*MAWASILIANO KATIKA UCHUMBA*
_Mahusiano ni nguvu ya kisaikolojia inayo vuta hisia na moyo wa mtu juu ya partner wake. Mahusiano hai,imara huwa kuna nguvu inayo chochea hisia,ambapo mtu huwa radhi kusema chochote na kufanya chochote kwa partner wake ili mradi amridhishe,na kumfurahisha partner wake. Hiyo ndo Saikolojia ya Mahusiano_
✍Nature ya mahusiano ni kwa kila mtu,awe ameokoka,mchungaji,nabii,mtume nk wote nguvu ni moja ya mahusiano, ila tofauti ni kwamba, *Mtu aliye okoka,aliye na Roho mtakatifu,hofu ya Mungu, Neno la Mungu,anajua katika mambo yote ya kimaisha, kunahitajika KIASI na hekima ya kulinda Ushuhuda na Utakatifu wenu* kwa maana hiyo nguvu ya saikolojia uwekwa sawa.
✍Kuna vitu vya kutofautisha, *_Mawasiliano ya sms, call au live ya kimahaba, na ya Kiupendo_* mawasiliano kwa mchumba wako yanayo lenga kufunua uchi,kutimiza hisia za ngono, kumfanya mtu atamani kutimiziwa kiu ya ngono, hayo ndo mabaya na makosa kwa wachumba WALIOOKOKA,ila kwa wapagani ni kawaidaa hawana mipaka,ila watapata shida ya kisaikolijia ya kuonjwa na kuachwa.
✍Ukweli ni kwamba unapokuwa na mchumba( Expected Wife,or Husband )mawasiliano yenu,ni tofauti naunavyowasiliana na mtu mwingine *_Na ndivyo inavyo hitajika, onyesha kupenda, onyesha kumjali,onyesha kuwa wa pekee,_* lugha za upendo, kama kumsifia alivyo mzuri, unavyo mpenda, nk,lugha za upendo, sasa usichanganye lugha za mahaba ya ngono na upendo, mambo ya *Umelala na nguo au uchi?, umevaa under wear gani? Maziwa yako yakoje, umbo la sehemu za siri likoje, njoo tulale wote, nikumbatie hapa nina baridi nk,hizo si lugha za upendo ni za mahaba,nazo uibua hisia za mwili,jambo ambalo upelekea kuingia katika zinaa kabla ya ndoa,au kujichua baada ya mazungumzo,na hiyo ndo athari zake* kujikinga tumia Lugha za upendo siyo za mahaba kwa mchumba wako, mkioana, tumia zote, moto ukipanda mna uhuru wa kuuzima na hakuna dhambi wala kuhukumiwa.
*By Ev Elisha Kazimoto*(0755444078)
Monday, 2 October 2017
AINA ZA MAWASILIANO YA WACHUMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment