:17)*
👉Upekee(kuwa wa pekee), ni hali ya kukutofautisha kati yako na wengine.
👉Upekee ni nguvu inayodhihirisha uwezo wako ulivyo tofauti na wengine.
👉Taa ya upekee ikizimwa,hutaonekana umuhimu wako popote,maana huna tofauti na yeyote.
✍Hizo ndizo taa ambazo zinamfanya mwanadamu kuishi maisha ya amani kiroho na kimwili.,zikizimwa furaha kwisha,wokovu mzigo
*2Nyakati 29:5-7*
5 akawaambia, Nisikieni, enyi Walawi; jitakaseni nafsi zenu sasa, mkaitakase na nyumba ya Bwana, Mungu wa baba zenu, mkautoe uchafu katika patakatifu. 

6 Kwa maana baba zetu wameasi, na kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wetu, wamemwacha, na kugeuzia mbali nyuso zao na makao ya Bwana, na kumpa maungo. 

7 Tena wameifunga milango ya ukumbi, na kuzizima taa, wala hawakufukiza uvumba, wala hawakumtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa katika patakatifu. 
✍Kuwa makini na wazima taa za ukumbini(moyo wako)
✍Hakikisha unatoa uchafu katika nyumba ya Bwana na uwashe taa.
✍Usikubali mtu mwingine(mchawi) akuambukize roho yake,tabia yake
✍Usiwe mtu wa kuiga matendo ya wahuni(wachawi/ya kichawi)taa yako isizimwe.
✍Ukigundua kuna baadhi ya taa zako hazina mwanga, tafuta watu walio sahihi kiroho wakusaidie kuwasha taa upya.
✍Wakimbie watu wote walio na taa hafifu,au zilizo zimwa, jiambatanishe na walio na taa zinazo waka.
✍Katika maombi yako omba sana,taa zako zisizimwe.
*_Imeandaliwa na Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078

No comments:

Post a Comment