Saturday, 21 October 2017

KISS KWA WACHUMBA

*Habari ndugu zangu*

*_Nina swali nalo ni...Je ni makosa kwa wapenzi kubusiana (kumbusu mwenzake)?_*

Anajibu: Ev Elisha Kazimoto (Baba Evan)
*WhatsApp* 0755444078

*_Katika swali hili, lugha iliyo tumika ni lugha tata (Ambiguity ), MPENZI( Mpenzi kwa maana ya watu walio katika mahusiano ya kimapenzi-wanaoshiriki sex? Au Mpenzi kwa maana ya mtu uliyenaye katika mahusiano anaoupendeza moyo wako(mpenzi-mchumba).?_*
Kwa namna yoyote ile nitoe taswira halisi, *Kama ni suala la Mpenzi, mnaoshiriki sex, busu yoyote haina shida, simple au deep kiss haina shida,maana sex ni more than kiss* (Angalizo kwa watu waliookoka,wana wa Mungu HATUNA MSAMIATI WA MPENZI wa sex, HATUNA MCHUMBA wa sex)
Kwa habari ya mchumba kuna vitu tunaviita *_Maadili ya Uchumba kwa watu waliookoka_* hapa ndipo tunapo tofautiana kati ya wachumba wapagani, wachumba wana dini,nawachumba watakatifu(waliookoka) *MAADILI NI PAMOJA NA:
1⃣ Kulinda Ushuhuda katika kipindi cha uchumba chote, msilete tafsiri itakayo fanya watu wawaone hamjaokoka(epuka kulitukanisha jina la Yesu kwa mwenendo,tabia yenu nk.
2⃣ Kuto fanya mambo yanayoweza chochea kwa kasi hisia za miiki yenu na kuwafanya muanguke kwenye dhambi ya zinaa( mfn, sex touching,sex plays,Kisses, hasa deep kiss, hug hasa Zero distance hug (hug ya dk 1,2,5,10...mnatafuta nini)🤔🤔
3⃣Kuto kutana kwenye mazingira ya uficho yanayoweza kuwaingiza katika vishawishi vya zinaa.
*KISS & HUG*
_Kiss na hug havina ubaya wowote,wala dhambi yoyote, suala nia yenu ya kiss na hug ni nini? Je mko huru kukiss na ku hug publically? Au mpaka muwe wa 2 tu?_
Kuna dhana na mwavuli wa kiss takatifu.... Huu ni uongo ni utumiaji wa maandiko vibaya kutimiza mahitaji ya kiihisia. Kiss takatifu haitofautiani kwa jinsia zote(ndo mtume Paul aliisema) sasa kama kaja yako,dada yako,mama,bibi, mchungaji wako mana mchungaji wako na mshirika wowote waweza mpa kiss hiyo hiyo unayotaka kumpa mchumba  wako basi hiyo ndo busu takatifu kwa watakatifu wote
Kinachoongelewa na vijana wasasa kuhusu kiss siyo kiss wanaongelea ROMANCE ila wanapunguza makali kwa kuiita kiss, hivyo si jambo jema kwa wachumba wakiroho kuromance(deep kiss) mnachokitafuta si ku express love, ila mna express sex feelings zitakazo wagharimu katika safari yenu.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*

No comments:

Post a Comment